JamiiForums
56.4K subscribers
32.6K photos
1.81K videos
29.8K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa taarifa kuwa Viongozi wakuu wa Chama wamekutana na Uongozi wa Jeshi la Magereza na kufahamishwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu amehamishiwa katika Gereza la Ukonga

CHADEMA imesema Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, John Heche, anatarajiwa kufika Gereza la Ukonga, leo Aprili 19, 2025 kwa ajili ya kumwona #TunduLissu na kuzungumza naye kuhusu hali yake

Ikumbukwe Aprili 18, 2025 baada ya CHADEMA kudai hawajui Lissu alipo kutokana na kumkosa katika Gereza la Keko, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi, alizungumza na JamiiForums na kusema “Bado sijazipata hizo taarifa, ngoja nifuatilie.”

Soma https://jamii.app/LissuUkonga

#JamiiForums #Democracy #Siasa #JFMatukio #Kuelekea2025
Aprili 11, 2025, Maeneo ya Kaskazini mwa Nchi ya China yalikumbwa na dhoruba iliyosababisha upepo mkali wenye kasi ya Kilomita 150 kwa Saa, ambapo Miti takriban 300 ilianguka na Magari kuharibika

Kutokana na athari hizo Mamlaka zilitoa tahadhari kwa Watu wenye uzito wa chini ya Kilogramu 50 kutotoka nje kwa kuhofia kubebwa na upepo

Eeeheee Mdau, dhoruba ikitokea Kilo zako zitakubeba au tutakupoteza? 😂😂😂

Mjadala https://jamii.app/UpepoChina

#JamiiForums #ChinaStorm #ClimateChange
DAR: Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA - Bara, John Heche, amesema amekutana na Mwenyekiti wao Taifa, #TunduLissu katika Gereza la Ukonga anakoshikiliwa ambapo Kiongozi huyo amewataka Wanachana wao kuendeleza mapambano

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara Ukonga - Mombasa, Heche amesema "Nimetoka gerezani na nimeonana na Lissu, kama mnavyojua alikamatwa na alifunguliwa kesi kubwa ya uhaini, ambayo hukumu yake ni kifo.”

Ameongeza "Wamemhamisha Lissu kutoka Keko kuja Ukonga bila kutaarifu wanafamilia yake, Nchi hii sio kikundi fulani kinachoamua kila kitu. Lissu amesema mapambano yaendelee na mimi nasema mapambano yaendelee."

Soma https://jamii.app/LissuUpdaatesApril19

#JamiiForums #Democracy #Siasa #JFMatukio #Kuelekea2025
JamiiAfrica is seeking for a Monitoring, Evaluation and Learning (MEL) Specialist that will play a key role in strengthening our results-based programming through rigorous monitoring, insightful evaluation, and learning systems that inform adaptive management and strategic decision-making.

Qualifications & Experience:
- Bachelor’s Degree in Monitoring & Evaluation, Social Sciences, Development Studies, Public Policy or a related field. A Master’s degree is an added advantage.
- At least 5 years of progressive experience in MEL roles within NGOs, donor- funded projects, or civil society organizations.
- Proven expertise in both quantitative and qualitative MEL methodologies, tools, and software (e.g., Excel, Power BI, KoboToolbox, SPSS, etc.).

Send your CV, a Cover Letter and three References to vacancies@jamii.africa with the subject line: MEL Specialist– JamiiAfrica

For more info visit https://jamii.app/MELSpecialist

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFOpportunities #JamiiOpportunities
Jumapili hii ya Pasaka ikupe msukumo na tumaini jipya, furaha na mafanikio katika yote unayoyafanya

Heri ya Sikukuu ya Pasaka

#HappyEaster #JamiiForums
Ukaguzi wa kiufundi wa ukarabati na ujenzi wa Soko la Kariakoo, Soko Kuu la Mwanza, na Kituo cha Mabasi cha Nyamhongolo umebaini mapungufu katika upangaji wa Miradi, Usanifu, na Usimamizi wa Mikataba, hali iliyosababisha ongezeko la gharama na ucheleweshaji wa Utekelezaji wa Miradi

