JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
VIDEO: Sehemu ya Umati wa Watu iliyojitokeza kupokea mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Iran, Jenerali Qassem Soleimani aliyeuawa na Marekani huko Iraq

- Maelfu ya Watu wamejipanga katika mitaa ya Miji ya Ahvaz na Mashhad huko Iran kutoa salamu za Mwisho
MOMBASA, KENYA: MCHUNGAJI AMUUA KWA KISU MKEWE NA YEYE KUJIUA

> Imeelezwa, Mchungaji Elisha Misiko wa Kanisa la Ground For Gods Gospel (3G) Ministries alimshambulia kwa kisu mkewe kisha na yeye kujiua

> Tukio hili limetokea wakati Ibada ya Jumapili ikiendelea

Soma > https://jamii.app/MauajiKanisani
KIGOMA: ZAIDI YA WATOTO 600 HUZALIWA KILA MWEZI KTK KAMBI ZA WAKIMBIZI

> Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoani humo wameeleza kutishwa na kasi kubwa ya kuzaliana kwa wakimbizi hao na hivyo wameitaka Serikali kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo ili kukabiliana na madhara makubwa siku zijazo ikiwemo baadhi ya wakimbizi hao kudai Taifa lao ndani ya Tanzania

Soma - https://jamii.app/IdadiKuzalianaWakimbizi
INDONESIA: JENGO LA GHOROFA 5 LAPOROMOKA MJINI JAKARTA

> Jengo hilo limeanguka leo asubuhi na mpaka sasa watu 8 wanadaiwa kujeruhiwa huku Mamlaka zikiendelea na zoezi la uokoaji kutokana na baadhi ya Raia kunasa kwenye vifusi

> Bado haijafahamika chanzo cha kuanguka kwake lakini inadhaniwa huenda ikawa imesababishwa na mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita

Soma - https://jamii.app/5StoreyBuildingCollapses
TABORA: MFAMASIA KIZIMBANI KWA KUIBA ARV HOSPITALINI

- Ni Francis Mlesa (33) ambaye ni Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga

- Anadaiwa kuiba chupa 30 za vidonge vya kufubaza Virusi vya UKIMWI (ARV) zenye thamani ya Tsh. 2,116,000

Soma https://jamii.app/MfamasiaKizimbani-TBR
KENYA: WATATU WAFARIKI KATIKA SHAMBULIO LA AL-SHABAAB

- Raia watatu wa Marekani wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa jana kwenye Kambi ya Jeshi iliyopo Lamu

- Pia, ndege 6 za jeshi ziliharibiwa katika tukio hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/WamarekaniWauawaLamu
MGOGORO WA MADARAKA VENEZUELA: BUNGE KUONGOZWA NA MASPIKA WAWILI

> Mpinzani wa Rais wa Venezuela, Juan Guaido amechaguliwa tena kuwa Spika wa Bunge na Wabunge wa Upinzani saa chache baada ya Mbunge mwingine wa upinzani, Luis Parra, kujitangaza kuwa Spika wa Bunge hilo

> Rais Nicolas Maduro amemtambua Luis Parra kama Spika mpya wa Bunge

Soma - https://jamii.app/VenezuelaParliamentaryCoup
CAG: WASIORUDISHA MIKOPO WANAKWAMISHA HESLB KUKOPESHA WANUFAIKA WENGINE

- Kuadimika kwa wanufaika hao kumepelekea uwezo wa Bodi kutoa mikopo kuwa mdogo

- HESLB imeshauriwa kushirikiana na Vyanzo/Taasisi nyingine kuboresha Kanzi Data yake

Soma - https://jamii.app/CAGTril1Mikopo
FAHAMU HISTORIA YA UTANI KATI YA KABILA LA WAHEHE NA WANGONI

> Utani wa kikabila unaaminika kuwa ni matokeo ya vita. Makabila mengi ambayo ni watani inadaiwa yaliwahi kupigana hapo zamani. Inadaiwa Wahehe na Wangoni waliwahi kupigana na hakukupatikana mshindi na ndipo walianza utani kila moja akitamba kuwa bora kuliko mwenzie

> Utani wa makabila haya mawili ni utani wenye heshima ambapo watu wa rika moja ndio ambao hutaniana, hauhusishi matusi kama ulivyo utani wa baadhi ya makabila

Je, unafahamu historia gani ya utani wa kikabila?

