Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu - Luisa Piccarreta
43 subscribers
298 photos
54 files
630 links
Fahamu kuhusu kutimia kwa Sala ya Baba Yetu kupitia Maandishi ya Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta, Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - Kuishi Utashi wa Mungu
Download Telegram
<<NOVENA KWA IMMAKULATA>>
Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA - BMUM**
**Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

🌟🌟🌟

Siku ya Tatu

Baada tu ya kutungwa katika mimba, Maria alikuwa akitekeleza zoezi la uabudu wake wa kwanza. Katika kutungwa kwake katika mimba Nafsi zote tatu za Mungu zilikutana na kukubaliana. Mungu Baba alimmwagia bahari ya Hekima, Mwana alimmwagia bahari ya Utakatifu, na Roho Mtakatifu alimmwagia bahari ya Pendo. Bahari hizo tatu zilipokutana, ndipo akatokea Maria, kiumbe kamili na timilifu kabisa kati ya wanadamu wote. Mara tu alipotungwa katika mimba, pale pale alifanya uabudu wake wa kwanza.

Nasi, pamoa na Mama Mtamu, tuanze kufanya ziara yetu ndani ya Utashi wa Mungu. Twende tukatwae uabudu mbalimbali wa kila kiumbe chenye roho na kisicho na roho, halafu tuchukue na turuke kwa ndege ya kila wazo, kwa ndege ya kila mtazamo wa jicho, ndege ya kila neno, ndani ya ndege ya kila mwonzi wa jua, turuke katika kila mmemetuko wa nyota mbali mbali, na katika kila sauti ya mbubujiko wa maji. Tunapowasili kwa Baba, sisi tukamtolee tendo la uabudu lililo endelevu na timilifu.

Sala ya Mshale:

Ee Mama yangu, kwa lile tendo lako la uabudu wa kwanza, uliotekeleza mbele ya Mungu, fanyiza kuwa, tokea sasa hivi na kuendelea, akili yangu, moyo wangu, vionjo vyangu vya upenzi, matamanio yangu na nafsi yangu nzima, vyote hivyo viwe daima ni tendo endelevu la uabudu.
<<NOVENA KWA IMMAKULATA>>
Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA - BMUM**
**Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

🌟🌟🌟

Siku ya Nne

Bikira, baada ya tendo la uabudu, alijiona ametajirika sana kwa zawadi zote na vipaji vilivyotolewa na Nafsi za Utatu Mtakatifu, ambao sasa walikuwa katika pilikapilika za kuendelea kumjazia neema mbalimbali za ziada. Huku akiwa amepigwa butwaa na hajielewi, Bikira alianguka kifudifudi mbele ya ule Utukufu wa Juu kabisa, akajitolea nafsi yake nzima, kama tendo lake la sadaka.

Alijitoa bila kusaza kitu chochote kwa ajili yake mwenyewe: wala siyo wazo, wala siyo utazamaji na wala siyo kauli yake, wala siyo upenzi wake, na wala siyo pigo lolote la moyo wake. Kishapo aliitazama dunia, akauona ule uharibifu wa roho nyingi mno za watu, ndipo akajitolea nafsi yake yote kwa ajili ya wokovu wa roho hizo.

Na sisi, ili kumtolea heshima, kuanzia mapema asubuhi ya leo, tunafanya ziara ya kuzunguka kupitia matendo ya Utashi wa Mungu huku tukiyatolea mawazo yetu, utazamaji wetu, kauli za maneno yetu nk, tunatolea yote katika roho ya sadaka.

Sala ya Mshale:

Ee Mama yangu, ninakuja miguuni pako na ninajitupa mikononi mwako. Naomba unimwagie moyoni mwangu pendo lako lote kwa kiasi cha kunijazia upendo wa kuweza kutoa sadaka ya akili yangu, sadaka ya moyo wangu na hata sadaka ya utashi wangu na sadaka ya nafsi yangu yote.
<<NOVENA KWA IMMAKULATA>>
Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA - BMUM**
**Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

🌟🌟🌟

Siku ya Tano

Baada ya lile tendo la kujitoa sadaka, Bikira aligeuka kuitazama dunia tena. Kwanza akaiona ile idadi ya watu waliokwisha kuhukumiwa kupotea, pili akayaona yale makosa yote yaliyotendeka na wanadamu tangu makosa ya yule mtu wa kwanza Adamu hadi ya huyu mwanadamu wa mwishoni, na tatu akawa anaona mbele yake vile vizazi vyote vya binadamu, yaani kizazi kilichopita, cha sasa na kile kijacho. Ndipo Bikira alitekeleza tendo lake la kwanza la kulipa fidia. Tendo lililokuwa timilifu kabisa! Ni timilifu kwa vile ni tendo lililojumuisha mambo yote, yaani kila wazo, kila utazamaji wa jicho, kila kauli ya neno, kila hatua na kila upenzi wa wanadamu wote.

