JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VENEZUELA: WAFUNGWA 25 WAFARIKI BAADA YA KUZUKA KWA GHASIA GEREZANI

> Ghasia hizo zimetokea katika gereza la Acarigua ambalo lilijengwa kwa ajili ya Wafungwa 250 lakini kwa sasa lina Wafungwa 540

> Katika tukio hilo Askari 20 wamejeruhiwa

Soma > https://jamii.app/VifoGerezaVenezuela
DR CONGO: Rais Felix Tshisekedi amemteua Robert Kidiaba kuwa Waziri wa Michezo

- Robert Kidiaba aliwahi kuwa mlinda mlango wa TP Mazembe na Timu ya Taifa ya DRC

- Januari 2019, Kidiaba alishinda Ubunge wa Jimbo la Katanga

Zaidi, soma > https://jamii.app/KidiabaWaziriDRC

#JFLeo #JFSports
MADIWANI WATAKA MUONGOZO WA KUFUNGUA MADAI YA MALIPO YA KOROSHO

> Wamemtaka Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee, kutoa kauli ya kuwahakikishia ni lini wakulima watalipwa kwa kuwa madiwani hukosa majibu ya uhakika kwenye mikutano ya maendeleo ya kata (WDC), na wanashangazwa kutotekelezwa kwa ahadi ya Serikali ya kuwalipa wenye chini ya kilo 1,500

Soma - https://jamii.app/MadaiMalipoKorosho
UMOJA WA ULAYA: KUJIUZULU KWA MAY HAKUTABADILI MPANGO WA BREXIT

> Umoja wa Ulaya umesema kuwa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza hakutobadili chochote kwenye msimamo wake wa makubaliano yaliyofikiwa kuiwezesha Uingereza kujiondoa kwenye Umoja huo

Soma - https://jamii.app/AUBrexitProceeds
MAMA WA KAMBO AMCHOMA MTOTO KWA MAJI YA MOTO

> Binti mwenye umri wa miaka 16 (jina limehifadhiwa) katika Manispaa ya Bukoba amelazwa katika Hospitali ya rufaa akiuguza majeraha anayodai kuyapata baada ya kuunguzwa kwa maji ya moto na mama yake wa kambo baada ya kumkuta akiwa amepika viazi bila kuambiwa

Soma - https://jamii.app/AchomwaMajiMoto
SERIKALI YATOA MUONGOZO KWA WAKAGUZI WA MIFUKO YA PLASTIKI

> Wakaguzi wameagizwa kutotumia nguvu ikiwemo kuwapiga au kuwabeba watu na kuwaweka ndani

> Haitakiwi kuwasimamisha watu au mtu na kumpekua au kupekua mizigo yake ili kutafuta mifuko ya plastiki

> Wakaguzi wanatakiwa kufanya ukaguzi madukani, magengeni, viwandani, masokoni, mipakani, kwenye maduka makubwa na sio kwenye makazi ya watu au magari

Soma - https://jamii.app/UkaguziMifukoPlastiki
KENYA: ZAIDI YA WAVUVI 100 KUTOKA TANZANIA WANASHIKILIWA KENYA

> Wanashikiliwa ktk Kaunti ya Kilifi kwa tuhuma za kuvuka mipaka ya uvuvi

> Wamekamatwa katika maeneo ya ziwa ya Kilifi, Watamu, Wesa, Ngomeni, Malindi, Uyombo, Mayungu na Kipini

Soma > https://jamii.app/WavuviTzVsKenya
JAFO: SHULE YA ASHIRA ILICHOMWA MOTO KWASABABU ZA HUJUMA

> Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), amesema moto ulioteketeza mabweni mawili ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira umesababishwa na hujuma na ameagiza ufanyike uchunguzi wa kina na kwa haraka ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria

Soma - https://jamii.app/HujumaMotoAshiraSec
PAPUA NEW GUINEA: WAZIRI MKUU AJIUZULU

> Peter O’Neill amejiuzulu baada ya kutofautiana na Wabunge wa chama chake wakidai ameshindwa kuongoza vema na kupelekea uchumi kushuka na hali ngumu ya maisha

