JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RAIS MAGUFULI AZURU KISIWA CHA RUBONDO

- Rais Magufuli akiwa safarini kuelekea Kisiwa cha Rubondo leo asubuhi. Rubondo ni moja ya Hifadhi za Taifa 22 zilizopo hapa nchini

- Itakumbukwa kuwa ndege moja ya ATCL ina jina la Hifadhi hiyo iliyopo katika Ziwa Victoria
TETESI ZA SOKA ZA USAJILI IKIWA BADO SAA CHACHE DIRISHA KUFUNGULIWA

- Inadaiwa Everton inaongoza katika mbio za kumsajili Mchezaji wa Real Madrid, James Rodriguez huku Manchester United ikidaiwa kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Everton, Dominic Calvert-Lewin

- Liverpool inadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Sevilla, Diego Carlos huku Chelsea ikielezwa kuzungumza na RB Leipzig ili kuangalia uwezekano wa kumsajili Mshambuliaji, Timo Werner
RAIS MAGUFULI: KIGWANGALLA NA PROF. MKENDA MALIZENI TOFAUTI ZENU. VINGINEVYO NAWATENGUA

> Ametoa siku 5 na kama watashindwa kufanya hivyo atatengua teuzi zao. Dkt. Hamis Kigwangalla ni Waziri wa Maliasili na Prof. Mkenda akiwa Katibu Mkuu

> Akiwa katika Hifadhi ya Rubondo amesema Katibu Mkuu hataki kumheshimu Waziri na Waziri hataki kwenda pamoja na Katibu Mkuu

> Rais Magufuli amesema anawatazama taratibu. Hawezi kuwa na watendaji aliowateua halafu kila siku wanagombana na mambo ndani ya Wizara hayaendi.

Soma > https://jamii.app/KigwangallaVsMkenda
VIETNAM: WAZIRI WA ZAMANI AFUNGWA MAISHA KWA MAKOSA YA RUSHWA

- Son Bac Nguyen amefungwa maisha huku aliyekuwa Naibu wake, Tuan Quoc Tran akihukumiwa kifungo cha miaka 14 kwa makosa ya rushwa yaliyoisababishia Serikali hasara ya USD Milioni 3

Zaidi, soma https://jamii.app/WaziriAfungwaMaisha-Vietnam
MTANDAO WA SIMU WA MTN WASHUTUMIWA KUFADHILI MAGAIDI

- Inadaiwa kutoa rushwa kwa Al-Qaeda na Taliban ili isitoe pesa nyingi za kulinda mitambo yao Afghanistan

- Fedha hizo zinadaiwa kutumika kwenye mashumbulio kati ya mwaka 2009 hadi 2017

Zaidi, soma https://jamii.app/MTNShutumaUgaidi
KOREA KUSINI: WAZIRI WA ZAMANI ASHTAKIWA KWA MAKOSA YA RUSHWA

- Waziri wa zamani wa Sheria, Cho Kuk ameshtakiwa kwa makosa 11 yakiwemo ya rushwa, uzuiaji wa Biashara na kughushi na madai mengine yanayohusiana na kashfa dhidi ya familia yake

Zaidi, soma https://jamii.app/WaziriAshutumiwaRushwa-SK
WAYNE ROONEY ASAJILIWA RASMI KUWA MCHEZAJI WA DERBY COUNTY

- Rooney (34) amejiunga rasmi na Derby County kwa mkataba wa miezi 18 hadi majira ya joto mwaka 2021

- Pia, atakuwa akijifunza mbinu za Ukocha kutoka kwa Kocha wa Rams, Phillip Cocu
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MAWAKILI NJE YA OFISI ZA NIDA

- Imesema haiwatambui wanaojiita Mawakili na kuwatoza Wananchi Tsh. 10,000 kama ada ya nyaraka mbadala ya Cheti cha Kuzaliwa

- Imesema kila ofisi ya NIDA itakuwa na Mawakili wa Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliMawakiliNIDA
PAPA FRANCIS AOMBA RADHI KWA KUMPIGA KIBAO MUUMINI

- Alimpiga kibao Mwanamke aliyemvuta mkono kwa nguvu wakati akisalimia watu kwenye Usiku wa Mwaka Mpya

- Amesema, "Tunapoteza uvumilivu muda mwingine. Naomba radhi kwa mfano mbaya nilioutoa"

Zaidi, soma https://jamii.app/RadhiPapaKibaoMwanamke
MBEYA: JENEZA LATELEKEZWA SOKONI LIKIWA JUU YA MEZA MBELE YA DUKA MOJA

- Wananchi wamepigwa na bumbuwazi baada ya kukuta Jeneza hilo asubuhi ya Mwaka Mpya

- Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa jeneza hilo lilikuwa limetumika

Zaidi, soma https://jamii.app/JenezaSokoniMbeya
SHINYANGA: ASKARI WA JESHI LA POLISI AKATWA UUME NA MKEWE KWA TUHUMA ZA USALITI WA NDOA

> Jeshi la Polisi linamshikilia, Frola Adam (23), kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata uume mume wake, anayefahamika kwa jina la Kazimiri

Soma > https://jamii.app/AskariAkatwaUume

#JFLeo
MBEYA: MBARONI AKIWA NA MIHURU 56 YA KUGHUSHI YA IDARA ZA SERIKALI

- Abraham Obedi (55) amekamatwa na mihuri hiyo ya Idara za Serikali na Ofisi Binafsi

- Baadhi ya mihuri ni ya Afisa biashara wa Halmashauri, Access Bank-Mbeya na TRA-Mbeya

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniMihuriKughushi
YANGA YAMTEUA ABEID MZIBA KUWA KAIMU MENEJA WA TIMU

- Imemteua Mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dismas Ten

- Dismas alisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa kina kuhusu sakata la Wachezaji wa klabu hiyo kuvaa jezi feki