JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RASMI: MBWANA SAMATTA AKUBALI KUJIUNGA NA KLABU YA ASTON VILLA

> Mshambuliaji huyo raia wa Tanzania siku ya kesho atasafiri hadi nchini England kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya

> Imeelezwa kuwa Aston Villa imekubali kulipa kiasi cha Paundi Milioni 9 sawa na zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 27 kwa ajili ya uhamisho wa Samatta

#JFSports
MATUMIZI YA INTANETI: VODACOM YAONGOZA KUWA NA GHARAMA KUBWA

> Kwa mujibu wa taarifa ya TCRA ya robo mwaka iliyoishia Septemba 2019 Vodacom hutoza Tsh. 205 kwa Megabyte (MB)

> Zantel hutoza Tsh. 93 kwa MB, huku wateja wa Airtel na Tigo wakilipa kiwango sawa ambapo gharama ya MB moja ni Tsh. 29

> Gharama zote hizi ni bila kodi na zinatozwa endapo mteja hajajiunga kifurushi

Soma - https://jamii.app/GharamaIntanetiTz
TANZANIA vs KENYA vs UGANDA: MSAMAHA WA RAIS

#KatibaTanzania, Ibara-45 (1), Rais anaweza kumsamehe kwa masharti au la, mtu aliyepatikana na hatia Mahakamani kwa kosa lolote

- #KatibaKenya, Ibara-172 (1): Kutakuwa na Msamaha utakaotekelezwa kwa Ombi la Rais kwa mtu yeyote kulingana na Ushauri wa Kamati ya Ushauri

- #KatibaUganda, Ibara-121: Kwa ushauri wa Kamati, Rais anaweza kumsamehe aliye hatiani kwa masharti au la, Kusamehe sehemu au adhabu yote, Kurahisisha adhabu kali aliyopewa

Zaidi, soma https://jamii.app/Katiba-TZvsUGvsKE
KESI YA KUMUONDOA TRUMP MADARAKANI: MASENETA 100 WAAPISHWA

> Maseneta 100 wameapishwa jana kama Baraza la Mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump ya matumizi mabaya ya madaraka na kuingilia Bunge

> Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Januari 21

Soma - https://jamii.app/Senates100ImpeachmentTrump
MTWARA: WAKULIMA WA KOROSHO WALIPWA TSH. BILIONI 68

> Wakulima wameanza kulipwa fedha zao ambapo awali malipo hayo yalikuwa yamechelewa

> Vyama 41 kati ya 87 vya Wilaya ya Nanyumbu na Masasi vimefunga msimu kwa sababu korosho zimekwisha

Soma https://jamii.app/WakulimaKoroshoMasasi
KIGOMA: JESHI LA POLISI LAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE

> Ni kutokana na sababu za kiusalama na taarifa za kiintelijensia zilizopo

> Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT Wazalendo amesema sababu hiyo haina mashiko

Soma - https://jamii.app/PolisiZuioMkutano
MABADILIKO YA TABIANCHI KUSINI MWA AFRIKA YASABABISHA BAA LA NJAA

> Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema watu milioni 45 kati ya watu milioni 345 wa Kanda hiyo wanakumbwa na Njaa Kali kufuatia ukame wa mara kwa mara, mafuriko na hali mbaya ya kiuchumi

Soma - https://jamii.app/Hunger45MilSouthernAfrica
NIDA: NAMBA ZA UTAMBULISHO (NIN) MILIONI 6 BADO HAZIJATUMIKA KUSAJILI LAINI ZA SIMU

> Namba 6,806,096 bado hazijatumika kusajili laini za simu kwa Alama za Vidole

> Wananchi wenye namba wametakiwa kusajili laini zao kabla ya tarehe 20

Soma - https://jamii.app/NidaUsajiliSimu
MPANGO WA NYUKLIA IRAN: MAREKANI YATISHIA KUONGEZA USHURU WA MAGARI

> Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amethibitisha kuwa Marekani imetishia kuongeza ushuru wa 25% kwa mauzo ya magari kutoka Ulaya

> Ongezeko hilo litatekelezwa iwapo Ulaya (Uingereza, Ufaransa na Ujerumani) haitaikemea Iran kuhusu Mpango wa Nyuklia

Soma - https://jamii.app/OngezekoUshuruMagariUS
ZANZIBAR: POLISI AFUKUZWA KAZI KWA KUSABABISHA KIFO CHA MTUHUMIWA

> Hussein Yahya Rashid (36), amekutwa na hatia ya kusababisha kifo cha Mussa Suleiman ambaye alituhumiwa kwa kosa la wizi kutokana na kumkabidhi mtuhumiwa huyo kwa Raia ambao walimshambulia hadi kumuua

