Isaack Nsumba
6.42K subscribers
1.44K photos
15 videos
140 links
Expert & Competent Teacher In Love, Relationship and Marriage.
Download Telegram
Isaack Nsumba
Nimependekezwa Kuwania Tuzo Ya "RELATIONSHIP EXPERT-MARRIAGE COACH OF THE YEAR." Kama Unaguswa Na Kazi Zangu, Pengine Hii Ikawa Ndio Nafasi Yako Ya Kunipa Maua Yangu Niyanuse NINGALI BADO NIKO HAI. Unaweza Kunipigia Kura Kadri Uwezavyo, Ili Kuhakikisha TUZO…
Jinsi Ya Kumpigia Kura ISAACK NSUMBA

(Relationship Expert | Marriage Coach)

>>>https://evopolls.com/polls/afriglomentz

Bonyeza Hiyo Link.

Ikifunguka Shuka Chini Kabisa Utakuta Category Ya MARRIAGE/FAMILY COACH

Bonyeza Jina La Pili (Isaack Nsumba)

Kisha Bonyeza "VOTE" IKifunguka Bonyeza "CONTINUE"

Ikifunguka Utaandika Idadi Ya Kura Unazonipigia (Kura 1 Ni 500)

Kisha Utachagua Njia Ya Malipo Ya Hiyo Hela Ya Kura (Inaweza Kuwa Kwa Simu)

Kisha Utabonyeza "COMPLETE PAYMENT" Kisha Utabonyeza "CONTINUE"

Kisha Utaingiza Namba Ambayo Ina Hicho Kiasi Cha Malipo Ya Idadi Ya Kura Ulizonipigia Kwa Kuanza Na Namba Bila 0 (Mfano 654 722 733)

Kisha Utabonyeza "PROCEED" Baada Ya Hapo Utaingiza Namba Ya Siri.

Kisha Utakatwa Hicho Kiasi Na Baada Ya Hapo Utakuwa Umenipigia Kura Tayari.

Unaweza Nipigia Kura Nyingi kadri Uwezavyo...Na Nitashukuru Sana!
Jinsi Ya Kumtunza Na Kumlinda Mwanaume, Ili Aendelee Kubaki Kwako...

1. Yajue Mahitaji Na Matarajio Yake Na Uyatimize Ipasavyo

Watu Huingia Na Hukaa Katika Mahusiano Kwa Manufaa Yao Binafsi.

Kinachomleta Mwanaume Kwako Ni Matarajio Anayotegemea Kuyapata Akiwa Na Wewe.

Yajue Na Umtimizie, Hawezi Baki Sehemu Ambapo Hapati Alichotarajia... Ataondoka!

2. Kuwa Chachu Ya Mabadiliko Yake Kimaisha

Msaidie Kuwa Bora Zaidi Bila Kumshinikiza Kwa Njia Hasi.

Mpe Msukumo Wa Kufanikisha Malengo Yake Kwa Kumtia Moyo...

Kumsaidia Kupanga, Na Kusherehekea Hatua Anazofanikisha.

Kuwa Mfano Wa Nidhamu, Maadili Na Bidii Ya Kazi, Mabadiliko Mazuri Yanaambukiza.

Hakuna Namna Mwanaume Anaweza Kumtupa Mwanamke Ambaye Ni Chachu Ya Yeye Kufanikiwa.

Kuwa Aina Hiyo Ya Mwanamke Sasa.

3. Mtengenezee Hofu Ya Kukupoteza

Hii Haimaanishi Kumtisha Au Kumfanya Ajisikie Vibaya,

Bali Kuendeleza Mvuto Wako Na Thamani Yako.

Kuwa Na Maisha Yenye Kusisimua, Kujijali, Na Kulinda Heshima Yako Binafsi.

Mwanaume Anayejua Kuwa Unajithamini Na Una Mchango Mkubwa Hutaka Kulinda Uhusiano.

Mfanye Ajue Alibahatika Kuwa Na Wewe Na Kama Asipokulinda Atakupoteza.

Na Endapo Akikupoteza Hatobahatika Kukupata Tena.

4. Mlinde Kwa Namna Ya Rohoni (Muhimu Sana!)

Ombea Afya Yake, Kazi Yake, Na Uhusiano Wenu.

Mpe Maneno Ya Faraja Na Nguvu Katika Nyakati Za Changamoto.