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 inaeleza kutokuwepo kwa tathmini ya kina ya hali ya majengo katika Masoko ya Kariakoo na Mwanza kulisababisha kutofafanuliwa kwa wigo wa Miradi, hali iliyosababisha mabadiliko yenye thamani ya Tsh. Milioni 757.02

Malipo ya Tsh. Bilioni 9.87 kwa upauaji wa nondo bila kubainisha vipimo vya nondo hizo. Pia, Tsh. Milioni 766.90 zililipwa kwa Washauri kama gharama za kurejesheka bila nyaraka za uthibitisho, jambo linaloashiria udhaifu katika udhibiti wa Fedha

Soma https://jamii.app/CAGMiradiMaendeleo

#RipotiYaCAG25 #RipotiCAG2025 #Uwajibikaji #CAGMiradiMaendeleo #Accountability #JamiiForums #Transparency
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DEMOKRASIA: Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa wito kwa Serikali ya #Tanzania kuwaachilia bila masharti Viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki, likisisitiza hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani ya taifa, hasa kuelekea mwaka wa uchaguzi.

Rais wa #TEC na Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa ameyasema hayo katika mkesha wa Pasaka uliofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Kagwa, Jimbo Katoliki Lindi

Soma https://jamii.app/WadaiHakiWaachiwe

#JamiiForums #Demokrasia #KuelekeaUchagua2025
ZANZIBAR: Goli pekee la Jean Charles Ahoua katika dakika ya 45+2 kwenye Uwanja wa Amaan, limeiwezesha #Simba kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya #Stellenbosch, katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika

Licha ya ushindi, Wachezaji wa Simba wamekosa nafasi kadhaa za wazi katika mtanange huo, hivyo mchezo wa marudio unatarajiwa kupigwa Aprili 27, 2025 kwenye Dimba la Moses Mabhida, Durban, Afrika Kusini

Mshindi baina ya pande hizo anatarajiwa kukutana na mshindi wa mechi kati ya RS Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria

Soma https://jamii.app/SimbaStellenbosch

#JamiiForums #JFSports #CAFCC
Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
Taarifa huru huwezesha #Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ufisadi, kuhamasisha ushiriki wa raia, na kuchochea ubunifu. Bila taarifa huru, maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi hulemazwa.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SHINYANGA: Mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria, Baba Askofu Dkt. Yohana Nzelu akizungumza na Waumini wa Kanisa hilo katika Ibada iliyofanyika Usharika wa Agape Kahama

Soma https://jamii.app/AskofuNzelu

#JamiiForums #Accountability #Governance
VATICAN: Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amefariki Dunia akiwa na umri wa Miaka 88

Vatican imetangaza kifo cha Papa Francis, leo Aprili 21, 2025 kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii

Alikuwa Papa wa kwanza kuzaliwa au kukulia nje ya Ulaya katika kipindi cha karne 12, wa kwanza kutoka Amerika, na wa kwanza kutoka shirika la Kijesuiti kushika wadhifa huo.

Soma https://jamii.app/PopeFrancisDies

#JamiiForums #JFMatukio #RIPPopeFrancis
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria, Askofu Dkt. Yohana Nzelu, akizungumza na Waumini katika Ibada iliyofanyika Usharika wa Agape Kahama, amegusia umuhimu wa Serikali kuwaondolea Wananchi hofu ya kuzungumza, kwa kuwa hali hiyo ikiendelea itasababisha visasi

Soma https://jamii.app/AskofuNzelu

#JamiiForums #Accountability #Governance
Maudhui potofu yanaweza kupotosha Umma, Kudhalilisha Watu, au hata kuchochea machafuko ya kijamii. Ni muhimu Jamii ifahamu na iwe na uwezo wa kutambua Maudhui ya aina hii.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anasema licha ya uwepo wa Magugumaji maeneo mengi ya Kando ya Ziwa Victoria, mbona haoni jitihada za Mamlaka husika kuyaondoa wakati yamekuwa kero kwa Watu na Vyombo vya usafiri?

Soma https://jamii.app/Magugumaji

#JamiiForums #Accountability #JFMdau2025 #Uwajibikaji