JamiiForums
55.9K subscribers
33.1K photos
1.93K videos
30.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JF EXCLUSIVE: MAURITIUS LEAKS NAME TANZANIA COMPANIES

> It has been revealed that at least four companies in Tanzania are in Mauritius Leaks – for now we are publishing one company, while continuing to track others

Continue reading > https://jamii.app/MauritiusLeaks1

#MauritiusLeaks
MWANZA: WATU 4 AKIWEMO AFISA MFAWIDHI WA RASILIMALI ZA UVUVI WAUAWA

> Wameuawa katika vurugu kati ya wakazi wa kisiwa cha Siza na Askari wa Jeshi la Polisi

> Afisa huyo wa Kanda ya Ukerewe amefariki dunia baada ya kupigwa na Wananchi

Soma => https://jamii.app/AfisaUvuviAuawa
KENYA: SERIKALI KUKAGUA WANAUME KAMA WAMETAHIRIWA

> Wizara ya Afya imesema uchunguzi huo unaoendeshwa na Shirika la Wanaume Kutahiriwa kwa Hiari (VMMC), unalenga kuimarisha vita dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi

> Uchunguzi huo unaolenga pia kufahamu idadi ya wanaume waliotahiriwa katika kaunti za Homa Bay, Kisumu, Siaya na Migori na utafanyika kwa miezi mitatu

Soma - https://jamii.app/UkaguziToharaMe
AFYA: Tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja; yaani vitamini, protini, wanga na mafuta

- Baadhi ya faida za tende ni kurekebisha matatizo ya tumbo, kuimarisha moyo, kuongeza nguvu na stamina ya kufanya mapenzi na kuongeza virutubisho kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha

Pata somo hili hapa => https://jamii.app/Afya-Tende
ARUSHA: WANANCHI WALALAMIKIA MALORI KUEGESHWA BARABARANI MUDA MREFU

> Wafanyabiashara na Watumiaji wa barabara katika mtaa wa Pare (Moivo) wamelalamikia kero ya magari Makubwa aina ya Fuso kuegeshwa barabarani kwa muda mrefu na kusababisha adha kubwa kwa watumiaji wa barabara

> Wamedai kuwa jambo hilo limekuwa la muda mrefu lakini wanasikitishwa kwa kutopatiwa ufumbuzi na mamlaka husika

Soma - https://jamii.app/KeroMaloriBarabarani
MICHEZO: Tamasha la ‘Simba Day’, linatarajiwa kurudishwa nyuma kutokana kuingiliana na ratiba ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo ya Msumbiji

> Simba wataanzia ugenini kucheza na timu hiyo ktk mchezo wa awali utakaochezwa Agosti 9, 2019

#JFMichezo
MAHAKAMA KUU ZANZIBAR KUFUTA KESI ZISIZOKAMILIKA USHAHIDI

> Ziara iliyofanywa hivi karibuni na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, imebaini mrundikano wa Mahabusu unaotokana na kusita kuendelea kwa kesi zao Mahakamani kwa kile kinachoelezwa kuwa ushahidi haujakamilika

> Aidha, sababu nyingine ya uwepo wa mrundikano wa Mahabusu unatokana na kuwekwa kwa masharti magumu ya dhamana

Soma - https://jamii.app/MudaUpeleleziKesi
KENYA: WAZIRI WA FEDHA NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

> Waziri Henry Rotich, Katibu wa Wizara hiyo na wenzao wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Milimani kujibu mashtaka yanayowakabili ya matumizi mabaya ya ofisi, kuanzisha mradi bila kuwa na mpango mahususi wa kuutekeleza, kukiuka taratibu za manunuzi na kula njama ili kujipatia fedha kinyume cha taratibu

Soma - https://jamii.app/RotichInCourt
POLISI NA TCRA KUCHUNGUZA SAUTI ZINAZODAIWA KUWA ZA VIONGOZI CCM

> Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema wanafanya uchunguzi wa sauti zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa kuwa ni za baadhi ya viongozi wastaafu wa CCM na Serikali

> Aidha, Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ameeleza kuwa suala hilo wamewaachia Jeshi la Polisi kwa kuwa ni jinai

Soma - https://jamii.app/UchunguziSautiViongozi
KUTEKWA MO DEWJI: HATI YA KUKAMATWA KWA RAIA 5 WA KIGENI YATOLEWA

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kuwakamata raia 4 wa Msumbiji na 1 wa Afrika Kusini ili wafikishwe kizimbani na kuunganishwa katika mashtaka ya kumteka Mfanyabiashara Mohammed Dewji

> Wanaosakwa ni Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issa Tomo, Zacarious Junior na raia wa Afrika Kusini, Phila Tshabalala

Soma - https://jamii.app/ForeignersDewjiAbduction
UINGEREZA: BORIS JOHNSON ATARAJIWA KUWA WAZIRI MKUU MPYA

> Hii ni baada ya kuchaguliwa kuwa kiongozi mpya wa Chama cha Wahafidhina (Conservative)

> Johnson amepata kura 92,153 dhidi ya kura 46,656 alizozipata Jeremy Hunt

Soma > https://jamii.app/BorisKiongoziTory
MALINZI NA MWESIGA WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU

> Wengine ni aliyekuwa Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, na aliyekuwa Karani, Flora Rauya

> Aidha, aliyekuwa Meneja wa TFF, Mariam Zayumba ameachiwa huru. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 6, 2019

Soma > https://jamii.app/Malinzi-MwesigaKesi
KENYA: WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI WATAKA KUMUUA MWENZAO KISA MAPENZI

> Wanafunzi 3 wa shule ya upili ya wasichana ya Makueni wanazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Makueni kwa jaribio la kumuua mwenzao kwa kumuwekea sumu kwenye chakula

> Walitumia kemikali walizoiba katika maabara ya shule ili kumuua Faustine Kivuva(15) anayemng’ang’ania mvulana wa shule ya wavulana ya Makueni

Soma https://jamii.app/WanafunziMauajiMpnz
AFRIKA KUSINI: MAHAKAMA YAIZUIA SERIKALI YA ZAMBIA KUIUZA KAMPUNI YA UCHIMBAJI WA SHABA YA KONKOLA

> Uamuzi umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu, Leicester Adams

> Serikali ya Zambia imemshauri Mwanasheria Mkuu kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo

Soma > https://jamii.app/KMCVsZambiaGvt
IKULU, DAR: RAIS MAGUFULI KUSHUHUDIA MAKABIDHIANO YA DHAHABU

- Atashuhudia makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa nchini Kenya itakayowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais Kenyatta

- Makabidhiano hayo yatafanyika leo kuanzia saa 4:00 asubuhi

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliKupokeaDhahabu-KE
ZANZIBAR: WATU 8 WAHOFIWA KUFA BAADA YA BOTI KUPOTEA BAHARINI

> Upepo mkali uliotoka jana katika mji wa Mcheweni Pemba umepelekea kupotea kwa boti mbili zikiwa na jumla ya watu 8

> Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba amesema licha ya juhudi za uokozi lakini bado watu hao hawajaonekana wala hawajapata taarifa yoyote hadi sasa

Soma - https://jamii.app/KupoteaBotiUpepo
KENYA: MUME AMCHOMA KISU 'HOUSEBOY' BAADA YA KUMFUMANIA NA MKE WAKE

> Kijana huyo mkazi katika Kaunti ya Kirinyaga maisha yake yako hatarini baada ya kuchomwa kisu na bosi wake ambaye alimkuta kitandani na mkewe

> Inadaiwa mume huyo aliondoka kuelekea kazini, lakini akagundua alikuwa amesahau kitambulisho ndipo alishangaa kumkuta mfanyakazi huyo kitandani na mkewe

Soma - https://jamii.app/BosiKisuHouseboy
IMF: UCHUMI WA DUNIA WAZIDI KUDORORORA

> Ripoti mpya ya robo mwaka ya Shirika la Fedha Duniani, imeonesha ukuaji mdogo wa uchumi kidunia huku ikionya kuhusu vita vya kibiashara

> Uchumi wa dunia umeendelea kukua kwa kasi ndogo ambapo katika mwaka 2019 unatarajiwa utakuwa kwa 3.2% na 3.5% kwa mwaka 2020

Soma - https://jamii.app/DecreaseWorldEconomy
SUDAN: WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAANDAMANA KUPINGA UTAWALA

> Wanashinikiza kupatikana kwa haki kwa wanafunzi wenzao waliouawa wakati wa maandamano ya kuuangusha utawala wa Rais Omar al-Bashir

> Baadhi ya wanafunzi hawataki kulipwa fidia na Serikali, badala yake wanataka waliohusika wauawe kama walivyouawa wenzao

Soma - https://jamii.app/UnivStudentsRiots