JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DRC: MAUAJI YA RAIA YAENDELEA, JESHI LALAUMIWA KWA KUSHINDWA KUWADHIBITI WAASI

> Waasi wa Kundi la ADF wameshambulia tena wananchi wa Mji wa Beni kwa risasi na kuuwa watu 22 katika eneo la Ndombi na Kamango

> Mwenyekiti wa Mashirika ya kutetea Haki za Binaadamu amelilalamikia Jeshi la nchi hiyo kwa kushindwa kuwatokomeza waasi wa ADF ambao wameshaua zaidi ya watu 100

Soma - https://jamii.app/MassShootingContinuesBeni
SERIKALI: HAKUNA UGONJWA WA MLIPUKO DAR

- Wizara ya Afya imekanusha uwepo wa mlipuko wa Ugonjwa wenye dalili kama za Malaria Jijini Dar

- Imesema ina mifumo imara ya ufuatiliaji magonjwa na itafuatilia kujua chanzo iwapo kutakuwa na mlipuko

Zaidi, soma https://jamii.app/WizaraAfyaUfuatiliaji
BOEING KUACHA KUZALISHA KWA MUDA NDEGE ZA 737 MAX KUANZIA JANUARI 2020

> Utengenezaji wa ndege hizo ulikuwa ukiendelea licha ya kuzuiwa kupaa kwa mezi 9 sasa baada ya kuhusika katika ajali 2 nchini Indonesia na Ethiopia na kuua watu zaidi ya 300

> Hata hivyo, imesema haitawafuta kazi wafanyakazi waliopo na 737 Max

Soma - https://jamii.app/SuspendProduction737Max
CHINA: WATU 14 WAMEFARIKI KATIKA MLIPUKO ULIOTOKEA MGODINI

- Watu wengine saba wameokolewa huku wengine wawili wakiwa bado wamekwama ndani ya mgodi huo wa Makaa ya Mawe na Gesi uliopo Kusini-Magharibi mwa China katika Mji wa Guizhou

Zaidi, soma https://jamii.app/MlipukoChinaMgodini
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MVUA KUBWA DAR: WANANCHI WAKWAMA, MIUNDOMBINU YAATHIRIKA

> Mvua kubwa ikiambatana na radi inaendelea kunyesha jijini Dar na miundombinu ya barabara inadaiwa kuathirika hivyo kupelekea watu kukwama kuendelea na shughuli zao za kila siku

> Bado athari zaidi ya mvua hizi zinazoendelea kunyesha hazijajulikana lakini wengi wanadai mvua ni kubwa jijini humo

#DarFloods #MvuaDar
RIPOTI: USAWA WA KIJINSIA MAENEO YA KAZI KUFANIKIWA BAADA YA MIAKA 257

> Ripoti ya World Economic Forum inayofuatilia usawa wa jinsia kwenye nchi 153 imebaini hali ya kutokuwa na usawa haitarajiwi kufutika mpaka mwaka 2276

> Imetabiri kuwa, itachukuwa miaka 99.5 kwa wanawake kupata usawa, ikiwa ni punguo kutoka miaka 108 katika utabiri wa 2018

Soma - https://jamii.app/ReportEqualityWork2019
ATHARI ZA MVUA: HUDUMA ZA MWENDOKASI KUPITIA JANGWANI ZASITISHWA

- Ni kutokana na mvua inayoendelea kunyesha katika Mkoa wa Dar na kusababisha sehemu mbalimbali za mkoa huo kujaa maji

- Wasafiri wanaotoka Mjini au Kariakoo wameshauriwa kutumia usafiri mbadala hadi Kituo cha Mwendokasi Morocco na waendao Mjini/Kariakoo wakifika Morocco watafute usafiri mbadala

Zaidi, Fuatilia https://jamii.app/AthariMvuaDar-Dec2019
TETESI: CARLO ANCELOTTI NA EVERTON WAFIKIA MAKUBALIANO YA AWALI

- Kwa mujibu wa Sky Sports, Carlo Ancelotti na Klabu ya Everton wamefikia makubaliano ya awali ya Kocha huyo kuinoa klabu hiyo

- Ancelotti, alifutwa kazi na Klabu ya Napoli ya Italia wiki iliyopita
KENYA: WATU WATATU WASHTAKIWA KWA KUWEKA SUMU KWENYE CHAKULA

> Mameneja 3 wa Shamba wamefikishwa Mahakamani kwa shtaka la kuweka sumu kwenye chakula na kusababisha vifo vya watu 4 na wengine 6 kuathirika

