JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MALAWI: JESHI LA POLISI LASHTAKIWA KWA KUTOCHUNGUZA KESI ZA UBAKAJI DHIDI YA MAAFISA WAKE

> Baadhi ya Polisi wanadaiwa kutumia upenyo uliotokea kipindi cha maandamamo Oktoba 2019 kufanya vitendo vya ubakaji kwa wanafunzi na wanawake katika maeneno ya Msundwe, M’bwatalika na Mpingu

Soma - https://jamii.app/PoliceAccusedGenderViolence
MICHEZO: Mchezo kati ya Yanga SC na Kagera Sugar umemalizika kwa Yanga kuadhibiwa na Kagera kwa kufungwa mabao 3 kwa 0 kwenye Uwanja wa Uhuru
-
Magoli ya Kagera Sugar yamefungwa na
Mhilu 13'
Ramadhan 67'
Mwalyanzi 90'
TANZANIA YAPOKEA MSAADA KUTOKA SWEDEN ILI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

> Tanzania imetia saini mikataba 2 ya msaada na Sweden kwa kupatiwa Tsh. Bilioni 240.95 ili kugharamia mpango wa maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2016/17 – 2021/2022 ikiwemo Elimu ya Msingi, Elimu Jumuishi, Elimu ya Watu Wazima na iliyo nje ya Mfumo Rasmi

Soma - https://jamii.app/MsaadaElimuSweden
DARASA LA SABA DAR KUFANYA MITIHANI KESHO, NECTA WATOA UFAFANUZI

> Kitachofanyika kesho si Mitihani ya NECTA, ni jaribio kwa walimu wa Mkoa huo baada ya kupewa mafunzo ya namna bora ya kutunga mitihani

> Lengo la mazoezi hayo ni kuhakikisha walimu wanakuwa na umahiri wa kutunga mtihani

Soma https://jamii.app/MtihaniNecta7
KICHUYA ASAJILIWA TENA SIMBA

- Simba SC imesajili tena Mchezaji Shiza Kichuya ambaye awali klabu hiyo ilimuuza kwenda klabu ya Pharco FC ya Misri

- Kichuya alivyokuwa Pharco FC alitolewa kwa mkopo kwenda Enppi FC

- Mkataba wake na Simba haujawekwa wazi ni wa muda gani
URUSI: BARAZA LA MAWAZIRI LAJIUZULU BAADA YA RAIS KUPENDEKEZA MABADILIKO YA KATIBA

> Baraza la Mawaziri akiwemo Waziri Mkuu wamejiuzulu baada ya Rais Vladimir Putin kupendekeza kufanyike kura ya maamuzi kufanyia marekebisho Katiba ili kuongeza Mamlaka ya Bunge la Nchi, japo mfumo wa Uongozi wa Bunge bado utadumishwa

> Wamedai hatua hiyo ya Putin ni kutaka kumdhoofisha mrithi wake

Soma - https://jamii.app/KujiuzuluSerikaliUrusi
KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI YA UINGEREZA, RESOURCES INDIANA KUISHITAKI TANZANIA

> Inaituhumu Tanzania kukiuka Protection and Promotion of Investments and International Law on Project

> Ukiukwaji ni baada ya Tanzania kurekebisha Sheria ya Madini

Soma https://jamii.app/ResourcesIndianaKesiTz
PAKISTAN NA AFGHANISTAN: WATU 160 WAFARIKI KUTOKANA NA MAPOROMOKO YA THERUJI
-
Kikosi cha Uokozi Nchini Pakistan kimepata miili ya watu 21 waliopoteza maisha kutokana na Maporomoko ya Theluji katika Jimbo la Kashmir na kuifanya idadi ya waliopoteza maisha nchini Pakistan na Afghanistan kufikia 160
-
Eneo lililoathirika zaidi ni la Kashmir ya Upande wa Pakistan, hususan bonde la Neelum
TEXAS, MAREKANI: HUKUMU YA KWANZA YA KIFO KWA MWAKA 2020 YATEKELEZWA

- John Gardner ameuawa kwa kuchomwa Sindano ya Sumu hapo jana baada kukutwa na Hatia ya kumuua mkewe

- Pia, alikuwa na historia ya muda mrefu ya dhuluma dhidi ya wake zake

Soma https://jamii.app/HukumuKifoMauajiMke
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UPDATE: Wabunge wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha Azimio la kumshtaki Rais Trump kwa kupiga kura 228 dhidi ya 193

