JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MATUMIZI YA SIMUJANJA KUONGEZEKA KWA KASI IFIKAPO 2024

> Utumiaji wa Simujanja (Smartphones) unakadiriwa kuongezeka kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya intaneti katika kiwango cha (3G) na mtandao wa 4G

> Usajili wa Simujanja utakua kwa haraka kila mwaka kwa 19% ambapo utahitajika usajili wa zaidi ya watumiaji milioni 30 ifikapo mwishoni mwa 2024

Soma - https://jamii.app/SmartphoneSubscriptionsGrowth
RAIS MAGUFULI AAGIZA VIJANA 800 WA JKT KUAJIRIWA

> Ameagiza vijana 800 wenye Shahada waliojitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa miaka 2 kuajiriwa Serikalini kuanzia Februari 2020

> Katika kipindi cha 2019/20 Serikali imetangaza nafasi 40,000 na ajira ambazo zinaanza Februari

Soma - https://jamii.app/AjiraSerikaliVijanaJKT
VIWANJA VYA NDEGE 208 VYAFUNGIWA KWA KUSHINDWA KUFUATA KANUNI ZA USAFIRI

> Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzani (TCAA) imetangaza kuvifunga viwanja hivyo vidogo baada ya kubainika kushindwa kufuata Kanuni za Usafiri wa Anga

> Kanuni zinakataza uendeshaji wa viwanja vya ndege bila kupata usajili au leseni inayotolewa na TCAA

Soma - https://jamii.app/ViwanjaNdege208Vyafutwa
Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo akifanya ufunguzi wa Choo kilichojengwa kwa Ufadhili wa Shirika la ADD International

> Ufunguzi huu umefanyika siku ya jana Desemba 22, 2019
MPYA: MWANDISHI BOLLEN NGETTI ADAIWA KUTEKWA NA WATU WASIOJULIKANA

Ikiwa ni siku 4 tangu Afisa wa Program na Elimu kwa Umma wa LHRC, Tito Magoti “atekwe” na watu wasiojulikana, zipo taarifa za hivi punde kwamba mwandishi wa Habari Bollen Ngetti naye ametekwa na wasiojulikana muda mfupi uliopita maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam

Watekaji wanadaiwa kutokomea na mwandishi huyo kusikojulikana

Tunaendelea kufuatilia ukweli wa taarifa hizi na tutawajuza kadri tutakavyopata taarifa zaidi

#FreeBollenNgetti #FreeTitoMagoti
UFILIPINO: WATU 11 WAFARIKI NA 300 KULAZWA BAADA YA KUNYWA POMBE YA MNAZI

> Takriban watu 11 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 300 kulazwa baada ya Kunywa Pombe ya mnazi walipokuwa kwenye sherehe za maandalizi ya Sikukuu ya Krismasi

> Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Laguna na Quezon, Kusini mwa Mji wa Manila ambapo kinywaji hicho hutumiwa sana kipindi cha sherehe na sikukuu

Soma - https://jamii.app/DeathCoconutAlcohol
IRINGA: MAHAKAMA YAMUACHIA HURU ABDUL NONDO KATIKA RUFAA ILIYOFUNGULIWA NA SERIKALI DHIDI YAKE

> Rufaa iliyokuwa imefunguliwa na Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Omary Nondo imetolewa hukumu ambapo Jamhuri imeshindwa kuithibitishia Mahakama Kuu kulingana na sababu za rufaa zilizoletwa

Soma - https://jamii.app/NondoAachiwaMahakama
MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA BOEING ATANGAZA KUJIUZULU

> Dennis Muilenburg ajiuzulu baada ya Boeing kusitisha kwa muda uzalishaji wa ndege aina ya Boeing 737 Max

> Boeing walichukua uamuzi huo baada ya ndege 2 aina kupata ajali na kuua watu zaidi ya 300

Soma https://jamii.app/BoengCEOAjiuzulu

#JFLeo
SAUDI ARABIA: MAHAKAMA YAWAHUKUMU KIFO WATU 5 KWA MAUAJI WA JAMAL KHASHOGGI

> Mahakama imesema hakukuwa na ushahidi wa kuhusika kwa Maafisa wa juu wa Serikali ktk mauaji hayo

