JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MWANACHAMA MKONGWE WA YANGA MZEE AKILIMALI AFARIKI

- Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amefariki leo alfajiri

- Amefariki katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani

Zaidi, soma https://jamii.app/MzeeAkilimaliAfariki
UN: SHERIA MPYA YA URAIA NCHINI INDIA NI YA KIBAGUZI

- UN imesema sheria hiyo ina misingi ya kibaguzi kwa kuwa inawatenga Waislam

- Sheria hiyo inaongeza mchakato wa Uraia kwa makundi ya walio wachache waliokimbia kutoka nchi kama Pakistani

Zaidi, soma https://jamii.app/UNSheriaUraiaInabagua
OMAR AL BASHIR AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA

- Rais huyo wa zamani wa Sudan amekutwa na hatia katika makosa ya Rushwa na Utakatishaji Fedha

- Pia, anakabiliwa na makosa ya Mauaji ya Kimbari na Uhalifu wa Kivita katika Mahakama ya ICC
DAR: MKURUGENZI WA JAMIIFORUMS ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO

- Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo ametunukiwa cheti hicho na Mtandao wa Madeni na Maendeleo Tanzania

- Maxence ni miongoni mwa watanzania wachache waliotambuliwa leo kwa mchango wao katika kutetea Haki za Binadamu nchini
MLIMBWENDE WA JAMAICA ASHINDA TAJI LA MLIMBWENDE WA DUNIA 2019

- Toni-Ann Singh (23) ametwaa taji hilo ikiwa ni mara ya 4 kwa Jamaica kushinda

- Mshindi wa 2 ni Ophely Mezino (Ufaransa) na wa 3 ni Suman Rao (India)

- Sylivia Sebastian aliiwakilisha Tanzania

Zaidi, soma https://jamii.app/MissWorld2019
NDEGE MOJA YA ATCL KUWASILI MWAKANI NA MBILI KUWASLI JUNI NA JULAI 2021

- Bombardier Q400 itawasili Mwezi Juni 2020 na Air-Bus 220-300(mbili), moja itawasili mwezi Juni na nyingine mwezi Julai 2021

- Aidha, Serikali imeweka wazi mpango wake wa kutaka kununua ndege ya mizigo

Zaidi, soma https://jamii.app/Ndege3Mpya2020
AFYA: UNAVIJUA VIASHIRIA VYA MTU ALIYEFARIKI?

- Kumekuwa na hoja kwamba baadhi ya watu hudhaniwa wamefariki kabla hata hawajafikwa na mauti hivyo yawezekana wapo wanaozikwa (kimakosa) wakiwa hai

- Wataalamu wanaeleza kuwa Ubongo ndio kiashiria kikubwa cha mtu kufariki na sio kusimama kwa mapigo ya moyo pekee yake

Jifunze zaidi kuwa kusoma > https://jamii.app/ViashiriaKifo
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest, watu 37 wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali hiyo
DODOMA: MKUU WA SHULE MBARONI AKIDAIWA KUMUOMBA MWANAFUNZI RUSHWA YA NGONO

- Ni Baraka Sabi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Serengeti ya Mkoani Mara

- Anadaiwa kufanya hivyo kwa Mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita ili ampatie cheti chake

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuMbaroni-NgonoMwanafunzi
KATAVI: WANANDOA WAUAWA KWA KUKATWA MAPANGA WAKIWA WAMELALA

> Noel Muswanya (37) na mke wake aliyetambulika kwa jina moja la Siwema (27) walivamiwa usiku wakiwa wamelala kisha kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Desemba 15

Soma - https://jamii.app/MauajiWanandoaMapanga
MPYA: Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar imetoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo (HESLB) kutekeleza maagizo 4

- Miongoni mwa maagizo ni kuwaingizia fedha Wanafunzi ambao hawajapewa tangu chuo hicho kifunguliwe

- Yasema, yasipotimizwa watakusanyika nje ya Ofisi za HESLB

Zaidi, soma https://jamii.app/WanafunziUDSMvsHESLB
UGANDA: WATOTO WALIOKUWA WAMETEKWA WAPATIKANA WAKIWA WAMEFARIKI

> Watoto hao 3 walitekwa Alhamisi ya wiki iliyopita na kisha kuachwa kwa ujumbe uliowataka wazazi kutoa pesa kiasi cha 500,000 za Uganda (Zaidi ya Tsh. 300,000)

