JamiiForums
56.4K subscribers
32.7K photos
1.81K videos
29.9K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
Maudhui potofu yanaweza kupotosha Umma, Kudhalilisha Watu, au hata kuchochea machafuko ya kijamii. Ni muhimu Jamii ifahamu na iwe na uwezo wa kutambua Maudhui ya aina hii.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anasema licha ya uwepo wa Magugumaji maeneo mengi ya Kando ya Ziwa Victoria, mbona haoni jitihada za Mamlaka husika kuyaondoa wakati yamekuwa kero kwa Watu na Vyombo vya usafiri?

Soma https://jamii.app/Magugumaji

#JamiiForums #Accountability #JFMdau2025 #Uwajibikaji
MANYARA: Timu ya #Yanga imefanikiwa kufikisha alama 70 katika Michezo 26 iliyocheza ya Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Fountain Gate Magoli 4-0 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwara, leo Aprili 21, 2025

Wafungaji wa Mchezo huo ni; Clement Mzize (mawili), Ki Aziz na Clatous Chama. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kubaki nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Simba yenye alama 57, Michezo 22 huku Fountain Gate ikisalia nafasi ya 11 ikiwa na pointi 29

Soma https://jamii.app/GateYanga

#Sports #JamiiForums #JFLigiKuu25
SINGIDA: Wakati akilalamikia ubora wa Barabara ya Singida – Babati – Arusha, Mdau mwingine wa JamiiForums anasema eneo la Endasak Wilaya ya Hanang Barabara ina Mashimo mengi pia

Anaongeza kuwa hali hiyo inaanzia Kata ya Masakta hadi Endasak na changamoto hiyo ni ya muda mrefu licha ya kuwa ni Barabara Kuu

Soma https://jamii.app/BarabaraSingidaBabati

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability #Governance
Ukaguzi wa taratibu za ununuzi wa vifaa vya ujenzi vilivyotumiwa katika OR-TAMISEMI chini ya Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwaajili ya ujenzi wa shule Mkoani Mara, ulibaini ununuzi wa vifaa vyenye thamani ya Tsh. 3,100,824,370 ulifanyika kinyume na masharti ya ununuzi wa Mwongozo wa Mamlaka ya Uthibiti wa Ununuzi wa Umma wa Utekelezaji wa Kazi za Ujenzi

Vifaa hivyo vilinunuliwa kutoka kwa Wazabuni ambao hawakuwa wameidhinishwa, au katika maduka yasiyokuwa na idhini ndani ya jamii husika au bila kuwa na makubaliano yoyote ya kimkataba kutoka kwa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA)

Hayo yamebainika katika Ripoti ya CAG 2023/24 na kuelezwa kuwa hilo linadhoofisha Kanuni za uwazi, uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma

Soma https://jamii.app/CAGMiradiMaendeleo

#RipotiYaCAG25 #RipotiCAG2025 #Uwajibikaji #CAGMiradiMaendeleo #Accountability #JamiiForums #Transparency
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka kushughulikia changamoto za miundombinu ndani ya Stendi ya Mabasi ya Nyegezi, akidai kuna Maji taka yanayotoka Chooni na kutiririka sehemu Watu wanapopita hali ambayo inaweza kusababisha Magonjwa ikiwemo Kipindupindu

Mdau anasema “Ndani ya Stendi kuna Vyakula vinauzwa, kuna Maduka ya bidhaa mbalimbali ikiwemo vinywaji, kwa hali hiyo Kipindupindu kinaepukwaje?

Soma https://jamii.app/NyegeziMajiTaka

#JamiiForums #PublicHealth #Accountability #JFMdau2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Abiria wamelazimika kuzuia basi la Mwendokasi kupita katika Kituo cha Kimara Mwisho baada ya kusubiri usafiri huo kwa saa kadhaa bila mafanikio, asubuhi ya leo Aprili 22, 2025

Ikumbukwe mara kadhaa Wadau wa JamiiForums.com wamekuwa wakilalamikia changamoto ya usafiri wa Mwendokasi ikiwemo kukaa muda mrefu kituoni

Soma https://jamii.app/MwendokasiMgomo

#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery


Video: Kagaba_GR
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JFKUMBUKIZI: Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumzia maendeleo ya Demokrasia, ikiwemo suala la #Uwazi na matumizi ya #Teknolojia katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya, wakati alipokuwa Kiongozi ya Timu ya Uangalizi ya Uchaguzi huo, Agosti 2022

Soma https://jamii.app/JKKenya2022

#JamiiForums #JFKumbukizi #Democracy #KenyaPolitics #Transparency
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Ally Mkii amefungua shtaka la Madai Mahakama Kuu, akiitaka Hospitali ya Aga Khan imlipe fidia ya Tsh. Bilioni 1.2, akidai uzembe wa kimatibabu umesababisha Mtoto wake akatwe mguu alipofika hapo kutibiwa

Wakili wa Ally, Pasensa Kurubone, amesema Washtakiwa ni Hospitali hiyo na Daktari aliyehusika, ambapo Mahakama imetupilia mbali pingamizi la Hospitali lililotaka shauri lisikilizwe na Mabaraza ya Waganga

Upande wa Ally Mkii amesema “Tulimpeleka Aga Khan Tawi la Mbagala, Mwaka 2022, baada ya vipimo tukapelekwa Aga Khan ya Mjini, wakasema ana mvunjiko mdogo, akafungwa POP. Ikatakiwa turudi baada ya Wiki 3, hali ikawa mbaya tukarudi baada ya Wiki, ikabainika POP imebana na kushindwa kupitisha Damu”

JamiiForums imewasiliana na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Aga Khan, Olayce Lotha aliyesema “Suala lipo chini ya Mkurugenzi wa Tiba na Afya pamoja na Wanasheria wetu, nalielekeza kwao kwa taarifa na ufafanuzi zaidi.”

Soma https://jamii.app/MadaiYaFidia

#JamiiForums #Accountability
Kitu gani Mpenzi/Mwenza wako amewahi kukufundisha?

Mjadala https://jamii.app/MafunzoMpenzi

#JamiiForums #Maisha #LifeLessons #JFChitChats #JFStories