JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Dkt Jonas Tiboroha, Meneja wa Simon Msuva, mchezaji wa Taifa Stars, amesema Msuva amejiunga na klabu ya Benfica ya Ureno kwa mkataba wa miaka 3 akitokea klabu ya Difaâ El Jadida

- Amesema ataanza kuitumikia Benfica Julai 2020 na sasa anaenda kwa mkopo katika klabu ya Panathinaikos ya Ugiriki
SADIO MANE ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2019

- Mchezaji huyo wa Senegal na Liverpool ameshinda tuzo hiyo dhidi ya Mohamed Salah (Liverpool, Misri) na Riyad Mahrez (Manchester City, Algeria)

- Anakuwa Msenegal wa pili kushinda tuzo hiyo baada ya El Hadji Diouf
VITA RASMI? IRAN YASHAMBULIA KAMBI ZA JESHI LA MAREKANI

> Imerusha makombora zaidi ya 10 ikilenga Majengo ya Marekani yaliyopo Kaskazini mwa Iraq zikiwemo Kambi za Ain al-Asad na Ebil

> Yaonya kufanya mashambulio zaidi iwapo Marekani itafanya shambulio jipya

> Trump asema kukicha (kwa muda wa Marekani) atatoa kauli rasmi

Soma https://jamii.app/IranShambuliKambiUSA
BREAKING: A Boeing 737 plane carrying 180 passengers and crew has crashed shortly after takeoff from Imam Khomeini Airport in Tehran

> The Ukranian Airlines plane crashed due to technical difficulties, according to ISNA

#PlaneCrash
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
IRAN: NDEGE YA UKRAINE ILIYOKUWA NA WATU 180 YAANGUKA

- Ndege hiyo imeanguka karibu na Mji wa Tehran dakika 3 baada ya kuruka ikitokea Uwanja wa Khomeini

- Hakuna taarifa zozote za majeruhi au vifo ila inaonesha hakuna mtu yeyote aliyepona

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeUkraineYaangukaIran
FAHAMU KUHUSU KIDOLE TUMBO (APPENDIX), DALILI ZAKE NA MATIBABU

> Kidole Tumbo hupatikana katika utumbo mkubwa na urefu wake ni kama kidole cha mwisho cha mkono. Huifadhi michanga au uchafu mdogomdogo kutoka kwenye chakula

> Dalili kuu ni maumivu ya tumbo kwenye kichembe au kitovu ambayo huongezeka kadiri muda unavyosogea na huambatana na kutapika, kushindwa kutembea na homa

> Kama ukichelewa kutibiwa, Appendix inaweza kuoza, kupasuka na kueneza uchafu ndani ya tumbo na damu na hivyo kusababisha kifo

Fahamu zaidi - https://jamii.app/DaliliTibaAppendix
#JFAfya
MIGUNA ATOLEWA KWENYE NDEGE KWA AMRI YA MAMLAKA ZA KENYA

- Air France jana imemshusha kwenye ndege Miguna Miguna aliyekuwa akielekea Nairobi

- Hatua hiyo inakinzana na taarifa ya awali, ambapo Serikali ilisema Miguna yupo huru kurejea Kenya

Soma https://jamii.app/AirFranceEjectsMiguna
CAMEROON: MLIPUKO WA BOMU WAUA 9 NA KUJERUHI 30

> Mlipuko umetokea baada ya kijana mmoja kuchukua kifaa cha kulipuka akidhani ni kipande cha chuma

> Tahadhari yatolewa juu ya uwepo wa mabomu na silaha ambazo zimetelekezwa au kupotea

Soma - https://jamii.app/DeathAccidentalBlast
UTAFITI MAREKANI: VIFO VITOKANAVYO NA ULEVI VYAONGEZEKA MARA 2

> Kulingana na uchambuzi mpya wa vyeti vya kifo, vifo vinavyohusiana na unywaji wa pombe kwa watu wenye umri wa miaka 16 na zaidi vimeongezeka kutoka vifo 35,914 mwaka 1999 hadi kufikia vifo 72,558 mwaka 2017