> Sir Julius Chan atachukua nafasi hiyo

Soma https://jamii.app/PMResignsPNG
MALAWI: MAHAKAMA KUU YAAMURU KURA KUHESABIWA UPYA

> Imeamuru kutotangazwa matokeo ya Urais hadi kura ktk Majimbo 10 zirudiwe kuhesabiwa

> Ni baada ya chama kikuu cha upinzani, Malawi Congress Party(MCP) kwenda kushitaki wakidai kura kuibwa

Soma https://jamii.app/MalawiVoteRecount
SINGIDA: MWALIMU WA MADRASA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA

> Daudi Idd Karata(26) amepewa hukumu hiyo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida kwa hatia ya kumnajisi Mtoto wa kike(8)

> Ajitetea kuwa yeye ni Mwalimu wa Dini na hawezi kutenda kosa hilo

Soma > https://jamii.app/JelaUnajisiMtoto
MAFURIKO BUKOBA: Mvua zinazoendelea kunyesha, zimesababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara baada ya daraja la Kanoni kufunikwa na maji

- Daraja la Kanoni ndilo linalounganisha barabara Kuu ya kwenda mikoani, lipo Hamugembe

Soma https://jamii.app/MafurikoBukoba
KENYA: KIJANA MBARONI KWA KUMPIGA MPENZI WA MAMA YAKE

- Mwenyekiti wa Polisi Jamii amesema, mtuhumiwa alimfuata mwanaume huyo na kumtaka amueleze kwanini yupo kwenye mahusiano na mamake huku akijua ameolewa

- Majeruhi amepelekwa hospitali

Soma > https://jamii.app/AmpigaMpenziMama
AFRIKA KUSINI YAAHIDI KUAJIRI WALIMU WA KISWAHILI KUTOKA TANZANIA

> Katika Mazungumzo na Rais Magufuli, Rais Ramaphosa amesema nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili wafundishe somo hilo katika shule za msingi na sekondari

Soma https://jamii.app/SwahiliTeachersSATZ
BRAZIL: WAFUNGWA 15 WAFARIKI KWENYE VURUGU ZILIZOTOKEA GEREZANI

- Wamefariki jana Mei 26 katika gereza moja lililopo kwenye jimbo la Amazonas baada ya vurugu baina yao(Wafungwa) kuzuka

- Walifariki ama kwa kukosa hewa au kuchomwa na vitu vya ncha kali ikiwemo miswaki

Zaidi, soma https://jamii.app/RiotBrazilPrison15Dead
IRAQ: WANACHAMA 3 WA DOLA YA KIISLAMU WAHUKUMIWA KUNYONGWA

- Mahakama moja nchini humo jana iliwahukumu kifo wanachama hao ambao ni raia wa Ufaransa

- Watuhumiwa hao ni miongoni mwa Wafaransa 13 waliokamatwa katika mapambano huko Syria

Zaidi, soma https://jamii.app/Wafaransa3KunyongwaIraq
UCHUMI: SEKTA ZINAZOONGOZA KWA KUTAKATISHA FEDHA ZATAJWA

> Ripoti ya Utakatishaji Fedha na Ugaidi ya mwaka 2016 iliyotolewa hivi karibuni imezitaja sekta zinazoongoza ni biashara ya magari, maduka ya kubadilishia fedha, biashara ya nyumba na madini

Zaidi, soma > https://jamii.app/SektaUtakatishajiFedha
TANGA: ANAYEDAIWA KUWA MGONJWA WA AKILI AUAWA BAADA YA KUUA WATU 2

- Mgonjwa huyo anayedaiwa kutoroka kwa mganga wa kienyeji amewaua Wanakijiji wa Kilometa 7, Wilayani Muheza

- Aliwaua kwa kuwapiga kwa fimbo huku yeye akiuawa na Wananchi

Zaidi, soma https://jamii.app/MgonjwaAkiliAua2-TA
RAIS MAGUFULI AONDOKA AFRIKA KUSINI, AELEKEA NAMIBIA

- Ameelekea Windhoek, Namibia baada ya kushuhudia kuapishwa kwa Rais Cyril Ramaphosa na kuzungumza naye

- Atafanya ziara rasmi nchini Namibia kutokana na mwaliko wa Rais Hage Geingob

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAendaNamibia