JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DODOMA: MKUU WA SHULE MBARONI AKIDAIWA KUMUOMBA MWANAFUNZI RUSHWA YA NGONO

- Ni Baraka Sabi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Serengeti ya Mkoani Mara

- Anadaiwa kufanya hivyo kwa Mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita ili ampatie cheti chake

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuMbaroni-NgonoMwanafunzi
KATAVI: WANANDOA WAUAWA KWA KUKATWA MAPANGA WAKIWA WAMELALA

> Noel Muswanya (37) na mke wake aliyetambulika kwa jina moja la Siwema (27) walivamiwa usiku wakiwa wamelala kisha kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Desemba 15

Soma - https://jamii.app/MauajiWanandoaMapanga
MPYA: Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar imetoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo (HESLB) kutekeleza maagizo 4

- Miongoni mwa maagizo ni kuwaingizia fedha Wanafunzi ambao hawajapewa tangu chuo hicho kifunguliwe

- Yasema, yasipotimizwa watakusanyika nje ya Ofisi za HESLB

Zaidi, soma https://jamii.app/WanafunziUDSMvsHESLB
UGANDA: WATOTO WALIOKUWA WAMETEKWA WAPATIKANA WAKIWA WAMEFARIKI

> Watoto hao 3 walitekwa Alhamisi ya wiki iliyopita na kisha kuachwa kwa ujumbe uliowataka wazazi kutoa pesa kiasi cha 500,000 za Uganda (Zaidi ya Tsh. 300,000)

> Familia ilitoa pesa hiyo lakini watekaji wakaomba pesa zaidi (Tsh. Laki 6) ambazo wazazi walishindwa kulipa

Soma - https://jamii.app/KidnapedKidsFoundDead
WIZARA YA AFYA: TUNAFUATILIA UGONJWA UNAODAIWA KUWAKUMBA WATU UKIWA NA DALILI KAMA ZA MALARIA

- Baadhi ya dalili ni Kikohozi, Mafua, Maumivu ya Kichwa na Homa Kali

- Unadaiwa kuwepo zaidi maeneo ya Kimara, Sinza, Ubungo na Kigogo jijini Dar

Zaidi, soma https://jamii.app/WizaraAfyaUfuatiliaji
KENYA: MWANAFUNZI AMUUA BINAMU YAKE WAKIGOMBANIA MWANAMKE

> Mwanafunzi wa Kidato cha 3 (20) anashikiliwa na Polisi Mjini Siaya kwa kosa la kumchoma kisu maeneo ya kifuani na begani na kumuua binamu yake, Otieno Nyaeka (45)

Soma - https://jamii.app/MauajiBinamuMapenzi
MICHEZO: Mwanariadha Eliud Kipchoge amewabwaga wanariadha wenzake na kunyakua taji la BBC la kuwa Mwanaspoti Bora wa mwaka Duniani
-
Kipchoge aliibuka kuwa chaguo bora na kunyakua taji hilo la BBC, kwa kuwabwaga washindani wenzake wakiwemo mwanariadha wa mazoezi ya viungo Simone Biles kutoka Marekani na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Raga ya Afrika Kusini Siya Kolisi
RUKWA: VIJANA WA JKT WADAIWA KUUA RAIA KWA KIPIGO

> Vijana 5 wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) wanadaiwa kuvamia Kituo cha Polisi na kuwapiga Sabato Mbalamwezi na Renatus Wankamba na kupelekea Sabato kupoteza maisha

> Sabato na Renatus walikamatwa kwa tuhuma za kuiba simu ya Tsh. 25,000

Soma - https://jamii.app/TuhumaJKTMauaji
AFYA: JINSI YA KUMSAIDIA MTOTO ANAYEKOJOA KITANDANI

> Ili kumsaidia, kwanza mtengenezee mtoto ratiba ya kukojoa kila baada ya muda fulani ili ubongo uzoee na kumtaarifu anapohisi kukojoa

> Mbadilishie muda wa kunywa vimiminika na usimwache na kiu muda mrefu (hasa usiku), anaweza kunywa asubuhi hadi alasiri ili apate muda wa kukojoa kabla ya kulala

> Unashauriwa usimuamshe mtoto usiku kukojoa kwani inamkosesha fursa ya kujenga tabia ya kudhibiti na kupambana na tatizo

Fahamu zaidi - https://jamii.app/MsaadaMtotoKikojozi
#JFAfya
NAIBU KATIBU MKUU ACT-WAZALENDO AJIUZULU BAADA YA MAZUNGUMZO YAKE KUVUJA

> Msafiri Mtemelwa ametangaza kujiuzulu kufuatia kuvuja kwa mazungumzo yake na Mbunge wa Moshi Vijijini (CHADEMA), Anthony Komu