> Wanaofariki sana ni wanaume wenye umri wa kati huku wanawake nao wakishika kasi ktk utumiaji vilevi

Soma - https://jamii.app/AlcoholDeathRateUS
UFILIPINO YAWAONDOA RAIA WAKE IRAQ

> Serikali imeongeza kiwango cha tahadhari na kuwahitaji Wafilipino kuondoka kutokana na hatari

> Wafilipino wanaweza kuondoka peke yao au kusindikizwa kwa msaada wa waajiri wao au Serikali ya Ufilipino

Soma https://jamii.app/FranceRemoveCitizensIraq
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOFUNGUA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA

> Mdau wa JamiiForums anasema Biashara ya duka la rejareja inahitaji mtu kuwa na roho ngumu kwani njia pekee ya kuendeleza biashara ni kuwatolea imani wateja na kuwapa hofu ya kukopa

> Anashauri wanaotaka kuanzisha biashara hii kuisimamia ipasavyo, kuweka urafiki pembeni, kukopesha wateja waaminifu na kuepuka kutumia hela za biashara kwenye masuala binafsi

Soma - https://jamii.app/MsingiBiasharaDukaRejareja
#JFBiashara
IRAN: WANAJESHI 80 WA MAREKANI WAMEUAWA

- Chaneli ya Iran, imetoa taarifa hiyo huku ikiwaita Wanajeshi hao kama 'Magaidi wa Amerika'

- Haikuonesha kithibitisho ila imesema makombora yote yaliyorushwa katika Kambi za Ain al-Asad na Erbil, yalifika

Soma https://jamii.app/IranShambuliKambiUSA
SERIKALI YAZUIA WATOTO KUKATALIWA SHULENI KWA KUKOSA VYETI VYA KUZALIWA

> Waziri Selemani Jafo amesema ni marufuku mwanafunzi kuzuiliwa kuandikishwa Darasa la Kwanza kwasababu ya kukosa Cheti cha Kuzaliwa

> Ameagiza, Watoto wote wapokelewa na waanze masomo huku wazazi wao wakiendelea kuwatafutia vyeti hivyo ndani ya miezi 4

Soma - https://jamii.app/UandikishajiShuleChetiKuzaliwa
UINGEREZA YALAANI SHAMBULIO LA IRAN

> Kambi zilizoshambuliwa ni za Muungano wa Kijeshi wa Marekani na Uingereza

> Kauli hii imekuja baada ya Iran kurusha makombora kadhaa Kaskazini mwa Iraq ikiwemo Kambi ya Ain al-Asad

Soma https - https://jamii.app/LondonTalksIranAttack
ZANZIBAR KUJA NA ADHABU ZA PAPO KWA HAPO ILI KUDHIBITI AJALI BARABARANI

> Serikali ya Zanzibar inakusudia kutunga Sheria ya Adhabu za ‘’Papo kwa Hapo’’ ili kudhibiti ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva kutofuata Sheria za Barabarani

> Moja ya adhabu inayopendekezwa ni kunyang’anywa leseni kwa dereva aliyesababisha ajali

Soma - https://jamii.app/SheriaAdhabuAjaliZNZ
MGOGORO MASHARIKI YA KATI: BAADHI YA MATAIFA YAANZA KUONDOA MAJESHI YAO IRAQ

- Uhispania, Canada na baadhi ya Washirika wamesema baadhi ya Wanajeshi watapelekwa Kuwait

- Ni baada ya NATO kusema itawaondoa baadhi ya Wanajeshi wake Wakufunzi

Soma https://jamii.app/MataifaMajeshiIraq
MKAKATI WA TAIFA DHIDI YA RUSHWA NA MPANGO WA UTEKELEZAJI(2017-2022): Kuanzia Juni 2018 na kuendelea, katika jitihada za kuimarisha mapambano dhidi ya Rushwa; Serikali imeanzisha na kutekeleza mfumo wa kompyuta wa kushughilikia malalamiko katika Ofisi za Umma na Binafsi na kuwataka wasimamizi kutoa majibu ya hatua zinazochukuliwa kwa malalamiko yanayopokelewa