JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KISUTU, DAR: MAHAKAMA YATAKA HAKI ITENDEKE KATIKA KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU

> Godfrey Gugal pamoja na wenzake wanatuhumiwa kwa kumiliki mali zeye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 3.6 kinyume na kipato chake halali

Zaidi, soma => https://jamii.app/KesiMhasibuPCCB
RUVUMA: BINTI WA MIAKA 26 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA 'BOYFRIEND' WAKE

> Aliyeuawa ni Beata Kafuru aliyepigwa risasi 3 za kichwani na James Paul (27), anayeelezwa kuwa ni mpenzi wake

> Chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi

Soma > https://jamii.app/RIPBeataKafuru
AFYA: FAIDA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO YENYE LIMAO ASUBUHI

> Maji hayo huongeza Kinga ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo, husafisha mfumo wa chakula, na kuondoa sumu mwilini

> Pia, huleta hewa/harufu safi kinywani

Kwa faida zaidi, soma => https://jamii.app/MajiLimao
#JFAfya
Treni imeacha njia maeneo ya Buguruni Chama na kusababisha msongamano mkubwa.

> Dereva unayetumia njia hiyo asubuhi hii, unashauriwa kutumia njia mbadala

Fuatilia zaidi > https://jamii.app/TreniImeachaNjiaBuguruni
KENYA: SERIKALI YAONDOA AMRI YA KUFUNGWA KWA TAASISI YA 'MARIE STOPES'

> Serikali ya Kenya imeondoa marufuku hiyo baada ya takwimu kuonesha kuwa Wanawake 320 wanalazwa na 7 wanafariki kila siku kwa kujaribu kutoa mimba kiholela

Zaidi, soma > https://jamii.app/MarieStopesKenya
IPTL INADAI FIDIA YA TSH. TRILIONI 6.5 BENKI YA STANDARD CHARTERED

> IPTL imeiomba Mahakama Kuu itamke rasmi kwamba Standard Chartered Bank (Hong Kong) si wadai wake na ibatilishe tuzo ilizopewa Ulaya bila kuwepo mhusika mkuu katika migogoro hiyo

> IPTL imeifungulia SCBHK kesi mbalimbali za madai ktk Mahakama Kuu, Dar

Soma - https://jamii.app/IPTLKudaiFidiaSCBHK
NDEGE YA AUSTRALIA YAFANYA MAJARIBIO YA SAFARI NDEFU BILA KUSIMAMA

- Qantas imekamilisha safari yake ya kibiashara ya maili 10,066 bila kusimama, ikifanya utafiti wa athari za safari ndefu zinazoweza kutokea kwa Marubani, Wafanyakazi na Abira

Soma https://jamii.app/NdegeAustraliaSafariNdefu
KENYA: AJISALIMISHA POLISI BAADA YA KUMUUA MWENZAKE WAKIGOMBEA KUMBIKUMBI

> Muriungi Kiyogere (35), mkazi wa Kaunti ya Tharaka-Nithi anadaiwa kumchoma kisu mara nne Daniel Mutiria Cece (36), kutokana na mzozo wa kugombea Kumbikumbi Jumapili jioni

> Alikimbilia Polisi kuwakwepa wanakijiji waliokuwa wakitaka kumuua

Soma - https://jamii.app/KifoUgomviKumbikumbi
HOJA: JE, NI AIBU KWA KIJANA MWENYE MIAKA ZAIDI YA 35 KUISHI KWA WAZAZI WAKE?

> Mdau wa JamiiForums anasema anasema wazazi wanashindwa kuishi kwa uhuru kwa sababu ya uwepo wako

> Anahoji, unawezaje kuendelea kula ugali wa shikamoo kwa umri huo?

Shiriki mjadala, hapa > https://jamii.app/JFHoja
UMUHIMU WA KUWASILIANA NA MWANAO

> Iwapo wazazi watadumisha mawasiliano ya karibu na watoto, hapatakuwa na haja ya kutumia nguvu nyingi kumjenga mtoto

> Tumia muda kuwasimulia watoto hadithi za chimbuko la familia yao. Hii itawapa nafasi ya kujivunia utu wao

> Jenga tabia ya kuandikiana jumbe za maneno kwenye karatasi. Hii inakupa fursa ya kujua kama anaweza kusoma na vilevile utapata kuuona mwandiko wake

> Kuwa na subira katika maongezi na mwanao. Mvumilie na jitahidi usiwe mwongeaji sana bali msikilizaji

Zaidi, soma - https://jamii.app/MbinuMawasilianoMtoto
#JFMalezi
MADHARA YA MVUA AFRIKA MASHARIKI: WATU 105 WAPOTEZA MAISHA

