JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBINU ZA KUKUWEZESHA KUFANYA BIASHARA KWA MTAJI MDOGO

> Chagua wazo la biashara unalolipenda na kuliweza vyema

> Anza na unachokijua pasipo kuhusisha mambo mengi mageni kwa kuwa huna pesa za kuyagharamia

> Waambie watu unachokifanya ili kupata wateja na kufahamika na usiogope kueleza kuwa unafanya biashara ya aina fulani

Soma - https://jamii.app/BiasharaMtajiMdogo
#JFBiashara
CHILE: NDEGE YA KIJESHI ILIYOKUWA NA WATU 38 YAPOTEZA MAWASILIANO ANGANI

- Ilikuwa na Wafanyakazi 17 na Abiria 21 ikielekea katika Kambi ya Jeshi huko Antarctica

- Shughuli za kuitafuta ndege hiyo zimeanza kwa kutumia ndege na meli za Jeshi

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeJeshiYapotea-CHL
👍1
SIKU YA HAKI ZA BINADAMU: VIJANA WANASIMAMIA HAKI ZA BINADAMU

- Kila Disemba 10 ni Siku ya Haki za Binadamu na mwaka huu Kaulimbiu ni 'Vijana Wanasimamia #HakiZaBinadamu'

- Kila mtu anatakiwa kupata haki bila kujali dini, rangi wala hadhi yake

Zaidi, soma https://jamii.app/SikuHakiBinadamu
KIGAMBONI, DAR: Mwenyekiti wa Mtaa wa Changanyikeni kata ya Toangoma aliyepita bila kupingwa kwa tiketi ya CCM ametiwa mbaroni kwa kosa la “wizi” wa TZS 12,000,000/-

> Ni Suzanne(Dionisia) Kamugisha

> Yadaiwa alizitumia kwa ajili ya Kampeni za Uchaguzi wa Ndani wa chama

Zaidi, soma https://jamii.app/MwenyekitiMtaaMbaroni-KGMB
DAR: ALI MUFURUKI AAGWA KATIKA UKUMBI WA JULIUS NYERERE

- Mwili wa Mfanyabiashara huyo utazikwa leo katika Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar

- Alizaliwa Novemba 15, 1958 na amekuwa Mwenyekiti na Mjumbe wa zaidi ya bodi 30 za Kampuni mbalimbali

Zaidi, soma https://jamii.app/AliMufurukiAagwa-Dar
SUDAN KUSINI: SPIKA AJIUZULU, ASHUTUMIWA KWA KUTOWASILISHA RIPOTI YA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI

- Spika wa Bunge, Anthony Lino Makana amejiuzulu baada ya Wabunge kutishia kumuondoa madarakani kwa kuzuia juhudi za kupambana na rushwa

Soma > https://jamii.app/SpikaSudanKusini
FINLAND: WAZIRI MKUU MDOGO DUNIANI KUAPISHWA WIKI HII

- Sanna Marin (34) aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi amechaguliwa baada ya Antti Rinne kujiuzulu

- Pamoja na kuwa Waziri Mkuu mdogo Duniani, atakuwa ni wa 3 wa kike kuhudumu katika taifa hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/SannaWaziriMkuuMdogo
JE, KUNA MBINU ZA KUDHIBITI 'CHUMA ULETE' KWENYE BIASHARA?

> Mwanachama wa JamiiForums anasimulia kuwa alianza kufanya biashara maeneo ya Kimara Jijini Dar es Salaam baada ya muda aliihamishia biashara yake Mkoani Mtwara

> Anapata fedha nyingi lakini tatizo zinapotea katika mazingira ya kutatanisha 'Chuma Ulete'

Soma ~ https://jamii.app/ChumaUleteMtwara
NBS: MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.2 KWA MWEZI MMOJA

- Mfumuko wa bei kwa Novemba 2019 umeongezeka hadi 3.8% kutoka 3.6% mwezi Oktoba 2019

- Baadhi ya vyakula vilivyoongezeka bei ni mchele kwa 6.6%, nyama 2.6%, maharage 8.6%

Zaidi, soma https://jamii.app/MfumukoBeiNov2019
CECAFA Senior Challenge: Timu ya Taifa ya Tanzania Bara #KilimanjaroStars imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Timu ya Zanzibar #ZanzibarHeroes

- Ditram Nchimbi amefunga goli hilo na kuipatia timu hiyo alama tatu za kwanza baada ya kufungwa katika mchezo wa kwanza

