JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KILIMO: MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA MFUMO WA UMWAGILIAJI

- Aina ya udongo; Udongo huathiri uhitaji wa maji hivyo Mkulima anapojua aina ya udongo, inakuwa rahisi kufahamu mfumo sahihi wa umwagiliaji ambao anatakiwa kutumia

- Hali ya hewa; Kwa mfano, Mfumo wa Sprinkler sio sahihi kutumika ikiwa sehemu ina upepo mkali, jua na joto. Inashauriwa kutumia mfumo wa matone ikiwa Shamba lipo eneo lenye hali ya joto

Zaidi, tembelea https://jamii.app/KilimoUmwagiliaji
SERIKALI YALIFUNGA KANISA KUTOKANA NA MGOGORO WA WAUMINI NA VIONGOZI

> Serikali ya Wilaya ya Moshi imelifunga kwa muda Kanisa la Evangelist Assembles of God (E.A.G.T) Mawenzi kutokana na uongozi wa juu wa Kanisa hilo kumuondoa Mchungaji Mwanzilishi wa Kanisa, Frank Mushi na kumleta Mchungaji mwingine bila ridhaa ya waumini

> Uongozi wa Kanisa umesema sababu ya kumuondoa Mchungaji huyo ni kutokuwa na Elimu ya Dini (Theology)

Soma - https://jamii.app/KufungwaKanisaMgogoro
UCHAGUZI MKUU MALAWI: Hawa ndio Majaji wa Mahakama ya Kikatiba waliobatilisha matokeo ya Uchaguzi wa Rais hapo jana

> Uchaguzi huo Mkuu ulifanyika Mei 2019 na ulibatilishwa Februari 3, 2020 kutokana na kasoro zilizokuwepo kwenye uchaguzi huo

> Uchaguzi utarudiwa tena ndani ya siku 150 kutokea jana kulingana na matangazo ya Tume ya Uchaguzi
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MAREKANI: SPIKA WA BUNGE ACHANA HOTUBA YA RAIS

- Nancy Pelosi amechana nakala yake ya Hotuba ya Rais Donald Trump baada ya Rais huyo kumaliza kuhutubia

- Rais Trump alitoa hotuba kuhusu ‘State of the Union’ Bungeni mbele ya Wabunge walioipigia makofi hotuba hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/NancyHotubaTrump
SHINYANGA: NYUMBA ZA WALIMU ZAGEUKA DANGURO, ZASABABISHA WANAFUNZI KUPATA UJAUZITO

> Ni majengo ya nyumba za Walimu katika Shule ya Sekondari Mwasele

> Hali hiyo imechochea Wanafunzi kupata ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo

Zaidi, soma - https://jamii.app/WanafunziUjauzito-SHY
UPDATE: VIRUSI VYA CORONA VYAENDELEA KUITESA DUNIA

- #coronavirus vimeua Watu 492 Ulimwenguni hadi sasa ikiwa ni ongezeko la Watu 65 ndani ya takriban saa 24

- Wengi waliofariki ni Raia wa #China huku Mji wa #Wuhan ukiongoza

- Zaidi ya Watu 24,500 wameathirika katika Nchi 25
FAO: NZIGE KUENDELEA KUZALIANA ZAIDI BARANI AFRIKA

> Taarifa iliyotolewa inasema janga la Nzige limetoa tishio kubwa kwa usalama wa chakula na maisha ya Watu huku Nzige hao wakiongezeka nchini Ethiopia na Somalia na kuelekea Kusini hadi nchini Kenya

> Ktk kipindi cha kuzaliana mwezi Februari idadi yao itaendelea kuongezeka katika nchi hizo

Soma - https://jamii.app/KuzalianaNzigeAfrika
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KABLA YA KUCHANWA HOTUBA, HIKI NDICHO KILITOKEA

- Awali, Rais Trump hakupokea salamu ya mkono ya Spika Nancy na haijawa wazi kama alipuuza au hakuona

- Baada ya kuchana Hotuba ya Trump, Spika Nancy amesema "Ilikuwa ni jambo la heshima kufanya, ukizingatia mbadala wake"

Zaidi, soma https://jamii.app/NancyHotubaTrump
KWANINI MARA NYINGI BAADA YA MTU KUSHTAKIWA, POLISI AU WAENDESHA MASHTAKA HUDAI UPELELEZI HAUJAKAMILIKA?

> Hii huweza kutokea kutokana na mazingira ya tuhuma, ushahidi na taarifa za ziada ambazo huweza kupatikana baada ya kesi kufunguliwa ila endapo vipengele vyote vya uhalifu havikukamilika itakuwa ni upotezaji wa muda kumshtaki Mtu na kumpeleka Mahakamani

> Shauri la Jinai likikaa Mahakamani kwa siku 60 bila ushahidi kukamilika, Mahakama italitupilia mbali shauri hilo na Mtuhumiwa kuachiwa huru

Tembelea - https://jamii.app/SheriaKutokamilikaUpelelezi
#JFSheria
ZITTO ADAI BARUA YAKE KWA BENKI YA DUNIA KUHUSU MKOPO WA ELIMU INAPOTOSHWA

> Amesema si lengo lake kuzuia misaada Nchini ila anafanya hivyo ili kuwalinda Watoto wa Kike wanaopata ujauzito wakiwa masomoni kwa madai ya kuwapo kwa ubaguzi katika mfumo rasmi wa elimu Nchini

Soma - https://jamii.app/ZittoBaruaMkopoWB
SPIKA NDUGAI ATAKA BUNGE KUWEKWA KWENYE VIVUTIO VYA WATALII

- Amesema, wao ni namba moja kwa kuangalia Watalii wanaoenda Bungeni hapo ndani ya Mwaka

- Amehoji kama Wizara ya Maliasili inajua kuwa Bunge linongoza katika vivutio kuliko hifadhi yoyote

Soma https://jamii.app/NdugaiBungeUtalii
SONGWE: MAFURIKO YASABABISHA VIFO VYA WATU WANNE

> ACP George Salala amesema wanne wamefariki baada ya kusombwa na mafuriko katika Wilaya za Mbozi na Ileje

> Amewataka wananchi kuwa makini wakati huu ambapo mvua zinaendelea kunyesha

Soma - https://jamii.app/MafurikoVifoSongwe
CHINA: WATANZANIA 85 WANATARAJIWA KUNYONGWA KWA KUJIHUSISHA NA DAWA ZA KULEVYA

> Watanzania 85 wanatarajiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya #DawaZaKulevya

> Aidha, Watanzania 265 wamekamatwa nchini humo kwa kosa hilo hilo na tayari 130 wamehukumiwa

Zaidi, soma - https://jamii.app/WatzKunyongwaDawaKulevya
KOREA KUSINI: MASHABIKI WALIPWA TZS 722,000 BAADA YA RONALDO KUKOSA MECHI

> Mahakama imeagiza waandaaji kuwalipa mashabiki wawili £240

> Wakili adai mashabiki hao walipata Shinikizo la kiakili baada ya kudanganywa #CR7 atakuwepo

Zaidi, soma - https://jamii.app/RonaldoFidiaKorea
MWENDELEZO: Mke wa Waziri Mkuu wa Lesotho amekamatwa na anatarajiwa kushtakiwa kwa kosa la kuhusika na mauaji ya Mke wa kwanza wa Waziri huyo mwaka 2017

- Maesiah Thabane, ambaye alitoroka nchini humo Januari 10, 2020 na kukimbilia Afrika Kusini amerudi nchini humo na kujisalimisha katika Kituo cha Polisi
IRAN: JASUSI WA SHIRIKA LA UPELELEZI MAREKANI (CIA) AHUKUMIWA KIFO

> Amir Rahimpour amehukumiwa kifo baada ya kutoa taarifa kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran

> Hii ni adhabu ya kwanza ya kifo kutolewa kwa kosa hili kwa takriban miaka 20

Soma - https://jamii.app/CIAIranKifo
HISTORIA NA MAISHA YA MZEE DANIEL ARAP MOI

> Alikuwa Rais wa pili wa Kenya aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 24 kuanzia 1978 hadi 2002. Kifimbo alichotembea nacho kila mahali, ni ishara ya uongozi katika jamii yake ya Kalenjin

> Moi alikuwa miongoni mwa Wakenya wachache walioteuliwa kuwa Wajumbe wa Baraza la Majimbo la Serikali ya Wakoloni wa Kiingereza 1955

> Mwaka 1967, Kenyatta alimteua Moi kuwa Makamu wake na alipofariki 1978 akiwa na miaka 84 ndipo Moi akarithi kiti chake

Fahamu zaidi - https://jamii.app/HistoriaRaisDanielMoi
#JFHistoria
EWURA YATANGAZA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA

> Imetangaza ongezeko la bei kwa mafuta yanayoingilia Bandari ya Dar kutokana na kushuka kwa thamani ya Tsh dhidi ya Dola ya Marekani na ongezeko la bei katika soko la Dunia

> Lita moja ya Petroli imepanda kwa Tsh 20 huku Dizeli ikiongezeka kwa Tsh 74 na Mafuta ya taa Tsh 44

Soma - https://jamii.app/PetrolDieselPriceRise
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU (PNEUMONIA) - 2

> Ugonjwa huu unaweza kumpata yeyote lakini kuna makundi ambao yapo katika hatari zaidi

> Watoto chini ya Miaka mitano ni waathirika wakubwa zaidi wa Pneumonia kwasababu Mfumo wao wa kinga mwilini unakuwa bado haujakomaa

> Walio na umri wa miaka 65 na kuendelea nao wanaweza kuumwa Homa ya Mapafu kutokana na kinga yao ya mwili kupungua

> Wenye matatizo ya kifua, wanaotumia mashine za kupumulia, wavuta sigara, wanywa pombe na waathirika wa madawa ya kulevya nao wana hatari ya kuumwa

Zaidi, soma - https://jamii.app/VisababishiPneumonia