Basi, na sisi tukiwa pamoja na Mama, tukikwea daima kwenda kwa Baba katika Utashi wa Mungu, tutakuwa tukitekeleza matendo yetu ya kulipa fidia kwa niaba ya wanadamu wote, yaani, fidia kwa ajili ya macho, kwa ajili ya kila neno nk.

Sala ya Mshale:

Ee Mama yangu, twaa huu moyo wangu mikononi mwako, nakuomba uubane kwako kwa nguvu zaidi na zaidi, kwa jinsi ya kuweza kujaza ndani yangu roho ya kweli ya kulipa malipizi.
<<NOVENA KWA IMMAKULATA>>
Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA - BMUM**
**Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

🌟🌟🌟

Siku ya Sita

Alipoyaona madhambi mengi wanayotenda wanadamu, Bikira alionja Moyo Wake ukimbana mno kwa maumivu. Tangu pale alianza ile sala yake endelevu, bila kukatisha katisha, sala kwa niaba ya watu wote.

Nasi sasa tuunganike naye Mama, kutekeleza kwa pamoja kile alichokuwa akifanya yeye. Kwa njia hiyo tuunganishe upya Mbingu na dunia zilizokuwa zimetenganishwa kwa dhambi.

Sala ya Mshale:

Ee Mama yangu, tafadhali unibanie kwenye Moyo wako wa kimama, ili kwa mapigo yako ya moyo, uujaze moyo wangu kwa ile roho ya sala ya kweli kwa ajili ya kumwomba Mungu, ili Utashi Wake ufike kutawala katika mioyo yote.
<<NOVENA KWA IMMAKULATA>>
Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA - BMUM**
**Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

🌟🌟🌟

Siku ya Saba

Bikira, yeye huyu aliyemkubwa kabisa kati ya Watakatifu, tangu nukta ile ya kwanza alipotungwa katika mimba, kamwe hakuacha chochote kitoroke toka Utashi wa Mungu. Hakuacha wala wazo, wala utazamaji wa jicho, wala kauli ya neno, na wala pumzi yake, hakuachilia vikatoroka. Yeye alikuwa akitenda kila kitu katika Utashi wa Mungu.

Leo hii, na sisi, tuunganishe wazo letu lolote, na lile wazo la kimungu. Tuunganishe utazamaji wetu, neno letu, matendo yetu, kwa matendo yale yale yaliyo ni ya Mungu. Kwa njia hiyo, sisi nasi tutaweza kutengeneza mwonzi mwingine wa jua utakaokuwa uking’aa na kuangaza pale juu ya Kichwa cha Malkia wetu.

Sala ya Mshale:

Ee Mama yangu, mimi najiunganisha nawe. Uifanye nafsi yangu nzima iwe inaishi daima ndani ya Utashi wa Mungu.
<<NOVENA KWA IMMAKULATA>>
Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA - BMUM**
**Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

🌟🌟🌟

Siku ya Nane

Ili kuweza kujaza tena ile ombwe ambayo, mbele ya Utukufu wa Mungu, imesababisha utovu wa shukrani kutoka kwa mwanadamu, na kwa tendo la Mungu kutuletea Mama aliye Mkuu na wa ajabu namna hii, na pia kwa tendo la kumkinga na dhambi ya asili, sisi tutatekeleza leo matendo tisa ya shukrani katika Utashi wa Mungu wa Juu, tutatoa shukrani kwa niaba ya wanadamu wote, tangu Adamu hadi yule wa mwishoni atakayekuwepo hapa duniani. Halafu, tutafanya matendo mengine tisa ya shukrani kwa Bikira mwenyewe kwa tendo la kutupokea sisi kama watoto wake, hata kama tu watovu wa shukrani, na hata kama huwa hatutambui na kuukiri upendeleo huo aliotupatia.

