JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KISARAWE: MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT MBARONI KWA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

> Mchungaji Shauri Steven anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa Darasa 5

> Sababu imetajwa kuwa tamaa za mwili ambapo alimlaghai kwa madai ya kumfanyia Huduma ya Maombi

Soma - https://jamii.app/MchMbaroniMimbaMwanfz
WAKENYA: MTI WA KRISMASI WA UWANJA WA NDEGE JOMO KENYATTA NI 'KITUKO'

- Mti huo umerembwa kwa mapambo ya Krimasi huku chini kukiwa na maboksi ya zawadi

- Wakenya Mitandaoni hawakuweza kuficha hisia zao huku wakilinganisha mti huo na mingine

Soma https://jamii.app/MtiKrismasiJKIA-Kenya
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ERICK KABENDERA KULA KRISMASI NA MWAKA MPYA RUMANDE

- Jamhuri imeeleza kuwa upelelezi bado haujakamilika

- Wakili wa Kabendera amesema bado wanaendelea kuzungumza na DPP kuhusu barua ya kukiri makosa

- Kesi kusikilizwa tena Januari 2, 2020

Zaidi, soma https://jamii.app/KesiKabendera-2020
NAFASI ZA KAZI NDANI YA TAASISI YA T-MARC TANZANIA

- Shirika hilo linalofanya kazi kuboresha Afya ya Umma na kukuza Maendeleo ya Jamii limetangaza nafasi 10 za kazi

- Sales Representatives (6), Accountant, Business Development Manager, Procurement Specialist na Marketing Manager

Zaidi, soma https://jamii.app/NafasiKaziT-Marc
MAMBO YA KUYAZINGATIA PINDI UTOAPO ADHABU KWA MTOTO WAKO

> Adhabu iendane na kosa: Endapo hautozingatia kosa na adhabu utatengeneza mazingira ya mtoto kutojengwa bali kubomolewa

> Epuka adhabu za kikatili kwa watoto: Kuadhibu sio kukomoa, adhabu lengo lake ni lazima liwe kumfundisha mtoto na sio kumuumiza

> Adhabu isitolewe kwa mtoto ambaye hajawahi kuelezwa lolote juu ya kosa alilolifanya: Mambo mengi sio makosa kwa watoto mpaka pale watakapoelezwa kuwa ni makosa

Zaidi, soma - https://jamii.app/MsingiAdhabuMtoto
UGANDA: AMSHUSHIA KIPIGO MKEWE KWA KUCHINJA JOGOO WA KRISMASI SIKU 10 KABLA YA SIKUKUU

- Mwanaume (50) katika Wilaya ya Budaka amemjeruhi vibaya Mke wake baada ya Mwanamke huyo kumchinja Jogoo aliyetakiwa kufanywa kitoweo siku ya Krismasi

Zaidi, soma https://jamii.app/AshambuliaMkwe-JogooKrismasi
ZIFAHAMU PESA 8 ZENYE NGUVU AFRIKA

> (1) Dinari ya Libya: Hii ndio pesa yenye nguvu zaidi Afrika ukiangalia thamani yake dhidi ya dola ya Marekani na nguvu yake ya kununua (Purchasing Power) ambapo Dola 1 = 1.38 Dinari za Libya

> (2) Dinari ya Tunisia: Hii ni pesa ya pili kwa Afrika ambayo dola 1 = 3.05 Tunisian Dinari. (3) Cedis ya Ghana: Ghana ni nchi pekee ya Afrika Magharibi ambayo ipo kwenye 8 Bora ya nchi zenye pesa yenye nguvu Afrika (Dola 1 = 5.50 Ghana Cedis)

Kuzifahamu zingine, soma - https://jamii.app/StrongCurrenciesAfrica
RAIS AWAONYA WANAOJENGA MABONDENI, AWATAKA WASIILAUMU SERIKALI

> Rais John Magufuli amewataka wananchi kujihadhari kwa kutojenga nyumba kwenye maeneo ambayo kuna Mkondo wa Maji