Kuwa Mtu Wa Siri Zake Na Msaada Wa Kiroho, Kiakili Na Kihisia.

Biblia Imesema "Mwanamke Atamlinnda Mwanaume" (Yeremia 31:22).

Manake, Ukifanya Hayo Mengine Pasipo Hili La Kiroho Unaweza Kumpoteza.

So Binuka, Jibebishe, Katika, Msaidie Lakini Usisahau Kumlinda Pia Kwa Jinsi Ya Rohoni.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
1
Jinsi Ya Kumtengenezea Mwanaume HOFU YA KUKUPOTEZA...

Thamani yako Kwake Inategemeana na Kiasi Cha Hofu Aliyonayo.

Asipokuwa na Hofu Atakutreat Vyovyote Atakavyoona Inafaa.

Ndio Maana, Nimekusudia Kukusaidia Uweze Kumtengenezea Hiyo Hofu.

1. Muoneshe Wanaume Wanaokutaka Wanamzidi Yeye

Hii Haitakiwi Kwa Kiburi Wala Dhihaka,

Bali Kwa Namna Yenye Busara.

Mwanaume Akiona Wanaume Wengine Wanathamini Thamani Yako,

Anaanza Kujua Ana Kitu Cha Thamani Mkubwa Ambacho Anatakiwa Kulinda.

2. Muoneshe Thamani Yako Katika Maisha Yake

Uwe Mchango Mkubwa Katika Furaha, Utulivu, Na Maendeleo Yake.

Mwanaume Asiyeona Thamani Yako Atadhani Hata Ukiondoka Maisha Yake Yataendelea Kama Kawaida.

Mfanye Atambue Wewe Ni Sehemu Muhimu Ya Ufanisi Wake.

Mfanye Ajue na Aone Anakuhitaji Uendelee Kuwepo Kwa Sababu Ya Thamani Yako.

3. Mfanye Ajue Kama Akikupoteza Hatokupata Tena

Kuwa Mwanamke Wa Kipekee Kwa Matendo, Nidhamu, Na Mvuto.

Mfanye Atambue Yeye Kubaki Na Wewe Ni Bahati Ambayo Si Kila Mwanaume Anaipata.

Na Akikupoteza, Hatapata Tena Mtu Kama Wewe.

Kama Akijua Ukiondoka Utarudi, Akikupoteza Anaweza Kukupata Tena Hatokuthamini.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
1
Aina Ya Mwanamke ASIYEFAA KUWA MKE NA MAMA...

1. Asiyeweza Kuvumilia Nyakati Ngumu.

Ushirikiano Wa Ndoa Na Malezi Ya Familia Una Changamoto Nyingi.

Mwanamke Asiye Tayari Kusimama Imara Kwenye Misukosuko Ya Maisha Ataathiri Ustawi Wa Familia.

Ni Muhimu Sana Mwanamke Awe Na Uwezo Wa Kusurvive Katika Nyakati Ngumu.

Nguvu Yake Inaweza Kukusaidia Wewe Pia Kama Mumeo.

Asiwe Mwanamke Ambaye Unapopitia Katika Kipindi Kigumu Badala Ya Kuwa Mfariji Anakuwa Tatizo Jingine.

2. Mwenye Matumizi Mabaya Ya Fedha.

Familia Inahitaji Nidhamu Ya Kifedha.

Mwanamke Anayependa Anasa Kupita Kipato Au Asiyepanga Matumizi Anaweza Kuiweka Familia Kwenye Matatizo Ya Kifedha.

Mwanamke Ni Msaidizi Kwa Mwanaume.

Anatakiwa Akusaidie Kudhibiti Matumizi Holela Ya Mwanaume.

Akiwa Na Matumizi Mabaya Ni Ngumu Sana Nyie Kutoboa.

3. Asiyetaka Kujifunza Na Kubadilika.

Maisha Hubadilika Na Changamoto Mpya Hujitokeza.

Mwanamke Asiye Tayari Kujifunza, Kusikiliza Ushauri, Au Kubadilisha Tabia Hafai.

Hakikisha Mkeo Anakuwa Ni Yule Mwanamke Aliye Tayari Kujifunza.

Aliye Tayari Kubadilika, Aliye Tayari Kukosolewa Na Kuboresha... Kama Hana Hii Sifa HAFAI HUYO.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
3
Mambo 3 Yanayosukuma UTOAJI WA MWANAUME....