> Watu 2 kati yao bado wapo ICU ambapo wameathirika ktk mifumo ya Neva na Ubongo

Soma - https://jamii.app/ManagersSuspectFoodPoisoning
ALIYEKUWA RAIS WA PAKISTANI AHUKUMIWA KIFO KATIKA KESI YA UHAINI MKUBWA

> Rais Pervez Musharraf (76) amehukumiwa kifo katika kesi ya Uhaini Mkubwa iliyohusisha kuweko kwa Dharura ya Kikatiba mnamo 2007

> Hukumu hiyo imetolewa leo wakati kiongozi huyo akiwa Mjini Dubai tangu alipoondoka Machi 2016 kwasababu za Kiafya na Kiusalama

Soma - https://jamii.app/PervezDeathPenaltyTreason
DAWASA YATOA TAHADHARI YA UPUNGUFU WA MAJI MKOA WA DAR

> Kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji leo hadi kesho ktk Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke na Tabata

> Pia, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Soma - https://jamii.app/TahadhariUpungufuMaji
ZAMBIA YAHALALISHA BANGI KWA AJILI YA BIASHARA

- Imehalalisha uzalishaji wa Bangi na uuzaji wa mmea huo nje ya nchi kwa matumizi ya Dawa ili kukuza Uchumi

- Haijawekwa wazi kama matumizi ya zao hilo kwa tiba yamehalalishwa ndani ya Zambia

Soma https://jamii.app/ZambiaYaruhusuBangi
MALEZI YA WATOTO NI TAALUMA SIO KITU CHA ASILI

> Kama zilivyo Taaluma nyingine, malezi ya watoto pia ni Taaluma hivyo ili mtu aimudu vizuri ni lazima ajifunze kwa njia rasmi au isiyo rasmi. Ni ngumu kujua namna nzuri ya kuisimamia afya ya mtoto bila kujua misingi na kanuni za afya ya mtoto

> Jifunze malezi kutoka kwa wazazi/walezi waliotangulia. Njia hii ni moja kati ya njia zinazotumiwa na watu wengi duniani lakini madhara yake ni endapo maarifa aliyonayo aliyetangulia sio sahihi basi yana hatari ya kuendelea kurithishwa

Fahamu zaidi - https://jamii.app/ElimuMaleziWatoto
#JFMalezi
APPLE, GOOGLE, TESLA NA MICROSOFT ZAFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUTUMIKISHA WATOTO MIGODINI

> Kesi hiyo imefunguliwa na familia 14 za DRC wakiyashutumu makampuni hayo kuwaruhusu watoto wadogo kuchimba madini aina ya Kobalti yanayotumiwa katika bidhaa zao

> DRC inazalisha 60% ya Kobalti Duniani na hutumiwa kutengenezea betri aina ya 'Lithium-ion' zinazotumika kuwasha Magari ya Umeme, Kompyuta Mpakato (Laptop) na Simu Janja

Soma - https://jamii.app/AppleGoogleMicrosoftLawsuit
DAR: CHADEMA YATAKIWA KUTOA BENDERA ZAKE BARABARANI NDANI YA SAA 2

- Mkurugenzi wa Ubungo, Beatrice Dominic ameitaka CHADEMA kuondoa bendera zake karibu na ukumbi wa Mlimani City

- Katika ukumbi huo CHADEMA inafanya Mikutano yake mbalimbali

Zaidi, soma https://jamii.app/BenderaCDM-Ubungo
KILIMANJARO STARS YATOLEWA KWENYE MICHUANO YA CECAFA

- Uganda imeitoa Tanzania Bara #KilimanjaroStars kwa kuifunga goli 1-0 katika mchezo wa Nusu Fainali

- Kilimanjaro Stars itachuana na Kenya kuwania Mshindi wa tatu huku Uganda ikichuana na Eritrea kwenye fainali
DAR: WANNE MBARONI KWA KUKUTWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZA FEDHA BANDIA

- Watu hao wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania

- Wamekutwa na Noti Bandia za Nchi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 578

Zaidi, zoma https://jamii.app/MbaroniNotiBandia
MWENDELEZO: Polisi wamefika eneo la Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar unapofanyika Mkutano wa CHADEMA na kuagiza bendera za chama hicho zilizowekwa kushushwa

- Awali, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic alikiandikia barua chama hicho kikuu cha Upinzani Nchini kutaka kishushe bendera hizo

Zaidi, soma https://jamii.app/BenderaCDM-Ubungo
MOSHI: WATU 15 WAJERUHIWA BAADA YA BASI KUGONGA MAGARI MENGINE 7

- Wamejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Mawenzi baada ya basi la Kampuni ya Harambee kudaiwa kupata hitilafu katika mvumo wake wa breki na kuparamia magari hayo 7 katikati ya Mji

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliMoshi15Wajeruhiwa