> Akitoa mifano ya maeneo ambayo wananchi wamejenga mabondeni, amewataka kuchukua tahadhari wanapojenga nyumba zao ili wasije wakailaumu Serikali baadaye

Soma - https://jamii.app/MagufuliUjenziBondeni
MICHEZO: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Vyama na Vilabu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
-
Uchaguzi huo umefanyika leo katika Hoteli ya Silver Springs, Uganda na Karia ataliongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka 4
SINGIDA: HAKIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

- Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mtinko, Bernard Kasanda (38) anatuhumiwa kupokea rushwa ya Tsh. 250,000

- Pia, alikutwa na visu 5 anavyodhaniwa kutumia kujihami wakati akipata maslahi hayo haramu

Zaidi, soma https://jamii.app/HakimuMbaroniRushwa-SNG
Donald Trump amekuwa Rais wa tatu katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya matumizi mabaya ya madaraka

- Hatua hiyo inampeleka moja kwa moja katika kesi dhidi yake itakayoamua ikiwa atabakia madarakani au la, uamuzi utakaotolewa na Baraza la ‘Senate’

Zaidi, soma https://jamii.app/TrumpImpeached
UCHAGUZI CHADEMA: MBOWE ACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA MWENYEKITI

> Freeman A. Mbowe ametangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa awamu nyingine baada ya kuibuka na kura 886 sawa na 93.5% dhidi ya Cecil Mwambe aliyepata kura 59 sawa na 6.2%

> Kura 3 zimeharibika

Soma > https://jamii.app/MboweTena
MWANZA: MAJI WILAYA YA MISUNGWI YALALAMIKIWA KUWA MACHAFU

> Inadaiwa kuwa, maji yanayotoka kwenye mabomba ni machafu na hayafai kwa matumizi ya Binadamu kwani yanatoka Ziwani moja kwa moja na kisha kusambazwa kwa Wananchi bila kutibiwa

> Wananchi wadai kuna ucheleweshwaji wa kuunganishwa na Mtandao wa Maji japo wamelipa gharama zote kama inavyohitajika

Soma - https://jamii.app/UchafuMajiMisungwi
WAKENYA 4 WADAIWA KUTEKWA NA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB

> Wakandarasi waliokuwa wakifanya ujenzi wa barabara kati ya Riba na Konton, Kaunti ya Wajir wanadaiwa kutekwa na kundi la watu wanaoshukiwa kuwa Wanamgambo wa Kikundi Kigaidi cha Al-Shabaab

> Kamishna Msaidizi wa Kaunti amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana jioni

Soma - https://jamii.app/KenyansKidnappedAlShabaab
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RONALDO APIGA 'BONGE LA GOLI' KUIPA USHINDI JUVENTUS

- Mshambuliaji Cristiano Ronaldo jana amefunga goli la kichwa lililozua gumzo katika mitandao ya kijamii

- Wakati akifunga goli hilo, Wataalamu wanasema aliruka urefu wa Mita 2.56 huku akikaa hewani kwa sekunde 1.5
VATICAN: PAPA AONDOA USIRI JUU YA KASHFA ZA UDHALILISHAJI WA KINGONO

- Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis ameuondoa usiri juu ya kashfa za udhalilishaji wa kingono kwa kufuta kanuni inayozuia kufichuliwa na kuchunguzwa kwa uhalifu huo

Zaidi, soma https://jamii.app/Papa-UsiriKesiUdhalilishaji
LIVERPOOL YATHIBITISHA KUMSAJILI TAKUMI MINAMINO

- Imethibitisha kumsajili Kiungo huyo Mshambuliaji (24), Raia wa Japan, kutoka Klabu ya Red Bull Salzburg ya Austria kwa Paundi Milioni 7.25 (Tsh. 21,893,401,752)

- Liverpool itasubiri hadi Januari 01 litakapofunguliwa dirisha la usajili kumuandikisha mchezaji huyo