JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UGANDA: WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI WATAKIWA KUPELEKA MAJINA YA WATEJA POLISI

- Polisi imesema, hiyo ni njia mojawapo ya kupambana na uhalifu

- Taarifa hizo zitakazokusanywa kila asubuhi zitatumiwa katika masuala ya Kiintelijensia

Zaidi, soma https://jamii.app/HoteliersGuestPolice-UG
RC PAUL MAKONDA AMTAKA IDRIS SULTAN KUFIKA POLISI

- Amemtaka Mchekeshaji huyo kufika Kituo chochote cha Polisi na huko atakuta ujumbe wake

- Ni baada ya Idris kuhariri picha ya Rais Magufuli na kuichapisha kwenye Mitandao yake ya Kijamii

Zaidi, soma https://jamii.app/MakondaIdrisPolisi
UGANDA: MSICHANA WA MIAKA 11 AFANYIWA UPASUAJI NA KUBADILI JINSIA, ASEMA AMETIMIZA NDOTO YA KUWA MVULANA

- Mtoto huyo alizaliwa akiwa na jinsi ya Kike lakini kadiri siku zinavyokwenda sehemu ya uke wake ilianza kubadilika na kuota uume

Soma => https://jamii.app/UpasuajiJinsiaMulago
KAGERA: KAIMU MENEJA KAMPUNI YA RANCHI YA TAIFA (NARCOS) KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

- Prof. Philemoni Nyangi, anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya Ofisi, Ubadhirifu na Uhujumu Uchumi

- Anadaiwa kupokea Tsh. Milioni 12 kwa aliyehitaji kitalu

Zaidi, soma https://jamii.app/KMenejaNARCOKizimbani
GUINEA-BISSAU: RAIS AMTANGAZA WAZIRI MKUU MPYA LAKINI WAZIRI MKUU WA SASA AGOMA KUACHIA NGAZI

- Rais Jose Vaz, amemtangaza Faustino Imbali kuwa Waziri Mkuu mpya

- Waziri Mkuu wa sasa, Aristides Gomes asema anaendelea na kazi kama kawaida

Soma > https://jamii.app/VazVsGomes
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UGANDA: Askari Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya Wanafunzi wanaondelea na mgomo katika Chuo Kikuu Makerere

- Wanafunzi wamedai Polisi hao wametumia risasi za moto dhidi ya Wanafunzi waliokuwa vyumbani ktk bweni la Mitchell

Soma > https://jamii.app/PolisiVsWanafunziMakerere
LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA: SIMBA SC YANYUKWA BAO 1 KWA 0 NA MWADUI FC

> Bao pekee la Mwadui FC limefungwa na Gerald Mathias kunako dakika ya 33 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo

#JFSports
BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA YAIPATIA TANZANIA TAKRIBAN TRILIONI 1.04

- Imetoa Dola za Marekani Milioni 180 za kujenga barabara za mzunguko Jijini Dodoma na Dola Milioni 275 za kujenga Uwanja wa Ndege wa Msalato zitaidhinishwa Novemba 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/AfDB-TanzaniaMsalato
JAFO: NIMEPOKEA MALALAMIKO 72 KATIKA UCHUKUAJI NA UREJESHAJI FOMU

- Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema amepokea malalamiko kutoka Kata 72 kuhusu dosari mbalimbali katika uchukuaji na urejeshaji fomu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Zaidi, soma https://jamii.app/JafoMalalamikoUchaguziMitaa
HT: Liverpool 2-3 Arsenal

#LIVARS #CarabaoCup
HALF TIME!

πŸ”΅ #CFC 0-1 #MUFC πŸ”΄

Rashford's penalty is the difference after 45 mins
FT: Liverpool 5-5 Arsenal

#penaltytime #LIVARS #CarabaoCup
FT: Chelsea 1-2 Man Utd

#CHEMNU #CarabaoCup2019
WANAUME WANAONYONYA MAZIWA YA WAKE ZAO WAONYWA

- Onyo hilo kali limetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Lishe katika Wizara ya Afya, Dkt. Grace Moshi

- Amesema, Wanaume wanaonyonya maziwa ya Wake zao wanaonyonyesha waache kwani wanawapunja watoto

Zaidi, soma https://jamii.app/OnyoWanaumeWanyonyaji
PAKISTANI: TAKRIBAN WATU 16 WAMEFARIKI BAADA YA TRENI KUWAKA MOTO

- Wengine 13 wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea mapema leo

- Moto umesababishwa na jiko la gesi lililolipuka wakati abiria wakipika chai ambapo ni Kinyume cha Sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/TrainFireKills16-PKST
UPDATE: Kwa mujibu wa The Associated Press, Maafisa wa Uokoaji wa Pakistani wamesema idadi ya vifo vilivyotokea kwenye treni iliyowaka moto vimefikia 62

- Aidha, Watu wengi wamejeruhiwa na kati yao wengi wao wapo mahututi. Shughuli za uokoaji zinaendelea

Zaidi, soma https://jamii.app/TrainFireKills16-PKST
SHINYANGA: MGONJWA WA AKILI AFUNGIWA CHUMBANI

- Shadrack Johanes(26), amefungiwa kwa miezi miwili akiwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni

- Ndugu wanadai hawana hela ya matibabu na wakimuacha anawatia hasara kwa kuharibu mali za watu

Zaidi, soma https://jamii.app/MgonjwaAkiliAfungiwa-SHY
KISUTU, DAR: WATUHUMIWA 3 WALIOSHTAKIWA KWA KUIBA TAUSI WA IKULU, WAHUKUMIWA KULIPA FIDIA YA MILIONI 6.8

- David Graha, Mohamed Hatibu na Mohamed Ally walikamatwa kwa tuhuma za kukutwa na Ndege 3 aina ya Tausi, wa Ikulu Jijini Dar

Zaidi, soma > https://jamii.app/WashtakiwaTausiFidia
UGANDA: GODFREY WAMALA AHUKUMIWA MIAKA 14 KWA HATIA YA KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANAMUZIKI RADIO

- Godfrey Wamala β€˜Troy’ amekutwa na hatia ya kumuua bila ya kukusudia Moses Ssekibogo(Mowzey Radio)

- Alimpiga Radio hadi akapoteza fahamu na kulazwa Hospitali ya Case alikofariki

Zaidi, soma > https://jamii.app/TroyKifoRadio
KENYA: MWAI KIBAKI ADAIWA KULAZWA HOSPITALINI. MSAIDIZI WAKE AKANUSHA

- Rais wa zamani, Mwai Kibaki (88) anadaiwa kulazwa kutokana na maumivu ya goti

- Msaidizi wake amesema, Kibaki hajalazwa ila alienda hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya

Zaidi, soma https://jamii.app/KibakiAdaiwaKulazwa