JamiiForums
55.9K subscribers
33.1K photos
1.92K videos
30.1K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
URUSI YAAZIMIA KUUNDA 'INTERNET' YAKE

- Bunge limepitisha muswada ambao ukiwa sheria, Taifa hilo litaunda Internet yake na kuacha kutumia inayotumika duniani

- Ni ili kujilinda na mashambulio ikiwemo kuzimiwa Internet na Mataifa yenye uwezo

Zaidi, soma https://jamii.app/RussiaUnplugInternet
SERIKALI: HAKUNA HAJA YA KUBADILI MUDA WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

- Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha amesema muda wa miaka 7 si kitu kibaya

- Amesema Serikali haijavunja sheria kwa hatua hiyo na inazingatia ubora wa elimu

Soma https://jamii.app/MudaElimuMsingi
KAKAMEGA, KENYA: MAPACHA WALIOTENGANISHWA WAKUTANA BAADA YA MIAKA 19

> Walizaliwa Agosti 15 mwaka 1999 katika Hospitali ya Kakamega ambayo kwa sasa ni Hospitali ya Rufaa

> Mama yao aliporuhusiwa kutoka Hospitali, alipewa Watoto 2 mmoja akiwa si wake

Zaidi kuhusu kisa hiki, soma > https://jamii.app/MapachaKakamega
RAIS WA TFF AKANUSHA KUPOKEA RUSHWA KUTOKA KWA RAIS WA CAF

- Wallace Karia amekanusha kuwa miongoni mwa waliopokea rushwa ya Tsh. Milioni 46 kutoka kwa Rais wa CAF, Ahmad Ahmad

- Amesema hakuwepo madarakani wakati uchaguzi wa CAF unafanyika

Zaidi, soma https://jamii.app/MadaiRushwaKariaTFF
RAIS MAGUFULI ATOA WIKI 1 TARATIBU ZA UWEKEZAJI KWA KAMPUNI YA SIT ZIKAMILIKE

- Ameziagiza Wizara ya Ardhi na Wizara ya Viwanda kukamilisha uwekezaji wa Kampuni ya Sugar Investment Trust(SIT) iliyocheleweshwa kuwekeza katika uzalishaji wa sukari tangu mwaka 2017

Zaidi, soma https://jamii.app/UwekezajiKampuniSIT
PERU: RAIS WA ZAMANI AJIUA KWA RISASI POLISI WALIPOTAKA KUMKAMATA

- Alan Garcia(69) amefariki baada ya kujipiga risasi kichwani leo wakati Polisi walipofika nyumbani kwake katika mji wa Lima kumkamata kwa kumuhusisha na vitendo vya rushwa

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisAjiuaAsikamatwePolisi-PERU
TotalAFCONU17: Mchezo kati ya timu ya UgandaU17 na timu ya TanzaniaU17(Serengeti Boys) umemalizika

- UgandaU17 imeibuka na ushindi wa goli 3-0, magoli yaliyofungwa na Kawooya Andrew katika dakika za 16 na 28 pamoja na Najib Yiga aliyefunga goli lake dakika ya 77
KENYA: UWANJA WA NDEGE WAFUNGWA KWA MUDA KUTOKANA NA TAHADHARI YA BOMU

- Ni Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta uliofungwa leo majira ya saa 7:00 mchana

- Ni baada ya abiria kwenye ndege ya Shirika la Kenya(KQ) kutamka neno “bomu”

Zaidi, soma https://jamii.app/JKIABombThreat
TRA: MWISHO WA MATUMIZI YA STEMPU ZA KARATASI NI APRILI 30, 2019

- TRA imepiga marufuku matumizi ya stempu za karatasi kwa bidhaa zote za sigara, pombe kali, mvinyo, bia na aina zote za vileo zenye stempu zisizo za kielektroniki

Zaidi, soma https://jamii.app/TRAStempuKaratasiMwisho
UEFA Champions: Mpira ni dakika ya 80, Man City wanaongoza kwa Goli 4 dhidi ya 3 za Spurs | On Aggr 4-4

