Utashi wa Mungu na Upendo wa Mungu - Luisa Piccarreta
42 subscribers
311 photos
56 files
688 links
Fahamu kuhusu kutimia kwa Sala ya Baba Yetu kupitia Maandishi ya Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta, Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - Kuishi Utashi wa Mungu
Download Telegram
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

SAA YA SABA:
PENDO-KUPINDUKIA LA SABA –
Pendo Linaloomboleza

Ile sauti ya kutoka ndani mwangu iliendelea kusema:

“Binti yangu, usiniache peke yangu katika upweke mkubwa huu na katika giza nene hili. Usitoke kwenda nje ya tumbo la Mama yangu. Ubaki ili uangalie lile Pendo-Kupindukia langu la saba. Ebu unisikilize.

Katika Kifua cha Baba Yangu, Mimi nilikuwa nina furaha daima. Hapakuwepo na jema ambalo Mimi nililikosa. Furaha, raha na kila kitu, vilipatikana kwa ajili yangu. Malaika wenye heshima walikuwa wakiniabudu na wakinitii mara nilipowaashiria. Ah, lakini kumbe Pendo-Kupindukia langu, naweza nikasema, likaja kubadili ile bahati yangu! Pendo-Kupindukia hili limenifunga na kunithibiti katika gereza hili la giza. Limenivulia mbali furaha zangu zote, raha zangu, na mema yote niliyokuwa nayo. Badala yake limenivika vazi la masikitiko yote ya wanadamu. Yote hayo yamefanyika ili kuweza kufanya mabadilishano; ili Mimi niweze kuwapatia wanadamu ile bahati yangu, furaha zangu, na heri yangu ya milele! Lakini, hilo lote lingekuja kuwa si kitu kabisa, endapo nisingekuta ndani yao ule ufedhuli wao mkuu na utovu wa shukrani na ule ujeuri wao wenye kiburi kabisa. Oh, ni jinsi gani Pendo langu la Milele lilivyoshituka na kushangaa mbele ya ufidhuli na ule utovu mkubwa wa shukrani! Ni jinsi gani Pendo hilo lilivyolia mbele ya usugu na uhuni huo wa mwanadamu! Ufidhuli huo ulikuwa ndio mwiba mkali sana ulionichoma zaidi kupita yote, na ndio uliotoboa kabisa Moyo Wangu tangu siku ile nilipoingia katika mimba hadi siku ile ya mwisho ya kufa kwangu. Ebu ukaangalie haka kamoyo kangu kadogodogo; Kamejeruhiwa na kanavuja na kububujika Damu. Ni Teso gani hili! Umivu gani kali nililolionja! Binti yangu, chonde usiwe na utovu wa shukrani kwangu, usiwe mfidhuli kwangu. Utovu wa shukrani na ufidhuli ndilo umivu kali kupita yote kwa Yesu Wako. Ni sawa na kunifungia milango yote mbele yangu, ili kuniacha nikibaki nje, niendelee kutetemeka na kuganda kwa baridi kali. Hata hivyo lakini, mbele ya ufidhuli huo mkuu na mbele ya utovu huo wa shukrani, Pendo langu halikukoma, ila badala yake lilitwaa sura na tabia ya Pendo linaloombaomba, Pendo linalosali, Pendo linalolalamika na kuomboleza kwa kupiga kelele. Hilo ndilo Pendo-Kupindukia langu la nane.”
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

SAA YA NANE:
PENDO-KUPINDUKIA LA NANE –
Pendo Masikini Ombaomba

Binti yangu, chonde usiniache peke yangu. Egesha kichwa chako juu ya tumbo la Mama yangu mpendwa kwa vile kutoka hapo wewe utaweza kusikiliza malalamiko na kilio changu na maombi yangu. Utakapoona kuwa malalamiko yangu na hata maombi yangu hayamshitui mwanadamu wa Pendo langu kuweza kunionea huruma, wewe utaona hapo hapo kuwa, Mimi ninajipanga kwa hiari yangu, kuchukua tabia ya mtu masikini kabisa kati ya watu walio ni ombaomba. Utaniona ninajaribu kunyosha kamkono kangu na kuanza kuomba huruma ya watu. Ninawaomba wanipe roho zao kama sadaka yao kwa Mimi masikini fukara. Nawaomba wanipe upenzi wao na roho zao. Kwa namna yoyote ile, Pendo langu lilikuwa likitaka kuushinda na kuupata ule moyo wa binadamu. Lakini, baada ya Pendo-Kupindukia langu kumjia mara saba ilionekana kuwa binadamu alikuwa anaendelea kunigomea bado, alikuwa amejifanya kiziwi; hakuwa ananijali Mimi kabisa, na wala hakutaka kamwe kujitoa kwangu. Ndipo Pendo langu likataka kumng’ang’ania na kumsukuma binadamu zaidi na zaidi. Kwa kweli ilibidi sasa Pendo langu lisitishe jitihada zake. Ingawa hivyo, halikukoma, ila badala yake liliamua kutoka nje ya mipaka yake, na nje ya vizuizi vyake na hata kutoka nje ya tumbo la Mama yangu. Pendo liliifanya sauti yangu itoke hadi ikawa inasikika nje kwa kila moyo wa mwanadamu na ikawa inasikika kwa namna ya kuvutia sana na kwa ushawishi mkubwa. Sauti hiyo ilisikika kwa njia ya sala, na maombi makali sana, na kwa njia ya maneno yenye kupenya kweli kweli. Je unajua nilikuwa ninauambia nini huo moyo wa mwanadamu?

‘Mwanangu, chonde unipe moyo wako: Mimi nitakupatia kila kitu unachotaka ili mradi tu ukubalie tubadilishane na moyo wako. Mimi nimeshuka toka mbinguni ili niufanye moyo wako kuwa mateka yangu! Chonde usinikatalie! Usinifanye nidanganyike na matumaini yangu! Nilipoona kuwa mwanadamu anazidi kuwa mgumu – kwa kweli wengi wakiwa wananigeuka na kunionyesha kisogo - basi hapo Mimi nilianza hatua ya kulalamika. Nikawa naunganisha vimikono vyangu vile vidogo na kuanza kulia machozi kwa sauti ya kukaukia na kukatikakatika kutokana na kwikwi zangu. Nikawa ninasema: ‘Chonde chonde! Mimi ni Ombaomba mdogo! Je, wewe, unapenda kunipatia moyo wako angalau kama mchango na sadaka yako kwa mie masikini?’. Je, hilo siyo Pendo-Kupindukia langu lililo kubwa kupita yote? Je, hilo si Pendo kuu kwamba Muumba wako, ili aweze kumkaribia mwanadamu, anatwaa umbo la mtoto mdogo, kusudi asiweze kumtisha mwanadamu, na wala asiweze kumletea hofu yoyote? Je hilo siyo Pendo la ajabu kwamba anajifanya mtoto, ili aweze kuwa anauomba moyo wa mwanadamu kwa mbinu za ombaomba ya masikini na fukara? Na je, hilo siyo Pendo-Kupindukia langu kwamba, alipoona kuwa mwanadamu hataki kumpatia moyo wake, Yeye anaomba, analalamika, na analia?!”

Kishapo nikawa ninasikia sauti ikisema: “Na wewe, je hutaki kunipatia moyo wako? Je labda hata wewe unapenda mimi niendelee kulalamika, niendelee kuomba omba na niendelee kulia ili wewe unipe moyo wako? Je unataka kunigomea kunipa hata sadaka hiyo ya masikini ombaomba ninayokusihi sana?” Alipokuwa akisema hayo, mimi nilikuwa nasikia jinsi alivyokuwa anashikwa na kwikwi. Nikasema: “Yesu Wangu, usilie, mimi nakupa moyo wangu, na ninakupa nafsi yangu yote kabisa”.

Ndipo ile sauti ya kutoka ndani mwangu ilisikika ikiendelea kusema: “Ebu endelea na sogea mbele zaidi kwenye Pendo-Kupindukia langu la tisa.”
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

SAA YA TISA:
PENDO-KUPINDUKIA LA TISA –
Pendo Linaloteseka

“Binti yangu, hali yangu yazidi kuwa ni ya mateso daima. Kama unanipenda, basi elekeza na kaza macho yako juu ya Mimi, ili uone kama utaweza kupeleka angalau kitulizo fulani kwa huyu Yesu wako Mdogo. Neno lako, hata likiwa ni dogo tu, la pendo, mpapaso wako na busu lako, vitaleta kitulizo na kusitisha kilio changu na kupunguza maumivu yangu.

