JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UPINZANI NAMIBIA WAGOMA KUTUMIA KISWAHILI KAMA LUGHA YA HIYARI KWA SHULE ZA SERIKALI

> Wasema kuna mambo ya muhimu ya kushinikiza kwa wakati huu kuhusu Mfumo wa Elimu

> Wizara ya Elimu ilisema itafanya Kiswahili Lugha ya Hiari 2021

Soma zaidi https://jamii.app/KswahiliNamibia
TANZANIA vs KENYA vs UGANDA: UCHAGUZI WA RAIS

- Katiba ya Tanzania inasema Mshindi wa Urais ni yule atakayepata Kura Nyingi kuliko Mgombea mwingine

- Katiba za Kenya na Uganda zinasema Mshindi wa Urais ni yule atakayekuwa amepata Zaidi ya Nusu ya Kura zote

Zaidi, soma https://jamii.app/Katiba-TZvsUGvsKE

#Katiba
MWANAFUNZI AGOMA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA, ADAI HANA AKILI

> Amesema mbele ya Mkuu wa Wilaya kuwa, yupo tayari kufungwa na sio kusoma

> Aomba ajifunze kushona Cherehani kwani anatamani kuwa Mwanamitindo

Soma - https://jamii.app/MwanafunziAkataaMasomo
JENGA TABIA YA KUAGA KILA UNAPOTOKA KWA KUTOA TAARIFA SAHIHI

> Ni taarifa kama Jina la unakokwenda, Mtu na Anuani ya mtu unayekutana naye na Muda utakaokuwa haupo

> Hii itarahisisha upatikanaji wako pindi utakapopatwa na matatizo

Soma https://jamii.app/TabiaKuagaUnapotoka
#JFLeo
DALILI ZA MLIPUKO WA NZIGE MKOA WA KILIMANJARO

> Mdau kutoka JamiiForums anadai kuwa, kuna kila dalili ya Nzige Tanzania

> Ni vema Serikali ikachukua tahadhari kabla ya tatizo kuwa kubwa zaidi

Some zaidi https://jamii.app/NzigeKilimanjaroTz
KIJANA AUNDA EMOJI KUUTANGAZA UZURI WA AFRIKA

> O'Plerou Denis Grebet (22), aliona Vyombo vya Habari vinazungumza upande mbaya wa Afrika (Umaskini na Njaa)

> Sanaa yake inaonesha kuwa Afrika ina vitu vya kustaajabisha Dunia

Soma Zaidi https://jamii.app/MwanafunziEmojisAfrika
KAGERA: AMUUA MWANAYE KWA KUMCHOMA MOTO MAKALIONI NA USONI

> Juma Daniel anatuhumiwa kumchoma moto mwanaye, na kumjeruhi sehemu za haja kubwa kwa kifaa cha ncha kali

> Ni baada ya mtoto huyo kujisaidia haja kubwa kitandani wakiwa wamelala

Soma - https://jamii.app/BabaAmuunguzaMwanaye-KGR
RASMI: MBWANA SAMATTA AKUBALI KUJIUNGA NA KLABU YA ASTON VILLA

> Mshambuliaji huyo raia wa Tanzania siku ya kesho atasafiri hadi nchini England kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya

> Imeelezwa kuwa Aston Villa imekubali kulipa kiasi cha Paundi Milioni 9 sawa na zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 27 kwa ajili ya uhamisho wa Samatta

#JFSports
MATUMIZI YA INTANETI: VODACOM YAONGOZA KUWA NA GHARAMA KUBWA

> Kwa mujibu wa taarifa ya TCRA ya robo mwaka iliyoishia Septemba 2019 Vodacom hutoza Tsh. 205 kwa Megabyte (MB)

> Zantel hutoza Tsh. 93 kwa MB, huku wateja wa Airtel na Tigo wakilipa kiwango sawa ambapo gharama ya MB moja ni Tsh. 29

> Gharama zote hizi ni bila kodi na zinatozwa endapo mteja hajajiunga kifurushi

Soma - https://jamii.app/GharamaIntanetiTz
TANZANIA vs KENYA vs UGANDA: MSAMAHA WA RAIS

#KatibaTanzania, Ibara-45 (1), Rais anaweza kumsamehe kwa masharti au la, mtu aliyepatikana na hatia Mahakamani kwa kosa lolote

- #KatibaKenya, Ibara-172 (1): Kutakuwa na Msamaha utakaotekelezwa kwa Ombi la Rais kwa mtu yeyote kulingana na Ushauri wa Kamati ya Ushauri