Haiwezekani Wanaume Woote Wakajitoa Sawa Kila Mtu Katika Mahusiano Yake.

Kila Utoaji Wa Mwanaume Anaoufanya Unakuwa Umesukumwa Na Mambo 3:

1. UWEZO Wake Wa Kujitoa

Uwezo Wa Kifedha Wa Mwanaume Ndio Unaoamua Ajitoe Kwa Kiasi Gani.

Hivyo Si Vizuri Kumfosi Ajitoe Zaidi Ya Uwezo Alionao.

Kubaliana Na Ule Uwezo Wake, Pokea Kujitoa Kwake Na Muoneshe Kuwa Unathamini.

2. MVUTO Wa Mwanamke

Mwanaume Anaweza Kujitoa Kwa Aisha 20,000 Ila Kwa Mwajuma Akatoa 100,000

Kwa Sababu Ya Tofauti Ya Mvuto Wao.

Kadri Mwanamke Anavyokuwa Na Mvuto,

Ndivyo Inavyomsukuma Mwanaume Kujitoa Zaidi.

Kwa Maneno Mengine, Katika Mazingira Haya Mwanaume...

Anajitoa Kulingana Na Jinsi Alivyomthaminisha Mwanamke Huyo.

Lakini Pia, Katika Mazingira Haya Mwanaume Anajitoa Kwa Hofu,

Akiamini Kuna Wanaume Wengine Wanaoweza Kujitoa Kwa Mwanamke Huyo Kwa Kiwango Kikubwa.

3. UPENDO Wa Mwanaume Kwa Mwanamke

Kuna Wakati Ambapo Mwanaume Anajitoa Kwa Kusukumwa Na Upendo.

Kwahiyo, Kule Kujitoa Kwake Kunawakilisha Kiasi Cha Upendo Alionao Kwa Huyo Mwanamke.

Ndio Maana, Mwanaume Anaweza Asiwe Na Uwezo Mkubwa,

Lakini Akajibidiisha Kujitoa Kwa Kiasi Kikubwa Kwa Sababu Ya Ule Upendo Alionao.

Kwa Namna Nyingine, Ni Sahihi Kusema:

Akipenda Kidogo Atajitoa Kidogo (Hata Kama Ana Uwezo Mkubwa),

Na Akipenda Sana Atajitoa Sana (Hata Kama Ana Uwezo Mdogo).

Na Hili Sio Geni, Hata Mungu Alifanya...

Anasema..."Kwa Maana JINSI HII Mungu Aliupenda Ulimwengu... Hata Akamtoa Mwanae Wa Pekee." Yohana 3:16

Anatuonesha Kwamba, Aliupenda Ulimwengu Kwa Kiasi Kikubwa Hadi Akaona Amtoe Tu Mwanae.

Kwahiyo Kilichousukuma Moyo Wa Mungu Kujitoa Si Kingine,

Bali Ni Ule Upendo Aliokuwa Nao Kwa Ulimwengu.

Hiyo Ndio Saikolojia Iliyojificha Nyuma Ya Kujitoa Kwa Mwanaume.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
3
Maeneo 4 Muhimu Kuyajadili Kwa Uwazi Kama Wanandoa...

1. Fedha

Jadilini Mapato, Matumizi, Mipango Ya Uwekezaji, Na Vipaumbele Vya Kifedha.

Uwazii Katika Fedha Unaondoa Migongano Ya Baadaye.

Jadilini Tabia Za Kila Mmoja Wenu Linapokuja Suala la Kifedha.

Jadilini Malengo Ya Kifedha, Vipaumbele na Mahali Pa Kuelekeza Nguvu Zenu.

2. Sex

Zungumzieni Matarajio, Mara Za Kushiriki,

Na Njia Za Kuhakikisha Kila Mmoja Anaridhika.

Kutozungumza Kuhusu Tamaa Na Matamanio Kunaweza Kuleta Umbali Kihisia.

Kila Mmoja Anatakiwa Kusema, Nini Huwa Kinamfurahia na Nini Huwa Hakimfurahishi.

Kila Mmoja Anatakiwa Kusema, Nini Anatamani Kufanyiwa.

Nini anadhani Akifanyiwa Atalifurahia Tendo.

Uwazi Katika Hili Eneo Unasaidia Kujua Mahali Pa Kuboresha.

