JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
INDIA: WAANDAMANAJI 100 WAKAMATWA WAKIPINGA MUSWADA WA KIBAGUZI

> Mandamano hayo yanapinga Muswada wa kuwapatia hifadhi ya kisiasa Wakimbizi waliokabiliwa na mateso katika nchi wanazotoka, huku ukiwabagua waumini wa Dini ya Kiislam

> Aidha, Mahakama imetangaza kuahirisha kusikiliza kesi ya madai kuhusiana na Muswada huo hadi Januari 2020

Soma - https://jamii.app/RiotsMuslimsBill
MADEREVA WA UBER NA BOLT KUFUNGUA KESI DHIDI YA KAMPUNI HIZO

> Chama cha Madereva wa Usafirishaji kwa Njia ya Mtandao (TODA) kimetoa siku 7 (kabla ya kufungua kesi) kukutana na wamiliki wa Uber na Bolt (Taxify) ili kujadiliana baada ya kuibuka kwa madai kuwa wamiliki hao wanachukua asilimia kubwa katika kila safari

Soma - https://jamii.app/MgogoroMaderevaUberTaxify
MIRADI 159 YA MAJI IMEKAMILIKA LAKINI HAITOI MAJI

- Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuchukuliwa hatua kwa Wakandarasi wote waliotekeleza miradi 159 nchini ambayo imekamilika ila haitoi maji au inayochukua muda mrefu kumalizika

Zaidi, soma https://jamii.app/Miradi159Maji
MAHAKAMA YASISITIZA KUMTAKA LISSU

- Mahakama ya Kisutu imesisitiza kumtaka Mahakamani Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi

- Lissu kupitia Mdhamini wake amesema bado anahofia usalama wake

- Kesi itatajwa tena Januari 20, 2020

Zaidi, soma https://jamii.app/MahakamaYamtakaLissu
TRUMP AWASHAMBULIA WABUNGE WALIOMPIGIA KURA YA KUONDOLEWA MADARAKANI

> Muda mfupi baada ya Baraza la Wawakilishi la Marekani kupitisha uamuzi wa kumshitaki Rais Donald Trump, mwenyewe ameitisha mkutano wa hadhara kuwashambulia vikali wajumbe wa Democrat waliopiga kura hiyo

> Wajumbe 230 waliidhinisha mashitaka hayo dhidi ya 197 waliopinga

Soma - https://jamii.app/TrumpTalksImpeachment
JOHN MNYIKA ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WA CHADEMA

- Baraza Kuu la CHADEMA limeridhia baada ya Mnyika kuteuliwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe

- Salum Mwalimu ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na Singo Benson Kigaila ni Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara

Zaidi, soma https://jamii.app/MnyikaKKuu-CDM
RIPOTI WHO: IDADI YA WATU WANAOTUMIA TUMBAKU DUNIANI YAPUNGUA

> Mwaka 2000, karibu theluthi tatu ya watu duniani wenye miaka 15 na zaidi walikuwa wakitumia Tumbaku, Sigara na bidhaa nyingine za Tumbaku

> Kila mwaka watu zaidi ya milioni 8 hupoteza maisha kutokana na athari za tumbaku ikiwemo watu milioni 1.2 ambao si wavutaji lakini wakiathirika na moshi wa wavutaji

Soma - https://jamii.app/RipotiMatumiziTumbaku
UTAFITI: MFUMO WA UTAMBUZI WA SURA UNATOA MATOKEO YASIYO SAHIHI KWA WASIO WAZUNGU

> Utafiti huo umetolewa na Taasisi ya Viwango na Teknolojia (NIST) ya Marekani ambapo imebainika mifumo ya Utambuzi wa Sura (Facial Recognition) ilitoa matokeo yasiyo sahihi kwa Wamarekani weusi na Waasia

> Kiwango cha makosa ni kikubwa sana na inaweza kusababisha watu wasio na hatia kufungwa gerezani

Soma - https://jamii.app/FacialRecognitionFalseIdentification
TCRA: LAINI ZISIZOSAJILIWA KWA KITAMBULISHO CHA NIDA ZITAFUNGWA BAADA YA DESEMBA 31

> Mamlaka ya Mawasiliano imesema hadi sasa laini za simu milioni 20 zimesajiliwa na ikifika Desemba 31, 2019 laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa Namba ya NIDA na kuthibitisha kwenye mifumo zitafungwa

