Swahili News
3.78K subscribers
108K photos
58.6K videos
28 files
266K links
🐾
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Azam Sports

VIWANJANI| “Prisons ilikuwa nafasi ya 15” maneno ya Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally akikumbuka wakati alipojiunga na Tanzania Prisons na watu aliowaomba ushauri kabla ya kukubali ‘ofa’

Amtaja Etiene Ndayiragije na Oscar Milambo.

Ni mahojiano maalumu yaliyofanywa na @kalugira_timzoo kupitia kipindi cha
(Imeandikwa na @allymufti_tz )
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

millardayo

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Jeshi la Polisi limemkamata Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania bara, John Heche katika eneo la Kariakoo alikokuwa akiongea na Wananchi leo April 22,2025.

CHADEMA wamesema baada ya Polisi kumkamata Heche walimpeleka kituo cha Polisi Msimbazi na kisha baadae kumtoa Kituoni hapo “Baadhi ya Viongozi wamefika kituo cha Polisi kati na kujibiwa kuwa hajafikishwa kituoni hapo”

Hatua hii inakuja baada ya CHADEMA kuijibu barua ya Polisi kuwa Heche atafanya mkutano wake Kariakoo kama ulivyopangwa licha ya zuio la Polisi kwa kile ambacho CHADEMA wamesema Polisi imechelewa kutoa taarifa ya zuio wakati tayari maandalizi yote yalikwisha fanyika.
#MillardAyoUPDATES
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

millardayo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amemjibu Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo kuhusu hoja aliyoiibua Bungeni kuhusu ubadhilifu wa fedha kwenye Jengo la Utawala la Jiji la Arusha.

Katika sehemu ya majibu ya hoja za Wabunge kutoka kwa Waziri Mchengerwa amejibu kuwa “TAMISEMI ni Wananchi na ni Serikali hasa niwathibitishie Watanzania hakuna senti ya Watanzania iliyopotea katika miradi yote hii miwili ni muhimu tutofautishe hoja za kujenga na lugha za kuchomea tuhuma zisizo na mzizi sio hoja ni cheche za siasa ambazo haziwezi kuwekwa kwenye taasisi zenye misingi ya sheria na miradi ya maendeleo haijengwi kwa maneno bali kwa mchakato” Mohamed Mchengerwa

Katika mchago wa Gambo wa April 16,2024 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2025/26 aliibua hoja ya ujenzi wa Jengo la gholofa 8 kujengwa kwa shilingi bilioni 9 jambo ambalo alimuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Miko..
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

millardayo

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo leo April 22, 2025.

Dorothy amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi wa Chama cha ACT Wazalendo, Shaweji Mketo katika Ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo zilizopo Dar es salaam.

Akiongea baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Dorothy Semu amesema “Nimechukua fomu hii kama ishara ya utayari wangu wa kumkabili Rais Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwasababu wameshindwa kuendesha nchi na kuwakomboa Watanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii”

“Nimechukua fomu kama ishara ya utayari wangu wa kuongoza mapambano ya kulinda thamani ya kura na misingi ya demokrasia nchini”

Dorothy Semu amesema atatoa dira na maono yake yaliyomsukuma kuchukua fomu kupitia hotuba kwa Taifa atayoitoa siku ya kurudisha fomu atayoitangaza hivi karibuni.
#MillardAyoUPDATES
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

millardayo

Mbunge wa Viti Maalum Esther Matiko ameomba muongozo wa Spika kwa kanuni ya 76 ya kanuni za kudumu za bunge akiomba bunge kusisimama kwa muda ili kujadili haki za abiria wa treni ya mwendokasi SGR anapopata dharura ya kuahirisha safari au kuchelewa na kubadilishiwa muda wa kusafiri ili tiketi yake isipotee.

Muongozo huo wa Matiko unatokana na swali la mbunge wa Viti Maalum Anatropia Theonest aliyetaka kujua zipi haki za Abiria wa Vyombo vya Moto nchini na kwa kiwango gani wanatambua haki zao.

“SGR ujio wake umesaidia sana na umekuwa mbadala wa abiria wa ndege na mabasi lakini haki inakuwa inapokwa ‘in a way’ kwa watumiaji wa SGR kwa mfano ikikata tiketi ukapata dharura au ukafika umechelewa, tiketi yako inakuwa imeharibika sasa nilikuwa naomba kuwepo na utaratibu wa kubadilisha iwapo mtanzania aliyekata tiketi aweze kubadilishiwa tiketi yake Kwenda kwenye muda mwingine ambao anataka kusafiri au akifika amechelewa aweze kupigwa penati abadilishiwe apewe tarehe nyingine aweze...
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

SportsArenaTz

Nikisema uhakika, naamaanisha uhakika!

Familia Huu ndio Mkeka wa mwisho wa ARENA FIXED kutumwa bure 🙏🏾
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

SportsArenaTz

Kikombe hiki Wasafi hawakukiepuka ☕️😅

BOOM SHAKALAKA 🚀 🚀🚀
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

SportsArenaTz

Kikombe kikatua Meridian ☕️

BOOM SHAKALAKA
🎊🎊🎊🎊🎊🎊🎊🎊🎊🎊
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

SportsArenaTz

☕️ Kikombe hiki Galsport hawakiepuki

BOOM SHAKALAKA
🎊🎊🎊🎊🎊🎊🎊🎊🎊🎊
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

Sakata la Mwijaku na Wanafunzi wa vyuo! BABALEVO afunguka mapya, atoa siri zote za ndani, makubwa!
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

BUNGE LAPITISHA KWA KISHINDO BAJETI YA TAMISEMI TRILIONI 11.78 KWA MWAKA 2025/2026
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ampokea katibu mkuu wa baraza la Ulaya Alain Berset katika ukumbi wa rais.
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Rais wa Uturuki Erdogan alipokutana na Katibu Mkuu wa Baraza la Ulaya Berset:

- Uturuki inatilia maanani mazungumzo chanya na ushirikiano na Baraza la Ulaya, huku pia ikiendelea na ushirikiano wake na Baraza hilo na mifumo mingine ya kimataifa ya haki za binadamu.
- Ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya Uislamu na chuki ya wageni kote Ulaya, na kusisitiza kwamba Baraza la Ulaya linapaswa kutilia maanani zaidi katika kushughulikia masuala haya.
- Mauaji ya Israeli huko Gaza yanaendelea; Ulaya inapaswa kupaza sauti yenye nguvu katika kushikilia sheria za kimataifa na haki za binadamu katika kukabiliana na uhasama wa Israeli
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akutana na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif katika Ikulu ya Rais jijini Ankara
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Rais wa Ghana John Dramani Mahama amemsimamisha kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo Gertrude Torkornoo
Taarifa kutoka ofisi ya rais zinasema atakaa pembeni hadi pale matokeo ya uchunguzi dhidi yake yatakapobainika. Kumewasilishwa malalamiko matatu dhidi ya Jaji Torkornoo
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Makamu Mwenyekiti wa chama cha upinzani Tanzania CHADEMA, John Heche amekamatwa na polisi.
Taarifa zinasema Heche alikamatwa wakati akiwa kwenye mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Kwa nini Papa huvaa pete?

Kila Papa, kiongozi wa kanisa Katoliki huvaa pete.

Inajulikana kama "Pete ya Mvuvi" Iliyopewa jina la Mtakatifu Petro, ambaye alikuwa mvuvi na kwa mujibu wa imani ya Kikatoliki, papa wa kwanza.