Soma - https://jamii.app/PolisiHatiaKifoMtuhumiwa
Rushwa huhusiana na udanganyifu unaohusisha kutotimiza wajibu, kujitambulisha kwa uongo au jaribio la kupotosha ukweli ili kujipatia faida ya fedha au manufaa mengineyo
-
Mkurugenzi wa Intelijensia wa TAKUKURU, Emmanuel Kiyabo aliwahi kusema, "Mtoa taarifa hapaswi kuogopa kwa kuwa anaweza kwenda Mahakamani kutoa ushahidi, hasa kwa kesi za rushwa kuhusu Huduma za Kijamii na uonevu."
UPDATE: RAIS WA URUSI ATEUA WAZIRI MKUU MPYA BAADA YA BARAZA LA MAWAZIRI KUJIZULU
-
Rais Vladimir Putin amemteua Mikhail Mishustin kuwa Waziri Mkuu mpya baada ya Baraza la Chini la Bunge kupitisha uteuzi huo kupitia upigaji wa kura
-
Waziri Mkuu wa Zamani, Dmitry Medvedev ameteuliwa kuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi
RIPOTI-2019: TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 91 KATIKA UTAWALA WA SHERIA

- Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na 'The World Justice Project' ikipima upatikanaji, utendwaji na Utambulikaji wa Utawala wa Sheria, Tanzania ipo nafasi ya 91 kati ya nchi 126

Soma https://jamii.app/Tanzania91UtawalaSheria-WJP
SHAMBULIO LA IRAN NCHINI IRAQ: WANAJESHI 11 WA MAREKANI WALIJERUHIWA

> Makao Makuu ya Jeshi la Marekani yamesema, Wanajeshi 11 wa Marekani walijeruhiwa katika shambulio la Iran dhidi ya Kambi ya Jeshi la Wanaanga ya Ain al-Assad lililofanyika Januari 8

Soma - https://jamii.app/11PersonnelInjuredAirbase
#JFLeo
UGANDA: JELA MIAKA 13 KWA KUMNAJISI NA KUMPA MIMBA MWANAE WA MIAKA 12

> Hii ni baada ya Mtuhimiwa kukiri makosa yake kwa Jaji

> Kuongea na Jaji ni hiyari kama ilivyoidhinishwa kwa muda Tanzania kuongea na DPP kuhusu Makosa ya Uhujumu Uchumi

Soma https://jamii.app/MimbaMwanaeUmri12
#JFLeo
LESOTHO: WAZIRI MKUU ATANGAZA KUJIUZULU KUFUATIA TUHUMA ZA MAUAJI YA ALIYEKUWA MKEWE

> Thomas Thabane hajasema sababu za kujiuzulu na hajazungumzia tuhuma zinazomkabili

> Mkewe mpya, Maesaiah Thabane anatafutwa na Polisi kwa mahojiano

Soma - https://jamii.app/WaziriKujiuzuluLesotho
BASHIRU AANZA ZIARA MKOANI KIGOMA

> Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ameanza Ziara ya Siku Tatu

> Aidha, barua ya Polisi yenye Kumbukumbu Namba KIG/A.24/60/VOL.1/114 ilimzuia Zitto Kabwe kufanya Mkutano wa Hadhara Jimboni mwake

Soma https://jamii.app/BahiruKigomaZitto
BARRICK KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 110 NORTH MARA

> Itafanya hivyo ili kumudu gharama za uendeshaji

> Mchakato huo utazingatia Sheria zote za Nchi kuhakikisha kila anayeguswa anapata Stahiki zake

Soma https://jamii.app/BarrickKupunguza
MTANZANIA APATA MABILIONI KWA KUUZA MFUMO WA KUNUNUA GESI KADRI UNAVYOTUMIA

> Andron Mendes ameiuzia Kampuni ya Uingereza, 'Circle Gas' mfumo huo kwa Tsh. bilioni 57.6

> Mradi huo umeshaunganisha Wakazi zaidi ya 1430 wa Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/MtanzaniaGesiBilioni
HAKI YA MWANAMKE KUTAFUTA ELIMU

- Chama cha Wanasheria wa Kike Zanzibar (ZAFELA) kimeandaa jarida la 'Haki za Mwanamke kwa Mujibu wa Qur'an na Sunnah za Mtume (S.A.W)'

- Kimesema Uislamu umetoa umuhimu Mwanaume au Mwanamke kutafuta elimu

Zaidi, soma https://jamii.app/UsawaElimuDiniKiislamu