> Aidha, hakuna mtoa huduma atakayeruhusiwa kufunga au kukatisha mawasiliano ya mtumiaji yeyote kabla ya muda uliopangwa

Soma - https://jamii.app/TCRAKufungwaLainiDesemba31
TANESCO YATAKIWA KUBAINI VYANZO VINGINE VYA NISHATI

- Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameiagiza Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha wanafanya tafiti kubaini vyanzo vipya vya uzalishaji umeme ili kuongeza kiasi cha nishati hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/TanescoVyanzoNishati
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Spika wa Bunge la Marekani akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa yote yanayoendelea kumpinga Rais Trump sio kwasababu anamchukia bali anamuona ni Rais dhaifu anayeshindwa kushughulikia matumizi mabaya ya silaha ambayo huwaathiri sana watoto nchini humo
KATAVI: MUUGUZI ADAIWA KUMBAKA MJAMZITO ALIYEKUWA AKISUBIRI KUJIFUNGUA

> Abednego Alfred (32), anadaiwa kumbaka mjamzito aliyekuwa amekwenda hospitali hapo kupata huduma ya kujifungua baada ya kushikwa na uchungu

> Baada ya kufanya kitendo hicho alitokomea kusikojulikana lakini polisi walifanikiwa kumkamata

Soma - https://jamii.app/MuuguziAbakaMjamzito
TITO MAGOTI ADAIWA KUCHUKULIWA NA WATU WASIOJULIKANA

> Tito ambaye ni Mfanyakazi wa LHRC inadaiwa kachukuliwa Mwenge, Jijini Dar

> Imedaiwa amechukuliwa na watu 5 waliovalia kiraia wanaodaiwa kumfunga pingu kabla ya kuondoka naye

> JamiiForums kwa kushirikiana na wadau kadhaa toka Asasi za Kiraia wanafuatilia kwa karibu tukio hili na taarifa za kina zitakuja kadiri zinavyopatikana

Soma https://jamii.app/FreeTitoMagoti

#FreeTitoMagoti
MWANDISHI CHRISTOPHER GAMAINA NA WENZAKE 3 WAACHIWA HURU

> Waandishi hao awali walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia nguvu na baada ya kukata rufaa Mahakama Kuu iliamuru kesi hiyo kusikilizwa upya chini ya Hakimu mwingine

> Wenzake ni Wilfred Makuna, Manga Msalaba na Zephania Mandia

Soma - https://jamii.app/GamainaAachiwaHuru
NIGERIA: MAHAKAMA YATANGAZA UKAHABA KATIKA TAIFA HILO SIO UHALIFU

> Mahakama Kuu Jijini Abuja imetangaza rasmi kwamba ukahaba katika Taifa hilo sio uhalifu tena katika Uamuzi wa kesi ya wanawake 16 waliokamatwa kwa kufanya ukahaba

> Pia, imeiagizia Serikali kuwalipa fidia wanawake hao

Soma - https://jamii.app/SexWorkNotCrime
SOLSKJAER: PAUL POGBA HAUZWI KATIKA DIRISHA LA USAJILI LA JANUARI

- Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesisitiza kuwa Paul Pogba(26) hataondoka majira haya ya baridi

- Amesema, Pogba aliyecheza michezo sita tu kwa msimu, bado yupo katika mipango yake
SERIKALI: HATUDAIWI NA WASTAAFU WA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

- Imesema, imewalipa Wastaafu hao kwa mujibu wa Hati ya Makubaliano iliyosajiliwa Mahakama Kuu

- Imesema, hadi Desemba 2013 Wastaafu 31,788 kati ya 31,831 walikwishalipwa

Soma https://jamii.app/WastaafuEAHawaidaiSerikali
MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA MALARIA YAPUNGUA NCHINI

> Kiwango cha ugonjwa wa Malaria kimepungua zaidi ya 50% ndani ya miaka 2 kutoka 14% mwaka 2015 hadi 7.3% mwaka 2017 huku vifo vikipungua 75%

> Watu wanaougua kwa maambukizi mapya nao wamepungua kwa zaidi ya 67%

Soma - https://jamii.app/PunguoMaambukiziMalaria