3. Kusaidia Ndugu Na Wazazi

Muwe Wazi Kuhusu Mipaka,

Kiasi Cha Msaada, Na Njia Za Kusaidia Bila Kuharibu Bajeti Yenu.

Msisahau, Moja Ya Sababu Ya Kwanini Baadhi Ya Ndoa na Familia ni Maskini Ni KWA SABABU YA MISAADA.

Hivyo Ni Muhimu Kuwa Na Hekima, Utaratibu na Muongozo Katika Kusaidia.

Ili Msijikute Kwamba, Mnasaidia Huku Ninyi Mkikaukiwa.

4. Tabia Za Kila Mmoja

Jadilini Tabia Zinazowakwaza,

Zinazowafariji, Na Njia Za Kuboreshana.

Tabia Zikiwekwa Wazi Mapema, Husaidia Kuepuka Migongano Mikubwa.

Kumbuka, Kulingana na Law Of Evaluation, Inayotaka Kujikagua na Kufanya Tathmini Kila Baada Ya Muda Fulani.

Ni Vigumu Kufanya Tathmini Itakayosaidia Kuboresha Ikiwa Haya Maeneo 4 Hamuwezi Kuyajadili Kwa Uwazi.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
1
[VIDEO YOUTUBE]; Ngazi Kubwa 3 Za MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO

>>>https://youtu.be/l1P6BA9T2TM

Ukishatazama Video, USISAHAU KUSUBSCRIBE
Nafasi 3 Ulizonazo Kama Mwanamke Kwa Mwanaume Wako...

1. Nafasi Yako Kama Mama Kwake

Kumlinda, Kumfariji, Kumsaidia, Na Kumpa Utulivu Wa Nyumbani.

Hii Ni Pamoja na Kujali Afya Yake.

Lakini Pia Kuhakikisha Amekula na Ameshiba Chakula Akipendacho.

Hii Pia Ni Nafasi Yako Ya Kuhakikisha Muda Woote Ni Msafi.

Muda Wa Kupumzika Pamoja na Kumkumbusha Mambo Muhimu.

Mwanaume Kama Mtoto Anahitaji Kulelewa.

NB; Unafanya Kwa Hekima, Sio Kwa Kumshurutisha.

2. Nafasi Yako Kama Mke Na Mpenzi

Kumvutia, Kumthamini, Kumjenga Kihisia Na Kimapenzi.

Kuhakikisha Anaridhika, Anafurahia Penzi.

Unapokuwa Katika Nafasi Hii Unakuwa Mfano Wa Kahaba.

Yaani Unajiweka Katika Nafasi Ya Kumhudumia Mwanaume Katika Namna Itskayomridhisha.

Hapa Usilete Umama, Usilete Udada, Usiwe Church Lady N.k

3. Nafasi Yako Kama Mtoto Wake Wa Kike

Kumfanya Ajisikie Wajibu Wa Kukutunza, Kukulinda, Na Kukuangalia Kwa Upendo.

Kumpa Nafasi Ya Kukulea, Kukuelekeza na Kukufundisha.

Katika Nafasi Hii Usisahau Kumuonesha Kuwa Unatambua Mamlaka Aliyonayo Kwako.

Usisahau Kumuonesha Kuwa Upo Chini Ya Uangalizi Wake

Muhimu; Hekima Sio Kuzijua Hizo Nafasi, Hekima Ni Kujua Jinsi Ya Kuswitch.

Yaani Kujua Uwe Nani Katika Wakati Upi.

Usiwe Mama Wakati Unapotakiwa Kuwa Mpenzi.

Usiwe Mtoto Wakati Unapotakiwa Kuwa Mama.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
Namna Sahihi Ya Kuishi Na Mwanaume Mwenye Ukuu...

Ipo Tofauti Kati Ya Kuishi na Mwanaume Wa Kawaida (Ordinary Man) na Mwanaume Mkuu (Extra-Ordinary)

1. Mheshimu

Toa Heshima Katika Maneno Yako, Matendo Yako, Na Mienendo Yako.

Mpe Heshima 2, Ya Kwanza Ni Kama Mwanaume Wako.

Na Heshima Ya Pili Ni Kulingana na Ukuu Alionao.

2. Muunge Mkono

Simama Naye Katika Maamuzi Yake, Changamoto Zake, Na Mafanikio Yake.

Katikati Ya Changamoto Onesha Kusimama Nae.

Onesha Kuwa Hata Ulimwengu Uende Kinyume Nae, Wewe Upo Pamoja Nae.