Zaidi, soma - https://jamii.app/UtaniKabilaNgoniHehe
#JFHistoria
ARUSHA: OFISI YA NIDA YAIBIWA VIFAA VYOTE VYA KAZI

- Ofisi ndogo za NIDA zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha zimeibiwa vifaa vya kazi

- Vifaa vilivyoibwa ni Kompyuta 4 na Kamera 3 pamoja na vifaa vingine vya kuingiza majina kwenye mfumo

Zaidi, soma https://jamii.app/WiziOfisiNIDA-AR
TRUMP AITISHIA IRAQ IWAPO ITAYAONDOA MAJESHI YA MAREKANI NCHINI MWAO

- Amesema iwapo Iraq itataka Majeshi yaondoke nchini humo wataiwekea vikwazo vya kiuchumi ambavyo havijawahi kutokea

- Amedai wamewekeza Mabilioni ya Dola kwenye Jeshi lililopo Iraq

Zaidi, soma https://jamii.app/IraqVsUSA
KENYA: WATU 4 WAKAMATWA KWA TUHUMA KUZICHUNGUZA KAMBI ZA JESHI

> Watu 3 wamekamatwa kwa kujaribu kuingia ndani ya Kambi ya Jeshi la Uingereza mjini Nanyuki, Kaunti ya Laikipia huku mtu mwingine akidaiwa kukutwa akipiga picha za Kambi ya KDF(Kenya Air Force Moi Air Base)

> Watatu hao ni Wakenya na mpiga picha Raia wa Canada

Soma - https://jamii.app/SuspectsSpyingMilitaryBases
MJUE BONDIA ALIYEKUWA ANAPIGANA KAMA KALEWA MAARUFU 'THE DRUNKEN MASTER'

> Emanuel Augustus/Emanuel Burton alianza mapambano kama bondia mwaka 1990 hadi mwaka 2011 ambapo watu wengi walikuwa hawaipendi tabia yake ya kujifanya kalewa akiwa ulingoni

> Alinyimwa ushindi mara nyingi na katika rekodi ya mapambano 78 aliyopigana, alishinda mapambano 38 pekee, huku mapambano 20 akishinda kwa Knock Out

Soma - https://jamii.app/HistoriaBondiaDrunkenMaster
MSHAMBULIAJI WA TP MAZEMBE ATUA NCHINI KUJIUNGA NA YANGA

- Yanga leo imethibitisha kumpokea mshambuliaji kutoka TP Mazembe ya Congo, Owe Bonganya

- Amekuja kwa mazungumzo ya kujiunga na Yanga na ataungana na kikosi kilichopo Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mpinduzi
AUSTRALIA: MOTO KATIKA MISITU WAUA WATU 20, WANYAMA 500 NA KUTEKETEZA EKARI MILIONI 15

> Huu ni moto mkali kuwahi kutokea na mpaka sasa zaidi ya tani 250 za 'Carbondioxide' zimezalishwa

> Moto huo unatabiriwa kuendelea kuwaka kwa wiki 1 zaidi

Soma https://jamii.app/BushFiresAustralia
POLISI YAMKAMATA BOBI WINE, YASIMAMISHA MKUTANO WA UPINZANI

- Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine na viongozi wengine wa upinzani wamekamatwa leo

- Walikuwa wakienda kuhudhuria mkutano ambapo Bobi angeeleza mipango yake ya Uchaguzi mwaka 2021

Soma https://jamii.app/BobiWineArrestedJan2020
KENYA: MTOTO WA MIAKA 10 AJITAHIRI KWA KISU

> Afanya kitendo hicho akihofia kutengwa na wenzake ambao tayari wametahiriwa

> Hali yake sio nzuri na wazazi wamelazimika kumrudisha nyumbani baada ya kushindwa kugharamia matibabu hospitalini

Soma - https://jamii.app/MtotoAjitahiriKisu
HOSPITALI YA MLOGANZILA YAJIBU TUHUMA ZA WAGONJWA WENGI KUFARIKI HOSPITALINI HAPO

> Taarifa ya hospitali imetaja kupungua kwa vifo vya wagonjwa kutoka 14.9% katika kipindi cha Julai - Septemba 2018 hadi 10.4% kipindi kama hicho 2019

> Pia, imekanusha madai ya kuwepo kwa madaktari wanafunzi na kusema kuna madaktari bingwa 52, madaktari wa kawaida 50 na madaktari tarajali 53

Soma - https://jamii.app/MloganzilaYajibuShutuma