> Mtemelwa amekiri kuwa alifanya mazungumzo na Komu, yenye lengo la kumshawishi mwanasiasa huyo kujiunga na chama chake

Soma - https://jamii.app/NKatibuACTAjiuzuluAudio
DAR: SERIKALI KUPINGA HUKUMU YA MALINZI

> Serikali imewasilisha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu, kupinga hukumu na adhabu iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu dhidi ya aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake, Celestine Mwesigwa

Soma - https://jamii.app/PingamiziHukumuMalinzi
DENI LAMUWEKA RUMANDE KOCHA WA KLABU YA TOTO AFRICANS

> Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ibrahim Mlumba anadaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kutokana na deni wanalodaiwa la Tsh. milioni 1

> Inadaiwa, Kocha huyo alitiwa mbaroni baada ya Klabu kushindwa kulipa deni wanalodaiwa Mkoani humo kwa takriban siku 11 walizokaa wakati wa mechi zao dhidi ya Mgambo Shooting na Milambo FC

#JFMichezo
KUBENEA AJITOA KUGOMBEA UONGOZI CHADEMA

> Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amesema Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu anafaa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, hivyo amejitoa kugombania nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba 18, 2019

Soma - https://jamii.app/KubeneaAjiondoaUchaguziCDM
TETESI: ARSENAL INAANGALIA UWEZEKANO WA KUMKABIDHI MIKEL ARTETA UKOCHA

- Maafisa wa Arsenal wanadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na wenzao wa Manchester City

- Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Vinai Venkatesham na Mwanasheria, Huss Fahmy wameonekana wakitoka nyumbani kwa Arteta

Zaidi, soma https://jamii.app/ArtetaUkochaArsenal
RAIS WA ZAMBIA ATAKA BALOZI WA MAREKANI NCHINI HUMO AONDOKE

> Uamuzi huo umekuja baada ya Balozi Daniel Foote kunukuliwa akitoa maoni yanayopinga adhabu ya kifungo cha miaka 15 waliyopewa Raia 2 wa Zambia kwa makosa ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga)

> Rais Lungu amesema, Zambia haihitaji watu wanaounga mkono matendo ya kishetani

Soma - https://jamii.app/USAmbasdZambiaKickedOut
MBOWE NA LISSU WAPENDEKEZWA KUGOMBEA UONGOZI CHADEMA

- Kamati Kuu ya CHADEMA imewapendekeza Freeman Mbowe na Cecil Mwambe kugombea Uenyekiti wa Chama hicho

- Imewapendekeza Tundu Lissu na Sophia Mwakagenda kuwania Makamu Mwenyekiti(Bara)

- Said Issa Mohamed amependekezwa kuwania Makamu Mwenyekiti Taifa kwa Tanzania Visiwani

Zaidi, soma https://jamii.app/KamatiUchaguziCHADEMA
DRC: MAUAJI YA RAIA YAENDELEA, JESHI LALAUMIWA KWA KUSHINDWA KUWADHIBITI WAASI

> Waasi wa Kundi la ADF wameshambulia tena wananchi wa Mji wa Beni kwa risasi na kuuwa watu 22 katika eneo la Ndombi na Kamango

> Mwenyekiti wa Mashirika ya kutetea Haki za Binaadamu amelilalamikia Jeshi la nchi hiyo kwa kushindwa kuwatokomeza waasi wa ADF ambao wameshaua zaidi ya watu 100

Soma - https://jamii.app/MassShootingContinuesBeni
SERIKALI: HAKUNA UGONJWA WA MLIPUKO DAR

- Wizara ya Afya imekanusha uwepo wa mlipuko wa Ugonjwa wenye dalili kama za Malaria Jijini Dar

- Imesema ina mifumo imara ya ufuatiliaji magonjwa na itafuatilia kujua chanzo iwapo kutakuwa na mlipuko

Zaidi, soma https://jamii.app/WizaraAfyaUfuatiliaji
BOEING KUACHA KUZALISHA KWA MUDA NDEGE ZA 737 MAX KUANZIA JANUARI 2020

> Utengenezaji wa ndege hizo ulikuwa ukiendelea licha ya kuzuiwa kupaa kwa mezi 9 sasa baada ya kuhusika katika ajali 2 nchini Indonesia na Ethiopia na kuua watu zaidi ya 300

> Hata hivyo, imesema haitawafuta kazi wafanyakazi waliopo na 737 Max

Soma - https://jamii.app/SuspendProduction737Max
CHINA: WATU 14 WAMEFARIKI KATIKA MLIPUKO ULIOTOKEA MGODINI

- Watu wengine saba wameokolewa huku wengine wawili wakiwa bado wamekwama ndani ya mgodi huo wa Makaa ya Mawe na Gesi uliopo Kusini-Magharibi mwa China katika Mji wa Guizhou

Zaidi, soma https://jamii.app/MlipukoChinaMgodini