3. Msikilize

Heshimu Maoni Yake Na Uoneshe Utayari Wa Kusikia Na Kuelewa.

Na Usiishie Tu Kusikiliza, Bali Nenda Mbali Kiasi Cha Kufanya Sawasawa na Maelekezo.

4. Mthamini

Onyesha Shukrani Kwa Juhudi Zake Na Thamani Yake Katika Maisha Yako.

5. Kuwa Smart Kichwani

Mara Nyingi, Aina Hii Ya Wanaume Huwa Wana Mawazo Mapana.

Ndoto Kubwa na Mambo Yanayohitaji Kuchakatwa Kwa Kutumia Akili Kubwa.

So Ni Muhimu Uwe Vizuri Kichwani,

Ili Akilileta Jambo Lake Kwako Liwe Limeisha.

6. Jitahidi Kuendana Nae.

Hili Nitalizungumza Kwa Namna 2.

Ya Kwanza Ni Kuendana Kimatendo Na Mitazamo.

Lakini Pia Kuendana Nae Kwa Jinsi Ya Nje.

Umebeba Heshima Yake, Hivyo Uwapo Nae Public Hakikisha Hauharibu.

Namna Ya Pili Ni Kukua Pamoja Nae, Yaani Usikubali Kuwepo na Gape.

Ukiruhusu Gape Watu Wataanza Kuona Kama Hamuendani.

Taratibu Nayeye Ataona Ni Kweli Hamuendani na Mnaweza Kuachana.

Kwa Jinsi Hii Wanawake Wengi Hupoteza Wanaume, Wakati Wao Wanakuwa Wenyewe Wamebweteka.

7. Muheshimishe.

Usikubali Kuwa Sababu Ya Mumeo Kuaibika, Aibu Za Wanaume Wakuu Huwa Zinavuma Sana!

Hivyo Mlindie na Kumtunzia Heshima, Linda Udhaifu Wake na Kutunza Siri Zake.

Maneno na Matendo Yako Uwapo Huko Nje Yasiwe Sababu Ya Aibu Kwake.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
1
Ufanye Nini Mwanamke Akikukataa...

1. Practice Abundance

Tambua Ulimwengu Una Wengi.

Usimwangalie Mwanamke Mmoja Kama Ndiyo Mwisho Wa Dunia.

Tambua Kuwa Kuna Wanawake Wengi Wenye Haiba, Upendo Na Heshima.

Jifunze Kuthamini Uwepo Wako Na Kuwa Wazi Kwa Fursa Mpya.

2. Reframe Rejection – Badili Mtazamo Wa Kukataliwa

Badala Ya Kuona Kukataliwa Kama Kushindwa, Kichukulie Kama Somo.

Pengine Hakuwa Sahihi Kwako, Au Muda Haukuwa Mzuri.

Kukataliwa Ni Sehemu Ya Maisha – Sio Kipimo Cha Thamani Yako.

3. Change Perception – Badilisha Jinsi Unavyojiona.

Usiruhusu Tukio Moja Likuvunje Kisaikolojia.

Jiamini, Jifunze, Na Boresha Tabia Zako Bila Kujilaumu Kupita Kiasi.

Kujiamini Na Kujithamini Huongeza Mvuto Wako Kwa Wengine.

4. Don’t Take It Personal – Usichukulie Kwa Uchungu Wa Moyoni

Kukataliwa Hakumaanishi Wewe Si Mzuri Au Haustahili Upendo.

Mara Nyingine Mtu Anakataa Kwa Sababu Zake Binafsi Zisizo Na Uhusiano Na Wewe.

Heshimu Uamuzi Wake Na Endelea Na Maisha Yako Kwa Amani.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
1
Usikimbilie Pombe Unapokuwa Katika Stress Au Maumivu...

Unapokuwa Na Maumivu, Huzuni Au Msongo Wa Mawazo,

Si Sahihi Kabisa Kuyakimbia Kwa Kutumia Pombe.

Pombe Haimalizi Tatizo – Inakupumbaza Kwa Muda Mfupi Tu.

Inaweza Kukufanya Ujisikie Mwepesi Kwa Muda,

Lakini Hiyo Ni Hisia Ya Muda Mfupi Isiyo Na Suluhisho La Kudumu.

Tatizo Linabaki Palepale, Linakusubiri Pombe Zikikata....Baada Ya "HANGOVERS" Kuisha.

