JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MVUA DAR: BARABARA YA JANGWANI YAFUNGWA

> Mvua yasababisha Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kufungwa baada ya maji kujaa

> Mamlaka ya Hali ya Hewa, imesema Mvua inatarajiwa kunyesha tena kesho Januari 17, 2020

Soma https://jamii.app/MadharaMvuaDar
LUKUVI AANIKA DHULUMA ZA MAOFISA MIKOPO BENKI

> Asema, baadhi yao hushirikiana na Madalali Matapeli kuwaibia Wananchi kwa kuuza nyumba zao kwa mnada bila kufuata taratibu

> Serikali yawataka wanaondesha Mtandao huo kuacha mara moja

Soma https://jamii.app/DhulumaOfisaBenki

#JFLeo
MBEYA: WATUMISHI 4 WA HOSPITALI WAKAMATWA KUTOKANA NA UTENDAJI MBOVU

> Naibu Waziri wa Afya ameagiza kuwekwa ndani na kutolewa katika nafasi zao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tukuyu na Afisa Ugavi

> Pia, amegiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa Mfamasia na Afisa Manunuzi wa Hospitali hiyo kutokana na usimamizi mbovu wa Stoo ya Dawa

Soma - https://jamii.app/DaktariMbaroniHudumaMbovu
MKAKATI WA TAIFA DHIDI YA RUSHWA NA MPANGO WA UTEKELEZAJI (AWAMU YA 3: 2017-2022)

- Vitendo vya Rushwa vinatafsiriwa kuwa ni kutoa, kupokea au kushawishi moja kwa moja au kitu chochote cha thamani kinachotolewa ili kupindisha utaratibu katika Utoaji wa Maamuzi

#KemeaRushwa
WAZIRI KAMWELWE: MUDA WA KUSAJILI LAINI ZA SIMU HAUTAONGEZWA

> Serikali haitaongeza muda baada ya siku 20 alizoongeza Rais Magufuli kumalizika

> Wananchi wameshauriwa kuwa makini katika siku zilizosalia kwani Wizi wa Kimtandao umeongezeka

Soma - https://jamii.app/MudaUsajiliLaini-TZ
MISRI, ETHIOPIA NA SUDAN ZAINGIA MAKUBALIANO KUHUSU MATUMIZI YA MTO NILE

> Nchi hizo zimefikia Makubaliano ya Awali ya kujaza maji kwenye Bwawa la Grand Renaissance

> Makubaliano ya mwisho yatafanyika Washington, Januari 28-29 mwaka huu

Soma - https://jamii.app/MakubalianoMtoNile
UPINZANI NAMIBIA WAGOMA KUTUMIA KISWAHILI KAMA LUGHA YA HIYARI KWA SHULE ZA SERIKALI

> Wasema kuna mambo ya muhimu ya kushinikiza kwa wakati huu kuhusu Mfumo wa Elimu

> Wizara ya Elimu ilisema itafanya Kiswahili Lugha ya Hiari 2021

Soma zaidi https://jamii.app/KswahiliNamibia
TANZANIA vs KENYA vs UGANDA: UCHAGUZI WA RAIS

- Katiba ya Tanzania inasema Mshindi wa Urais ni yule atakayepata Kura Nyingi kuliko Mgombea mwingine

- Katiba za Kenya na Uganda zinasema Mshindi wa Urais ni yule atakayekuwa amepata Zaidi ya Nusu ya Kura zote

Zaidi, soma https://jamii.app/Katiba-TZvsUGvsKE

#Katiba
MWANAFUNZI AGOMA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA, ADAI HANA AKILI

> Amesema mbele ya Mkuu wa Wilaya kuwa, yupo tayari kufungwa na sio kusoma

> Aomba ajifunze kushona Cherehani kwani anatamani kuwa Mwanamitindo

Soma - https://jamii.app/MwanafunziAkataaMasomo
JENGA TABIA YA KUAGA KILA UNAPOTOKA KWA KUTOA TAARIFA SAHIHI

> Ni taarifa kama Jina la unakokwenda, Mtu na Anuani ya mtu unayekutana naye na Muda utakaokuwa haupo

> Hii itarahisisha upatikanaji wako pindi utakapopatwa na matatizo

Soma https://jamii.app/TabiaKuagaUnapotoka
#JFLeo
DALILI ZA MLIPUKO WA NZIGE MKOA WA KILIMANJARO