> Mwana Mfalme, Mohammed bin Salman alikuwa akituhumiwa husika

Soma > https://jamii.app/WauajiKhashoggi
#JFLeo
SHERIA: OFISI YA MSAJILI INAWAJIBIKA KUHAKIKISHA MAWASILIANO MAZURI KATI VYAMA NA SERIKALI

> Kusimamia Chaguzi za ndani za Vyama vya Siasa na kuhakikisha ziko Huru na Haki

> Kutoa muongozo na taratibu za mapato na matumizi ya fedha ndani ya Vyama vya Siasa

Soma > https://jamii.app/AheriaVyamaSiasa
CHINA YATANGAZA KUPUNGUZA USHURU KWA BIDHAA ZA KIGENI

> Itapunguza ushuru kuanzia Januari 2020 kwenye zaidi ya bidhaa 850 ikiwemo Nyama ya Nguruwe, Dawa za Pumu na baadhi ya Vifaa vya Teknolojia

> Tangazo hilo linafuatia makubaliano ya muda ya kibiashara na Marekani katika Vita vya Ushuru wa Bidhaa

Soma - https://jamii.app/ChinaUshuruBidhaaNje
FAIDA ZA KUTOA PONGEZI KWA MTOTO WAKO

> Pongezi hutoa hamasa kwa watoto kufanya mambo mazuri zaidi: Tabia inayopongezwa hukua zaidi na inayoadhibiwa hudumaa zaidi katika maisha ya mtoto

> Kwa kumpongeza mtoto wako utamfanya ajue kuwa unafuatilia juhudi zake hali itakayomfanya azidishe kufanya mambo mazuri anayoyafanya au kuyakamilisha

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/FaidaKupongezaMtoto
BENKI YA AfDB YATOA FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA TANZANIA NA KENYA

> Benki ya Maendeleo Afrika yatoa Euro milioni 345 kusaidia ujenzi wa barabara za Mombasa-Lunga, Lunga/Horohoro na Tanga-Pangani-Bagamoyo katika awamu ya kwanza

> Umoja wa Ulaya umechangia Euro milioni 30 ikiwa ni asilimia 7.7 ya gharama za mradi kwa Serikali ya Kenya

Soma - https://jamii.app/AfDBFedhaUjenziTzKe
KENYA YATOA TAHADHARI YA DALILI ZA UWEPO WA SHAMBULIO LA KIGAIDI

> Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari kuhusu vitisho vya uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya

> Inspekta Jenerali wa Polisi amewataka wananchi kuwa waangalifu katika maeneo ya kuabudu na katika vituo vya usafiri wa umma

Soma - https://jamii.app/TahadhariUgaidiSikukuu
INDONESIA: TAKRIBAN WATU 26 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA BASI KUANGUKA MTONI
-
Takriban Watu 26 wamepoteza maisha na wengine 13 kujeruhiwa nchini Indonesia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupoteza uelekeo na kuanguka katika korongo la Mto
-
Ajali hiyo ilitokea jana usiku katika Mkoa wa Sumatra Kusini mwa nchi hiyo ambapo basi hilo lilikuwa limebeba abiria karibu 50
-
Zoezi la uokoaji bado linaendelea kutokana na baadhi ya abiria kutoonekana na hivyo huenda wakawa wamepotelea ndani ya mto
BOLLEN NGETTI APATIKANA MAENEO YA TABATA SEGEREA, DAR

> Mwanaharakati huyo na Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, alipotea Desemba 23 kwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana

> Amekuwa akitekwa mara kwa mara na kutekwa kwake jana ilikuwa ni mara ya 4

Soma - https://jamii.app/NgettiApatikanaTabata
MAREKANI YAMUITA BALOZI WAKE WA ZAMBIA ALIYEKOSOA ADHABU KWA WAPENZI WA JINSIA MOJA

> Marekani imemuita Balozi Daniel Foote nyumbani baada ya kukosoa uamuzi wa Jaji nchini Zambia kuwafunga wanaume 2 kifungo cha miaka 15 kwa kupatikana wakifanya mapenzi mwaka 2017

> Rais Edgar Lungu alimtaja Balozi huyo kama miongoni mwa watu wasiotakiwa katika Taifa hilo na kuitaka Marekani kumuondosha

Soma - https://jamii.app/USCallsFooteHome