Ebu sikiliza, binti yangu: Baada ya kutoa Pendo-Kupindukia langu kwa mara nane, na baada ya binadamu kujibu kwa kunigomea vibaya kabisa, Pendo langu halikukubali kushindwa; bali, baada ya lile Pendo-Kupindukia la nane, Pendo likaamua sasa kuongeza Pendo-Kupindukia la tisa. Hilo likawa ni Pendo la zile hofu, yale mahangaiko, zile dukuduku za moto mkali, pamoja na ile miali ya moto wa matamanio. Nilikuwa natamani kabisa kutoka nje ya tumbo la Mama ili hatimaye nionekane kwa mwanadamu kusudi niweze kumkumbatia kila mmoja. Hamu hiyo kali ilinisababishia Teso kali mno juu ya Ubinadamu Wangu ule mdogo uliokuwa haujazaliwa bado. Teso hilo kali lilinipelekea hadi kutoa ile pumzi yangu ya mwisho. Kumbe lakini, katika dakika ile ya mwisho, ule Umungu Wangu – ambao kamwe haukuweza kutengana nami – ukawa unanipatia na kunitia dosi za uhai hata nikawa naongezewa uhai mpya ulioniwezesha kuendelea kuvumilia yale maumivu yangu makali na kuweza kurudia kufariki tena na tena kwa mara nyingine. Hilo ndilo likawa ni Pendo-Kupindukia langu la tisa: Kusulibiwa, na maumivu, na kufariki kwa Pendo kwa jinsi endelevu ya kurudiarudia daima kwa ajili ya mwanadamu! Oh, ni mateso yaliyoje marefu ya kudumu na makali kwa muda wote wa miezi tisa! Oh, ni jinsi gani Pendo lilivyonikaba kooni, lilivyonifanya niwe ninazimia! Kama nisingekuwa nimeushikilia Umungu pamoja Nami, Umungu ambao ndio uliokuwa unanipa mara kwa mara uhai katika zile mara zote nilipokuwa naelekea kumalizika, Pendo lingekuwa tayari limenimeza na kunimaliza hata kabla kabisa ya kujitokeza kwenye mwanga wa siku, yaani kabla ya kuzaliwa kwangu”.

Kishapo, aliongezea kusema: “Ebu uniangalie, ebu unisikilize jinsi ninavyoteseka vikali; jinsi moyo wangu huu mdogo unavyogonga, unavyohangaika, unavyoungua. Ebu unitazame: Sasa ndiyo nakufa!”. Kukaingia kimya kizito na cha kina! Mimi nilijionja ninakufa, nilijisikia damu yangu ikiganda ndani ya mishipa yangu yote ya damu. Nikawa ninatetemeka. Nilimwambia: “Pendo Langu, Uhai Wangu, chonde usifariki, usiniache peke yangu. Si Wewe unataka pendo; basi na mimi nitakupenda Wewe; sitakuacha tena. Unipe hiyo miali yako ya moto ili niweze kukupenda zaidi, na ili niweze kujimaliza kabisa mimi mwenyewe kwa ajili yako”..’
HATUA TISA ZA PENDO KUPINDUKIA**
LA NENO ALIYEJIMWILISHA NDANI YA TUMBO LA BIKIRA MARIA

Kutoka Makala ya Mtumishi wa Mungu
LUISA PICCARRETA,
Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu


**Neno la Kiitalia ni ‘Eccessi di amore’. Tumetafsiri kama Pendo-kupindukia. Yaani: Pendo linalozidi kiasi, Pendo la ziada. Kiingereza = excessive love, excess of love, extreme love.

❤️🌟❤️🌟❤️🌟

HITIMISHO LA NOVENA

(Luisa anaandika):

Ndivyo nilivyopitisha siku zangu za Novena. Vigilia ya Noeli ilipokuwa inakaribia, nilijionja ninawaka upendo wa pekee sana. Nilikuwa nipo peke yangu chumbani, halafu mbele yangu, alijitokeza Mtoto Yesu, mzuri kabisa. Ni kweli; lakini alikuwa akitetemeka huku akininyoshea mikono yake akitaka kunikumbatia. Basi nami nikasimama kumkimbilia ili nikamkumbatie. Kumbe lakini, nilipokuwa nataka nimshike, Yeye alitoweka. Tukio hili lilijirudia mara tatu. Niliguswa sana, na niliwaka upendo na kutekwa hivi hata nashindwa kuelezea.
“Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokuambia, maana Herode anakusudia kumuua huyu mtoto.” (Mt 2; 13)

Bikira Maria Mtakatifu kwa Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta - ya "Bikira Maria katika Ufalme wa Utashi wa Mungu" - Siku Ya Ishirini Na Nne🖋📖📘

Roho Anazungumza na Malkia Wake Anayekabiliwa na Mateso:

Mama yangu Mtawala Mkuu, Binti yako mdogo anahitaji kuja magotini pako ili awe mwenzi wako. Natambua kuwa uso wako leo umefunikwa na masikitiko, hata machozi fulani yanadondoka toka machoni kwako. Kichanga mzuri anatetemeka, anapiga chafya na analia. Mama Mtakatifu, naunganisha maumivu yangu pamoja na ya kwako, ili nikufariji na ili kutuliza kilio cha Kichanga wa Mbinguni. Lakini, lo, Mama yangu, usinikatalie kunifunulia siri. Je kuna nini kinachotishia kifo cha Kichanga Wangu mpenzi?

Fundisho la Mama Malkia:

Binti yangu mpenzi sana, Moyo wa Mama yako leo umejaa na kuvimba kwa upendo na kwa teso hata siwezi kujizuia kulia. Unakumbuka ujio wa Wafalme Mamajusi, ambao walichokoza mambo pale Yerusalemu walipoingia kuulizia juu ya Mfalme mpya. Herode katili, akihofia kupinduliwa toka kwenye kiti chake, amekwishatoa agizo la kumwua Yesu Wangu Mtamu, Uhai Wangu mpendwa pamoja na watoto wengine wote.

Binti yangu, mateso yalioje! Yule aliyefika kutoa uhai kwa watu wote na Yule aliyefika duniani kuleta zama mpya za amani, za furaha, za neema, sasa wanataka kumwua. Ufidhuli gani huu! Chuki gani hii! Ah, Binti yangu, ona upofu wa utashi wa binadamu unakofikia! Ni hadi kufikia ukatili huu wa kufunga kamba mikono ya Muumba mwenyewe, na hadi kujikweza na kujifanya mmiliki wa Yule aliye Muumba! Kwa hiyo basi, Binti yangu, unionee huruma Mimi, na jaribu kutuliza kilio cha Mtoto Mtamu. Yeye analia kwa ajili ya ufidhuli wa binadamu, ambao mara tu baada ya kuzaliwa Kwake, wanamtaka afe, na kwa hiyo tunalazimika sasa kukimbia ili tumwokoe. Mtakatifu Yosefu amekwisha kupewa taarifa na Malaika kwamba tutoroke mapema na kukimbilia nchi ya kigeni. Wewe Binti mpenzi utusindikize na wala usituache peke yetu, na Mimi nitakuwa nikiendelea kukupatia mafundisho yangu juu ya mabaya makubwa ya utashi wa binadamu.
Lazima ufahamu pia kuwa mara mtu anapojitenga na Utashi wa Mungu, ni papo hapo anavunja uhusiano na Muumba Wake. Kila kitu kilichofanywa na Mungu hapa duniani kimekuwa ni kwa ajili ya mtu, kila kitu kilikuwa ni mali yake, lakini binadamu, kwa kugoma kutekeleza Utashi wa Mungu, akapoteza haki zake zote; na twaweze kusema kuwa hakujua tena aelekee wapi. Ndivyo basi alianza kuwa mkimbizi na mhamiaji masikini, kuwa mhujaji asiyeweza kumiliki hata chumba cha kudumu, na imekuwa hivyo siyo tu kwa upande wa roho, bali hata kwa upande wa kimwili. Mambo yake yote yakawa yanabadilika badilika kwa binadamu duni huyu. Na kama ilitokea baadhi ya mambo yake yakastahimili, basi imekuwa ni kutokana na nguvu ya mastahili ya huyu huyu Kichanga wa Mbinguni. Ndivyo hivyo kwani uzuri wote na ukuu wote wa Uumbwa uliandaliwa na Mungu, kwa ajili ya kuwapatia watu wale watakaokuwa wanatekeleza Utashi wa Mungu, na watakaokuwa wameishi katika Ufalme Wake. Wengine wote, kama wanabahatika kuambulia kitu chochote, basi wanakuwa ni watoto wevi wa Muumba wao. Na inaeleweka. Ni kwa vile hawataki kutekeleza Utashi wa Mungu, lakini hata hivyo wanataka faida na manufaa yanayomilikiwa na Utashi huo!