Sala ya Mshale:

Ee Mama yangu, wewe uliye ndiye uazo nma utimilifu wa Neema, naomba uimwagie neema hiyo moyoni mwangu ili niweze kumshukuru Mungu kwa kukukinga wewe na dhambi ya asili.
<<NOVENA KWA IMMAKULATA>>
Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA - BMUM**
**Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

🌟🌟🌟

Siku ya Tisa

Tutoe heshima yetu kwa yale machozi ya kwanza ya Mama yetu aliyoyamwaga mbele ya Umungu. Ilikuwa ni tangu wakati ule ambapo Mungu alipokuwa akiangalia ule udogo wa yule aliyekuwa analia, yaani, yule aliye mdogo na papo hapo ni mkubwa, yule aliye mdogo lakini papo hapo ni mwenye nguvu, mdogo lakini anayeng’aa na kuangaza, yeye ambaye ni tegemeo la mambo yote yahusuyo wokovu! Mungu aliguswa mno, ukalainishwa moyo wake, mwishowe akashawishika mara kuamua kumleta Mwana wake ashuke duniani.

Na sisi leo, tutafanya ziara yetu ndani ya Utashi wa Mungu ili kutembelea kazi zake, tutazunguka mara tisa, kukusanya machozi yote ya wanadamu yanayotapakaa na yatakayotapakaa juu ya ardhi leo na hadi siku ya mwisho wa dunia. Tutayachukua machozi hayo yote, na kuyafikisha, na kuyaingiza katika tumbo la Mama, ili yeye akayafikishe mbele ya Utukufu wa Mungu, na hatimaye ayageuze hayo yote kuwa machozi ya uongofu na upendo.

Sala ya Mshale:

Ee Mama yangu, machozi yako na yateremke ndani ya moyo wangu ili moyo wangu ufanywe kuwa laini zaidi. Kama umekuwa na maovu, sasa uongoke kuwa moyo mwema, kama umekuwa tayari ni mwema, basi sasa moyo wangu utakatifuzwe. Tena, machozi yako yashuke na kuingia katika mioyo ya wanadamu ili wote wapate kuongoka.
<<NOVENA KWA IMMAKULATA>>
Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA - BMUM**
**Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu

🌟🌟🌟

Siku ya Sherehe

Leo, tutoe heshima mara tisa kwa Bikira Maria, tukiushukuru Utashi wa Mungu kwa kutupatia huyu kama Malkia wetu, kama Mama, na kama mwombezi wetu.

Kishapo tutasali Atukuzwe mara tisa, kulingana na Kwaya Tisa za Malaika. Tunawaomba Malaika waungane nasi kwa ajili ya kumtolea Maria ule Utukufu wote, unaozidi kusambaa na kukua, Utukufu ambao Utashi wa Mungu huwa unaubeba ndani yake.

Halafu tutawaingiza hao Malaika wote na Watakatifu wote ndani ya Utashi huo wa Mungu ili kwa pamoja tukatoe kwa Maria Utukufu ulio stahiki kwake na ambao amekuwa akinyimwa na wanadamu.

Sala ya Mshale:

Ee Mama yangu, uliye ni Malkia wa wote, njoo ushike utawala na ushike mamlaka yako juu ya wote, na ufanyize wote wakujue Wewe ni nani.
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU CHA MBINGU - Juzuu Na. 23 - Desemba 22, 1927🖋📃📖📔

“Ninapoteua mwanadamu fulani kwa ajili ya utume, ambao lazima ulete manufaa kwa familia ya binadamu ya ulimwengu mzima, huwa kwanza kabisa naweka na kuingiza mema yote ndani ya mtu huyo, ambaye lazima ajazwe ndani yake hayo mema yote, katika kiwango cha kufurika kabisa, kwani watu wengine watapasika kuja kuchukua mema hayo, ingawa kama pengine hawatafaulu kuchukua mema yote yaliyopo ndani ya mteule huyo.

Hicho ndicho kilichotokea katika Malkia Immakulata, ambaye aliteuliwa kuwa Mama wa Neno wa Milele, na hivyo akawa ni Mama wa watu wote waliokombolewa: Chochote ambacho walipasika kutenda, na chema chochote walichopasika kukipata, vilikuwa vyote vimefungiliwa na kupigiliwa, kama vile ndani ya tufe la jua, ndani ya Malkia Mtawala wa Mbingu.

Kwa jinsi hiyo wakombolewa wote wanatembea kuzunguka jua la Mama wa Mbingu, na kwa hiyo na yeye, zaidi ya kuwa Mama mpendevu kabisa, hatendi kitu kingine isipokuwa kumwaga mionzi yake juu ya wana wake.

