JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BRAZIL HATARINI KUPOTEZA HAKI YA KURA UN KUTOKANA NA ADA YA UANACHAMA

> Hadi sasa nchi wanachama 54 hazijalipa michango ikiwemo Brazil ambayo inadaiwa na Umoja huo zaidi ya dola milioni 415

> Kwa mujibu wa ibara ya 19 ya sheria ili Brazil isipoteze haki hiyo inapaswa kulipa dola milioni 126 kufikia mwishoni mwa mwaka 2019

Soma - https://jamii.app/BrazilDebtUNFee
KENYA: WATU 10 WAPOTEZA MAISHA KWENYE SHAMBULIO LA KIGAIDI

> Takriban watu 10 wamefariki katika kaunti ya Wajir siku ya Ijumaa baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi Al-Shabaab kushambulia basi

> Kati ya waliofariki wapo Askari Polisi 7, Daktari pamoja na raia 2

Soma https://jamii.app/WajirTerrorAttack
VICHOCHEO VINAVYOWEZA KUMUATHIRI MTOTO MWENYE PUMU

> Mabadiliko ya halijoto: Mabadiliko haya huweza kupelekea dalili za pumu na hata kusababisha kushikwa na pumu

> Kichocheo cha vumbi: Vumbi huchangia kwa kiasi kikubwa sana kushikwa na pumu. Vumbi lipo kila mahali lakini jitihada zinaweza kufanyika ili kulipunguza nyumbani

> Wanyama pia huweza kusababisha dalili za pumu hasa paka, mbwa na kuku. Viumbe hawa mara nyingi wanatumia vumbi kama njia ya kujikuna na kuondoa wadudu katika miili yao

Tembelea - https://jamii.app/VichocheoPumuMtoto
MICHEZO: Klabu ya Chelsea yanyukwa bao 3 kwa 1 na Everton

> Magoli ya Everton yamefungwa na Richarlison dakika ya 5 na Calvert-Lewin aliyefunga dakika ya 49 na 84

> Goli pekee la kufutia machozi la Chelsea FC limefungwa na Mateo Kovačić kunako dakika ya 52

#JFLeo #JFSports
RIPOTI: UMASIKINI WAPUNGUA TANZANIA KWA ASILIMIA 2

> Umaskini wa mahitaji muhimu umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007, asilimia 28.2 mwaka 2012, hadi asilimia 26.4 mwaka 2018

> Umaskini wa chakula umepungua kutoka asilimia 22 mwaka 1991/92, asilimia 19 mwaka 2000/01, asilimia 17 mwaka 2007, asilimia 10 mwaka 2011/12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017/18

Soma - https://jamii.app/TakwimuHaliUmasikini
MASUMBWI: Bondia Anthony Joshua kutoka nchini England amempiga kwa pointi bondia Andy Ruiz Jr. kutoka Mexico

- Wawili hao wamepambana usiku huu katika pambano la marudiano Uzani wa Juu lililofanyika nchini Saudi Arabia

- Anthony Joshua alipigwa na Andy Ruiz Jr. kwa TKO katika pambano lao la mwezi Juni 2019

#RuizVsJoshua2 #JFLeo
DELHI, INDIA: ZAIDI YA WATU 30 WAMEFARIKI BAADA KIWANDA KULIPUKA

> Mlipuko huo umetokea asubuhi ya leo na imeelezwa kuwa wengi wa waliofariki ni Wafanyakazi wa Kiwanda hicho waliokuwa wamelala

> Zaidi ya watu 50 wamejerujiwa

Zaidi, soma > https://jamii.app/FactoryBlazeDelhi
TANZIA: MFANYABIASHARA ALI MUFURUKI AFARIKI

- M/Kiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech Investment Group, Ali Mufuruki amefariki dunia leo

- Aliwahi kuwa Mkurugenzi Huru, Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania kabla ya kujiuzulu

Soma > https://jamii.app/RIPMufuruki
TANZIA: MHUBIRI NA MWINJILISTI REINHARD BONNKE AFARIKI DUNIA

- Bonnke amefariki akiwa na umri wa miaka 79

- Atakumbukwa kwa kuweka rekodi ya wahudhuriaji wengi katika mikutano yake aliyoifanya ktk mataifa mengi ya Afrika ikiwemo Tanzania

Soma > https://jamii.app/RIPBonnke
IRAN: WATU 81 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA HOMA YA MAFUA

> Watu 81 wamepoteza maisha kwa sababu ya Homa ya Mafua nchini Iran huku wiki iliyopita, watu 8,333 wamefikishwa hospitalini wakilalamika kuandamwa na Mafua Makali

