JamiiForums
56.2K subscribers
32.8K photos
1.85K videos
30K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
MWANAUME WA MIAKA 69 ATAKA MAHAKAMA AMRUDISHIE UMRI WA MIAKA 49

> Emile Ratelband amehoji: kama inawezekana kubadili jina kwanini asiruhusiwe kubadili umri?

> Asema badiliko hilo litamsaidia kuwa na mahusiano na Wanawake vijana zaidi

Soma ~ https://jamii.app/EmileChangingAge
SERIKALI IMEANZA KUJENGA DARAJA JIPYA LA MTO WAMI

- Mkandarasi Power Construction Corporation kutoka China amesaini mkataba tangu Juni 28 mwaka huu

- Litakuwa na urefu wa mita 513.5 na upana wa mita 11.85 na litagharimu Tsh. Bilioni 67.8

Soma https://jamii.app/DarajaJipyaWamiKujengwa
SERIKALI YAWATAKA WANUNUZI WA KOROSHO KUTAJA TANI WANAZOHITAJI NDANI YA SIKU 4

> Wanunuzi wametakiwa kuwasilisha barua zao wakieleza ni tani ngapi wanahitaji

> Baada ya siku 2 kupita Serikali haitaruhusu Kampuni yoyote kununua zao hilo

Soma ~ https://jamii.app/UnunuziKorosho
POLISI WAMPIGA RISASI ANAYESADIKIWA KUCHOMA VISU WATU

- Polisi nchini Australia wamempiga risasi Muhunzi mtengeneza visu anayedaiwa kuchoma visu watu watatu na kumuua mmoja mjini Melbourne

- Alipigwa baada ya kuwavamia na kuwatishia Polisi

Soma https://jamii.app/PolisiRisasiMuhunzi
SAKATA LA MASHOGA: SERIKALI YASEMA KAMWE HAITAWARUHUSU WANANCHI KUBADILI MATUMIZI YA VIUNGO VYAO

> Imesema haitawaruhusu Wananachi wa Tanzania kubadili matumizi ya kiungo cha kutolea haja kwa matumizi ambayo Mungu hakuyakusudia

Soma ~ https://jamii.app/SerikaliVsMashoga
CHUO KISHIRIKI CHA KUMBUKUMBU YA STEFANO MOSHI CHAFUTIWA USAJILI

- TCU yaamuru Wanafunzi Chuoni hapo wahamishiwe Kampasi ya Chuo hicho iliyopo Masoka, Moshi

- Aidha, kozi 9 zimefutwa katika Vyuo 4 huku Wanafunzi wanaozisoma wakitakiwa kuhama

Zaidi, soma https://jamii.app/SMMUCoYafutwa
MADENI YASABABISHA NDEGE YA SHIRIKA LA RYANAIR ISHIKILIWE UFARANSA

> Mamlaka ya Anga ya Ufaransa imeishikilia Ndege hiyo aina ya Boeing 737 katika Uwanja wa Bordeaux

> Hii ni baada ya mazungumzo rasmi ya kiofisi kuhindwa kuzaa matunda

Soma ~ https://jamii.app/RyanairSeized
TANI 1.2 ZA SAMAKI ZAKAMATWA MKOANI KAGERA

- Idara ya uvuvi imekamata samaki aina ya sangara wenye thamani ya Tsh. Milioni 10.3 waliopatikana kwa uvuvi haramu

- Samaki hao wamegawiwa kwa taasisi mbalimbali zikiwemo baadhi ya shule za sekondari

Zaidi, soma https://jamii.app/SamakiWakamatwaKGR
SERENGETI, MARA: ASKARI MAGEREZA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI MDOMONI

- Yohana Tangawizi amejiua na kuacha ujumbe kuwa sababu za kujiua ni kuugua tumbo muda mrefu

- Lakini pia inaelezwa kuwa alifunguliwa jalada la kumpa mimba mwanafunzi wa sekondari

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariAjiuaSRNGT
Scheduled Maintenance: JF ‘inaweza’ potea hewani leo Novemba 10, 2018

- Kuanzia saa 9 Alasiri(1500Hrs) yatafanyika matengenezo ili kuboresha huduma zetu na ulinzi kwa Watumiaji na Jukwaa lenyewe

- Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa muda huo

Asante

Zaidi, Fuatilia https://jamii.app/JFMaintenance-2018
WATU 28 WAFARIKI KWA MABOMU NCHINI SOMALIA

- Ni katika mashambulizi matatu ya mabomu ya kutegwa kwenye magari, mjini Mogadishu jana Novemba 09

- Milipuko imetokea karibu na Makao makuu ya Kitengo cha Uchunguzi wa makosa ya Jinai, CID

Zaidi, soma https://jamii.app/28WafaSomalia
TANZANIA YADAIWA ZAIDI YA TSH. BILIONI 400 KWENYE MAHAKAMA ZA KIMATAIFA

- Ni madai katika Mahakama za Kimataifa kutokana na mashauri 13 yaliyofunguliwa

- Hata hivyo, Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi asema hakuna shauri lililotolewa uamuzi hivyo fedha hizo si madeni halisi

Zaidi, soma https://jamii.app/TZDeniMahakamaNje
Rais Magufuli leo Novemba 10, 2018 amekagua magari ya Jeshi, Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ

- Magari hayo yanaweza kutumika kubebea Korosho katika mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara) iwapo wanunuzi wa zao hilo hawatazinunua baada ya siku ya Jumatatu saa kumi jioni

Zaidi, soma https://jamii.app/MagariJWTZKorosho
SHAIBU AUAWA KWA KUMBAKA MTOTO NA KUMUAMBUKIZA UKIMWI

- Mkazi kijiji cha Lego Muro mkoani Kilimanjaro, Theobist Gabriel(68) ameuawa na Wananchi baada ya kudaiwa kumbaka mtoto wa miaka 12

- Baada ya vipimo mtoto alibainika kuambukizwa UKIMWI

Zaidi, soma https://jamii.app/ShaibuAuawaMoshi