Anawamwagia mionzi ili kuwalisha kwa mwanga wake, kuwalisha kwa utakatifu wake na kwa pendo lake la kimama.

Lakini ni mionzi mingi mingapi anayosambaza, ambayo haichukuliwi na wanadamu kwa vile katika ufidhuli wao, hawajitahidi kusogea na kusonga mbele kwenda kumzunguka huyu Mama wa Mbinguni?...”
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU CHA MBINGU - JUZUU Na. 30 – Aprili 30, 1932🖋📃📖📔

Jinsi gani kuishi ndani ya Utashi wa Mungu ni zawadi ya Pendo na Ukarimu wa Mungu

Ni budi uelewe kuwa kuishi ndani ya Utashi Wetu ni zawadi ambayo Ukarimu Wetu hupenda kutoa kwa wanadamu. Na kwa zawadi hiyo, mwanadamu atajiona kuwa amebadilika: Toka ufukara anapata utajiri, kutoka kwenye udhaifu anakuwa na nguvu, kutoka ujinga anapata uelewa. Kutoka kuwa mtumwa wa tamaa chafu chafu anageuka kuwa mfungwa mtamu na wa hiari kabisa wa Utashi ulio Mtakatifu sana, ambao hautamteka kama mfungwa tena, bali utamfanya awe mfalme anayejitawala mwenyewe. Atakuwa mfalme wa himaya za kimungu na wa vitu vyote vilivyoumbwa. [...] Lile paji la Utashi Wetu ambao hutolewa kama zawadi, litabadili ule mkasa wa kusikitisha wa vizazi vya wanadamu, isipokuwa kwa yule ambaye kwa hiari yake anataka abaki katika masikitiko yake. Zaidi, itakuwa hivyo, hasa kwa vile zawadi hiyo ilikuwa imekwishatolewa tayari kwa binadamu pale mwanzoni mwa kuumbwa kwake, lakini kwa utovu wa shukrani, yeye mwenyewe aligoma na kusukumia mbali kwa tendo lile la kutekeleza utashi wake wakati alipojitenga na Utashi Wetu.

Sasa, mtu yule anayekubali na kuwa tayari kutekeleza Utashi Wetu, anakuwa akiandaa nafasi, anasafi sha mazingira, na anapamba mahali penye hadhi stahiki pa kuja kuweka zawadi kubwa kama hiyo, zawadi isiyokuwa na kikomo. Wale watu wenye uelewa kuhusu FIAT watasaidia na wataandaa kwa namna ya ajabu sana jinsi ya kuipokea zawadi hiyo. Na kile ambacho hawajakipata bado hadi leo hii, watakipata kesho. [...] Kuishi ndani ya Utashi Wangu siyo mali ya mwanadamu fulani, na wala si kitu chini ya mamlaka na uwezo wake, bali ni zawadi tu ambayo mimi naiandaa na kuitoa pale ninapotaka, kwa yule ninayemtaka na katika nyakati ninazotaka. Hiyo ni zawadi ya Mbingu iliyoandaliwa kutoka kwenye Ukarimu Wetu Mkuu na kutoka Pendo Letu lisiloweza kuzimika.

Hatimaye, kwa njia ya zawadi hiyo, familia ya binadamu itajisikia kweli imeungana hivi na Muumba wake, kiasi kwamba haitaonja tena kuwa mbali Naye. Badala yake, itajionja kuwa karibu sana Naye na kana kwamba imekwishakuwa sasa ni Familia ileile ya Mungu na kwamba inaishi pamoja Naye katika Ikulu ileile ya Mfalme.
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA


Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

Na vittabu vingine. Angalia site ⬇️⬇️⬇️

www.divinewilldivinelove.com/Kiswahili-/-Swahili/
UTANGULIZI**

Luisa anaandika maneno haya:

Nilipokuwa na umri wa miaka yapata 17, nikiwa najiandaa kwa Sikuu ya Noeli Takatifu, nilifanya Novena ya Noeli Takatifu kwa kutekeleza matendo mbalimbali ya fadhila na ya kujinyima. Nilifanya Novena hiyo hasa kwa ajili ya kuheshimu na kuienzi ile miezi tisa ambayo Mpendwa Wangu Yesu aliishi ndani ya tumbo la Mama Yake. Kila siku nilifanya tafakari ya saa tisa juu ya Fumbo la Umwilisho.

