JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ORODHA YA MATAJIRI DUNIANI: JEFF BEZOS BADO ANAONGOZA KWA UTAJIRI

- Kwa mujibu wa Bloomberg Billionaire Index, Mwanzilishi wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos anaongoza kwa utajiri

- Ni tofauti na ilivyotarajiwa kuwa atapoteza nafasi hiyo baada ya kupeana talaka na mkewe
MWANZA: ACHANWA TUMBO KWA KUHOJI MATUMIZI YA FEDHA ALIYOACHA NYUMBANI

- Ni Benedictor Gogogo (48) anayesema alimuachia mkewe Tsh. 10,000

- Amesema alichanwa akiwa amelala baada ya kumpiga kofi mkewe aliyemjibu vibaya kuhusu matumizi yake

Zaidi, soma https://jamii.app/MkeAmtoaMumeUtumbo
KENYA: WATATU WAFARIKI BAADA YA AL-SHABAAB KUTEKA BASI

- Kamishna wa Polisi wa Kaunti ya Lamu amesema Washambuliaji hao wamewaua watu hao na kuwajeruhi wengine watatu katika eneo la Nyongoro kwenye barabara ya Lamu-Garsen

Zaidi, soma https://jamii.app/AlShabaabAttackBus-KE
NJOMBE: MBARONI KWA KUMPIGA NA KUMSABABISHIA KIFO MKEWE

- Josephat Mtega (24) anashikiliwa kwa tuhuma za kumsababishia kifo mkewe kutokana na majeraha ya kipigo

- Angelina Sanga (24) anadaiwa kupigwa vibaya na Josephat baada ya kugombana

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniKifoMkewe
MAREKANI YAMUUA KIONGOZI WA VIKOSI VYA QUDS VYA JESHI LA IRAN

- Jenerali Qasem Soleimani ameuawa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Baghdad

- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Javad Zarif amesema hatua hiyo ni hatari na uchokozi wa Kishenzi

Zaidi, soma https://jamii.app/KiongoziQudsAuawa
TABORA: POLISI KUANZA MSAKO WA WANAOTAKA KUJINYONGA

- Kamanda wa Polisi mkoani humo, Barnabas Mwakalukwa amesema kufuatia matukio ya watu wawili kujinyonga, mwaka huu wataanza msako kuwabaini wanaotaka kujinyonga na kuwapeleka Mahakamani

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKusakaWanaotakaKujinyonga
MAREKANI YAWATAKA WANANCHI WAKE KUONDOKA IRAQ

- Ubalozi wa Marekani nchini Iraq umewataka Raia wake wanaoishi nchini humo kuondoka mapema iwezekanavyo

- Ni kutokana na kuongezaka kwa vurugu ambapo Ubalozi huo pia umezingirwa na Waandamanaji

Zaidi, soma https://jamii.app/MarekaniRaiaKuondokaIraq
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
LUDACRIS NA FAMILIA YAKE WAPATA URAIA WA GABON

- Mwanamuziki wa Marekani, Christopher Brian Bridges maarufu Ludacris, sasa ana uraia wa Gabon na atakuwa na uraia wa nchi mbili

- Ludacris, Mkewe, Eudoxie Mbouguiengue na familia yake walipatiwa Uraia huo Januari 02, 2020
KAGERA: BABA WA KAMBO AMUUA MTOTO WA MIAKA MITATU

- Leonard Kishenya (36), amemuua mtoto wake wa kambo Caren Crispine (3) kwa kumkata na panga

- Anatuhumiwa kufanya hivyo baada ya kuzuka ugomvi kati yake na mke wake, Domina Andrew (30)

Zaidi, soma https://jamii.app/BabaKamboAmuuaMtoto
TUNDURU: SHEREHE WANAZOFANYIWA DARASA LA SABA ILI WAKAOLEWE, ZAPIGWA MARUFUKU

> DC wa Tunduru, Julius Mtatiro ameiambia JamiiForums sherehe hizo huhusisha Wazazi kushona sare na kuwapokea kwa maandamano Wanafunzi baada ya kumaliza mitihani

Soma > https://jamii.app/MtatiroVsWazaziTunduru
TETESI: ARSENAL YAMTAKA BOATENG. CHELSEA KUKOMAA KWA DEMBELE

- Arsenal inadaiwa kumuwinda beki wa Bayern Munich, Jerome Boateng (31) anayedaiwa kutaka kuondoka

- Chelsea inahusishwa kumjumuisha Olivier Giroud katika kumnunua Moussa Dembele baada ya Lyon kukataa £34m
SIMBA YAMSAJILI MIQIUSSONE KUTOKA UD SONGO

- Simba leo imemtambulisha kiungo wa Kimataifa wa Msumbuji, Luis Jose Miqiussone aliyesaini mkataba wa miaka minne

- Awali, kiungo huyo alikuwa akihusishwa na Yanga, lakini miamba hiyo ya Msimbazi imefanikiwa kuipata saini yake
KARIAKOO DERBY: SIMBA NA YANGA KUTUNISHIANA MISULI LEO

- Wakati homa ya mchezo wa Watani wa Jadi ikiendelea kupanda, katika mechi 10 zilizopita Simba imefunga magoli 10 kipindi cha pili na katika kipindi cha kwanza imefunga magoli 10

- Yanga nayo imekuwa moto kipindi cha pili kwa kufunga magoli 8 na katika Kipindi cha kwanza imefunga magoli 6

Je, ni Mashabiki wa timu gani kutoka na kicheko leo Taifa?

Fuatilia https://jamii.app/YanayojiriSimbaYanga
IRAQ: MAZISHI YA QASSEM SOLEIMANI YAFANYIKA

> Maelfu ya Raia wa Iraq wamekuwa wakiimba 'Kifo cha Marekani' wakati wa mazishi ya Kamanda, Qassem Soleimani na Mkuu wa Jeshi la Akiba Abu Mahdi al-Muhandis

> Makamanda hao maarufu wameuawa kwa shambulio la anga lililofanywa na Marekani
MWANAHABARI WA DW ADAIWA KULISHWA SUMU

> Deokaji Makomba amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kufikishwa akiwa hajitambui

> Ndani ya Basi la Ally's alipewa vipande vya Biskuti na abiria aliyepandia njiani

Soma > https://jamii.app/DeokajiSumuBasi
MICHEZO: Klabu ya Simba inapata goli la kuongoza dhidi ya Klabu ya Yanga kupitia goli lililofungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 42

- Goli la Simba limepatikana kupitia mkwaju wa penati baada ya Meddie Kagere kuchezewa rafu na Beki Kelvin Yondani ndani ya eneo la hatari

Fuatilia https://jamii.app/YanayojiriSimbaYanga