JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MADHARA YA MICHORO MWILINI (TATTOOS)

> Unaweza kukosa fursa mbalimbali kama kuajiriwa Jeshini

> Madhara mengine ni Saratani ya Ngozi, kuwa na aleji/mzio, matatizo kipindi cha kufanya kipimo cha MRI na kushindwa kuchangia damu

Soma https://jamii.app/MadharaTattoo
DEWJI AJIUZULU UENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SIMBA

- Mohamed Dewji ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya Simba kupoteza Fainali ya Kombe la Mapinduzi

- Amesema atabaki kama Mwekezaji, akiendeleza miundombinu na Soka la Vijana

Soma https://jamii.app/DewjiAjiuzuluSimba
BARCELONA YAMTUPIA VIRAGO KOCHA WAKE

- Klabu ya Barcelona imemfukuza Kocha Ernesto Valverde (55) na kumtangaza Kocha wa Zamani wa Real Betis, Quique Setien (61) kuchukua nafasi yake

- Inaelezwa kuwa, Barcelona chini ya Valverde, mara kadhaa imecheza Soka lisiloshawishi

#JFLeo
TAKUKURU ARUSHA: WATUHUMIWA 22 WALIPANDISHWA KIZIMBANI OKTOBA HADI DESEMBA, 2019

> Miongoni mwa watuhumiwa ambao walishtakiwa kipindi hicho ni Askari Polisi, Wafanyabiashara na Watumishi wa Umma na mashauri yao bado yanaendelea Mahakamani

Soma https://jamii.app/Mbaroni22-TakukuruAR
MAREKANI YAIONDOA CHINA KWENYE ORODHA YA WADHIBITI WA KIWANGO CHA KUBADILISHA FEDHA

> Ripoti iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani inasema, kwa sasa hakuna Nchi Mshirika wa Kibiashara wa Marekani anayefikia vigezo vya kisheria vya kudhibiti thamani ya sarafu yake

Soma - https://jamii.app/USCurrencyExchangeChina
DKT. BASHIRU: UCHAGUZI SIO NAMBA, UCHAGUZI NI UAMUZI WA UMMA

> Katibu Mkuu wa CCM amesema Uchaguzi sio Namba, Uchaguzi ni Uamuzi wa Umma, namba ni kitu cha baadae kwasababu Wananchi hufanya maamuzi kabla ya Siku ya Kupiga Kura, siku ya kupiga kura ndio siku ya kudhihirisha uamuzi wao

Soma - https://jamii.app/BashiruMaanaUchaguzi
KAMPUNI YA DHAHABU YA CANADA KUISHITAKI SERIKALI YA TANZANIA KWA KUKIUKA MIKATABA

> Kampuni ya Winshear Gold Corp imeitaarifu Serikali ya Tanzania nia ya kuishitaki kwenye Mabaraza ya Usuluhishi ya Kimataifa baada ya kukiuka Mikataba ya Uwekezaji kati ya Tanzania na Canada

> Ikiwa matokeo hayatapatikana ndani ya miezi 6 ijayo, Kampuni itawasilisha madai yake mbele ya Baraza la Usuluhishi la Kimataifa na kutafuta fidia kwa uharibifu

Soma - https://jamii.app/WinshearIntentSubmitArbitration
TIKETI ZOTE ZA MABASI KUKATWA KIELEKTRONIKI KUANZIA MWEZI UJAO

> Katibu wa TABOA, Enea Mruto amesema, Mfumo wa Kielektroniki utawarahisishia wateja kupata tiketi na kuondoa msongamano

> TABOA wanashirikiana na TRA kufanikisha mpango huu

Soma - https://jamii.app/ElectronicBusTickets
FAHAMU UNYANYASAJI WA WATOTO KWA WATOTO WAWAPO MASHULENI (BULLYING)

> Unyanyasaji wa watoto kwa watoto wawapo mashuleni unaweza kujidhihirisha katika namna nyingi ikiwemo kusukumwa hovyo, kupigwa, kuitwa majina yasiyofaa, matusi au vitisho

> Hali hii huweza kumuathiri mtoto kisaikolojia na kihisia na kumtengenezea mazingira ya kutokujiamini, kukosa furaha, kujiona ni mtu wa kushindwa kila siku na kujitenga na wenzake

Kwa mjadala zaidi - https://jamii.app/ChildBullyingSchools
MICHEZO: Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba @moodewji ametangaza kurudi kwenye wadhifa huo baada ya kutangaza kujiuzulu kutokana na mwenendo wa Timu hiyo kutokuwa mzuri

> Kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema “Mimi ni Simba damu damu, Tuko pamoja”

#JFMichezo
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI 4 KUIWAKILISHA TANZANIA KATIKA NCHI MBALIMBALI
-
Walioapishwa ni Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi kuwa Balozi Afrika Kusini, Dkt. Modestus Fransics Kipilimba kuwa Balozi Namibia
-
Wengine ni Profesa Emmanuel Mwaluko Mbennah kuwa Balozi Zimbabwe na Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi Nigeria