Kwa Hiyo, Usiweke Imani Kwa Pombe Kama Mfariji Wa Maumivu.

Badala Yake, Tafuta Suluhisho La Kudumu:

Omba, Ongea Na Mtu, Pumzika, Andika Hisia Zako Au Tafuta Msaada Wa Kitaalamu Unapohitaji.

Kumbuka: Kutatua Tatizo Kwa Akili Iliyo Huru Ndiyo Ushindi Wa Kweli.

Usikubali Kuwa Mfungwa Wa Starehe Ya Muda Inayochelewesha Uponyaji Wako.

Chagua Njia Za Afya – Kwa Mwili, Akili Na Roho Yako.

Nakuhakikishia, Pombe Haijawahi Kuwa Suluhisho La Stress Na Maumivu.

Ninawajua Watu Wengi Ambao, Walipokutana Na Maumivu Au Stress Walitumia Pombe.

Lakini, Nasikitika Kusema Kwamba Hali Ilizidi Kuwa Mbaya Zaidi Siku Za Mbeleni.

Ndio Maana Sitaki Na Kwako Itokee Hivyo.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
2
Mbinu 2 Zitakazokusaidia Kumsahau Ex Wako na Kukabiliana na Upweke Baada Ya Penzi Kuvunjika

Kati Ya Changamoto Inayowakumba Wengi Ni Kuendelea Kutembea Na Kumbukumbu Za Wenzi Walioachana.

Kama Unakumbana Na Hii Changamoto Kuna Njia 2 Unaweza Kuzitumia.

1. Rebound Relationship Technique

Hii Ni Mbinu Ya Kuingia Kwenye Uhusiano Mpya Haraka Baada Ya Kuachana,

Ili Kuziba Pengo La Kihisia.

Mbinu Hii Inakusaidia Kujisahaulisha Maumivu Ya Zamani Kwa Ku-Focus Kwenye Mtu Mpya.

Kama Utatumia Mbinu Hii Kuwa Makini Usije Ingia Katika Penzi Ambalo Litakutesa Baadae.

2. Filler Dating Technique

Hii Mbinu Lengo Lake Ni Kukufanya Usijihisi Mpweke...

Wengi Wakiachana Huwa Wanakaa Kama Wanaomboleza.

Huwa Wanapoteza Hamu Ya Kuchangamana Na Wengine...Kwa Sababu Wanaugulia Maumivu.

Katika Mbinu Hii Unatoka Na Watu Mbalimbali Bila Kujihusisha Kwa Kina,

Ili Kuondoa Upweke Na Kurudisha Kujiamini.

Hii Ni Mbinu Ya Mpito Inayoweza Kukuandaa Kwa Mahusiano Bora Ya Baadaye.

Muhimu Kukumbuka Kuwa, Hauwezi Kumsahau Ex Wako...

Ila Unaweza Mkumbuka Pasipo Kufanya Chochote.

Au Kuwa Na Kumbukumbu Juu Yake Zisizo Na Madhara Kwako.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
3
Namna Sahihi Ya Kuishi Na MWENZI MWENYE HASIRA KUPITA KIASI...

1. Kuwa Mtulivu Wakati Wa Mlupuko Wake.

Usijibu Hasira Kwa Hasira. Tulia, Sikiliza Na Usubiri Hali Ipoe Kabla Ya Kujibu.

Wakati Mwingine Hasira Huchochewa Zaidi Na Majibizano.

Ili Kuepuka Hilo Usiingie Katika Kujibizana.

2. Tafuta Chanzo Cha Hasira Zake.

Mara Nyingine Hasira Hutokana Na Shida Zilizofichwa Kama Msongo, Hofu Au Uchovu.

Kujua Chanzo Kunasaidia Kuishughulikia.

Mtu Mmoja Alisema Tatizo Ukilielewa Vizuri Umelitatua Kwa Asilimia 50%

(Problem Well Defined Is A Problem Half Solved)

Kujua Chanzo Cha Hasira Zake Ni Hatua Nzuri Ya Kulishughulikia Hilo Tatizo.

3. Weka Mipaka Yenye Afya

Weka Masharti Ya Mawasiliano Yenye Heshima.

Kama Imefikia Katika Hatua Ya Maneno Ya Kejeli, Kipigo Au Matusi CHUKUA HATUA ZAIDI.