Binti mpenzi, ona jinsi tunavyokupenda Mimi na huyu Kichanga mpendwa, ambaye katika pambazuko la kwanza la maisha Yake, anapasika kwenda uhamishoni katika nchi ya kigeni, kwa ajili ya kukukomboa wewe toka uhamishoni, ambako utashi wa kibinadamu umekupeleka, kwa ajili ya kukuita na kukukumbusha usiishi katika nchi hiyo ya kigeni, bali urudi katika nchi yako uliyopewa na Mungu tangu ulipoumbwa, yaani kuishi katika Ufalme wa FIAT Kuu. Binti ya Moyo wangu, uone uchungu juu ya machozi ya Mama yako na juu ya machozi ya Kichanga huyu Mpendwa Mtamu. Sisi tunalia tukikuomba usifanye kamwe utashi wako ila tunakusihi na hata tunakuapisha: rudi ndani ya tumbo la Utashi wa Mungu ambaye anakuchuchumia sana!

Sasa Binti mpendwa, tukiwa kati ya lile teso la ufidhuli wa binadamu na ile furaha na raha tele tele alizokuwa anatupa FIAT ya Kimungu, na kati ya sherehe ya Uumbwa wote waliyokuwa wakimfanyia Kichanga Mtamu, dunia ilianza kubadilika: dunia iliota nyasi mpya, na ilianza kuchipusha maua chini ya miguu yetu, kwa ajili ya kutoa heshima, kwa Muumba Wake. Jua kwa upande wake lilikuwa linamwangalia na likawa linamchuchumia kwa kumumulikia na kumwangaza kwa nuru yake kwani lilionja limepata heshima kumtolea mwanga wake na joto lake. Upepo ulikuwa unampapasa na kumbembeleza, na kundi kubwa la ndege, mithili ya wingu walikuwa wanateremka na wakawa wanatuzunguka huku wakiimba kwa sauti zao nyembamba za aina aina, wakileta misiki yao murua ya kumbembeleza Kichanga mpendwa alale, na pengine walitoa musiki wa kumtuliza wakati akilia hadi naye akarudia usingizi wake. Binti yangu kwa vile Utashi wa Mungu ulikuwa ndani yetu, tulikuwa na uwezo na madaraka juu ya kila kitu.

Baada ya siku kadhaa tulifika Misri. Na kisha kupita kitambo kirefu, Malaika wa Bwana alimtaarifu Mtakatifu Yosefu kuwa, turejee katika nyumba ya Nazareti, kwa vile yule mbaya na mdhalimu na mwuaji alikuwa tayari amekufa. Ndivyo tulivyotoka Misri na kurejea nchini kwetu tulikozaliwa.

Misri ni mfano wa utashi wa binadamu, ni nchi iliyojaa miungu. Popote ambapo Mtoto Yesu alikuwa akipita alikuwa anawaangusha chini miungu hao na kishapo aliwatupa ndani ya moto wa milele. Je ni miungu wangapi unao utashi wa binadamu! Miungu ya majigambo, miungu ya kujitafutia makuu na vyeo, na miungu wa tamaa ambao wanamvamia masikini mwanadamu! Kwa hiyo tafadhali angalia sana umsikilize Mama yako. Ili nisikuachilie ukafanya utashi wako. Nitajitahidi kufanya kila sadaka, na ikitakiwa hata sadaka ya maisha yangu, ili nikupatie lile Jema Kuu la wewe kuishi daima katika tumbo la Utashi wa Mungu.
Roho Anazungumza na Mama Malkia Wake:

Mama Mtamu kabisa, nikushukuruje kwa kunifanya nielewe hasara kubwa ya utashi wa binadamu! Basi mimi ninakuomba, kwa teso ulilolipata katika uhamisho wa kwenda Misri, uisaidie roho yangu iweze kutoka katika nchi ya uhamisho uliosababishwa na utashi wangu na halafu unisaidie nirudi kwenye makao yangu asilia katika nchi nzuri ya Utashi wa Mungu.

Sadaka Ndogo:

Leo, kwa heshima yangu utatolea vitendo vyako vikiunganishwa na vya kwangu, katika sala ya shukrani kwa Mtoto Mtakatifu. Umwombe aingie katika Misri ya moyo wako, ili akaigeuze yote kuwa Utashi wa Mungu.

Sala ya Mishale:

Mama yangu, umfungilie Yesu Mdogo katika moyo wangu ili akanipange upya katika Utashi wa Mungu.
Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo Torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana (Lk 2; 22)

Bikira Maria Mtakatifu kwa Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta - ya "Bikira Maria katika Ufalme wa Utashi wa Mungu" - Siku Ya Ishirini Na Tatu 🖋📖📘

.....Binti yangu mpenzi, tafadhali usiondoke kwanza, baki hapa kando yangu. Unifuate popote. Tayari zinatimia siku arobaini tangu alipozaliwa Mfalme Mdogo Yesu. FIAT ya Kimungu ndiyo inatuita kwenda Hekaluni kwa ajili ya kutekeleza sheria ya kumtolea Mtoto Wangu. Haya tukaenda Hekaluni. Ndiyo mara yangu ya kwanza kutoka na Mtoto Wangu mtamu. Mshipa wa maumivu ulipasuka, moyoni mwangu. Nilikuwa nakwenda kumtolea kama sadaka, kama mhanga wa wokovu wa watu wote! Kwa hiyo tuliingia Hekaluni na tukaabudu Ukuu Mtukufu wa Mungu. Walimwita kuhani. Mimi nilimtoa Mtoto na kumweka mikononi mwake Kuhani, ikiwa ndilo tendo la kumtolea Kichanga wa Mbinguni kwa Baba wa Milele. Nilimtolea sadaka kwa ajili ya wokovu wa wote. Nilimwachia Mtoto ndani ya mikono ya Kuhani. Hapo Kuhani alimtambua kuwa alikuwa ndiye Neno wa Mungu. Alishangilia kwa furaha kuu! Kishapo Kuhani alibadilika na kutwaa uso wa kinabii na kuanza kutabiri juu ya mateso yangu yote ...... Oh, ona jinsi FIAT Kuu, kwa ile sauti ya kutetemesha, ilivyogonga kengele ya kusambaza teso katika Moyo wangu wa kimama, teso lililosababishwa na ule mkasa wa kifo, wa maumivu yote ya Mtoto Wangu Kichanga! Na kilichonichoma zaidi yalikuwa ni yale maneno ambayo yule Nabii Mtakatifu aliyaelekeza kwangu akisema: “Huyu Kichanga kipenzi atakuwa ni wokovu na angamizo la wengi na atakuwa ni ishara ya mambo kinzani”.

Kama Utashi wa Mungu usingenishikilia, ningekufa pale pale kwa mateso yale tu! Kumbe lakini, ulinitia uhai na ulitumia fursa hiyo kutengeneza Ufalme wa mateso ndani ya Ufalme wa Utashi Wake. Kwa namna hiyo, zaidi ya ile haki yangu ya kuwa Mama juu ya watu wote, nilipata sasa haki ya kuwa pia Mama na Malkia wa mateso yote. Ah, ndiyo kweli kwa mateso yangu nimejipatia senti za kulipia madeni ya watoto wangu na hata kulipia madeni ya watoto wale wakorofi na wasio na shukrani.

Sasa, Binti yangu, ni lazima ujue pia kuwa katika mwanga wa Utashi wa Mungu nilikwisha kuyajua mateso yote ambayo yangenihusu na hata zaidi ya yale aliyonieleza Nabii yule wa Mungu. Lakini, katika dakika ile ya tendo lile rasmi kabisa la kumtolea Mwanangu, kusikia neno hilo linarudiwa kwangu, nilionja kujeruhika vibaya sana, hivi hata Moyo wangu ukawa unatoka damu na kusababisha mipasuko ya kina rohoni mwangu.

Nisikilize Mimi Mama yako zaidi: Katika maumivu yako, katika kukabili mateso ambayo huwa hayakosekani, usivunjike moyo kamwe. Kwa upendo wa kijasiri ukubali Utashi wa Mungu uchukue nafasi yake ya kifalme katika maumivu yako ili ugeuze maumivu hayo kuwa senti za thamani isiyo na mipaka. Kwa senti hizo utaweza kulipa madeni ya ndugu zako ili kuwagomboa toka utumwa wa utashi wa binadamu na hivyo kuwawezesha kuingia tena katika Ufalme wa FIAT ya Kimungu kama watoto huru.
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Septemba 16, 1921**🖋📃📖📔

Yesu katika Ikulu ya Herode, wanamvalisha kama kichaa, wanamdhihaki.

Nilikuwa nikitekeleza Saa ya Mateso wakati Yesu Wangu Mta-mu alipokuwa katika ikulu ya Herode huku akiwa amevalishwa kama kichaa na akidhihakiwa. Yesu Wangu Mpendevu, alijitokeza na kujionyesha akaniambia:

“Binti Yangu, haikuwa ni wakati ule tu ambapo nilivalishwa vazi kama kichaa, nikazihakiwa na kuchezewa, bali hata leo hii wanadamu huendelea kunisababishia maumivu hayo, yaani naendelea kupata dhihaka kutoka kwa aina zote za watu. Iwapo mtu anakwenda kuungama na bila kuzingatia makusudio yake ya kuacha dhambi, hiyo ni dhihaka kwangu. Iwapo Padre anaungamisha, anahubiri, na anaadhimisha Sakramenti wakati maisha yake hayafanani na maneno yake, wala hayaendani na hadhi ya Sakramenti anazoadhimisha, huyo ananichezea na ananifanyia dhihaka kwa kila neno analosema na kwa kila Sakramenti anayoadhimisha. Wakati katika Sakramenti Mimi nilikuwa nawarejeshea uzima mpya, wao lakini wananifanyia utani na dhihaka. Na kwa kuzikufuru Sakramenti wao wananiandalia Mimi lile vazi la kunivika ukichaa. Iwapo wakubwa wanaoongoza wanaagiza watu walio chini yao watoe sadaka na majitoleo, wakiwaagiza pia fadhila, sala na kujikatalia, wakati viongozi wenyewe wanatafuta maisha ya raha, ya anasa, na ya ubinafsi, hao wananitendea dhihaka nyingi mno. Iwapo viongozi wa kiraia na wa Kanisa wanadai kushika taratibu na sheria huku wenyewe wakiwa ni wahalifu wa kwanza, hizo huwa ni dhahaka wanazonitendea.

Oh! Ni dhihaka ngapi wanazonifanyia! Ni nyingi hivi hata nimechoka! Hasa pale wanapotia sumu ya ubaya chini ya mambo mema. Ah! Ni jinsi gani wanavyonichezea kana kwamba Mimi ni mpira na kigari chao! Lakini muda wowote wa sasa au wa baadaye hukumu ya Haki Yangu itawachezea kwa kuwaadhibu vikali. Wewe usali na kunilipa fidia kwa dhihaka hizi ambazo zinanitesa kweli na zinazosababisha hata nisijitambue Mimi ni nani.”

Baada ya kurejea tena, kwa vile mimi nilikuwa najiyeyusha nafsi yote ndani ya Utashi wa Mungu, (Yesu) aliniambia:

“Binti mpenzi sana wa Utashi Wangu, Mimi ninangoja kwa hamu zoezi lako hilo la kujiyeyusha ndani ya Utashi Wangu. Lazima ujue kuwa Mimi nilipokuwa nawaza katika Utashi Wangu, ndivyo nilikuwa nayaingiza mawazo yako ndani ya Utashi Wangu huku nikiyaandalia pia mahali na nafasi. Na Mimi nilipokuwa natenda nilikuwa naingiza matendo yako ndani ya Utashi Wangu. Na ndivyo ilivyokuwa kwa mambo mengine yote yaliyobakia. Sasa lakini, kile nilichotekeleza sikukifanya kwa ajili ya Mimi, kwani sikuwa nina hitaji lolote, bali nilifanya kwa ajili yako. Kwa sababu hiyo, Mimi ninakungojea ndani ya Utashi Wangu ili ufike kuchukua nafasi zako ambazo Ubinadamu Wangu ulikuandalia. Hatimaye uje utekeleze vitendo vyako juu ya vitendo vile vilivyoingizwa na Mimi. Hapo sasa huwa ninaridhika na ninapata furaha timilifu pale ninapokuona wewe ukitenda kile kile nilichofanya Mimi”.

**Tazama Kitabu Saa 24 za Mateso ya BWYK
Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 18 - Agosti 15, 1925🖋📃📖📔

Vitu vyote vilivyoumbwa hutembea kuelekea kwa binadamu. Sikukuu ya Kutwaliwa Bikira Maria Mbinguni ilitakiwa iwe inaitwa: ‘Sikukuu ya Utashi wa Mungu’.

Mimi nilikuwa nikiendelea na zoezi langu la kujiyeyushia mimi mwenyewe ndani ya Utashi wa Mungu kwa minajili ya kumrudishia Yesu Wangu upendo wangu mdogo na shukrani kwa yale yote aliyoutendea uzao wa binadamu katika Uumbwa. Ndipo Yesu Wangu Mpendwa, huku akija ndani mwangu, akitaka kuongeza thamani kwenye upendo wangu mdogo, akaanza kutenda na yeye vitendo vile nilivyokuwa nikifanya mimi. Pindi akifanya hivyo aliniambia hivi:

“Binti Yangu, vitu vyote vilivyoumbwa vilikuwa vimefanywa kwa ajili ya binadamu, na kwa hiyo, vyote vinakimbilia kuelekea kwake binadamu. Vitu hivi havina miguu, lakini vyote vinatembea, vyote vina mwendo fulani au wa kumfikia binadamu au mwendo wa kujifanya vifikiwe naye binadamu. Mwanga wa jua huanza kule juu kabisa kwenye Mbingu ili kuweza kumfikia mwanadamu, ili kumwangazia na ili kumpasha joto. Maji hutembea hadi kuweza kufikia matumboni mwa mwanadamu ili kutuliza kiu chake na ili kumburudisha. Mmea, mbegu, hutembea, hukausha ardhi, hutengeneza tunda lake kwa ajili ya kujitoa kwake binadamu. Hakuna kitu chochote kilichoumbwa ambacho hakichukui hatua fulani au kufanya mwendo fulani kuelekea kwa yule ambaye kwake Mtengenezaji Mkuu alikuwa amekielekeza kitu hicho wakati wa uumbaji, yaani kuelekea kwa binadamu. Utashi Wangu Mimi unazingatia kabisa utaratibu, harmonia, na unashikilia vitu vyote katika njia inayokwenda kwa wanadamu, na kwa namna hiyo, ni Utashi Wangu ndio unaotembea daima katika vitu vilivyoumbwa ukielekea navyo kwa mwanadamu. Hausimami kamwe. Upo daima katika mwendo na umejaa mwendo ukielekea kwa yule ambaye anampenda mno – mwanadamu. Lakini ajabu, ni nani anayewazia kusema asante kwa Utashi Wangu ambao unamletea mwanga wa jua, unamletea maji ya kunywa ili kutuliza kiu chake, unamletea mkate kushibisha njaa yake, unamletea tunda, unamletea ua kwa ajili ya kumburudisha, na unamletea vitu vingine vingi vingi sana ili kumfanya afurahi? Je si neno la haki tu kwamba, kama Utashi Wangu Mimi unafanya kila kitu kwa ajili yake, binadamu huyo naye afanye kila liwezekanalo ili kutimiza Utashi Wangu?

Oh, laiti ungejua wewe, sherehe unayofanya huu Utashi Wangu, ndani ya vitu vilivyoumbwa, wakati ule unapomtumikia na unapoambatana na mtu ambaye anatimiza Mapenzi Yangu! Utashi Wangu unakuwa umekaa na unatenda kazi ndani ya mwanadamu na Utashi Wangu ule unaotenda kazi ndani ya vitu vingine vilivyoumbwa, pale vinapokutana pamoja huwa wanabusiana, wanapatanisha mambo, wanafanyiana upendano na wanatunga hata utenzi, wanafanya na uabudu kwa Muumba Wao. Hapo hutokea lile tukio kubwa kabisa la Uumbwa wote. Vitu vilivyoumbwa hujiona na kujisikia vimepewa heshima kubwa sana wakati vinapokuwa vikimtumikia mwanadamu ambaye ndanimo amehuishwa na ule Utashi Wenyewe, ambao ndio unatengeneza uhai ule wa kwao. Kinyume chake lakini, huo Utashi Wangu Wenyewe, huingia katika uchungu ndani ya hivyo hivyo vitu vilivyoumbwa, pale unapopasika umtumikie mtu ambaye hatekelezi Mapenzi Yangu. Ndipo inapotokea mara nyingi sana kuwa vitu vilivyoumbwa, husimama na kupingana na kukabiliana na binadamu. Vitu hivyo vinampiga na vinamwadhibu mwanadamu, na kwa hilo vinajitwalia madaraka kuwa juu ya binadamu. Ni kwa vile vitu hivyo vimekuwa vikihifadhi bila dosari yoyote, na kuuzingatia kwa utii ule Utashi wa Mungu uliovihuisha tangu siku ya kwanza ya kuumbwa kwao. Lakini binadamu ameteremka na kushuka kilindini kwa kosa la kutozingatia ndani yake ule Utashi wa Mwumbaji Wake”.

Baada ya hapo mimi niliingia katika kuwaza juu ya Sikukuu ya Mama yangu wa Mbinguni aliyechukuliwa katika Mbingu. Na Yesu Wangu Mtamu, kwa sauti laini kabisa na ya kunigusa sana moyoni aliongeza kusema:
“Binti Yangu, tukitaka jina halisi la Sikukuu hii, ilibidi iitwe: ‘Sikukuu ya Utashi wa Mungu’. Ilikuwa ni utashi wa kibinadamu ndio uliofunga Mbingu, ndio uliovunja na kukata kile kiungo cha mwanadamu na Muumba Wake, ndio uliofungulia matatizo yakatoka nje kwa mwanadamu, ulifungulia maumivu na mateso, ndio uliokomesha zile sikukuu ambazo mwanadamu alipasika kuzifaidi kule Mbinguni. Sasa lakini, huyu kiumbe mwanadamu, aliyekuwa ndiye Malkia wa vitu vyote, kwa kutimiza Mapenzi ya Utashi wa Milele, daima na katika kila kitu, yaani unaweza ukasema kuwa, uhai wake ulikuwa ni Utashi wa Mungu peke yake, ndiye aliyefungua Mbingu na ndiye aliyeunganisha tena Yule aliye ni wa Umilele na mwanadamu; na ndiye akafaulu kufanya zirejeshwe tena zile Sikukuu za Mbinguni kati ya Mungu na mwanadamu. Kila tendo alilokuwa anatekeleza katika Utashi Mkuu, likawa ni Sikukuu iliyokuwa ikianzia kule Mbinguni, matendo yake yakawa ni majua aliyoyatengeneza kuwa mapambo ya Sikukuu hii, matendo hayo yakawa ndio musiki aliokuwa anautuma kuja kufurahisha Yerusalemu ya Mbinguni. Kwa jinsi hiyo chimbuko halisi na la kweli la Sikukuu hii ni Utashi wa Milele unaotenda kazi na unaokaa ndani ya Mama Yangu wa Mbinguni, Utashi uliotenda mambo makuu kabisa ndani yake Mama huyu, Mama aliyeduwaza na kustaajabisha Mbingu na dunia, Mama aliyeufunga hata Umilele kwa minyororo ya vifungo vya upendo visivyoweza kuyeyuka kamwe, Mama aliyemteka Neno hadi kumwingiza ndani ya tumbo lake. Na hata wale Malaika wenyewe waliokuwa wametekwa na Mama huyu wakawa wanarudiarudia kusema kati yao: ‘Utukufu wote huu watokea wapi? Heshima yote hii, Ukuu wote huu na matendo makubwa haya ambayo hayajawahi kuonekana tunayoona sasa ndani ya Mwanadamu huyu wa pekee, yote haya hutokea wapi? Na halafu ajabu, tunamwona akitokea uhamishoni!’ Wakiwa wameshikwa na mshangao mkubwa sana waliutambua Utashi wa Muumba Wao kama ndiyo Uhai wa Mama na ndio uliokuwa unatenda kazi ndani yake. Mara hiyo, wakitetemeka kwa uchaji wakawa wanasema: ‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Heshima na Utukufu kwa Utashi wa Bwana Mtawala Wetu, na Utukufu na Mtakatifu mara tatu kwa Yeye Mama aliyefaulu kutekeleza huu Utashi Mkuu!’
Ni kwa hoja hii, umekuwa ni Utashi Wangu ndio ambao umekuwa unasherehekewa na unaendelea kusherehekewa katika Siku ya Kuchukuliwa Mbinguni kwa Mama Yangu Mtakatifu. Ilikuwa ni Utashi Wangu pekee ndio uliomfanya apande juu kabisa hata kumtofautisha na watu wote. Mambo yake yote yangebakia kuwa si kitu kama asingekuwa ndani yake na hili jambo Kuu kabisa la Utashi Wangu. Ilikuwa ni Utashi Wangu ndio uliompatia rutuba ya kimungu na ukamfanya awe Mama wa Neno. Ilikuwa ni Utashi Wangu ndio uliomfanya awaone na awakumbatie wanadamu wote kwa pamoja, huku akijifanya Mama wa wote na akawa anawapenda wote kwa pendo la Umama wa kimungu. Utashi Wangu, kwa kumfanya Mama awe Malkia wa wote, ulimwezesha kuwa na mamlaka juu ya himaya yote na kuanza kutawala. Ndiyo kusema, tangu siku ile Utashi Wangu ulipopata Utukufu na Heshima za kwanza, na ulipopata matunda tele tele ya kazi yake katika Uumbwa, siku ile ulipoanza kuadhimisha Sikukuu Yake ambayo haitawahi kukatishwa. Yote hiyo ni Sikukuu kwa ajili ya kutukuza utendaji ambao Utashi Wangu ulikwisha kuufanikisha ndani ya Mama Yangu mpendwa. Ingawa kama Mbingu ilikuwa imefunguliwa na Mimi, na ingawa kama Watakatifu wengi walikuwa tayari wamekwisha kupata Makao ya Mbinguni wakati huyu Malkia wa Mbinguni alipochukuliwa katika Mbingu, lakini hata hivyo, ni yeye huyu Mama ndiye hasa ambaye amekuwa ni chanzo asilia na ndiye huyu aliyekuwa kapewa jukumu juu ya kila kitu cha Utashi Mkuu. Ni kwa hoja hiyo, Utashi Mtakatifu, ili kuweza kuadhimisha Sherehe ya kwanza kwa ajili ya Utashi Mkuu, ulimsubiria yeye Mama, ambaye ndiye aliyekuwa ameutolea heshima kubwa kabisa, na ambaye aliyekuwa amebeba ndani yake ule muujiza mkuu halisia wa Utashi Mtakatifu. Huyu Malkia wa ajabu aliingia katika Himaya, akiwa amezungukwa na majeshi ya Mbinguni yaliyokuwa yakimsindikiza, akiwa na kiwiliwili chake kikiwa kimezungukwa na Jua la Milele la Utashi Mkuu. Oh, ilipomwona huyo Malkia akiingia hivyo, ona jinsi Mbingu yote ilivyoanza kuutukuza, kuushangilia, na kuusifu Utashi wa Milele! Wote wa Mbinguni walikuwa wanamwona amefunikwa na maweza ya FIAT Kuu. Hapakuwa ndani yake na pigo la moyo hata moja tu ambalo halikuwa halijagonga mhuri wa hiyo FIAT. Wakiwa wamepigwa butwaa waliendelea kumwangalia huku wakisema: ‘Kwea, kwea juu, kwea juu zaidi! Ni vema na haki kabisa kwamba Wewe uliyekuwa umeiheshimu kabisa FIAT Kuu, na kwamba sisi tupo sasa katika Makao ya Mbinguni kutokana na hii FIAT Kuu, Wewe sasa twaa kiti cha utawala kilicho cha juu kabisa na Wewe uwe sasa Malkia wetu!’ Na heshima kuu kabisa aliyokuwa ameipata Mama Yangu ikawa ni kuona na kushuhudia Utashi wa Mungu ukitukuzwa”.
Vinapatikana na unaweza ku download:

KITABU cha MBINGU - JUZUU NA. 11

KITABU cha SALA MBALIMBALI

Na vittabu vingine. Angalia site ⬇️⬇️⬇️

www.divinewilldivinelove.com/Kiswahili-/-Swahili/
"Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa,...." (Lk 3; 21)

💫🕊 Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA, Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - Kitabu: ZIARA YA ROHO KATIKA UTASHI WA MUNGU - SAA YA KUMI NA TANO🕊💫

Tumfuate Yesu kule jangwani. Tunapofika na kusimama pale kwenye mto Yordani, tumwombe atupatie Ubatizo wa wokovu wa Utashi wa Mungu ili kusudi watu wote waupate Uhai Wake.

Ewe Chema Changu Kikuu cha Mbinguni, mimi naharakisha kukufuata kwani vinginevyo muda hautanitosha kuweza kukufuatilia katika yote. Ninakuona tayari umejiandaa kutoka kwenda jangwani. Unamkumbatia Mama yako ukimbana kwenye Moyo wako unaoumia na kulia kwa pendo, na unamwambia: “Kwaheri, ubaki hapa, Ee Mama. Ninakuachia FIAT Yangu ya Kimungu, iwe hapa kama msaada kwako badala yangu, iwe kama uhai wako na kama mjumbe wa mawasiliano kati ya Mimi na Wewe’ . Utashi Wangu utakuwa unakuambia kila kitu atakachokuwa anatenda Mwanao, na wewe utakuwa ukinifuata katika kila kitu, kiasi kwamba, hata kama utakuwa mbali, FIAT itakuwa inakuleta karibu kabisa nami, hata tutajiona kuwa ni kitu kimoja tu”.

Ewe Yesu, nipe mkono wako na unichukue nije Nawe, ili chochote utakachokuwa unatenda kisiweze kunitoroka akilini mpaka niweze kufungilia ndani yake ile ‘Ninakupenda’ yangu, kwa ajili Yako, kusudi nikuombe Ufalme wa Utashi Wako wa Kimungu juu ya dunia. Kwa hiyo, wakati Wewe unaendelea kutembea peke yako, mimi ninakufuata hatua kwa hatua nikiwa nimebeba kauli yangu ya ‘Ninakupenda, Ninakuabudu, Ninakuheshimu, Ninakushukuru’. Katika kila pumzi yako nataka nikufanye uwe ukipumua ‘Ninakupenda’ yangu. Kila moja la neno lako nalifungilia ndani ya ‘Ninakupenda’ yangu. Katika kila mtazamo wa jicho lako nataka uwe unakutana na ‘Ninakupenda’ yangu. Na wakati unapowasili pale Yordani mimi napenda nitiririshe ‘Ninakupenda’ yangu ndani ya maji yale. Natiririsha kwa jinsi kwamba, kama vile Mtakatifu Yohane Mbatizaji alivyotiririsha maji kichwani pako kwa ajili ya kukubatiza, ndivyo sasa na Wewe uonje kuwa Binti Yako Mdogo kamwe hatakuacha peke yako bali anaambatana nawe kwa njia ya ‘Ninakupenda’ yake. Kwa kutiririsha kauli hiyo katika maji yale anataka akuombe Wewe utoe maji ya ubatizo ya Utashi Wako wa Kimungu kwa ajili ya wanadamu wote, ili huo uwe ndio mwanzo wa Ufalme Wake. Ewe Pendo Langu, katika tendo la kisherehe la Ubatizo wako, napenda nikuombe neema moja ambayo Wewe kwa uhakika hutanikatalia: Ninakuomba kwamba, kwa mikono yako mitakatifu, uibatize hii roho yangu ndogo katika maji yaletayo uzima na ya uumbaji ya Utashi Wako wa Kimungu. Ninaomba hilo ili kusudi roho yangu isionje kamwe, isione, na wala isiujue uhai mwingine isipokuwa uhai wa FIAT Yako. Ah, kweli kabisa, ninakuomba kwamba uwepo wangu usiwe ni kitu kingine, bali uwe ni tendo moja pekee la Utashi Wako.
Ewe Yesu Wangu, Pendo Langu tamu, mimi ninakufuata kwenda jangwani. ‘Ninakupenda’ yangu haitakuacha peke yako katika jangwa hili. Nitabaki kuwa kando yako usiku na mchana. Nitakapokuona, ukiwa na masikitiko sana, ukiwa na mahangaiko, unapokufa kwa pendo, na nitakapokuona ukisali na ukilia kutokana na upweke wa Utashi Wako wa Kimungu baada ya wanadamu kuutoroka, mimi nitabaki kando yako. Wewe unaonja mara moja na hai kabisa maumivu ya Utashi huu wa Kimungu, siyo tu kwa vile hautawali kati ya wanadamu, bali kwa vile Utashi huu umeachwa katika upweke mithili ya jangwani, ni kama umeachwa uhamishoni. Kwa hiyo Ubinadamu Wako Mtakatifu mno unalia na unaomba, kwa niaba ya familia yote ya binadamu, kwamba zile tashi mbili, yaani, ule wa Kimungu na ule wa kibinadamu, budi zikutane na zijipatanishe zenyewe. Utashi wa kibinadamu unauita Utashi wa Mungu, ili kuuruhusu uje utawale, na Utashi wa Mungu unasamehe juu ya kipindi kile kirefu, ambamo wanadamu walikuwa wameushika na kuuzuia uhamishoni. Mimi nayachukua machozi yako na kuyafanya yawe ni ya kwangu, sala zako ziwe ni za kwangu, vionjo vya kifo vya Moyo Wako unaoungua kwa pendo, navyo viwe ni vya kwangu. Naendelea kukifuatilia kila kitu kwa ‘Ninakupenda’ yangu. Natengeneza minyororo mitamu ya pendo, na ninaingiza nafsi Yako yote ya Kimungu ndani yake kwani ninataka nikuvute kwa lazima ukubali kunipa Ufalme wa Utashi Wako wa Kimungu hapa duniani. Ebu sikiliza Ewe, Uhai Wangu, mbona ni yenyewe mapigo ya Moyo Wako, ni matamanio yako Mwenyewe, ni machozi yako, ni maumivu yako, ndiyo hayo yanayotaka na yanayoomba Ufalme wa FIAT Yako. Kwa hiyo basi, endapo hutaki kunisikiliza mimi, basi nakuomba ujisikilize Wewe Mwenyewe, na unipe jibu kusudi tutoke katika jangwa hili huku ukiniambia hivi: “Ah, ndiyo basi! Ufalme wa Utashi Wangu utafika hapa duniani!”

Ewe Yesu Wangu, Moyo wa moyo wangu, ninakuona ukiharakisha mpango wa kutaka kutoka jangwani. Naona unapitia tena kule kwenye mto Yordani ili, kwa upendo, ukamchungulie tena mpenzi wako Yohane. Moyoni mwake unatia mafuriko ya pendo na neema, na halafu kwa haraka haraka unaendelea na safari hadi kuifikia nyumba yako ya Nazareti, ambako pendo la Mama wa Mbinguni linakuita kwa mfululizo. Na tazama, Oh, nini hiki ninachoshuhudia kikinivuta hapa mbele yangu! Mama na mtoto wanarukiana, huyu katika mikono ya mwenzake, na kwa kuyeyushiana, hawa wawili wanatengeneza pendo moja tu. Maadam Malkia wa Mbinguni amekuwa akionja hitaji kali mno la kumwona tena Mtoto wake. Moyo wake wa kimama ulikuwa umeunguzwa moto wakati huu alipokuwa hayupo, wakati yeye Mama alikuwa anatamani kujimwaga ndani ya Mwanae, ili aweze kupokea umande wa Pendo Lake, ili asibaki ameteketezwa na miali ile ya moto, iliyokuwa ikimtafuna. Na Yesu, Mkombozi Wangu wa Mbinguni, kwa upande Wake, alikuwa naye akionja hitaji kali sana ya pendo la Mama. Ni kwa sababu hiyo alirukia mikononi mwa Mama Yake kusudi akatoe pendo na kupokea pendo. Hata mimi, nikiwa nimeshika ule mwali mdogo wa moto wa ‘Ninakupenda’, narukia katika makumbatio yenu hayo yaliyo safi sana, narukia katika makaribiano yenu, narukia katika mioto ya pendo la Mama na Mtoto wake, na kwa wote wawili, Mama na Mtoto, ninawasihi ninyi nyote mnipatie Ufalme wa Utashi Wenu. Ewe Mama Mtakatifu, urudie pamoja nami na usali pamoja nami, kwamba Utashi wa Mungu ujulikane, utawale, hapa duniani kama kule Mbinguni.
Wakati huu ambapo Mama na Mtoto wanajipumzisha kidogo katika pendo lao na wakati wanapochukua uhai, papo hapo wanajiandaa kwa ajili ya kukabili hali ya kuachika ya kipindi kirefu zaidi. Tayari Yesu Wangu, ambaye daima mtu hawezi akamfikia katika kiwango cha Pendo Lake, anachukua njia ile inayoelekea kwenye maisha yake ya hadharani. Anamkumbatia kwa nguvu kabisa Mama Yake, kwenye moyo wake, kwa ajili ya kumtia nguvu huyu Mama, kwa mara nyingine anaaga na anatoka peke yake kabisa, kwa ajili ya kwenda kueneza Neno lake la Kimungu kwa mataifa, kwenda kuunda wafuasi wake, na kwenda kutangaza Injili Takatifu.

Baba yetu...,
Salamu Maria...,
Atukuzwe Baba...
"Mwanangu, umesamehewa dhambi zako" (Marko 2; 5)

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Novemba 16, 1921** 🖋📃📖📔

Leo asubuhi, Yesu alionekana akiwa daima amefungwa kabisa: alifungwa mikononi, miguuni, na kiwiliwili chote. Toka shingoni Mwake kulining'inia minyororo miwili ya chuma. Minyororo na kamba vilimbana na kumkaza sana hata Mwili Wake Mtukufu ulishindwa kujimudu kabisa. Ni jinsi gani hali yake ilivyokuwa ngumu! Hata mawe yangeweza kulia machozi! Na hapo Yesu Chema Changu kikuu aliniambia:

“Binti Yangu, katika kipindi cha Mateso Yangu, maumivu Yangu mengine yote yalinijia kwa mtindo wa ushindano, yaani ya-linifikia kwa zamu za kubadilishana moja baada ya lingine. Kila umivu linalofuata lilikuwa ni kali zaidi kwani kila mtesaji Wangu alitaka ajulikane kuwa yeye ni hodari zaidi katika ukatili kuliko mwenzake. Walifanya zamu wakipokezana kama walinzi. Katika zamu zao hizo hakuna aliyewahi kufungua minyororo au kamba Zangu. Ndivyo nilivyokokotwa hadi kufika mlimani Kalvario. Nilikuwa nimefungwa daima! Mara kadhaa waliongeza minyororo na kamba kwani walihofu nisije nikakimbia na pia walilenga kunidhihaki na kunichezea. Maumivu mengi mangapi niliyoyapata! Ni jinsi gani nilivyovurugika, nilivyonyenyekeshwa, nilivyodhalilishwa! Ni mara ngapi nilivyojikwaa na minyororo hiyo hadi kuanguka chini!

Hata hivyo nilijua fika kwamba katika minyororo hiyo kulikuwa fumbo kubwa na fidia kubwa: binadamu anapoanguka katika dhambi mara nyingi hubaki amefungwa na minyororo ya hiyo dhambi yake. Kama ni dhambi kubwa basi mnyororo yake ni ya chuma, kama ni dhambi ndogo minyororo yake ni ya kamba. Kwa binadamu aliyeanguka katika dhambi, wakati anapojaribu kutembea katika jambo jema lolote, huwa anajisikia kubanwa miguuni na ile minyororo ambayo inamfanya ashindwe kutembea na kutenda hilo jema na badala yake hatua zake zinakuwa zimebanwa. Minyororo ya dhambi inamfanya aone maumivu ya nerva, inamfanya adhoofike, na inamfanya arudie kuanguka tena katika dhambi. Anapojaribu kutenda kitu anaonja kubanwa mikononi na minyororo hiyo hata kupelekea ajione kutokuwa na mikono ya kutendea jema lolote. Vishawishi na tamaa, zinapomwona mtu huyo amefungwa na kubanwa namna hiyo, huwa vinafanya sikukuu na kusherehekea huku vikisema: ‘Ushindi hakika ni wetu!’. Na kwa vile binadamu alikuwa ni mfalme na mtawala, sasa vinamchekelea kwa kuwa kafanywa kuwa mtumwa wa matamaa machafu. Ona jinsi mwanadamu anavyoharibika na kuchafuka anapoingia katika hali ya dhambi! Mimi, ili niweze kuikata hiyo minyororo yake, nimeamua Nami niwe nimefungwa na wala nisiachwe kamwe bila minyororo ili niiandae hiyo minyororo Yangu kuwa tayari kwa ajili ya kuivunja na kuikata minyororo ya dhambi za binadamu”. Na pindi maadui waliponipiga mateke, wakinisukuma na kuniangusha chini, Mimi nilikuwa nanyosha Mikono Yangu ili niifungue minyororo hiyo na kumweka mwanadamu katika uhuru wake tena”.

Wakati alipokuwa anaeleza hayo, mimi nilikuwa nawaona karibu watu wote waliokuwa wamefungwa kwa minyororo. Walinitia huruma sana. Nikawa ninamwomba Yesu agusishe minyororo ya kwake ile kwenye minyororo ya hao watu, ili kwa mgusano huo minyororo ya wanadamu ipate kubomolewa yote”.

**Tazama Kitabu Saa 24 za Mateso ya BWYK
Harusi ya Kana
Na siku ya tatu palikuwa na harusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. (YOHANA 2; 1-2)

Bikira Maria Mtakatifu kwa Mtumishi wa Mungu Luisa Piccarreta - ya "Bikira Maria katika Ufalme wa Utashi wa Mungu" - Nyogeza - Fikara Ya Sita (Siku ya 25B) 🖋📖📘

Roho Anazungumza na Mama Yake wa Mbinguni:

Mama Mtakatifu, nimefika, nipo pamoja nawe na pamoja na Yesu Mtamu, kwa ajili ya kuhudhuria Ndoa mpya, kwa ajili ya kuona makuu na kuelewa fumbo kuu, na kwa ajili ya kuona Pendo lako la kimama kwangu na kwa watu wote linafikia wapi. Lo, Mama yangu, shika mkono wangu mikononi mwako na uniweke juu ya magoti yako. Unimwagie Pendo lako, takasa akili yangu, na unieleze kwa nini ulipenda kuhudhuria harusi hii.

Fundisho la Malkia wa Mbingu:

Mwanangu mpenzi sana, Moyo wangu umevimba kwa Pendo, na nimekuwa na dukuduku ya kukueleza hoja kwa nini Mimi na Mwanangu Yesu tulipenda kuhudhuria hii harusi ya Kana. Je wewe unadhani ilikuwa kwa sababu tu ya sherehe fulani? La hasha, Binti, kuna mafumbo ya kina. Hebu uwe makini na Mimi nitakueleza mambo mapya, nitakueleza jinsi Pendo langu kama Mama lilivyojionyesha na kujitangaza kwa namna usiyoweza kusadiki na nitakuonyesha pia namna Pendo la Mwanangu lilivyoleta ishara halisi za Ubaba na za Ufalme kwa ajili ya wanadamu.

Basi sasa nisikilize. Mwanangu alikuwa ametoka kurejea toka jangwani na akawa anajiandaa kwa maisha ya Utume Wake Hadharani. Lakini, kabla ya hilo alipenda akahudhurie harusi hiyo, na ndiyo maana alikubali kualikwa. Tulikwenda, siyo hasa kwa hoja ya kusherehekea, bali kwa ajili ya kutenda mambo makubwa kwa faida ya vizazi vya binadamu. Mwananagu alishika nafasi ya Baba na nafasi ya Mfalme katika familia wakati Mimi nikashika nafasi ya Mama na ya Malkia. Kwa uwepo wetu pale tulileta upya utakatifu, uzuri, na utaratibu wa harusi iliyokuwa imewekwa na Mungu pale Eden. Yaani, harusi ile ya Adamu na Eva waliofungishwa ndoa na Aliye Juu na Mkuu, kwa lengo la kuijaza dunia na watu na hivyo kuongeza na kukuza vizazi vya baadaye. Ndoa ndio msingi wa kutegemeza chimbuko la uhai wa vizazi. Tunaweza tukaita ni shina ambalo kwalo dunia inapata kujazwa. Mapadre na watawa ni matawi. Kama pasingekuwepo shina basi hata matawi yasingekuwa na uhai. Ndiyo maana, kutokana na dhambi, kwa kitendo cha kujitenga na Utashi wa Mungu, Adamu na Eva walipoteza utakatifu, uzuri na utaratibu wa familia. Na Mimi, Mama yako, niliye Eva mpya nisiye na doa la dhambi, pamoja na Mwanangu tulikwenda kurejesha kile ambacho Mungu alikitenda pale Eden. Mimi nilijiweka kuwa Malkia wa familia na nikawa naomboleza neema ya FIAT ya Kimungu kutawala tena katika familia, neema ya kuwepo familia zitakazokuwa chini yangu na neema ya Mimi kushika nafasi ya Malkia katika familia hizo.

Siyo hilo tu, Binti yangu. Pendo letu lilikuwa linawaka. Tulipenda kuwaonyesha jinsi gani na kiasi gani tuliwapenda na pia kuwapatia fundisho lililo la juu kabisa kupita mafundisho mengine. Ona ni namna gani: Pindi karamu ilipokuwa inanoga kweli, divai ikawa imeisha. Moyo wangu wa Mama ulijisikia vibaya sana kwa hoja ya pendo kwani nilipenda kutoa msaada. Basi, huku nikijua fika kuwa Mwanangu ni mweza yote, kwa sauti yangu ya kusihi na kuomboleza, lakini Nikwa na uhakika kuwa atanisikiliza tu, nilimwambia: “Mwanangu, wanaharusi hawana divai zaidi”. Na Yeye alinijibu: “Saa yangu haijafika ya kutenda miujiza”. Nami nikifahamu pasi shaka kuwa asingeweza kunikatalia kile alichokuwa anakiomba Mama yake, niliwaambia wale waliokuwa wakitumikia mezani: “Tekelezeni kile atakachowaambia Mwanangu, nanyi mtapata kile mtakacho, na kwa kweli mtapata hata na zaidi na cha kuwatoshelezeni kabisa”.
Binti yangu, katika maneno hayo machache nilikuwa nimetoa fundisho lenye manufaa, la lazima, na zuri kabisa kwa mwanadamu. Nilikuwa nazungumza kwa Moyo wa Mama nikisema: “Watoto wangu, Je mnataka kuwa watakatifu? Tekelezeni Utashi wa Mwanangu. Msibadili kile anachowaambia, ndivyo mtakuwa na ufanano naye na mtakuwa na utakatifu wake chini ya mamlaka yenu. Je mngependa mabaya yote yakome? Tekelezeni kile anachowaambia Mwanangu. Je mngependa neema yoyote ile hata ikiwa ni ngumu? Tekelezeni kile anachowaambia na anachopenda. Je mnataka hata mahitaji ya lazima ya maisha ya kawaida? Tekelezeni asemacho Mwanangu. Hoja ni kwamba, katika maneno yake, katika kile anachosema na anachotaka, ndanimo kumefungiliwa namna ya uwezo ambao pindi anapozungumza, neno lake linakuwa ndani yake tayari na kile mnachoomba; na uwezo huo unafanya neema mnazohitaji zijitokeze papo hapo rohoni mwenu. Ni watu wangapi wanaojiona wamejaa mateso, wadhaifu, wamejeruhiwa na mateso, wanaonewa, wana mikosi, na wenye matatizo? Ndiyo wanasali na kusali zaidi, lakini kwa vile hawatekelezi kile asemacho Mwanangu hawaambulii chochote, na Mbingu yaelekea kuwa imefungwa kwa ajili yao. Hilo linaleta sikitiko na uchungu kwa Mama yako, kwani naona kwamba pale wanaposali, papo hapo wanakwenda mbali na kisima yanapokaa mema yote. Kisima hicho ni Utashi wa Mwanangu.

Wahudumu walitekeleza kweli kile ambacho Mwanangu kawaambia, yaani: “Yajazeni makasiki na maji na yapelekeni mezani”.

Mpenzi Wangu Yesu alibariki maji yale na yakageuka pale pale kuwa divai bora sana. Oh, mara elfu, heri sana kwa yule anayetekeleza kile asemacho na apendacho Yeye! Kwa tendo hilo, Mwanangu alinipa heshima kubwa kabisa, na akanifanya kuwa Malkia wa miujiza. Ndiyo sababu ya kutaka niungane Naye, na alitaka na ombi langu katika kutenda ule muujiza, wa kwanza. Yeye alinipenda mno hivi hata akataka kunipa nafasi ya kwanza ya Malkia hata katika miujiza na alifanya hivyo siyo kwa maneno tu, bali kwa matendo. “Kama mnataka neema na miujiza, njoni kwa Mama Yangu. Mimi sitaweza kumkatalia chochote kile anachotaka”.

Zaidi ya neno hilo, Binti yangu, kwa tendo la Mimi kuhudhuria harusi hii, Mimi nilitazama karne zijazo na niliangalia Ufalme wa Utashi wa Mungu hapa duniani. Niliziangalia pia familia na nikawa naziombea ziweze kuwa ishara ya Pendo la Utatu Mtakatifu, kusudi Ufalme Wake uwepo na utende kazi Yake. Na kwa haki zangu za Mama na Malkia, nilitilia maanani sana moyoni uwepo wa mamlaka ya Ufalme huo. Na kwa vile nilimiliki chimbuko, nilikuwa nikiwaandalia wanadamu neema zote, misaada, na utakatifu, uliotakiwa kwa ajili ya kumudu kuishi ndani ya Ufalme mtakatifu wa namna hiyo. Kwa sababu hiyo nazidi kurudia: “Fanyeni kile anachowaambia Mwanangu”.

Binti yangu, nisikilize: Kama unataka kumiliki kila kitu, usimtafute mwingine. Unifurahishe basi na kuniridhisha kwa kuniruhusu nikufanye wewe kuwa Binti yangu wa kweli na Binti wa Utashi wa Mungu. Na hapo Mie nitachukua jukumu la kufungisha ndoa kati yako na FIAT, na kwa kuwa Mama yako wa kweli, nitaithibitisha ndoa hiyo kwa kukupatia mali ya posa ya Uhai wenyewe wa Mwanangu na kama zawadi, nitakupa Umama wangu na fadhila zangu zote.
Roho Anazungumza na Mama Malkia Wake:

Mama wa Mbinguni, yanipasa nikushukuru mara ngapi kwa pendo unalonipa mimi, na kwa kuwa katika kila kitu unachotenda umekuwa unanifikiria mimi daima, na pia kwa vile unaniandalia na kunipatia neema hizo ambazo kwazo Mbingu na dunia zinabaki kuduwaa, kushangaa na kuvutiwa pamoja nami, sasa wote kwa pamoja tunasema: “Asante! Asante!”. Lo, Mama Mtakatifu, chonga katika moyo wangu haya maneno yako matakatifu: “Fanya kile anachowaambia Mwananagu”, ili auanzishe ndani yangu Uhai wa Utashi wa Mungu ambao ninautamani na ninautaka kabisa. Na wewe Mama, ugonge mhuri juu ya utashi wangu wa kibinadamu kusudi upate kuwa daima chini ya mamlaka ya Utashi wa Mungu.

Sadaka Ndogo:

Katika matendo yetu yote tuwe tunaelekeza masikio yetu kumsikiliza Mama wa Mbinguni anayetuambia: “Fanyeni kile anachowaambia Mwanangu”, ili tufanye yote kwa ajili ya kutimiza Utashi wa Mungu.

Sala ya Mishale:

Mama Mtakatifu, uje moyoni mwangu na unitendee ule muujiza wa kuniwezesha nitawaliwe na kumilikiwa na Utashi wa Mungu.