- #KatibaUganda, Ibara-121: Kwa ushauri wa Kamati, Rais anaweza kumsamehe aliye hatiani kwa masharti au la, Kusamehe sehemu au adhabu yote, Kurahisisha adhabu kali aliyopewa

Zaidi, soma https://jamii.app/Katiba-TZvsUGvsKE
KESI YA KUMUONDOA TRUMP MADARAKANI: MASENETA 100 WAAPISHWA

> Maseneta 100 wameapishwa jana kama Baraza la Mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump ya matumizi mabaya ya madaraka na kuingilia Bunge

> Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Januari 21

Soma - https://jamii.app/Senates100ImpeachmentTrump
MTWARA: WAKULIMA WA KOROSHO WALIPWA TSH. BILIONI 68

> Wakulima wameanza kulipwa fedha zao ambapo awali malipo hayo yalikuwa yamechelewa

> Vyama 41 kati ya 87 vya Wilaya ya Nanyumbu na Masasi vimefunga msimu kwa sababu korosho zimekwisha

Soma https://jamii.app/WakulimaKoroshoMasasi
KIGOMA: JESHI LA POLISI LAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE

> Ni kutokana na sababu za kiusalama na taarifa za kiintelijensia zilizopo

> Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT Wazalendo amesema sababu hiyo haina mashiko

Soma - https://jamii.app/PolisiZuioMkutano
MABADILIKO YA TABIANCHI KUSINI MWA AFRIKA YASABABISHA BAA LA NJAA

> Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema watu milioni 45 kati ya watu milioni 345 wa Kanda hiyo wanakumbwa na Njaa Kali kufuatia ukame wa mara kwa mara, mafuriko na hali mbaya ya kiuchumi

Soma - https://jamii.app/Hunger45MilSouthernAfrica
NIDA: NAMBA ZA UTAMBULISHO (NIN) MILIONI 6 BADO HAZIJATUMIKA KUSAJILI LAINI ZA SIMU

> Namba 6,806,096 bado hazijatumika kusajili laini za simu kwa Alama za Vidole

> Wananchi wenye namba wametakiwa kusajili laini zao kabla ya tarehe 20

Soma - https://jamii.app/NidaUsajiliSimu
MPANGO WA NYUKLIA IRAN: MAREKANI YATISHIA KUONGEZA USHURU WA MAGARI

> Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amethibitisha kuwa Marekani imetishia kuongeza ushuru wa 25% kwa mauzo ya magari kutoka Ulaya

> Ongezeko hilo litatekelezwa iwapo Ulaya (Uingereza, Ufaransa na Ujerumani) haitaikemea Iran kuhusu Mpango wa Nyuklia

Soma - https://jamii.app/OngezekoUshuruMagariUS
ZANZIBAR: POLISI AFUKUZWA KAZI KWA KUSABABISHA KIFO CHA MTUHUMIWA

> Hussein Yahya Rashid (36), amekutwa na hatia ya kusababisha kifo cha Mussa Suleiman ambaye alituhumiwa kwa kosa la wizi kutokana na kumkabidhi mtuhumiwa huyo kwa Raia ambao walimshambulia hadi kumuua

Soma - https://jamii.app/PolisiHatiaKifoMtuhumiwa
Rushwa huhusiana na udanganyifu unaohusisha kutotimiza wajibu, kujitambulisha kwa uongo au jaribio la kupotosha ukweli ili kujipatia faida ya fedha au manufaa mengineyo
-
Mkurugenzi wa Intelijensia wa TAKUKURU, Emmanuel Kiyabo aliwahi kusema, "Mtoa taarifa hapaswi kuogopa kwa kuwa anaweza kwenda Mahakamani kutoa ushahidi, hasa kwa kesi za rushwa kuhusu Huduma za Kijamii na uonevu."
UPDATE: RAIS WA URUSI ATEUA WAZIRI MKUU MPYA BAADA YA BARAZA LA MAWAZIRI KUJIZULU
-
Rais Vladimir Putin amemteua Mikhail Mishustin kuwa Waziri Mkuu mpya baada ya Baraza la Chini la Bunge kupitisha uteuzi huo kupitia upigaji wa kura
-
Waziri Mkuu wa Zamani, Dmitry Medvedev ameteuliwa kuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi
RIPOTI-2019: TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 91 KATIKA UTAWALA WA SHERIA

- Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na 'The World Justice Project' ikipima upatikanaji, utendwaji na Utambulikaji wa Utawala wa Sheria, Tanzania ipo nafasi ya 91 kati ya nchi 126

Soma https://jamii.app/Tanzania91UtawalaSheria-WJP