4. Tumia Mawasiliano Yenye Upole

Ongea Kwa Lugha Tulivu, Tumia “Ninahisi” Badala Ya “Wewe Umekuwa” Ili Kupunguza Migongano.

Usipende Kuushambulia Utu Wake Wala Udhaifu Wake.

Hii Inaweza Ikasaidia Kutokulipuka.

5. Msaidie Kutafuta Msaada.

Kama Hasira Imekithiri Na Kuathiri Mahusiano,

Mshauri Huku Ukimsaidia Kutafuta Msaada.

Kuna Msaada Wa Aina 2, Aina Ya Kwanza Ni Msaada Wa Kisaikolojia.

Kama Chanzo Cha Hasira Zake Ni Cha Kisaikolojia Basi Utakuwa Msaada Sahihi.

Aina Ya Pili Ni Msaada Wa Kiroho, Huu Utamfaa Endapo Chanzo Chs Hasira Zake Ni Kifungo Fulani Cha Kiroho Kinachomshikilia.

Mimi Pia Nimewahi Kuwa Na Tatizo La Mlipuko Wa Hasira, Nafanya Maamuzi Afu Baadae Najutia Sana!

Hivi Sasa Hilo Tatizo Sina, Nina Zile Hasira Kama Walizonazo Binadamu Wengine, Ambazo Sio Tatizo.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
[VIDEO YOUTUBE]; Sababu 4 Za Mwenzi Wako KUBADILIKA KITABIA

>>>https://youtu.be/31jA8U2saVk

Ukishatazama Video, USISAHAU KUSUBSCRIBE
Sababu Za Kuachwa / Kuachika Mara Kwa Mara...

1. Madhaifu Yanayojirudiarudia

Wakati Mwingine, Madhaifu Yaliyomlimbiza Mtu A Yanaweza Kumkimbiza Mtu B.

Hii Itatokea Endapo, Utaingia Katika Mahusiano Mapya Bila Kuyashughulikia.

Ni Muhimu Sana Kujifanyia Tathmini Binafsi (Self Evaluation)

Ili Kujiuliza Nini Sababu Zilizopo Nyuma Ya Kuachwa Kwako.

Ukizijua Zishughulikie Ili Isitokee Kwamba Ukaachwa Tena.

2. Rough Date

Rough Dating Ni Kuingia Katika Mahusiano Shaghalabagala.

Kuna Watu Ambao Leo Penzi Lake Limevunjika,

Kesho Yuko Katika Penzi Jipya (Hakuna Kupoa).

Na Kwa Sababu Hajapata Muda Wa Kufanya Assesment Ili Kujua Kwanini Penzi La Mwanzo Lilivunjika.

Unakuta Na Katika Penzi Jipya Anafanya Kosa Lilelile Na Anaachwa Tena.

Wakati Mwingine Mahusiano Yako Yanaweza Yakawa Yanavunjika Mara Kwa Mara Kwa Sababu...

Hauna Utaratibu Mzuri Wa Kuingia Katika Mahusiano.

3. Unmet Expectations

Kinachomfanya Mtu Aje Kwenye Maisha Yako Ni Matarajio Anayotegemea Kuyapata Kutoka Kwako.

Hayo Ndiyo Yanamleta Na Ndiyo Yatamfanya Aondoke Akiyakosa.

Ikiwa Wa Kwanza Ulishindwa Kumpatia Kile Alichoatarajia Akakuacha.

Wapili Nae Akija Akashindwa Kupata Alichoatarajia Automatically Atakuacha Nayeye.

Usije Ukapuuza Matarajio Ya Mwenzi Wako Kutoka Kwako.

Ikitokea Umeshindwa Kuyafikia Matarajio Yake Unatengeneza Nafasi Kubwa Ya Mtu Huyo Kuondoka Katika Maisha Yako.

Kwanini Aendelee Kubaki Kwako Ikiwa Hapati Kile Alichoatarajia Kukipata?

Yapo Matarajio Ambayo Hata Yasipofikiwa Hayana Madhara.

Na Yapo Ambayo Yasipofikiwa Yana Nguvu Kiasi Cha Kufanya Ukaachika.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
Onyo: Usipuuze Dalili Hizi Katika Mahusiano Mapya...

1. Ubinafsi (Selfishness)

Kama Mwenza Anaonesha Kujali Zaidi Maslahi Yake Kuliko Yako,

Ni Ishara Ya Ukosefu Wa Usawa Katika Mahusiano.

