JamiiForums
55.8K subscribers
33.1K photos
1.94K videos
30.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFRIKA KUSINI: WAGENI WAKESHA VITUO VYA POLISI KUKWEPA KUUAWA

> Watu 3 wameuawa huku takribani wengine 50 wakitafuta hifadhi kwenye vituo vya Polisi katika mji wa Durban kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na baadhi ya raia wa Afrika Kusini, wanaopinga uwepo wa wageni nchini humo wakidai wanamaliza ajira

> Tukio hilo limetokea leo, Aprili 1

Zaidi, soma https://jamii.app/NativesVsForeignersSA
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RAIS MAGUFULI AFIKA KUMPA POLE MBUNGE WA IRINGA MJINI KWA KUFIWA

- Akiwa na Mke wake, Janeth Magufuli wametoa mkono wa pole kwa familia na heshima za mwisho kwa mwili wa Tryphosa Sanga aliyekuwa dada wa Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliMsibaDadaMsigwa
FAHAMU KUHUSU MAUMIVU YA KIUNO, MGONGO NA NYONGA

> Tatizo hili huweza kumpata mtu yeyote na huweza kusababishwa na namna mbaya ya kulala/godoro, Kubeba mizigo kwa kuinama, Kulala kwa muda mrefu na matumizi mabaya ya Mto, UTI sugu na Umri-kuzeeka

> Ukipuuza maumivu haya hupelekea kushindwa kufanya tendo la ndoa, kupooza kwa baadhi ya viungo na unaweza kushindwa kutembea au kunyanyuka endapo umekaa au umelala

Tembelea - https://jamii.app/MaumivuKiunoNyonga
#JFAfya
MUUAJI WA KIM JONG NAM KUACHIWA MEI BAADA YA KUKAA MAHABUSU MIAKA 2

> Mwanamke mmoja (30) raia wa Vietnam anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya Kim Jong-Nam ambaye ni kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 3 gerezani na ataachiwa mwezi ujao, baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka miwili

Soma - https://jamii.app/KimNamMurderTrial
#JFInternational
JamiiForums pinned a video
MADUKA 82 KATI YA 87 YA KUBADILI FEDHA JIJINI DAR YALIKUWA NA VIASHIRIA VYA KUTAKATISHA FEDHA

- Hayo yamebinishwa na Gavana wa BoT, Prof. Florens Luoga aliyeongeza kuwa Maduka hayo yalibainika katika uchunguzi ambao unaendelea bado nchini kote

Zaidi, soma https://jamii.app/MadukaFedha82KiukaSheria
KENYA: GAVANA WA SAMBURU AMEKAMATWA NA TUME YA KUPAMBANA NA RUSHWA

- Gavana Moses Lenolkulal amekamatwa na Tume hiyo na kuzuiliwa katika katika Makao Makuu ya Tume

- Inaelezwa ni kwasababu ya sakata la kifisadi la mafuta lililogharimu Ksh. Milioni 84(Tsh. 1,680,000,000)

Zaidi, soma https://jamii.app/SamburuGovernorArrestedKE
KIFO CHA MSANII NIPSEY HUSSLE: LAPD YADAI KUMUONA MSHTAKIWA NA INAMTAFUTA

- Aliyempiga risasi anahusishwa na makundi ya kihuni(gang)

- Nipsey alikuwa anaandaa makala inayomuhusu Dr. Sebi, wengine wanaamini inaweza kuwa sababu ya kifo chake

Zaidi, soma https://jamii.app/NipseyDeath
REA YAPEWA SIKU 28 KUFIKISHA NA KUWASHA UMEME KYELA

> Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa siku 28 kwa Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini(REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha ujenzi wa njia ya umeme(Km 20) na kuwashwa kwenye Kata za Nkokwa na Ipande

Zaidi, soma https://jamii.app/REAUmemeKyela
RAIS MAGUFULI KUWASILI MKOANI MTWARA KATIKA ZIARA YA SIKU 2

- Anatarajiwa kuwasili mkoani humo leo Aprili 02 majira ya asubuhi kwa ziara ya kikazi

- Ataweka jiwe la msingi la upanuzi wa Uwanja wa ndege na kuzungumza na Wananchi

Zaidi, soma https://jamii.app/ZiaraMagufuliMtwara
KAMATI YA BUNGE YA MAADILI IMEMTIA HATIANI CAG

- Mwenyekiti wa Kamati, Emmanuel Mwakasaka amesema Prof. Mussa Assad ametiwa hatiani kuhusu kauli yake ya 'udhaifu wa Bunge'

- Alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya UN

Zaidi, soma https://jamii.app/CAGAtiwaHatiani
GARI LA MAFUNDI WA UMEME LAPATA AJALI

> Takribani watu 3 wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa ktk ajali ya gari la mafundi wa mradi wa kuzalisha umeme Mto Kagera eneo la Rusumo Wilayani Ngara

> Umeme huo ni kwa ajili ya Tanzania, Rwanda na Burundi
MAREKANI YASITISHA MISAADA AMERIKA YA KUSINI

> Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitisha misaada kwa mataifa matatu katika bara la Amerika Kusini ambayo ni Guatemala, Honduras na Salvador

> Mataifa hayo yalishindwa kuwazuia raia wao kuingia nchini Marekani kinyume cha sheria

Soma - https://jamii.app/USCutsAidsCA
#JFInternational
1
2
3
4