Soma - https://jamii.app/UapishoMabalozi
#JFLeo
NIGER: MKUU WA MAJESHI AFUKUZWA KUTOKANA NA WANAJESHI 89 KUUAWA

> Mkuu wa Jeshi la Niger amefukuzwa kazi kutokana Wanamgambo wa Kijihadi kuwaua wanajeshi 89 walipovamia Kambi ya Jeshi

> Viongozi wengine waandamizi 3 wa Jeshi hilo wamevulia nyadhifa zao baada ya Kikao cha Baraza la Mawaziri

Soma - https://jamii.app/ArmyChiefGenSackedNiger
PEMBA: MAALIM SEIF NA SALIM BIMANI WATUHUMIWA KUFANYA MKUTANO BILA KIBALI

> Viongozi hao kwa sasa wameachiwa kwa dhamana na Chama chao kupitia Mtandao wa Twitter kimedai walifanya Mkutano wa ndani usiohitaji kibali

Soma - https://jamii.app/ViongoziACTPolisi
RAIS WA ZAMBIA AYATAKA MATAIFA YA ULAYA KUACHA KUINGILIA UONGOZI WA AFRIKA

> Rais Edgar Lungu amesema, haikubaliki kwa watu wa nje kuamuru jinsi Nchi za Afrika zinavyopaswa kuongozwa kwasababu Afrika inapaswa kuruhusiwa kuamua jinsi inavyojitawala badala ya kuamrishwa na watu wa nje

Soma - https://jamii.app/OutsidersAfricanGovernment
TRAFIKI ANAYEDAIWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI HAJULIKANI ALIPO

> Polisi walisema wamemtia nguvuni, lakini taarifa zimedokeza kuwa hajawahi kamatwa

> Jumbe za simu, zinathibitisha mahusiano yao. Mtoto alisema hata simu alipewa na huyo polisi

Soma https://jamii.app/TrafikiMimbaMwanafunzi
TANZANIA vs KENYA: ISEMAVYO KATIBA KUHUSU KUSHTAKIWA KWA RAIS

- Katiba zote (Tanzania Ibara ya 46 (1) na Kenya Ibara ya 143 (1)) haziruhusu Rais kufunguliwa shauri la jinai awapo madarakani

- Ibara ya 143 (2) ya Katiba ya Kenya inapinga pia Rais kufunguliwa shauri la madai

- Ibara ya 46 (2) ya Katiba ya Tanzania inapinga Rais kufunguliwa shauri la Madai lakini inatoa vigezo vya kufungua shauri hilo

#Katiba #JFLeo
IRAN YAWAKAMATA WALIOITUNGUA KIMAKOSA NDEGE YA UKRAINE

> Tangazo limetolewa baada ya Rais Hassan Rouhani kutaka iundwe Mahakama Maalum kushughulikia mkasa huo

> Msemaji wa Mahakama, hakubainisha idadi ya watu waliotiwa mbaroni kuhusiana na mkasa huo

Soma https://jamii.app/UkrainePlaneShootArrest
MAMBO MUHIMU YA KUFANYA UNAPOHITAJI MSAIDIZI WA KUKULELEA MTOTO

> Fanya mahojiano na msaidizi kabla ya kumpokea. Endesha mafunzo kwa msaidizi ili kumjengea uwezo zaidi. Fuatilia maisha yake ili kujua historia yake

> Awe na umri wa miaka 18 na kuendelea. Malipo ya msaidizi yasiwe madogo sana. Jenga mahusiano mazuri na msaidizi. Zingatia elimu/ufahamu wa msaidizi

Some https://jamii.app/MsaidiziKuleaMtoto
#JFMalezi
WATU WENGI HUFARIKI KUTOKANA NA DAWA BANDIA ZILIZOSAMBAA AFRIKA

> Dawa hizo mara nyingi huwa zimeisha muda wake wa matumizi au ziko chini ya kiwango, au dawa za kughushi

> Kati ya asilimia 30 hadi 60 ya dawa bandia zinatoka China na India

Soma https://jamii.app/DeathFakeMedicines
IJUE SHERIA YA MTOTO TANZANIA

> Haki za Mtoto kwa Mujibu wa Sheria (2009) ni pamoja na Haki ya kuishi, Haki ya kupumzika, Haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa, Haki ya kutokubaguliwa, Haki ya kuishi na wazazi wake na Haki ya kupata huduma bora za elimu, malazi, matibabu kwa ajili ya ustawi wake

> Haki ya kushiriki michezo na shughuli za kiutamaduni,Haki ya kunufaika na kutumia kwa uangalifu mali za wazazi wake, Haki ya kutoa maoni, kusikilizwa na kutoa maamuzi na Haki ya kutoajiriwa katika ajira zenye madhara

Zaidi, soma - https://jamii.app/SheriaHakiMtoto
#JFSheria