Swahili News
3.78K subscribers
108K photos
58.6K videos
28 files
266K links
🐾
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

“Walanguzi kutoka ughaibuni wamekuja na njia mpya ya kuiba mali asili yetu au Bio-Piracy”

-
Shirika la kuwahudumia wanyama pori la Kenya (KWS) limetibua njama ya walanguzi walioingia nchini humo kama watalii kumbe nia yao ilikuwa kuiba na kusafirisha wadudu takriban elfu 5 wenye thamani ya dola $7000
katika masoko huko Asia na bara Ulaya.

-
Raia hao wawili kutoka Ubelgiji na mmoja kutoka Vietnam wanasubiri hukumu katika kesi ya kwanza kama hiyo.

-
Je Afrika ifanye nini kulinda mali asili vivutio na bio anuai yake?
Tuandikie hapo chini 👇🏿
-
-
-
🇰🇪
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

Papa Francis, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 88, alifanya safari kadhaa barani Afrika katika kipindi chote cha uongozi wake.
-
Katika safari zake barani Afrika, Papa alitaka kueneza ujumbe wa amani na upatanisho katika nchi zilizokumbwa na migogoro.
-
Akiwa barani Afrika, Papa Francis pia aliwatawaza makadinali kadhaa, wakiwemo wale wa kwanza kabisa wa mataifa madogo ya Afrika.
-
Je safari zake zilileta matokeo yapi kwa Afrika? Pangusa kushoto kufahamu zaidi
-
-
-
️️➟ @HabariTz ✰✰✰
️️➟ @HabariTz ✰✰✰
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

millardayo

Rubia ni oili maalumu kwaajili ya magari yanayotumia dizeli, iliyoidhinishwa na zaidi ya watengenezaji wakuu 200 wa magari makubwa. Rubia imejaribiwa na kuidhinishwa na watengenezaji wakuu wa Vifaa Halisi (OEMs).

Sifa za oili ya Rubia:
- Rubia ni ulinzi dhabiti dhidi
ya uchakavu wa injini.
- Huboresha ufanisi wa injini.
- Hurefusha uhai wa injini na
kupunguza gharama za
matengenezo.
- Huboresha usafi wa injini na
kuimarisha ulinzi wa injini.
- Hupunguza matumizi ya
mafuta.

Jipatie oili za Rubia zinazopatikana katika vituo vya mafuta vya @totalenergies_tz TotalEnergies na mawakala walioidhinishwa.
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

millardayo

Brazil imetangaza siku saba za maombolezo kufuatuia kifo cha Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Brazil, nyumbani kwa idadi kubwa kabisa ya Waumini wa Kanisa Katoliki duniani kote, itaomboleza kifo cha Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Baba Mtakatifu Francis kwa siku saba.

Akitoa tangazo hilo Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva amesema ulimwengu umepoteza sauti ya heshima na hisani, Waumini walishiriki Ibada kote Brazil kumuombea Papa Francis aliyefariki dunia mapema Jumatatu katika makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican akiwa na umri wa miaka 88.

Kwa mujibu wa ripoti ya Vatican ya mwezi March, Brazil nchi ya wakazi milioni 182, ndiyo yenye idadi kubwa ya Wakatoliki duniani kote.

Takwimu zinaonesha kiasi watu bilioni 1.4 ni sehemu ya Kanisa Katoliki duniani.
#MillardAyoUPDATES
(✍️ DW Kiswahili)
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

millardayo

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha wa Tanzanja Alphonce Simbu, kwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Mbio ya Boston (Boston Marathon) akimwambia amefanya kazi nzuri.