> Hali hiyo ilimepelekea msongamano wa wagonjwa na wengine kutibiwa wakiwa wamesimama

Soma - https://jamii.app/VifoHomaMafua
MASHIRIKA YA KIRAIA DRC YAIOMBA ICC KUCHUNGUZA MAUAJI YA RAIA

> Mashirika ya Kiraia na Wadau mbalimbali Duniani, yameitaka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ktk Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuchunguza mauaji yanayoendelea Wilayani Beni

> Tangu mwezi Novemba, watu zaidi ya 100 wameuawa baada ya kushambuliwa na waasi wa ADF Nalu

Soma - https://jamii.app/ICCAssistanceBeniMassKilling
TANZIA: ALIYEKUWA BALOZI WA TANZANIA URUSI AFARIKI

> Aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi katika Serikali ya Awamu ya Nne, Balozi Jaka Mwambi amefariki leo Desemba 8, 2019

> Pia, marehemu aliwahi kuwa Mkuu wa Mikoa ya Tanga, Rukwa na Iringa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara

Soma - https://jamii.app/RIPBaloziMwambi
SHINYANGA: WANAUME WADAIWA KUWAOZESHA WATOTO WAO WADOGO KWA POMBE

- Wanawake katika Kijiji cha Penzi wamewashutumu Wanaume kwa kuwaozesha watoto wao bila kuwajulisha kwa kubadilishana na jagi la pombe wawapo vilabuni au mifugo aina ya ng’ombe

Zaidi, soma https://jamii.app/WanaumeKuozaBinti-SHY
Bodi, Uongozi na Wafanyakazi wote wa Jamii Forums tunaungana na Watanzania wote kusheherekea Kumbukumbu ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika
MLIMBWENDE WA AFRIKA KUSINI ATWAA TAJI LA MISS UNIVERSE

- Zozibini Tunzi (26) ameshinda taji hilo katika mashindano yaliyofanyika Atlanta, Georgia

- Madison Anderson (Puerto Rico) amekuwa mshindi wa pili huku Sofía Aragó (Mexico) akiwa mshindi wa tatu

Zaidi, soma https://jamii.app/MissUniverse2019-SA
MBEYA: AUAWA AKITUHUMIWA KUWATESA WANANCHI KWA UCHAWI

- Polisi inawashikilia Watu watatu wakidaiwa kumuua John Mwakarundwa(62), Mkazi wa Kijiji cha Nkunga, Rungwe

- Wananchi walikuwa wakimtuhumu Marehemu kununua uchawi Malawi na kuwatesa nao

Zaidi, soma https://jamii.app/AdaiwaMchawiAuawa
NEW ZEALAND: MMOJA AFARIKI NA TAKRIBAN 27 HAWAJULIKANI WALIPO KUTOKANA NA MLIPUKO WA VOLKANO

- Watu 23 wameokolewa katika Mlipuko huo uliotokea kwenye Mlima uliopo Kisiwa cha 'White Island'

- Polisi imesema kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka

Zaidi, soma https://jamii.app/MlipukoVolkanoNewZealand
MIAKA 58 YA UHURU: RAIS MAGUFULI ASAMEHE WAFUNGWA 5,533

- Amesema, ameshuhudia mrundikano wa wafungwa ambapo hadi leo kuna Wafungwa 17,547 na Mahabusu 18,256

- Amesema, baadhi yao wamefungwa kutokana na makosa madogo yakiwemo ya kuiba kuku

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAhameheWafungwa5533
TIMU YA TAIFA YA URUSI YAFUNGIWA KUSHIRIKI MICHEZO MIKUBWA

- Wakala wa Kupambana na Dawa za Kuongeza Nguvu (WADA) wameifungia Timu ya Soka ya Urusi

- Haitashiriki michuano ya Olimpiki ya mwaka 2020 na Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar

Zaidi, soma https://jamii.app/TimuUrusiYafungiwa
MBINU ZA KUKUWEZESHA KUFANYA BIASHARA KWA MTAJI MDOGO

> Chagua wazo la biashara unalolipenda na kuliweza vyema

> Anza na unachokijua pasipo kuhusisha mambo mengi mageni kwa kuwa huna pesa za kuyagharamia

> Waambie watu unachokifanya ili kupata wateja na kufahamika na usiogope kueleza kuwa unafanya biashara ya aina fulani

Soma - https://jamii.app/BiasharaMtajiMdogo
#JFBiashara