JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI YAKANUSHA KUTAKA KUONDOA MAJESHI YAKE IRAQ

> Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper amekanusha madai kuwa Majeshi yake yanataka kuondoka Iraq, baada ya barua kutoka kwa Jenerali wa Marekani kupendekeza waondoke

> Ni baada ya Wabunge wa Iraq kuwataka Wanajeshi hao waondoke

Soma - https://jamii.app/RemovalUSSoldiersIraq
FINLAND: WAZIRI MKUU APENDEKEZA SIKU NNE ZA KUFANYA KAZI KWA WIKI

> Waziri Mkuu Sanna Marin, amesema wananchi wana Haki ya kutumia muda mwingi na Familia zao

> Pia, Waziri huyo amependekeza kazi kufanywa kwa Saa Sita pekee kwa siku

Soma - https://jamii.app/Finland4DayWorkingWeek
SIMIYU: MAHITAJI YA CHANJO YA HOMA YA INI NI MAKUBWA KULIKO UWEPO WA CHANJO

> Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu inakabiliwa na Uhaba wa Chanjo kutokana na kasi kubwa ya wananchi wanaojitokeza kupima na kupatiwa chanjo ya Ugonjwa wa Homa ya Ini

> Ndani ya miezi 6, wananchi 251 sawa na 3.2% wamejitokeza kupata huduma ya Homa ya Ini na kati ya hao 8 waligundulika kuumwa

Soma - https://jamii.app/UhabaChanjoHomaIni
WATU 4 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KULISABABISHIA JESHI LA POLISI HASARA YA TSH. MILIONI 798.7

> Afisa wa Polisi, Emmanuel Mkilia na Wafanyabiashara 3, wamefikishwa Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kujipatia kiasi hicho cha pesa kutoka Jeshi la Polisi kwa kujifanya wameweka Mfumo wa Taarifa za Watuhumiwa waliokamatwa kwenye Vituo 8

Soma https://jamii.app/PolisiKizimbaniHasaraMil798
KLABU ZA UINGEREZA ZAMUWINDA NYOTA WA TANZANIA, MBWANA SAMATTA
-
Nahodha wa Timu ya Tanzania, Mbwana Samatta anaweza kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya England ambapo inadaiwa Klabu za Brighton, Crystal Palace na Norwich zinataka kumsajili
-
Samatta mwenye miaka 27, aliyeifungia Genk katika mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, ana 'Release Clause' ya Tsh. Bilioni 25.7 (Yuro Milioni 10) kwenye mkataba wake
-
Akiwa ametokea TP Mazembe mwaka 2016, Samatta alifanikiwa kuwa Mfungaji Bora katika Ligi ya Ubelgiji katika msimu ulioisha na kuwa Mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kushinda tuzo ya Coveted Soulier D’ébène
MVUTANO WA MAREKANI NA IRAN: MAREKANI YADAIWA KUMNYIMA 'VISA' WAZIRI WA IRAN

> Marekani imekataa kutoa 'Visa' kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif, ambaye alitarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York Alhamisi wiki hii

Soma - https://jamii.app/USDeniesVisaIranMinister
PEP GUARDIOLA: KAMWE SIWEZI KUFUNDISHA MANCHESTER UNITED NA REAL MADRID

> Kocha huyo wa Manchester City amesema bora aende likizo ya kufundisha soka kuliko kukubali kuifundisha Man UTD

> Je, unadhani nini kimepelekea kauli hii ya Pep?

Soma > https://jamii.app/GuardiolaVsManUtd

#JFSports
TETEMEKO LA 6.5 LAIKUMBA PUERTO RICO NA KUATHIRI MAKAZI NA HUDUMA ZA KIJAMII

> Tetemeko hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, likiwa ni kubwa zaidi katika matetemeko ambayo yamepiga maeneo ya Amerika siku za hivi karibuni

> Limefuatana na lingine lenye ukubwa wa 5.8 ambalo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu

Soma - https://jamii.app/EarthquakesPuertoRico
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KISUTU: KESI YA TITO MAGOTI YAPIGWA TENA KALENDA

- Kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi imeahirishwa hadi Januari 21 baada ya Jamhuri kudai upelelezi haujakamilika

- Upande wa Utetezi umetoa rai kwa Jamhuri kutokamata Watu kabla haijapeleleza

Soma https://jamii.app/KesiMagotiKalenda
NJIA 6 ZA KUPATA MATOKEO CHANYA KUTOKA KWA MTOTO

> Njia zinazoweza kumuwezesha mzazi/mlezi kupata matokeo mazuri katika kumkuza na kumuendeleza mtoto wake kijamii, kiafya, kielimu au kitabia ni hizi zifuatazo:

> Kumrubuni mtoto wako. Kupongeza mtoto wako. Kuadhibu mtoto wako. Kumtishia mtoto wako. Kumfundisha mtoto wako. Kuwa mfano kwa mtoto wako

> Njia za kuleta matokeo chanya kwa watoto zipo nyingi na kila moja inafanya vizuri katika hali tofautitofauti, hakuna hata njia moja kati ya hizo nilizozieleza hapo juu ambayo inaweza kuingia katika kila hali kwenye maisha ya mtoto

SOMA: https://jamii.app/MatokeoChanyaMtoto
#JFMalezi
UJUMBE WA LEO KUTOKA TAKUKURU: Mtumishi yeyote akiwa ni muumini wa Rushwa hafai kuwa Mtumishi wa Umma. Jukumu la kupambana na Rushwa ni la kila mmoja wetu.

#KemeaRushwa
BASATA YAMFUTIA USAJILI DUDU BAYA

- Godfrey Tumaini maarufu 'Dudu Baya' amefungiwa kujishughulisha na shughuli zozote za sanaa kuanzia leo

- Dudu Baya aligoma kwenda BASATA jana alikoitwa kuhojiwa juu ya video zake zenye maneno yasiyo na maadili

Zaidi, soma https://jamii.app/BasataUsajiliDudubaya
MIGUNA MIGUNA ASHINDWA KURUDI KENYA, AZUIWA BERLIN

> Tahadhari ilitolewa asiondoke Uwanja wa Berlin kuelekea JKIA Kenya au nchi yoyote Afrika

> Zuio hili linakuja baada ya Mahakama ya Juu kuagiza Serikali kumruhusu Miguna kurejea nchini humo

Zaidi, soma - https://jamii.app/MigunaAzuiwaAirportGRM
IRAN: WATU ZAIDI YA 35 WAFARIKI KWENYE TUKIO LA KUAGA MWILI WA JENERALI SOLEIMAN

> Waombolezaji zaidi ya 35 wamepoteza maisha huku wengine takriban 200 wakijeruhiwa kutokana na msongamano wa mamilioni ya watu waliojitokeza mjini Kerman kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jenerali Qasem Soleimani aliyeuawa na Marekani

> Kifo chake kimeleta mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran huku Iran ikitishia kulipiza kisasi

Soma - https://jamii.app/DeathsSoleimanMemorial
DODOMA: MWANACHUO ANASWA NA TAKUKURU AKIJARIBU KUHONGA AONGEZEWE UFAULU

> TAKUKURU inatarajia kumfikisha Mahakamani James Kwangulija, mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa Shahada ya Kwanza ya Ualimu Chuo Kikuu cha St. John na wenzake sita kwa kutoa hongo ya Tsh. 900,000 kwa Msimamizi wa Mitihani

> James ametenda makosa hayo Kinyume cha Kifungu cha 15 (1)b cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329, Marejeo ya 2018

Zaidi Soma https://jamii.app/MwanachuoMbaroniRushwa
Baadhi ya maoni ya Wananchi waliyoyatoa katika Mitandao ya Kijamii kupitia kurasa za JamiiForums baada ya Hospitali ya Mloganzila kujibu tuhuma za kulalamikiwa kuwa kumekuwa kukitokea vifo vingi katika Hospitali hiyo

- Katika majibu yake, Hospitali hiyo ilisema vifo vya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo vimepungua kutoka asilimia 14.9 iliyokuwepo katika kipindi cha Julai - Septemba 2018 hadi asilimia 10.4 kipindi kama hicho 2019
MWANZA: WATU 7 MBARONI KWA KUJIFANYA MAAFISA USALAMA WA IKULU

- Wamekuwa wakiwatapeli Wananchi na baadhi ya Watumishi wa Serikali kwa kujifanya wako katika kazi maalum

- Walikuwa wakitumia gari walilodai ni sehemu ya Msafara wa Viongozi Wakuu

Zaidi, soma https://jamii.app/Matapeli7Mbaroni-MWZ
MICHEZO: Dkt Jonas Tiboroha, Meneja wa Simon Msuva, mchezaji wa Taifa Stars, amesema Msuva amejiunga na klabu ya Benfica ya Ureno kwa mkataba wa miaka 3 akitokea klabu ya Difaâ El Jadida

- Amesema ataanza kuitumikia Benfica Julai 2020 na sasa anaenda kwa mkopo katika klabu ya Panathinaikos ya Ugiriki
SADIO MANE ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2019

- Mchezaji huyo wa Senegal na Liverpool ameshinda tuzo hiyo dhidi ya Mohamed Salah (Liverpool, Misri) na Riyad Mahrez (Manchester City, Algeria)

- Anakuwa Msenegal wa pili kushinda tuzo hiyo baada ya El Hadji Diouf