SAA YA KWANZA:
PENDO-KUPINDUKIA LA KWANZA –
Pendo la Kiutatu

Kwa muda wa saa moja, nilijipeleka mwenyewe kwa mawazo, hadi ndani ya Paradisini, na kuanza kuwazia juu ya Utatu Mtakatifu Mtukufu: Mungu Baba akiwa anamtuma Mwanae aje duniani, Mwanae akiwa anatii Utashi wa Baba kwa hiari na utayari wote, na Roho Mtakatifu akiwa anakubali na kuunga mkono.

Akili yangu, ikawa inaduwaa na kustaajabu katika kulishangaa fumbo Kubwa la namna hii, kushangaa Pendo katika ushirikiano na ukubaliano wa jinsi hiyo, Pendo lililo sawa kwa namna ile, Pendo kali namna ile kati Yao, na lakini lote likiwa ni kwa ajili ya wanadamu. Papo hapo nikawa nawazia juu ya ufidhuli na utovu wa shukrani kutoka upande wa binadamu, na hasa utovu wa shukrani kutoka upande wangu mimi mwenyewe! Kuhusu wazo hili, ningeweza kuendelea kubaki nimezama nalo, siyo kwa saa ile moja tu, bali ningebaki nalo bado hata kwa kutwa nzima. Kumbe lakini, nikasikia sauti kutoka ndani yangu ikiniita kuniambia: “Yatosha hivyo kwa sasa. Njoo ili upate kuona zaidi ya hili Pendo Langu la kupindukia kiasi”.



**Sehemu ya kwanza ya Tafakari ya Novena kwa kila siku imechukuliwa kutoka Juzuu Na. 1 la Kitabu cha Mbingu.
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

SAA YA PILI:
PENDO-KUPINDUKIA LA PILI -
Pendo Lililojihinisha

Kishapo basi, akili yangu ilinichukua na kunipeleka hadi ndani ya tumbo la Mama na pale ikabaki imeduwaa kushangaa kabisa. Akili yangu ikawa inawazia tena jinsi Mungu Yule, aliye Mkuu vile kule mbinguni, anavyoweza kujihinisha Yeye Mwenyewe kwa namna hii: sasa amerudi kuwa kadogodogo mno, amefungwa na kubanwa mahali pafinyu namna hii, amebanwa hadi kushindwa kujimudu tena, na amebanwa hata karibu anashindwa kupumua. Toka ndani mwangu ikaja sauti inayoniambia: “Je unaona ni jinsi gani nimekupenda wewe? Chonde, nipatie kanafasi kakubwa kidogo zaidi katika moyo wako! Ondoa kila kitu kisichohusiana na Mimi, kusudi uweze kunipatia nafasi zaidi, yenye kunipa bahati ya kuweza kujimudu kidogo na hivyo niweze angalau kupumua!”

Moyo wangu ukavunjika sana. Nikawa ninamwomba Yesu radhi sana. Nikawa namwahidia kuwa natoa nafsi yangu yote iwe yake. Nikawa nalia nikitokwa na machozi. Lakini, hata hivyo, nakuambia, katika kuvurugika kwangu, nilikuwa narudia kutenda zile kasoro zangu mbalimbali! Ee Yesu, umekuwa daima mwema ilioje, kwa huyu masikini mwanadamu duni!
Vinapatikana na unaweza ku download:

KITABU cha MBINGU - JUZUU NA. 11

KITABU cha SALA MBALIMBALI completo

Na vittabu vingine. Angalia site ⬇️⬇️⬇️

www.divinewilldivinelove.com/Kiswahili-/-Swahili/
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

SAA YA TATU:
PENDO-KUPINDUKIA LA TATU –
Pendo Linalotafuna na Kuchakaza

Kutoka tafakari ya pili, nikaingia katika hatua ile ya tatu. Sauti toka ndani mwangu iliniambia:

“Ebu laza kichwa chako juu ya tumbo la Mama Yangu. Tazama mpaka ndani kabisa ya tumbo hilo na uangalie ule Ubinadamu Wangu mdogo: Pendo Langu lilikuwa linanimaliza kabisa; angalia mioto ile ya Pendo, na mabahari yale makubwa ya Pendo la Utashi Wangu yalivyokuwa yakinifurika, yakiniteketeza hadi kuwa majivu; yalizusha na kuongeza dhoruba zake hata zikaenea popote, na kuwafikia watu wa vizazi vyote, kuanzia mtu yule wa kwanza hadi mtu yule wa mwishoni kabisa mwa nyakati.

Nao Ubinadamu Wangu mdogo ulikuwa ukichomwa na kuteketezwa kati ya miale ile mingi mno.

Lakini je, unajua lile Pendo langu la milele linanidai Mimi nitafune na kumeza kitu gani? Lo, linataka nimeze ndani mwangu zile roho za watu. Kwa hiyo basi, nilikuwa nimefurahi pale nilipoweza kuzimeza roho zote na hivyo nikawa nimebaki nikiwa nimezibeka katika mimba yangu: Mimi nilikuwa ni Mungu na ilinipasa niwe ninatenda mambo kama Mungu. Ilinipasa nizibebe roho zote hizo ndani ya mimba yangu. Pendo langu lisingethubutu kuniacha hivi hivi katika amani kama ningediriki kuacha kuipokea roho yoyote ile hata moja tu. Ah, binti Yangu, angalia vema zaidi katika tumbo la Mama yangu, kaza sana macho yako juu ya ule Ubinadamu Wangu, uliokuwa mimbani mwa Mama na pale utagundua hata roho yako ikiwa mimbani pamoja nami; utagundua pia ile miali ya moto wa Pendo langu iliyokuwa inakumeza hata wewe. Lo, ni jinsi gani nimekuwa ninakupenda, na ni jinsi gani ninavyokupenda hata sasa!

Mimi nikawa nazidi kuvurugika na kutojitambua ndani ya Pendo kubwa lile; sikuelewa tena namna ya kutoka nje ya hali hiyo na kuachana nayo. Ndipo sauti ilisikika ikiniita kusema: “Binti Yangu, jambo hilo bado siyo kitu. Ebu sogea na ujibane zaidi kwangu. Nyosha mikono yako kwa Mama yangu mpendwa, ili naye akusogeze karibu zaidi na tumbo lake la kimama. Sasa, ebu angalia tena, na kuutazama Ubinadamu Wangu mdogo, ukiwa katika ile mimba, na halafu endelea kutazama Pendo-kupindukia langu la nne.”
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

SAA YA NNE:
PENDO-KUPINDUKIA LA NNE –
Pendo Tendaji

“Binti yangu, kutoka kuliangalia Pendo linalomeza, sasa njoo ukaone Pendo langu linalotenda mambo. Kila mtu ambaye nilimbeba katika mimba, naye alinibebesha Mimi mtumba wa madhambi yake, alinibebesha madhaifu yake, na hata matamaa yake. Pendo langu likaniamrisha kupokea huo mtumba wa kila mtu. Isitoshe, si kwamba nilibeba mimba ya roho za watu tu, bali nilibeba maumivu ya kila mtu, nilibeba pia malipizi na fidia zile, ambazo kila mmoja wao angepasika kuzitoa na kumpatia Baba Yangu wa mbinguni. Kwa minajili hiyo, Mimi nilipoingia katika Mimba ya Mama, Mateso yangu hayo yaliingia pia pamoja nami. Ebu unichunguze vizuri nikiwa pale tumboni mwa Mama yangu wa mbinguni. Ebu ona jinsi Ubinadamu Wangu mdogo ulivyokuwa umepigika na majeraha mengi! Ebu ona jinsi hako kakichwa kangu kadogo kalivyokuwa kamevalishwa taji la miiba, hata kwamba ninapobana mashavu yangu, macho yangu huwa yanatoa na kutiririsha mito ya machozi. Na wala siwezi kujimudu ili kufaulu kujipangusa machozi haya. Chonde, shituka kidogo ukanionee huruma Mimi: Ebu upanguse na kuyakausha haya macho yangu toka machozi hayo mengi mno, unipanguse wewe uliye na mikono yako bado huru kuweza kunitendea hilo! Hiyo miiba ni taji la mawazo mengi mengi machafu yanayojaa na kufurika ndani ya akili za kibinadamu. Lo, ni jinsi gani inavyonichoma na kunitoboa zaidi, hata kupita ile miiba inayozalishwa na ardhi! Ebu endelea kuangalia zaidi na uone ni masulubu marefu yalioje yatakayoendelea kunikumba kwa miezi tisa! Wakati wote huo nilikuwa siwezi kabisa kujimudu, sikuweza kutembeza kiungo chochote, iwe kidole, iwe mkono na wala mguu. Nilikuwa nimebaki hapa daima, bila ujimudu wowote, na wala hapakuwepo hata kanafasi kwa mimi kuweza kujitikisa, au kujimudu angalau hata kidogo kabisa. Usulubu mrefu na mkali ulioje! Pamoja na mateso hayo, ebu ongezea ukweli kwamba, matendo yote maovu ya wanadamu, yalikuwa yakinijia katika umbo na mtindo wa misumari iliyokuwa ikinitoboa mikononi na miguuni kwa kujirudia mara kwa mara.