> Familia ilitoa pesa hiyo lakini watekaji wakaomba pesa zaidi (Tsh. Laki 6) ambazo wazazi walishindwa kulipa

Soma - https://jamii.app/KidnapedKidsFoundDead
WIZARA YA AFYA: TUNAFUATILIA UGONJWA UNAODAIWA KUWAKUMBA WATU UKIWA NA DALILI KAMA ZA MALARIA

- Baadhi ya dalili ni Kikohozi, Mafua, Maumivu ya Kichwa na Homa Kali

- Unadaiwa kuwepo zaidi maeneo ya Kimara, Sinza, Ubungo na Kigogo jijini Dar

Zaidi, soma https://jamii.app/WizaraAfyaUfuatiliaji
KENYA: MWANAFUNZI AMUUA BINAMU YAKE WAKIGOMBANIA MWANAMKE

> Mwanafunzi wa Kidato cha 3 (20) anashikiliwa na Polisi Mjini Siaya kwa kosa la kumchoma kisu maeneo ya kifuani na begani na kumuua binamu yake, Otieno Nyaeka (45)

Soma - https://jamii.app/MauajiBinamuMapenzi
MICHEZO: Mwanariadha Eliud Kipchoge amewabwaga wanariadha wenzake na kunyakua taji la BBC la kuwa Mwanaspoti Bora wa mwaka Duniani
-
Kipchoge aliibuka kuwa chaguo bora na kunyakua taji hilo la BBC, kwa kuwabwaga washindani wenzake wakiwemo mwanariadha wa mazoezi ya viungo Simone Biles kutoka Marekani na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Raga ya Afrika Kusini Siya Kolisi
RUKWA: VIJANA WA JKT WADAIWA KUUA RAIA KWA KIPIGO

> Vijana 5 wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) wanadaiwa kuvamia Kituo cha Polisi na kuwapiga Sabato Mbalamwezi na Renatus Wankamba na kupelekea Sabato kupoteza maisha

> Sabato na Renatus walikamatwa kwa tuhuma za kuiba simu ya Tsh. 25,000

Soma - https://jamii.app/TuhumaJKTMauaji
AFYA: JINSI YA KUMSAIDIA MTOTO ANAYEKOJOA KITANDANI

> Ili kumsaidia, kwanza mtengenezee mtoto ratiba ya kukojoa kila baada ya muda fulani ili ubongo uzoee na kumtaarifu anapohisi kukojoa

> Mbadilishie muda wa kunywa vimiminika na usimwache na kiu muda mrefu (hasa usiku), anaweza kunywa asubuhi hadi alasiri ili apate muda wa kukojoa kabla ya kulala

> Unashauriwa usimuamshe mtoto usiku kukojoa kwani inamkosesha fursa ya kujenga tabia ya kudhibiti na kupambana na tatizo

Fahamu zaidi - https://jamii.app/MsaadaMtotoKikojozi
#JFAfya
NAIBU KATIBU MKUU ACT-WAZALENDO AJIUZULU BAADA YA MAZUNGUMZO YAKE KUVUJA

> Msafiri Mtemelwa ametangaza kujiuzulu kufuatia kuvuja kwa mazungumzo yake na Mbunge wa Moshi Vijijini (CHADEMA), Anthony Komu

> Mtemelwa amekiri kuwa alifanya mazungumzo na Komu, yenye lengo la kumshawishi mwanasiasa huyo kujiunga na chama chake

Soma - https://jamii.app/NKatibuACTAjiuzuluAudio
DAR: SERIKALI KUPINGA HUKUMU YA MALINZI

> Serikali imewasilisha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu, kupinga hukumu na adhabu iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu dhidi ya aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake, Celestine Mwesigwa

Soma - https://jamii.app/PingamiziHukumuMalinzi
DENI LAMUWEKA RUMANDE KOCHA WA KLABU YA TOTO AFRICANS

> Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ibrahim Mlumba anadaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kutokana na deni wanalodaiwa la Tsh. milioni 1

> Inadaiwa, Kocha huyo alitiwa mbaroni baada ya Klabu kushindwa kulipa deni wanalodaiwa Mkoani humo kwa takriban siku 11 walizokaa wakati wa mechi zao dhidi ya Mgambo Shooting na Milambo FC

#JFMichezo