> Matokeo ya mwisho yataamua nani anasonga mbele

#MCITOT #UCL
FT Results #UCL #PORLIV #MCIVSTOT #MCTOT | Liverpool & Spurs zinasonga mbele
MADEIRA, URENO: WATALII 28 KUTOKA UJERUMANI WAFARIKI KATIKA AJALI

> Wamefariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka

> Watu 21 wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu katika hospitali moja huko Santa Cruz

Soma > https://jamii.app/AjaliMadeira
KENYA: MAMA MWENYE NYUMBA AMUUA MPANGAJI WAKE KWA DENI LA TSH. 11,400/=

> Loice Kasembeli(Mama Kelele) anashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na mauaji ya mpangaji wake(Mwanaume)

> Maiti yakutwa ndani ya nyumba yake ikiwa na majeraha shingoni

Soma > https://jamii.app/LandladyKillTenant
TETEMEKO LA UKUBWA WA 6.1 KWENYE KIPIMO CHA RICHA LAIKUMBA TAIWAN

> Tetemeko hilo limetokea saa 7:01 mchana kwa saa za Taiwan

> Huduma za usafiri wa treni zimesitishwa katika Jiji la Taipei kutokana na tetemeko hilo

Zaidi, soma => https://jamii.app/TetemekoTaiwanHualien
IMF YAILAUMU TANZANIA KWA KUTOCHAPISHA MATOKEO YA UTAFITI

> Machi 18/2019, IMF ilifanya kikao cha mashauriano kuhusu hali ya uchumi na Tanzania

> IMF imeeleza kuwa mpaka sasa Mamlaka za Tanzania hazijachapisha taarifa ya kikao hicho

Soma > https://jamii.app/IMFVsTanzaniaGvt
TOZO YA KUPIMA, KURASIMISHA MAKAZI KISHA KUPATA HATI YA KIWANJA, YASHUSHWA

- Waziri wa Ardhi, William Lukuvi ameshusha tozo hiyo kutoka Tsh. 250,000 hadi Tsh. 150,000

- Amesema lengo la Serikali ni kutoa hati 500,000 ndani ya miezi mitatu

Zaidi, soma https://jamii.app/TozoUrasimishajiMakazi
KENYA: WAFANYAKAZI 52 WA HOSPITALI YA NAIROBI WAUGUA KIPINDUPINDU

- Idadi hiyo imeripotiwa leo kutokea 23 iliyoripotiwa awali na wote wamelazwa hospitalini

- Wataalamu wa afya wametembelea hospitali hiyo kuchunguza chanzo na namna ya kuzuia

Zaidi, soma https://jamii.app/NairobiHospitalCholera
MAREKANI: WANASAYANSI WAFUFUA UBONGO WA NGURUWE ALIYEKUFA

- Wamefufua ubongo huo ikiwa ni saa nne baada ya mnyama huyo kuchinjwa

- Utafiti huo unaonesha kufa kwa seli za ubongo kunaweza kuzuiwa na baadhi ya mifumo kwenye ubongo kuunganishwa

Zaidi, soma https://jamii.app/SayansiYafufuaNguruwe
JOSEPH MBILINYI(SUGU) AGOMA KUSOMA HOTUBA AKIDAI 80% YA MANENO YAMEONDOLEWA

- Agoma kusoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari kutoka kambi ya Upinzani Bungeni

- Naibu Spika, Dkt. Tulia amesema maneno hayo yalikuwa yakikiuka kanuni za Bunge

Zaidi, soma https://jamii.app/SuguAgomeaHotuba
TABORA: MTOTO ATUPWA CHOONI KATIKA SHULE YA SEKONDARI KAZIMA

- Mtoto huyo anayekadiriwa kuwa na siku 1 amekutwa kwenye choo cha Wasichana

- Aidha, Mkuu wa shule amesema huenda aliyefanya hivyo ni Mwananchi kwani Wanafunzi wake hupimwa mimba

Zaidi, soma https://jamii.app/MtotoAtupwaChooni-TBR