Rais Samia amesema “Ushindi wako ni matokeo ya kujituma kwa bidii, maandalizi mazuri, nidhamu yako kuanzia jeshini, kwenye mazoezi hadi kwenye mashindano, ukilibeba kwa heshima ya hali ya juu jina la nchi yetul

“Endelea kuipeperusha vyema bendera ya Taifa letu”
#MillardAyoUPDATES
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

millardayo

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema leo April 22,2025 Jijini Dar es salaam kwa niaba ya Wafuasi wenzake wa kundi la G 55 ndani ya Chama cha CHADEMA, amesema kitendo cha Chama hicho kutosaini kanuni za maadili ya uchaguzi kimekatisha ndoto za Watu wengi waliojiandaa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Mrema amesema “Tuliposhauri Chama (CHADEMA) kikasaini (kanuni za maadili) tulikuwa tunafahamu madhara ya kutosaini, kwasababu kundi la G55 linaundwa na Watu ambao wamewahi kugombea ubunge nchini na wengine wamewahi kuwa Wabunge kwa miaka 15 wapo G 55, wametunga sheria na wanafahamu kanuni”

“Kwahiyo sio kundi la Watu ambao wanasema bila kuwa na ufahamu na uelewa, jana nimemsikia Msaidizi mmoja wa Kiongozi wa Kitaifa Bwana Odero ameanzisha nae mchango anasema anataka kwenda Mahakamani kupinga kanuni, Mwanasheria Mkuu wa Chama alipoulizwa mtaenda Mahakamani hakujibu hilo swali, kwasababu anajua kwenda Mahakamani ni baada ya uchaguzi,..
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

SportsArenaTz

✈️🇿🇦 || Kikosi cha wachezaji 23 wa SIMBA SC kitaondoka kesho asubuhi kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaopigwa Jumapili ijayo.
.
Kikosi kitaondoka na Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ambapo itapitia Johannesburg kabla ya kuunganisha kuelekea Durban ambapo ndipo kutakapopigwa mchezo huo.
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Kulingana na Vatican, mazishi ya Papa Francis yatafanyika Aprili 26, kuanzia saa nne asubuhi.
Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa makadinali uliofanyika mapema Jumanne.
\
Mapema mwezi Februari, Papa Francis alilazwa kwenye hospitali ya Gemelli, akisumbuliwa na maradhi ya Nimonia.

Aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya siku 38, akiendelea na matibabu kwenye makazi yake ya Vatican kabla ya kufariki dunia jumatatu ya Aprili 21, akiwa na miaka 88.
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Sikiliza muhtasari wetu wa habari ya siku ya Jumanne, 22 Aprili.

🎧 Sikiliza hapa:
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Rais wa Kenya WIlliam Ruto ameanza ziara yake ya kiserikali ya siku nne nchini China ambapo atajadiliana masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na mwenyeji wake Xi Jinping.
- Viongozi hao wawili wanatazaamiwa kusaini makubaliano ya kibiashara kuleta mageuzi ya kiuchumi, maendeleo endelevu na ushirikiano wa kimataifa.
- Rais Ruto pia anatarajiwa kuongoza Kongamano la Biashara kati ya Kenya na China, ambalo litaleta pamoja zaidi ya makampuni 100 kutoka nchi mbili hizo kwa lengo la kutafuta fursa mpya za kibiashara na uwekezaji.
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
️️➟ @HabariTz ✰✰✰

TRT Afrika Swahili

Wakristo duniani wamekusanyika katika maeneo mbalimbali kuomboleza kifo cha Papa Francis.

Waombolezaji wamekusanyika huku wakimkumbuka kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kwa upendo wake kwa maskini na ujumbe wa amani.
Azam Sports

Nusu Fainali Coppa Italia Jumatano hii.

Inter Milan watakuwa San Siro wakiwakaribisha AC Milan

Katika nusu fainali ya kwanza AC Milan akiwa mwenyeji walitoka sare ya 1 - 1.

Mchezo huu utachezwa kuanzia saa 4:00 usiku na kuruka mbashara kupitia

Je, ni Inter Milan au AC Milan nani kwenda fainali?
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Azam Sports

: Wachambuzi @hinjojr na @hamisa_24 waujadili msimamo wa NBC Premier League na kuzigusa baadhi ya timu ambazo zipo katika hatari ya kushuka daraja.

(Imeandikwa na @allymufti_tz)
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Azam Sports

VIWANJANI: Tujikumbushe tambo za Mtenje Albano wa Fountain Gate siku moja kabla ya mechi yao dhidi ya Yanga SC pale Tanzanite Kwaraa.