JamiiForums
56.3K subscribers
32.7K photos
1.82K videos
29.9K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
DAR: Shauri la jinai linalomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu linadaiwa litafanyika kwa njia ya Mtandao leo Aprili 24, 2025

Hata hivyo taarifa zisizo rasmi zinadai Lissu amegoma kushiriki katika Kesi hiyo kwa njia ya Mtandao akitaka afikishwe Mahakamani. Juhudi za kupata taarifa rasmi za Mamlaka zinaendelea

Kwa mujibu wa Wakili ambaye ni sehemu ya jopo la Mawakili wanaomtetea Lissu, ameiambia JamiiForums kwamba tayari wameingia Mahakama (Virtual court) kwa ajili ya kuanza kusikiliza kesi zinazomkabili mteja wao.

Soma https://jamii.app/LissuKesi

#JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Demokrasia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#HAKIZABINADAMU: John Pambalu (Mkurugenzi wa Mafunzo CHADEMA), Twaha Mwaipaya, Lucas Ngoto (Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti) pamoja na baadhi ya Wanachama wengine wamedaiwa kupigwa na kuumizwa leo Aprili 24, 2025

Soma https://jamii.app/PambaluKupigwaPolisi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Motisha huja na kuondoka, ni hisia ya muda. Nidhamu ni maamuzi ya kila Siku ya kufanya kile kilicho sahihi hata kama huna hamasa.

Mafanikio ya kweli yanategemea nidhamu, si motisha pekee.

Tunakutakiwa Wikiendi njema

#JamiiForums #Lifelessons #Maisha
UINGEREZA: Chama cha #LiberalDemocrats kimependekeza mpango wa kutoza faini ya hadi Pauni 1,000 (takriban Tsh. 3,589,596) kwa Watu wanaosikiliza Muziki au kutazama Video kwa sauti kubwa katika Usafiri wa Umma

Lengo ni kukabiliana na tabia zisizo za kiungwana na kulinda Haki ya Abiria wanaotamani safari tulivu. Serikali imesema iko tayari kuangalia wazo hilo na inatafiti namna ya kulitekeleza

Utafiti wa hivi karibuni umeonesha asilimia 38 ya watu hukumbana mara kwa mara na kelele zisizotakiwa kutoka kwa wengine kwenye Usafiri wa Umma, huku wengi wao wakihisi kutokuwa huru kukemea tabia hiyo.

Soma https://jamii.app/FineHeadphoneDogders

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #PublicTransport #HeadphoneDogders #UKPolitics
DAR: Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Jeshi la Polisi, wa kutumia weledi na kuepuka matumizi ya nguvu kupita kiasi hasa kwa kesi zinazohusisha Viongozi wa Kisiasa au Umma

LHRC imesema kilichotokea Aprili 24, 2025 kwa baadhi ya Watu kukamatwa wakati wakielekea Mahakamani kufuatilia shauri la Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu hakipaswi kutokea, kwa kuwa ni haki ya Mwananchi kufuatilia mwenendo wa kesi dhidi ya ndugu yake au kiongozi wake

Kituo hicho kimesema kinaishauri Mahakama kuulinda uhuru iliyopewa kwa mujibu wa Ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wivu mkubwa

Soma https://jamii.app/KamataKamata

#JamiiForums #Democracy #HumanRights #CivilRights #Kueleke2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema #Demokrasia ni majadiliano, hoja na maelewano kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano katika kujenga taifa na siyo vurugu kama ambavyo baadhi ya Wanasiasa hasa wa upinzani wanavyofikiri na kupiga kelele

Amesema hayo Wilayani Kongwa, Aprili 24, 2025 na kuongeza "Sasa wewe ukose 60% ugombee 40%, uweke Watu hawana sifa, ushindwe halafu uende Umoja wa Mataifa, huko utaenda lakini sisi tutakuwa tumeshamaliza hiyo kazi.”

Soma https://jamii.app/WasiraDemokrasia

#JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
HISTORIA: Baada ya Uhuru wa Tanganyika Mwaka 1961, Tabora Hotel iliwekwa chini ya usimamizi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na ikajulikana kama 'Tabora Railway Hotel'

Ilitumika kama mahali pa kupokea Wageni na kuwa Jukwaa la Mikutano ya Viongozi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wasomi katika Miaka ya 1970 na 1980

Mwaka 2003, Hoteli hiyo ilifanyiwa ukarabati na kubadilishwa jina tena na kuwa "Orion Tabora Hotel." Maboresho haya yalihusisha kuongeza majengo Mawili mapya yaliyopewa majina ya Mirambo Wing na Nyamwezi Wing

Fahamu Historia hii zaidi https://jamii.app/HistoriaTaboraHotel

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFKumbukizi
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Chama cha #Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakijapokea taarifa rasmi kuhusu alipo mjumbe wa Baraza Kuu la Chama hicho, Hilda Newton, ambaye alikamatwa jana Aprili 24, 2025 katika eneo la Mahakama ya Kisutu

Akizungumza leo Aprili 25, 2025, Naibu Katibu Mkuu wa #CHADEMA Bara, Amani Golugwa, amesema walitegemea jina la Hilda litatajwa kwenye taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa jana na Kamanda Muliro, lakini halikuwemo.

Soma https://jamii.app/HildaCDMHajapatikana

#HakiZaBinadamu #JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights
DAR: Jana, Aprili 24 Taasisi ya JamiiAfrica ilizinduliwa rasmi ikichukua nafasi ya iliyokuwa “Jamii Forums”

Uzinduzi huo uliambatana na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taasisi wa miaka 6 unaoelekeza dira mpya ya kujipanua kiutendaji (operational expansion) ndani na nje ya Tanzania; na katika kuchechemua kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi, mamlaka zinazojibu na kuwajibika kwa wananchi na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala anuai ya kimaendeleo

JamiiAfrica ambayo pia inasimamia majukwaa ya JamiiForums, JamiiCheck, Stories of Change, Fichua Uovu na JamiiData imenuia kupanua wigo wa kukuza Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora kidijitali na nje ya mtandao kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali

Soma https://jamii.app/UzinduziJamiiAfrica

#JamiiForums #Rebranding #JamiiAfrica