> Spika Nancy Pelosi amesaini uamuzi huo sambamba na Timu ya Wabunge wa Democratic ambao wataendesha mashtaka ya kesi hiyo itakayoanza Januari 21

#JFLeo
MVUA DAR: BARABARA YA JANGWANI YAFUNGWA

> Mvua yasababisha Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kufungwa baada ya maji kujaa

> Mamlaka ya Hali ya Hewa, imesema Mvua inatarajiwa kunyesha tena kesho Januari 17, 2020

Soma https://jamii.app/MadharaMvuaDar
LUKUVI AANIKA DHULUMA ZA MAOFISA MIKOPO BENKI

> Asema, baadhi yao hushirikiana na Madalali Matapeli kuwaibia Wananchi kwa kuuza nyumba zao kwa mnada bila kufuata taratibu

> Serikali yawataka wanaondesha Mtandao huo kuacha mara moja

Soma https://jamii.app/DhulumaOfisaBenki

#JFLeo
MBEYA: WATUMISHI 4 WA HOSPITALI WAKAMATWA KUTOKANA NA UTENDAJI MBOVU

> Naibu Waziri wa Afya ameagiza kuwekwa ndani na kutolewa katika nafasi zao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tukuyu na Afisa Ugavi

> Pia, amegiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa Mfamasia na Afisa Manunuzi wa Hospitali hiyo kutokana na usimamizi mbovu wa Stoo ya Dawa

Soma - https://jamii.app/DaktariMbaroniHudumaMbovu
MKAKATI WA TAIFA DHIDI YA RUSHWA NA MPANGO WA UTEKELEZAJI (AWAMU YA 3: 2017-2022)

- Vitendo vya Rushwa vinatafsiriwa kuwa ni kutoa, kupokea au kushawishi moja kwa moja au kitu chochote cha thamani kinachotolewa ili kupindisha utaratibu katika Utoaji wa Maamuzi

#KemeaRushwa
WAZIRI KAMWELWE: MUDA WA KUSAJILI LAINI ZA SIMU HAUTAONGEZWA

> Serikali haitaongeza muda baada ya siku 20 alizoongeza Rais Magufuli kumalizika

> Wananchi wameshauriwa kuwa makini katika siku zilizosalia kwani Wizi wa Kimtandao umeongezeka

Soma - https://jamii.app/MudaUsajiliLaini-TZ
MISRI, ETHIOPIA NA SUDAN ZAINGIA MAKUBALIANO KUHUSU MATUMIZI YA MTO NILE

> Nchi hizo zimefikia Makubaliano ya Awali ya kujaza maji kwenye Bwawa la Grand Renaissance

> Makubaliano ya mwisho yatafanyika Washington, Januari 28-29 mwaka huu

Soma - https://jamii.app/MakubalianoMtoNile
UPINZANI NAMIBIA WAGOMA KUTUMIA KISWAHILI KAMA LUGHA YA HIYARI KWA SHULE ZA SERIKALI

> Wasema kuna mambo ya muhimu ya kushinikiza kwa wakati huu kuhusu Mfumo wa Elimu

> Wizara ya Elimu ilisema itafanya Kiswahili Lugha ya Hiari 2021

Soma zaidi https://jamii.app/KswahiliNamibia
TANZANIA vs KENYA vs UGANDA: UCHAGUZI WA RAIS

- Katiba ya Tanzania inasema Mshindi wa Urais ni yule atakayepata Kura Nyingi kuliko Mgombea mwingine

- Katiba za Kenya na Uganda zinasema Mshindi wa Urais ni yule atakayekuwa amepata Zaidi ya Nusu ya Kura zote

Zaidi, soma https://jamii.app/Katiba-TZvsUGvsKE

#Katiba
MWANAFUNZI AGOMA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA, ADAI HANA AKILI

> Amesema mbele ya Mkuu wa Wilaya kuwa, yupo tayari kufungwa na sio kusoma

> Aomba ajifunze kushona Cherehani kwani anatamani kuwa Mwanamitindo

Soma - https://jamii.app/MwanafunziAkataaMasomo
JENGA TABIA YA KUAGA KILA UNAPOTOKA KWA KUTOA TAARIFA SAHIHI

> Ni taarifa kama Jina la unakokwenda, Mtu na Anuani ya mtu unayekutana naye na Muda utakaokuwa haupo

> Hii itarahisisha upatikanaji wako pindi utakapopatwa na matatizo

Soma https://jamii.app/TabiaKuagaUnapotoka
#JFLeo