JamiiForums
56K subscribers
33K photos
1.91K videos
30.1K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
JE, TUENDELEE KUWAZIKA WAFU AU TUANZE KUWACHOMA MOTO?

> Mdau wa JamiiForums anasema kuwa Watanzania tunaongezeka kwa kasi sana huku eneo la ardhi likibaki kuwa lile lile

> Muda mwingine Serikali hulazimika kuhamisha makaburi ili kupisha miradi ya maendeleo

Soma ~ https://jamii.app/KuzikaVsKuchomaMoto
LINDI: SERIKALI YAAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE KWENYE FEDHA ZA MIRADI YA UJENZI

> Milioni 700 za ukarabati wa Hospitali ya Nachingwea hazijatumika hadi leo

> Milioni 400 za ujenzi Kituo cha Afya Kilimarondo zimeisha na ujenzi haujakamilika

Soma ~ https://jamii.app/UchunguziFedhaNachingwea
AUAWA AKIJARIBU KUZUIA MSICHANA KUBAKWA

- Mkazi wa kijiji cha Mnolela, Wilayani Lindi, Issa Selemani(62) auawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana

- Alikuwa akizuia Mwanafunzi(12) wa darasa la 5 shule ya msingi Nikowela asibakwe

Zaidi, soma https://jamii.app/AuawaAkizuiaUbakaji
SHIRIKA LA MARIE STOPES LATAKIWA KUACHA KUTOA HUDUMA YA UTOAJI WA MIMBA

> Bodi ya Madaktari(Kenya) imelitaka shirika hilo kuondoa matangazo ya utoaji mimba ktk tovuti zake

> Upande wa Tanzania wasema hawajawahi kuhusika na shughuli hizo.

Soma ~ https://jamii.app/KenyaVsMarieStopes
CANADA NJIA PANDA KUHUSU KUTOA MISAADA KWA TANZANIA

- Gazeti la 'The Globe and Mail' limeripoti nchi hiyo inatafakari iwapo izuie misaada kwa Tanzania ila inahofia kuadhibu raia wasio na hatia

- Sababu ni sakata la ushoga na mambo ya kisiasa

Zaidi, soma https://jamii.app/CanadaAid-Tanzania
LESOTHO vs TANZANIA: WAZIRI MWAKYEMBE AJIPANGA KUJIELEZA KWA RAIS MAFUGULI

- Asema atamueleza Rais kuwa kufungwa bao 1 kwenye mchezo huo ni bahati mbaya

- Aeleza "Milioni 50 tulizopewa zimesaidia kufungwa bao 1 tu pengine tungefungwa hata 6"

Zaidi, soma https://jamii.app/MwakyembeStarsMagufuli
WAVUVI KUTOKA TANZANIA WARIPOTIWA KUKAMATWA NCHINI KENYA

> Mamlaka ya nchi ya Kenya zawakamata Wavuvi 16 raia wa Tanzania kwa tuhuma za kuvuka mpaka na kutumia vifaa haramu vya uvuvi

> Wamekamatwa ufukwe wa Ziwa Victoria Kaunti ya Migori

Soma ~ https://jamii.app/TZFishermensArrested
KAMPUNI YA NDEGE YA FAST JET PLC KUJIONDOA KATIKA SOKO LA TANZANIA

- Kampuni ya Fastjet Plc iliyoorodheshwa katika soko la hisa la London, Uingereza inatarajia kuuza hisa zake 49% zilizopo katika Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania

Soma https://jamii.app/FastJetPlcKuuzaHisa
JE, WAJUA KUNA SIKU YA WANAUME DUNIANI?

- Novemba 19 ni siku ya Wanaume duniani kama ilivyo Machi 8 siku ya Wanawake duniani

- Baadhi ya malengo ni kuhamasisha utu, kutilia mkazo hali ya afya kwa Wanaume na kuboresha mahusiano ya kijinsia

Zaidi, soma https://jamii.app/SikuWanaume-Nov19
ARUSHA: MADUKA YA KUBADILI FEDHA ZA KIGENI YADAIWA KUWEKWA CHINI YA ULINZI

- Ulinzi mkali umeimarishwa kwenye maduka karibu yote yanayohusika na biashara ya hiyo

- Yadaiwa kuna operesheni maalum ambayo bado haijafahamika inahusu nini

Zaidi, soma https://jamii.app/ArushaForexShops
AFYA: Je, wafahamu faida za tunda la papai?

> Hupunguza kuganda kwa damu, hupunguza hatari ya kupata kansa ya kibofu na juisi yake hujenga kinga ya mwili na kuzuia magonjwa ya moyo.

> Pia, mbegu za papai hutibu homa ya matumbo(Typhoid)

Jifunze zaidi | Tembelea https://jamii.app/FaidaJuisiPapai
MBARONI KWA KUGHUSHI RISITI YA MALIPO YA KOROSHO

- Ni karani Chama Msingi cha Makonga, Asma Rajab na Mohammed Namkunga anayedaiwa kuwa mpenzi wake

- Inadaiwa Namkunga alikwenda na viroba 2 ila Asma aliandika kwenye cheti amepeleka kilo 200

Zaidi, soma https://jamii.app/WaghushiRisitiKorosho
WAASI WA HOUTHI WATANGAZA KUSITISHA MAPIGANO YEMEN

- Ni mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia

- Watafanya hivyo iwapo majeshi ya Saudi na washirika wake yanataka amani

Zaidi, soma https://jamii.app/WaasiMapiganoYemen
MWANDISHI WA VITABU CHINA, AFUNGWA JELA MIAKA 10

- Mwandishi Liu ambaye ni Mwanamke alihukumiwa kwa kuandika na kuuza kitabu chenye maudhui ya mapenzi ya jinsia moja

- Kutengeneza na kusambaza maudhui ya ngono ni kinyume cha sheria China

Zaidi, soma https://jamii.app/MwandishiAfungwaJelaCHN
SHERIA YA KUMFUNGA ALIYEMPA MIMBA MWANAFUNZI MIAKA 30 ILITUNGWA KIMIHEMKO

- RC Mtwara, Gelasius Byakanwa asema SOSPA ilitungwa kwa jazba na mihemko ya Wanaharakati sababu haimuwajibishi mtoto wa kike

- Pia yamfanya mtoto akue bila mzazi mmoja

Zaidi, soma https://jamii.app/SOSPAIlitungwaKimihemko
ELIMU YA KODI YATAJWA KUWA KATIKA MCHAKATO WA KUINGIZWA KWENYE MTAALA WA ELIMU

> TRA yasema iko katika mchakato wa kuhakikisha elimu ya kodi inafundishwa kuanzia madarasa ya chini.

> Yasema wafanyabiashara wengi huona kulipa kodi ni mzigo

Soma ~ https://jamii.app/ElimuYaKodi
SAKATA LA KUHAMA KWA MBUNGE KATANI(CUF): JAMES MBATIA ATAJWA KUWA CHACHU YA KUMSIHI ASIHAME

> Mbunge wa Vunjo(NCCR), James Mbatia ameeleza kuwa Katani alimwambia anataka kuchukua uamuzi mgumu kwasababu anaona giza ndani ya CUF.

Zaidi, soma => https://jamii.app/KujiuzuluKatani