> Mdau kutoka JamiiForums anadai kuwa, kuna kila dalili ya Nzige Tanzania

> Ni vema Serikali ikachukua tahadhari kabla ya tatizo kuwa kubwa zaidi

Some zaidi https://jamii.app/NzigeKilimanjaroTz
KIJANA AUNDA EMOJI KUUTANGAZA UZURI WA AFRIKA

> O'Plerou Denis Grebet (22), aliona Vyombo vya Habari vinazungumza upande mbaya wa Afrika (Umaskini na Njaa)

> Sanaa yake inaonesha kuwa Afrika ina vitu vya kustaajabisha Dunia

Soma Zaidi https://jamii.app/MwanafunziEmojisAfrika
KAGERA: AMUUA MWANAYE KWA KUMCHOMA MOTO MAKALIONI NA USONI

> Juma Daniel anatuhumiwa kumchoma moto mwanaye, na kumjeruhi sehemu za haja kubwa kwa kifaa cha ncha kali

> Ni baada ya mtoto huyo kujisaidia haja kubwa kitandani wakiwa wamelala

Soma - https://jamii.app/BabaAmuunguzaMwanaye-KGR
RASMI: MBWANA SAMATTA AKUBALI KUJIUNGA NA KLABU YA ASTON VILLA

> Mshambuliaji huyo raia wa Tanzania siku ya kesho atasafiri hadi nchini England kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya

> Imeelezwa kuwa Aston Villa imekubali kulipa kiasi cha Paundi Milioni 9 sawa na zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 27 kwa ajili ya uhamisho wa Samatta

#JFSports
MATUMIZI YA INTANETI: VODACOM YAONGOZA KUWA NA GHARAMA KUBWA

> Kwa mujibu wa taarifa ya TCRA ya robo mwaka iliyoishia Septemba 2019 Vodacom hutoza Tsh. 205 kwa Megabyte (MB)

> Zantel hutoza Tsh. 93 kwa MB, huku wateja wa Airtel na Tigo wakilipa kiwango sawa ambapo gharama ya MB moja ni Tsh. 29

> Gharama zote hizi ni bila kodi na zinatozwa endapo mteja hajajiunga kifurushi

Soma - https://jamii.app/GharamaIntanetiTz
TANZANIA vs KENYA vs UGANDA: MSAMAHA WA RAIS

#KatibaTanzania, Ibara-45 (1), Rais anaweza kumsamehe kwa masharti au la, mtu aliyepatikana na hatia Mahakamani kwa kosa lolote

- #KatibaKenya, Ibara-172 (1): Kutakuwa na Msamaha utakaotekelezwa kwa Ombi la Rais kwa mtu yeyote kulingana na Ushauri wa Kamati ya Ushauri

- #KatibaUganda, Ibara-121: Kwa ushauri wa Kamati, Rais anaweza kumsamehe aliye hatiani kwa masharti au la, Kusamehe sehemu au adhabu yote, Kurahisisha adhabu kali aliyopewa

Zaidi, soma https://jamii.app/Katiba-TZvsUGvsKE
KESI YA KUMUONDOA TRUMP MADARAKANI: MASENETA 100 WAAPISHWA

> Maseneta 100 wameapishwa jana kama Baraza la Mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump ya matumizi mabaya ya madaraka na kuingilia Bunge

> Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Januari 21

Soma - https://jamii.app/Senates100ImpeachmentTrump
MTWARA: WAKULIMA WA KOROSHO WALIPWA TSH. BILIONI 68

> Wakulima wameanza kulipwa fedha zao ambapo awali malipo hayo yalikuwa yamechelewa

> Vyama 41 kati ya 87 vya Wilaya ya Nanyumbu na Masasi vimefunga msimu kwa sababu korosho zimekwisha

Soma https://jamii.app/WakulimaKoroshoMasasi
KIGOMA: JESHI LA POLISI LAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE

> Ni kutokana na sababu za kiusalama na taarifa za kiintelijensia zilizopo

> Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT Wazalendo amesema sababu hiyo haina mashiko

Soma - https://jamii.app/PolisiZuioMkutano
MABADILIKO YA TABIANCHI KUSINI MWA AFRIKA YASABABISHA BAA LA NJAA

> Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema watu milioni 45 kati ya watu milioni 345 wa Kanda hiyo wanakumbwa na Njaa Kali kufuatia ukame wa mara kwa mara, mafuriko na hali mbaya ya kiuchumi

Soma - https://jamii.app/Hunger45MilSouthernAfrica