JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DODOMA: ASKARI WA FFU KIZIMBANI KWA JARIBIO LA KUUA MTOTO

> Aliyekuwa Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Christopher Charles (23) amefikishwa Mahakamani akishitakiwa kwa kosa la kujaribu kumuua mpwa wake

> Kesi imeahirishwa mpaka Novemba 7, 2019 na Mshtakiwa amerudishwa rumande

Soma - https://jamii.app/MjombaKuuaMpwa
MARA: AMKATA MASIKIO MKEWE BAADA YA KUPOTEZA SIMU YAKE

> Polisi Mkoani Mara wanamsaka Bwana Magori, Mkazi wa Serengeti, akidaiwa kumkata masikio yote Mkami Mwitonyi (22) kwa madai ya kupoteza simu yake

> Alimning’iniza Mkewe juu ya dari na kumkata masikio huku akimtishia kumchinja

Soma - https://jamii.app/MeAkataMasikioKe
ZIMBABWE: WABUNGE WA UPINZANI WAZUIWA KUWAHOJI MASWALI MAWAZIRI HADI WAKUBALI KUWA MNANGAGWA NI RAIS HALALI

> Kiongozi wa Chama cha MDC, Nelson Chamisa alikataa kuukubali ushindi wa Emmerson Mnangagwa baada ya uchaguzi 2018

Zaidi, soma > https://jamii.app/WapinzaniZimb
SERENGETI: ASKARI WA HIFADHI AKATWA MKONO NA JANGILI ALIYEMKAMATA AKICHUNGA NG'OMBE MBUGANI

- Askari Deus Mwakajegera(35) amekatwa mkono wa kushoto na Mtu huyo aliyetajwa kuwa jangili aliyeingia ndani ya Hifadhi katika Kijiji cha Bisarara

Soma > https://jamii.app/AskariTANAPAMkono
SOMALIA YAIKABIDHI KENYA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB

> Polisi kutoka Somalia wamewakabidhi Polisi wa Kenya watuhumiwa 2 wa ugaidi wa Kundi la Al-Shabaab, ikiwa ni sehemu ya juhudi za pamoja za kuzuia mashambulizi ya kuvuka mipaka

> Polisi wamesema, wapiganaji hao walihusika na shambulizi lililotokea Oktoba 12 huko Liboi, ambapo Polisi 11 waliuawa

Soma - https://jamii.app/SomaliaWanamgamboAlshabaab
ZAMBIA: MGONJWA WA KWANZA WA POLIO ARIPOTIWA TANGU MWAKA 1995

- Mtoto wa Kiume wa miaka 2 amebainika kupooza baada ya chanjo ya Polio kushindwa kufanya kazi vizuri

- 2015 Tanzania ilipongezwa na UNICEF kwa kutokuwa na Wagonjwa wa Polio

Zaidi, soma > https://jamii.app/PolioZambia2
CONAKRY, GUINEA: WANANCHI WAANDAMANA KUPINGA RAIS CONDE KUWANIA MUHULA WA TATU, 9 WAUAWA

- Maelfu ya Wananchi wameandamana wakipinga mkakati wa kubadili kifungu cha Katiba ili kutoa nafasi kwa Alpha Conde kuwania muhula wa 3

Zaidi, soma => https://jamii.app/MaandamanoGuinea
KISUTU, DAR: WATU WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUIBA TAUSI WA IKULU

- Waliofikishwa Mahakamani ni Mohamed Hatibu, Mohamed Ally na David Graha na kushtakwia kwa kutenda kosa hilo kati ya Julai 1, 2015 na Oktoba 14, 2019

Zaidi, soma > https://jamii.app/WiziTausi
WATOTO 3 KATI YA 1000 HUZALIWA NA ULEMAVU WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI

> Watoto 1000 wanaozaliwa kila siku Tanzania, 3 kati yao huzaliwa na matatizo ya ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi, idadi ambayo kwa mwaka hufikia watoto 4800

> Chanzo ni upungufu wa madini ya 'Folic Acid' na virutubisho muhimu wakati wa ujauzito

Soma - https://jamii.app/MaadhimishoMgongoWaziKichwaKikubwa
WAPINZANI WAPINGA MPANGO WA SILAHA ZA NYUKLIA RWANDA

> Kiongozi wa chama cha upinzani cha Green nchini Rwanda, Frank Habineza amepinga mpango wa nchi yake kujenga kiwanda cha nyuklia kwa ushirikiano na Urusi akisema utakuwa na athari mbaya kwa wananchi pamoja na Taifa lenyewe

Soma - https://jamii.app/OppositionRejectsNuclearDeal
JIFUNZE KILIMO CHA UYOGA

> Mdau wa JamiiForums.com anadai kuwa aina za uyoga zinazofaa kulimwa Tanzania ni zile zinazostawi vizuri kwenye maeneo ya joto la wastani wa nyuzi joto 20c hadi 33

> Ili kuzalisha uyoga inabidi kuwa na chumba chenye paa na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa uyoga

> Malighafi zitumikazo kuzalisha uyoga ni pamoja na mabua, majani ya mpunga, ngano, pumba za mpunga au mahindi, masalia ya miwa baada ya kukamua ambayo hukatwa, huchemshwa na kutandazwa kwaajili ya mbengu kupandwa

> Uyoga huwa tayari kuchumwa siku tatu baada ya vichwa/pini kuonekana. Uyoga uvunwe kwa mkono kwa kushika katikati ya shina la uyoga kisha zungusha hadi uyoga ung’oke

Fahamu zaidi, soma - https://jamii.app/KilimoUyoga
SANTIAGO, CHILE: ZAIDI YA WATU MILIONI 1 WAANDAMANA

> Ni maandamano makubwa kuwahi kutokea baada ya yale ya mwaka 1988 dhidi ya utawala wa kidikteta wa Pinochet
ZIMBABWE WAANDAMANA KUPINGA VIKWAZO VYA MAREKANI NA UMOJA WA ULAYA

> Marekani na Ulaya imewawekea vikwazo maafisa wengi waandamizi wa Zimbabwe pamoja na Rais Mnangagwa kwa madai ya kukiuka haki za binadamu na udanganyifu katika Uchaguzi Mkuu, miaka iliyopita

> Rais Mnangagwa amesema vikwazo hivyo vimeathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Zimbabwe

Soma - https://jamii.app/ZBWProtestSASanctions
MVUA MKOANI TANGA: TAKRIBAN WATU 8 WAFARIKI

> Takriban Watu nane (8) wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya gari aina ya Noah kutumbukia kwenye daraja ktk eneo la Sindeni barabara kuu ya Handeni - Korogwe, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Tanga
ABIRIA WANAOSAFIRI DAR, ARUSHA NA KILIMANJARO WAKWAMA NJIANI KWA SAA 20

> Abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Arusha, Kilimanjaro na nchi jirani na waliotoka Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali wamekwama tangu jana, saa 5 asubuhi Wilayani Korogwe na Handeni kutokana na maji yaliyotokana na mvua kupita juu ya daraja la Mandera na kulisomba daraja la Handeni

Soma - https://jamii.app/AbiriaWakwamaMvua
HOJA: FANI YA UFUNDI WA MAGARI IMEJAA WATU WASIO NA ELIMU HIYO, WASOMI TUNAKWAMA WAPI?

> Mdau wa JamiiForums amesema yeye ni Mhitimu wa Mechanical Engineering na amejikita katika Ufundi wa Magari

> Anasema, watu mahiri katika fani hiyo ni wale ambao hawakwenda shule

Kwa mjadala, fungua > https://jamii.app/UfundiMagariElimu