Basi, ndivyo alivyokuwa anaendelea kunisimulia umivu moja baada ya lingine, mateso yote ya kishahidi ya Ubinadamu wake mdogo. Kama ningekuwa napenda kuelezea maumivu yote, hakika ingekuwa ni kirefu mno. Kutokana na masimulizi yake hayo, mimi nilianguka katika kulia machozi. Moyoni nikawa nasikia sauti ikiniambia: “Binti yangu, ningependa nikukumbatie, lakini kumbe siwezi kwani nafasi haipo kabisa; pili siwezi kabisa kujimudu, na tena kwa umri wangu huu mdogo, siwezi kufaulu kulitenda hilo bado. Ningependa kuja kwako, lakini kumbe siwezi kutembea bado. Kwa sasa, ebu wewe unikumbatie Mimi; uje wewe kwangu na baadaye, nitakapokuwa nimetoka nje ya tumbo la Mama, itakuwa ni Mimi nitayekuja kwako”.

Lakini, katika fantasi zangu, nikawa namkumbatia, nikawa nambania kwa nguvu kwenye moyo wangu. Ndipo ikasikika sauti toka ndani mwangu iliyokuwa inasema: “Yatosha kwa sasa binti yangu. Endelea kuwaza juu ya Pendo-Kupindukia langu la tano”.
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

SAA YA TANO:
PENDO-KUPINDUKIA LA TANO –
Pendo Katika Upweke

Baada ya hapo ile sauti ya kutoka ndani yangu iliendelea kusikika ikisema: “Binti yangu, chonde usijivute mbali na Mimi; chonde usiniache peke yangu; Pendo langu linahitaji kuwa na mwenzi. Hilo ndilo Teso lingine la kupindukia la Pendo langu, yaani kwamba, halitaki kabisa kubaki peke yake. Lakini, je unafahamu linahitaji kubaki likiwa na nani? Linahitaji kubaki likiwa na mwanadamu. Ona ya kwamba ndani ya tumbo la Mama yangu, pamoja na Mimi, wamo wanadamu wote wakiwa wamebebwa wote katika mimba pamoja nami. Mimi nipo pamoja nao kama Pendo lao daima. Natamani niwe nawatamkia daima, ni jinsi gani ninavyowapenda; ninatamani kuzungumza nao, ili niwaeleze furaha zangu na pia uchungu wangu. Nataka niwaeleze kwamba, nimekuja kuwa kati yao, ili niwafanye wawe na furaha, ili niwafariji, ili niwaeleze kwamba, nitakuwa nakaa kati yao kama ndugu yao mdogo ili niwe kumpa kila mmoja mema yangu yote, ili niwape Ufalme Wangu kwa gharama ya kifo changu. Natamani niwapatie mabusu yangu na mapapaso yangu. Nataka niwe ninajiburudisha kwa kucheza nao. Lakini ni mateso mangapi yaliyoje ambayo wananiletea! Yuko yule anayenitoroka, yule anayekuwa kiziwi hata asitake kusikia lolote, mwingine anadiriki kuninyamazisha nisizungumze, mwingine anadharau mema yangu, na hataki kujali kabisa Ufalme Wangu. Hao wote, badala ya mabusu yangu na mapapaso yangu ninayowapa, wao wananionyesha tabia ya kutonijali na tabia ya kunisahau Mimi. Burudani yangu ile ninayotaka, wao wa wanabadili kuwa kilio changu cha uchungu.