#JFLeo
UGANDA: WATU 36 WAFARIKI KUTOKANA NA MAFURIKO

- Watu wengi bado hawajulikani walipo kutokana na mafuriko ya mvua zinazonyesha Mashariki mwa Uganda

- Aidha, maporomoko ya udongo yamewaacha maelfu ya watu bila makazi

Zaidi, soma https://jamii.app/UgandaFloods-Death36
MPYA: Milio ya risasi imerindima kati ya Al-Shabaab na Walinzi wa Hoteli ya Kifahari ya SYL katika Mji Mkuu wa Somalia, Mogadishu

- Al Shabaab wamevamia hotel hiyo karibu na Makazi ya Rais inayotumiwa zaidi na viongozi wengi wa Kisiasa

- Idadi ya Vifo bado haijajulikana

Zaidi, soma https://jamii.app/AlShabaabSYLHotel-Somalia
KENYA: MBARONI KWA KUSIMAMISHA MSAFARA WA RAIS NA KUOMBA KAZI

- Mwanaume mmoja, Uvinalies Nyabuto amekamatwa kwa kuusimamisha msafara wa magari wa Rais Uhuru Kenyatta

- Alishika bango la kumuomba Rais Kenyatta kazi kwenye Majeshi ya Ulinzi

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniKumsimamishaRais-KE
SOMALIA: AL SHABAAB WALIOTEKA HOTELI KWA SAA 7 WAUAWA

- Majeshi ya Ulinzi yamefanikiwa kuwaua Wanamgambo wote watano walioteka hoteli ya Kifahari ya SYL huko Mogadishu

- Aidha, watu wengine watano wakiwemo raia wawili wameuawa katika tukio hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/AlShabaabSYLHotel-Somalia
MICHEZO: KLABU YA NAPOLI YAMTIMUA KOCHA CARLO ANCELOTTI

- Timu ya Napoli ya Italia imemfukuza kazi kocha wao Carlo Ancelotti ikiwa ni chini ya masaa matatu baada ya kuiongoza timu hiyo kuingia hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Soma > https://jamii.app/AncelottiVsNapoli
#JFSports
RIPOTI: TATHMINI YA KIWANGO CHA KUJIFUNZA TANZANIA

- Taasisi za Twaweza na Uwezo Tanzania zinazindua ripoti hiyo ya mwaka 2019 leo jijini Dar

- Tangu mwaka 2011 ripoti hizo zimetoa mchango madhubuti katika kuongeza uelewa wa hali ya kisomo nchini

Fuatilia https://jamii.app/RipotiKiwangoKujifunza2019
MAREKANI YAWAWEKEA VIKWAZO VIONGOZI WA JESHI LA MYANMAR

- Marekani imefanya hivyo dhidi ya Viongozi wanne wa Kijeshi wa Myanmar akiwemo Mkuu wa Jeshi

- Marekani inalituhumu Jeshi la Myanmar kwa kukiuka haki za binadamu dhidi ya Warohingya

Zaidi, soma https://jamii.app/MarekaniVikwazoMyanmar
BALOZI WA SAUDI ARABIA NCHINI UTURUKI AZUIWA KUINGIA MAREKANI

- Marekani imemzuia Mohammed al-Otaibi, aliyekuwa Balozi wakati Mwanahabari Jamal Khashoggi alipouawa

- Khashoggi aliuawa ndani ya Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Uturuki mwaka jana

Zaidi, soma https://jamii.app/BaloziSaudiMarufukuUSA
RIPOTI: KIINGEREZA BADO TATIZO KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI

- Katika Tathmini ya #Uwezo ya mwaka 2017, takribani 85% ya wanafunzi wa darasa la 3 walishindwa kusoma insha fupi ya Kiingereza ya darasa la 2

- Kwa upande wa wanafunzi wa darasa la 7, takribani nusu (53%) walishindwa kusoma insha hiyo hiyo ya darasa la 2

Je, kuna umuhimu wa Serikali kuangalia upya lugha ya ufundishaji katika shule za Sekondari iwapo Kiingereza ni tatizo kwa wanafunzi wa shule za Msingi?

Jadili na Fuatilia https://jamii.app/RipotiKiwangoKujifunza2019
KENYA: GAVANA MIKE SONKO AACHIWA KWA DHAMANA

- Gavana huyo wa Nairobi ameachiwa kwa dhamana ya pesa taslimu Ksh. Milioni 15 au bondi ya Ksh. Milioni 30

- Pia, anatakiwa kutokwenda ofisini na akitaka vitu vyake atasindikizwa na Wapelelezi

Zaidi, soma https://jamii.app/SonkoAachiwaDhamana