Mwenzi Wa Jinsi Hii Mara Zoote Atakuwa Anajizingatia na Kujibeba Yeye Zaidi.

2. Udhibiti Kupita Kiasi (Over Controlling)

Anapojaribu Kudhibiti Maamuzi Yako, Marafiki Zako, Na Muda Wako Bila Heshima Kwa Uhuru Wako, Chukua Hatua Mapema.

Ni Kweli, Mwenzi Wako Kuna Mamlaka Fulani Atakuwa Nayo.

Lakini Isizidi Kiasi Cha Kugeuka na Kuwa Kero.

3. Kutegemea Kupita Kiasi (Over Dependency)

Kama Ana Kuletea Mzigo Mkubwa Wa Kihisia Au Kifedha Mapema Sana,

Ni Dalili Ya Kutojiamini Au Kutokua Tayari Kimaisha.

Ni Kweli Tunategemeana, Lakini Utegemezi Uliokithiri Unaweza Kukufanya Uhisi Kuelemewa.

Lakini Pia, Mtu Anaekutegemea Kupita Kiasi Hawezi Kuwa Msaada Kwako.

4. Kuficha Mambo Kupita Kiasi (Over Secret)

Kuficha Sana Maisha Yake, Mambo Muhimu,

Au Historia Yake Bila Sababu Za Msingi Kunaweza Kuashiria Tatizo La Uaminifu.

Ni Kweli, Hatutakiwi Kuwa Wawazi Kupita Kiasi, Lakini Pia Hatutakiwi Kuwa Wasiri Kupita Kiasi.

Mwenzi Ambae Anakuficha Vitu Vingi, Hasa Vile Muhimu Ambavyo Kimsingi Hakupaswa Kukuficha Hiyo Sio Ishara Nzuri.

5. Kukwepa Majukumu (Avoiding Responsibilities)

Mtu Anapokataa Kuitikia Wajibu Wake Wa Kihisia, Kifedha, Au Kijamii Mapema Katika Uhusiano, Ni Dalili Ya Kukosa Uaminifu Na Utayari.

Kwa Harakaharaka Ni Dalili za Mtu Asiyefaa Kabisa.

Kwa Sababu Haiwezekani Mtu Aje Katika Maisha Yako Afu Mtengeneze Maisha Mazuri Ikiwa Hayupo Tayari Kuwajibika.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa
Ufanye Nini Endapo Utagundua Kuwa Upo Katika Penzi La Kushea...

1. Kubali Ukweli (Accept The Truth)

Usijidanganye Au Kujaribu Kupuuza Dalili.

Wala Usijifariji...Ukishajua Upo Katika Penzi La Kushea, Kwanza Kubali Ukweli Huo.

Kubali Kwamba HAPA SIPO PEKEANGU.

2. Tathmini Thamani Yako (Evaluate Your Worth)

Kumbuka Wewe Ni Wa Thamani.

Usiruhusu Kupunguzwa Heshima Yako Kwa Kukubali Kugawana Mapenzi Bila Ridhaa Yako.

Tafakari Na Kisha Jiulize, Unastahili Kushea Mapenzi na Mtu?

Jibu Utakalopata Litakusaidia Kufanya Maamuzi.

3. Weka Mipaka (Set Boundaries)

Amua Kama Unataka Kuendelea Au Kuondoka, Lakini Hakikisha Mipaka Yako Iko Wazi.

Katika Level Hii Unasema Kila Unachotaka Kiwe.

4. Zungumza Kwa Uwazi (Communicate Clearly)

Kama Kuna Nafasi Ya Mazungumzo,

Basi Zungumza Na Mwenza Wako Kuhusu Hali Ilivyo Na Matarajio Yako.

Katika Mazungumzo Yenu Tafuta Kujua Sababu za Kushea.

Kisha Muulize Yeye Anafikiria Nini.

5. Fanya Maamuzi Yenye Afya (Make Healthy Decisions)

Chagua Kitu Kitakachokulinda Kiakili, Kihisia Na Kimaisha. Kuondoka Sio Kushindwa, Ni Kujilinda.

NB; Mimi Sijasema Uondoke, Nimekutajia Options Kadhaa, Wewe Utachagua Unayoona Ni Bora Kwako.

By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya:

1. Comment Kitu Ulichojifunza

2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi

3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye

4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi

Isaack Nsumba

#Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa