JamiiForums
56.1K subscribers
32.9K photos
1.87K videos
30K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
KIJANA AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUBAKA MTOTO

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Igunga, Tabora, imemuhukumu Elius Mgashi (20) kwa kosa la kubaka mtoto wa kaka yake (14)

> Alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Septemba 14 na 19, 2018

Soma - https://jamii.app/JelaUbakajiMtoto
IRAN YAONYA VIKOSI VYA KIJESHI VYA KIGENI KUKAA NJE YA GHUBA YA UAJEMI

- Rais wa Iran, Hassan Rouhani ameonya kuwa vikosi vya nje vinatishia usalama wa eneo la Ghuba ya Uajemi

- Amesema vimesababisha uchungu na masikitiko, havipaswi kutumika katika Ghuba hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/IranVikosiKijeshiGhuba
MANYARA: MUME AJIUA BAADA YA KUMCHOMA MKE KISU NA KUMTOA UTUMBO

> Bwana mmoja maarufu 'Cheusi' amejiua kwa kunywa sumu baada ya kumpiga Anna Alphonce na kisha kumchoma kisu mpaka kumtoa utumbo

> Chanzo ni wivu wa mapenzi ambapo Anna naye amefariki usiku wa kuamkia leo

Soma - https://jamii.app/MeAjiuaKisuMke
IGP SIRRO ALALAMIKIA UNAFIKI NDANI YA JESHI LA POLISI

> Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania IGP Simon Sirro amesema tatizo linalolisumbua Jeshi la Polisi ni tabia ya unafiki na kusema kuwa yeye hakujichagua na wala hawawezi kuwa wawili kwenye nafasi moja

> Aidha, amelipongeza Jeshi kwa kukomesha mauaji ya raia yaliyokuwa yakitokea Kibiti, Pwani

Soma - https://jamii.app/SirroVsUnafikiPolisi
MAHAKAMA KUU, UINGEREZA: UAMUZI WA WAZIRI MKUU KUSIMAMISHA BUNGE NI KINYUME NA SHERIA

- Imesema Waziri Mkuu Boris Johnson alitenda kinyume na sheria alipositisha Bunge kwa muda wa wiki 5, na kusababisha Nchi kuingia katika mgogoro wa Kikatiba

Zaidi, soma https://jamii.app/MahakamaVsWaziriUK
SERIKALI IMEMWITA MWAKILISHI WA WHO KUFAFANUA TAARIFA ZINAZOSAMBAA

> Imemwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini ili kupata kwa kina hoja za Shirika hilo zinazosambaa kupitia vyombo vya habari

> Mwakilishi huyo amedaiwa kusisitiza kuwa Shirika hilo halijasema wala halina ushahidi wowote kuwa Tanzania kuna Ebola

Soma - https://jamii.app/TZSummonsWHORep
KENYA: SERIKALI YATAKA VIONGOZI WA MAKUNDI YA WHATSAPP KULIPIA LESENI

- Pendekezo lipo katika Muswada wa kurekebisha Sheria ya Habari na Mawasiliano

- Pia, watatakiwa kutunza rekodi za Wanakikundi na kuzikusanya kwa Mamlaka itakapohitajika

Zaidi, soma https://jamii.app/KEWhtAppGrpLicenses
INDONESIA: WANANCHI WACHOMA MAJENGO BAADA YA MWALIMU KUWATUKANA WANAFUNZI

> Maandamano ya vurugu katika jimbo la Papua, Mashariki mwa Indonesia yasababisha vifo 27 na kujeruhi 72

> Yamesababishwa na uvumi kwamba Mwalimu wa shule ya Upili aliwatukana wanafunzi kwa maneno ya Ubaguzi

Soma - https://jamii.app/DeathTollsPapua
KLABU BINGWA AFRIKA: ZAHERA ATAMBA KUIFUNGA ZESCO NYUMBANI

- Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema wanajiandaa kikamilifu kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco

- Anaamini mchezo utakuwa mgumu na Zesco haijawahi kupoteza nyumbani ila watahakikisha wanavunja mwiko huo
RWANDA: MWANASIASA MAARUFU WA UPINZANI AUAWA

- Kiongozi wa Chama cha FDU-Inkingi, Victoire Ingabire amesema Mratibu wa chama, Syridio Dusabumuremyi ameuawa kwa kuchomwa visu

- Idara ya upelelezi imesema imewakamata washukiwa 2 wa tukio hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/MratibuFDU-InkingiAuawa
JAMHURI YAWASILISHA MAPINGAMIZI KWENYE KESI YA WAGOMBEA KUPITA BILA KUPINGWA

- Ni katika kesi ya kupinga Wagombea wanaopitishwa bila kupingwa kutangazwa washindi

- Moja ya mapingamizi ni kuwa mfungua shauri hilo hana uhalali wa kufanya hivyo

Zaidi, soma https://jamii.app/JamhuriMapingaziKesiWagombea
JAJI WARIOBA: KUNA MATUKIO YANAYODHOOFISHA UMOJA NA UZALENDO WA TAIFA

> Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania amesema kuna dalili za uwepo wa matukio yanayodhoofisha umoja, uzalendo na mshikamano wa Taifa

> Amesema nguvu ya Tanzania ni umoja, mshikamano na uzalendo na kwamba ni muhimu tuvilinde

Soma - https://jamii.app/WariobaUmojaUzalendo
ALGERIA: VICHANGA WAPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA WODI KUUNGUA MOTO

> Watoto wachanga nane wamepoteza maisha, baada ya moto kuwaka kwenye Wodi ya wazazi eneo la Mashariki mwa Aljeria katika mji wa El Ouedo usiku wa kuamkia leo

> Walionusurika ni watoto 11, wanawake 107 na wafanyakazi 28, hadi kufikia alfajiri ya leo

Soma - https://jamii.app/NewbornDeadWardFire
SOKA: Klabu ya #Colchester imeiondoa Klabu ya #Tottenham kwenye kombe la #CarabaoCup kwa mikwaju ya Penalti 4 -3 baada ya kucheza dakika 90 bila kufungana

#THFC:
🔵 #CUFC:
WAZIRI MAHIGA: WASHTAKIWA WA UHUJUMU UCHUMI WAANZA KUOMBA MSAMAHA

- Waziri huyo wa Katiba na Sheria, amesema washtakiwa hao wameanza kutuma maombi kwa kasi

- Amesema DPP lazima ayachambue maombi hayo kwa kushirikiana na Idara ya Upelelezi

Zaidi, soma https://jamii.app/WahujumuUchumiMaombi
BUSEGA: MKURUGENZI NA WATUMISHI 3 WATUHUMIWA KWA UBADHIRIFU WA FEDHA

> Mkurugenzi Anderson Njiginya na wataalam 3 wa Idara ya Ardhi wametakiwa kurejesha Tsh. Milioni 55.58 ambazo zimetumika kulipa malipo hewa katika mradi wa upimaji na urasimishaji viwanja 3700

> Kiasi hicho kimebainika kulipa majina hewa ya wananchi walioingizwa ndani ya mradi, kulipa posho watumishi wasiohusika na mradi, pamoja na 'Double Payment' katika uendeshaji wa shughuli za mradi huo katika eneo moja

Soma - https://jamii.app/UbadhirifuMkgBusega
MAREKANI: UCHUNGUZI WA KUMUONDOA TRUMP MADARAKANI WAANZA

> Rais Donald Trump anatuhumiwa kuiomba Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa Joe Biden na pia anachunguzwa kutokana na vitendo vyake vingi vinavyovunja Katiba

> Baraza la Wawakilishi linamshutumu kwa kufanya matumizi mabaya ya madaraka

Soma - https://jamii.app/TrumpFormalImpeachment
RC SHINYANGA: KILICHOONEKANA MAENEO YA NDEMBEZI SIO VOLCANO

- Kilichotokea ni Volcano ya Tope ambayo hutoka ardhini ikiwa na joto la kawaida tofauti na Volcano ya Ujiuji

- Hali hiyo inatokana na mtikisiko na mgandamizo wa matabaka ya miamba

Zaidi, soma https://jamii.app/VolcanoTopeUfafanuzi-SHY
UTEUZI: MWENYEKITI WA BODI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU ATEULIWA

- Rais Magufuli amemteua Dkt. Amina Suleiman Msengwa kushika nafasi hiyo

- Dkt. Msengwa ni Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM)

Zaidi, soma https://jamii.app/UteuziAminaSuleiman