Oh, ona jinsi nilivyo kwa kweli; ni mpweke kabisa, hata kama kwa nje naonekana kuwa kati ya watu wengi sana. Na, oh, ni jinsi gani huu upweke wangu unavyonielemea! Sina mtu wa kumwelezea neno, sina mtu wa kuniliwaza kwa mazungumzo na wala kwa pendo. Ninabaki kuwa daima mwenye masikitiko na mkimya kwani ninapojaribu kuzungumza, hakuna anayenisikiliza. Ah, binti yangu, ninakuomba na ninakusihi usiniache peke yangu katika upweke huu! Chonde unikarimu kwa kuniwezesha kuzungumza, endapo wewe utakuwa hiari kunisikiliza. Basi, ebu unielekezee sikio lako katika mafundisho nitakayokupatia sasa: Mimi ni Jalimu kati ya Majalimu! Ni mambo mengi mangapi ninayotaka kukufundisha! Endapo utahiari kunisikiliza, basi utanisaidia nisitishe kulia na nitaanza kucheza na kuburudika na wewe. Je wewe hutaki kucheza na Mimi?

Pindi nilipokuwa najikabidhi kwake, na huku nikiwa namhurumia katika upweke wake, ile sauti ya kutoka ndani mwangu ilinijia na kuendelea kusema: “Basi, basi, inatosha. Sasa endelea kuwaza juu ya Pendo-Kupindukia langu la sita.”
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

SAA YA SITA:
PENDO-KUPINDUKIA LA SITA –
Pendo Linalokataliwa

““Binti yangu, njoo hapa, na umwombe Mama yangu mpendwa akupatie ngalau kanafasi kadogo ndani ya tumbo lake la kimama, kusudi wewe mwenyewe uweze kujionea hali halisi ya mateso na ya uchungu inayonikabili Mimi sasa”. Ndipo, katika mawazo yangu nikawa namwona Mama yetu Malkia. Kwa ajili ya kumridhisha na kumfurahisha Yesu, akawa ananiandalia nafasi ndogo na akawa ananiweka mimi pale ndani. Lakini kumbe ndani pale palikuwa na giza nene hivi hata sikuweza kumwona Yesu, ila nikawa nasikia tu pumzi zake. Na Yeye toka ndani mwangu alisikika akiniambia:

“Binti yangu, ebu angalia Pendo-Kupindukia lingine la kwangu. Mimi ni Mwanga wa Milele. Jua ni kivuli tu cha Mwanga wangu, lakini unaweza kuona sasa, ni umbali wa hadi wapi ambako Pendo langu limenifikisha. Je, sasa waweza kuona Mimi nipo katika mahabusu gani haya ya giza hili nene? Hapa ndani hakuna hata ufa wa kupitisha mwonzi moja wa mwanga. Kwangu hapa ni usiku totoro daima, halafu ni usiku bila nyota yoyote, ni usiku bila pumziko lolote, ni kukesha tu daima. Mateso gani haya! Ufinyu wa mahabusu haya, ufinyu usioniruhusu angalau kujimudu kidogo tu! Giza nene totoro la namna hii! Na hata suala la pumzi yangu, oh, ni jinsi gani ilivyoniwia vigumu kupumua! Pumzi yangu ilivyobanwa! Ninaweza kuvuta hewa na kupumua kupitia pumzi ya Mama yangu tu basi! Halafu, ongeza hapo, ile giza inayoletwa na makosa ya wanadamu; kila kosa lililotendeka limekuwa ni giza kwangu, na hivyo unapoyaunganisha na kuyajumlisha makosa hayo yote, kwa pamoja yanatengeneza bahari yenye kilindi cha giza linaloenea bila ufuko wowote. Mateso gani hayo! Oh, Pendo-Kupindukia langu: Umenifanya nihame toka kwenye bahari ya Mwanga Mkuu, na kutoka kwenye uwanja wangu na toka kwenye eneo langu lenye upana mkuu, halafu umenitumbukiza katika kilindi hiki cha giza nene na chenye ufinyu huu, kiasi kwamba nakosa kabisa uhuru wa kupumua! Na yote hayo ni kwa sababu tu ya kuwapenda wanadamu!”.

Na pindi akiwa anayasema maneno hayo, alikuwa akilalamika kwa sauti iliyokuwa inakatikakatika kooni mwake kwa hoja ya ufinyu wa nafasi. Halafu akawa analia machozi. Na mimi nikawa naingia pia katika kilio cha machozi. Huku nikiwa ninamshukuru na ninamhurumia, nikawa natamani kumletea mwanga kidogo kwa njia ya pendo langu, kama alivyokuwa amewahi kuniambia. Lakini halafu, je ni nani anayeweza kuelezea mambo yote? Sauti ile ile ya kutoka ndani mwangu iliongezea kusema:

“Basi, yatosha kwa sasa. Endelea mbele kwenye Pendo-Kupindukia langu la saba.”