> Nchini Tanzania, takriban watu 16 wamefariki, Sudan Kusini, watu zaidi ya 200,000 wameathiriwa na Kenya, zaidi ya watu 1,000 wameyakimbia makazi yao

> Rwanda, watu 70 wamefariki na 177 kujeruhiwa. Nyumba 4,095 na hekta 6,708 zimeharibiwa huku wanyama 167 wakifa

Soma - https://jamii.app/MadharaMvuaEAC
CCM YAFUTA KURA ZA MAONI BAADHI YA SEHEMU, UCHAGUZI KURUDIWA

> Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema kumekuwa na madai ya rushwa, upendeleo na kanuni za kuchuja wagombea hazikuzingatiwa kwenye baadhi ya maeneo

> Pia, kulikuwa na rafu za kuchomoa majina kwenye masanduku ya kura na masanduku kubomolewa

Soma - https://jamii.app/MarudioKuraMaoniCCM
RUKWA: RC AAGIZA KUKAMATWA KWA WALIMU 2 WANAOTUHUMIWA KUBAKA NA KUWAPA MIMBA WANAFUNZI

> RC Joachim Wangabo ameagiza kukamatwa kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya, Dastan Mlelwa na Mwalimu mmoja wa Shule ya Sekondari Mpui

Zaidi, soma => https://jamii.app/RCRukwaVsWalimu
ZIMBABWE: TEMBO 55 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA UKAME

> Tembo 55 wamekufa njaa tangu Septemba 2019 katika Mbuga ya Taifa ya Hwange kutokana na ukame wa zaidi ya miezi 2

> Theluthi moja ya watu nchini humo wameripotiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula

Soma - https://jamii.app/UkameVifoTembo
UGANDA: AFISA WA MAGEREZA (MWANAMKE) APORWA SILAHA, ALIKUWA AKIPIGA SOGA WHATSAPP

> Hadijah Katono ameporwa silaha na kijana aliyekuwa amejihami kwa Mkuki

> Kijana huyo alimpiga mara 2 kisha kuchukua bunduki hiyo aina ya AK-47 na kutokomea

Soma https://jamii.app/MpigiPrisonOfficer
TTCL YAKUBALI KUPELEKA HUDUMA YA INTANETI BURUNDI

> Shirika la TTCL limesaini mkataba huo na Kampuni ya Mawasiliano ya Mkongo wa Taifa ya Burundi (BBS) wenye thamani ya Tsh. bilioni 13.8

> Mkataba huo utatekelezwa nchini Burundi kwa miaka 10

Soma > https://jamii.app/TTCLVsBSS
VLADMIR PUTIN: TUNAWEZA KUISAIDIA AFRIKA BILA MASHARTI YA NCHI ZA MAGHABIRI

> Rais wa Urusi amesema nchi yake inaweza kuisaidia Afrika bila masharti ambayo huambatanishwa kwenye misaada ya Mataifa ya Magharibi

> Amesema, Mataifa ya Magharibi yanatoa mashinikizo na vitisho dhidi ya Serikali Huru za Kiafrika ili kurejesha utawala wa kikoloni na kulinyonya Bara la Afrika

Soma - https://jamii.app/PutinMisaadaAfrika
SAME: WANANCHI WALALAMIKA WAJAWAZITO KUTUMIA CHUMBA KIMOJA NA WANAOSAFISHWA VIDONDA

> Inadaiwa ukosefu wa Wodi ya Wajawazito katika Zahanati ya Lugulu iliyopo Wilaya ya Same, umesababisha wanaotaka kujifungua watumie chumba kimoja na wagonjwa wanaosafishwa vidonda

> Aidha, baada ya kujifungua wanawake walikuwa wakibebeshwa uchafu kutokana na kukosekana kwa shimo maalum la kutupia taka zitokanazo na Uzazi

Soma - https://jamii.app/UkosefuWodiWajawazito
KUSUASUA KWA UJENZI WA KIWANDA CHA TANGA FRESH: SERIKALI YAUNDA TUME YA UCHUNGUZI

> Serikali imebaini mtambo wa kusindika maziwa ya muda mrefu ulionunuliwa, ulikwishatumika na umenunuliwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni 6

Kwa habari zaidi, soma > https://jamii.app/UchunguziTangaFresh
MAREKANI: RAIS MSTAAFU JIMMY CARTER AANGUKA NA KUVUNJIKA NYONGA, AKIMBIZWA HOSPITALI

> Jimmy Carter(95) sasa amelazwa katika Kituo cha Afya cha Phoebe Sumter baada ya kuanguka na kuvunjika nyonga

> Aliiongoza Marekani mwaka 1977 hadi 1981

Soma > https://jamii.app/JimmyCarterPelvic