JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KISWAHILI CHAZIDI KUSAMBAA DUNIANI

- Klabu ya soka ya Italia ya AS Roma ipo kwenye mkakati wa kutumia Kiswahili katika moja ya kurasa zake za Mitandao ya Kijamii

- Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, imesema siku chache zijazo itafungua ukurasa wake rasmi wa Kiswahili
MWANARIADHA MWINGINE WA KENYA AVUNJA REKODI YA DUNIA

- Brigid Kosgei (25) avunja rekodi ya muda wa kukimbia marathon kwa Wanawake akiwa kwenye Marathon ya Chicago

- Ameweka rekodi ya kumaliza mbio kwa 2:14: 04 akivunja rekodi iliyokuwepo kwa dakika moja na Sekunde 21

Zaidi, soma https://jamii.app/KosgeiAwekaRekodi
SERIKALI KUZIPATIA RUZUKU KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI

- Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imeahidi hayo baada ya kuridhishwa na Wananchi katika vijiji vilivyonufaika, walivyoboresha maisha yao na kujikwamua katika umasikini

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliRuzukuMasikini
MIAKA 20 YA KUMBUKIZI YA KIFO CHA BABA WA TAIFA

- Leo Oktoba 14, 2019 ni Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki katika Hospitali ya Mt. Thomas Jijini London, Uingereza

- Mwalimu Nyerere alizaliwa Butiama, Mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprill 1922, alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na ndiye mwasisi wa Itikadi ya ‘Ujamaa na Kujitegemea’
BAADA YA KUSTAAFU SOKA, PETR CECH AGEUKIA ICE HOCKEY

- Aliyewahi kuwa golikipa wa Chelsea na Arsenal, Petr Cech (37) ameanza kucheza mchezo wa Ice Hockey ambapo jana ameokoa penati 2 na kusaidia timu yake kushinda

- Wiki iliyopita aliingia mkataba na timu ya Guildford Phoenix inayocheza Ligi ya Kitaifa ya South 2, nchini England
BOEING YA PILI YA TANZANIA YAFANYIWA MAJARIBIO

- Boeing 787-8 Dreamliner imefanyiwa majaribio Jumamosi Oktoba 12, 2019 huko Marekani

- Hata hivyo, siku ya kupokea ndege hiyo iliyoandikwa ‘Rubondo Island - Hapa Kazi Tu’ haijawekwa wazi

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeRubondoMajaribioTZ
TISHIO LA UGAIDI KENYA: USALAMA WAIMARISHWA KAUNTI YA MANDERA

> Polisi katika Kaunti ya Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya wapo ktk tahadhari, baada ya kuripotiwa kuonekana kwa washukiwa 20 wa kundi la kigaidi la Al Shabaab

> Magaidi hao walionekana katika maeneo ya Bale-Ilman Mala na Kutulo siku ya Ijumaa

Soma - https://jamii.app/AlShabaabGangSpotted
FAO YATOA TAHADHARI YA MAGONJWA SUGU KUTOKANA NA MILO MIBOVU

> Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), limeitahadharisha Tanzania kuwepo kwa ongezeko la idadi ya watu walio katika hatari ya kupata Shinikizo la Damu, Kisukari, Magonjwa ya Moyo, Kiharusi na Saratani kutokana na milo mibovu, aina ya maisha ya kutofanyisha miili kazi na unene uliopitiliza

Soma - https://jamii.app/MagonjwaUlajiMbovu
KIMBUNGA HAGIBIS JAPAN: VIFO VYAFIKIA TAKRIBAN WATU 30

> Zaidi ya waokoaji 110,000 wamepewa kazi ya kuwatafuta na kuwaokoa watu walioathiriwa na kimbunga hicho kilichotokea Jumamosi

> Takriban watu 16 hawajulikani walipo na nyumba zaidi ya laki tano hazina umeme

Soma - https://jamii.app/DeathTollHagibisTyphoon
MDAU: BOYFRIEND WANGU MCHAFU SANA, KANISHINDA

- Mdau anasema “Mimi sio mtu msafi sana ila Mwanaume huyu amenishinda. Ni mtu mzuri na nimekuwa naye kwa miezi 8 sasa, mwanzo sikuwa nimemuelewa ila huyu Mwanaume ni mchafu sana.”

- Anaendelea “Chumba chake ni kichafu. Huna nasafisha, nisiposafisha hakutaniki. Akioga usiku kabla ya kulala asubuhi haogi, analala na Mwanamke asubuhi anaenda kazini hivyo hivyo. Nikisema anasema nampanda kichwani.”

Kushiriki mjadala, tembelea https://jamii.app/BoyfriendMchafuSana
UGANDA: ASKARI AKAMATWA KWA KUMUUA MTUHUMIWA KWA RISASI

> Askari Polisi ktk Wilaya a Sironko amekamatwa kwa kumpiga risasi Mathew Wodeya (23) akiwa nyumbani kwake baada ya kudaiwa alijaribu kukataa kukamatwa

> Wodeya alikuwa akituhumiwa kwa kosa la kunajisi ambapo alipigwa risasi tumboni, shingoni na kifuani

Soma - https://jamii.app/PoliceShotDeadSuspect
ZINGATIA MUONGOZO HUU KATIKA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

> Zingatia usafi wa vyombo na mazingira ya kuku kwani uchafu ni mama wa magonjwa. Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni

> Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe bandani na kufukiwa

> Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa na Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja

> Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na hakikisha unaziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia bandani

Kujua zaidi, soma - https://jamii.app/UfugajiKukuKienyeji
MAASKOFU WA KATOLIKI KURATIBU MPANGO WA KUMTANGAZA MWL. NYERERE MTAKATIFU

- Mpango huo ulioanzishwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Musoma Mkoani Mara umehamishiwa Jimbo Kuu la Dar chini ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC)

Zaidi, soma https://jamii.app/NyerereMtakatifu-TEC
RAIS MAGUFULI: TUMEMUENZI NYERERE KWA KUFUFUA MASHIRIKA YA UMMA NA KUSIMAMIA NIDHAMU

> Amesema Serikali imefanya mambo mengi katika kumuenzi Baba wa Taifa ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu Serikalini, kuyafufua Mashirika ya Umma, kurejesha nidhamu katika Utumishi wa Umma na kulinda Rasilimali za Taifa

> Amesema jitihada zote zimelenga katika kuziishi fikra za Baba wa Taifa ambaye alilijenga Taifa katika misingi ya Ujamaa na Kujitegemea

Soma - https://jamii.app/MagufuliKumuenziNyerere
CUF: KUTOFANYIKA KWA MIKUTANO YA KISIASA NI SABABU YA WATU KUTOJIANDIKISHA KUPIGA KURA

> Chama cha Wananchi (CUF) kimesema mikutano ya kisiasa huhamasisha wananchi kujiandikisha na kujua umuhimu wa kufanya hivyo katika uchaguzi

> Sababu nyingine ni kufanyika kwa uchaguzi usio huru na haki, kupatikana kwa washindi wanaopita bila kupingwa na viongozi waliochaguliwa kuhama vyama vya upinzani na kwenda CCM

Soma - https://jamii.app/CUFUandikishajiKura
KENYA: MABAKI YA MIILI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA ETHIOPIAN AIRLINE YAWASILI

- Wakenya leo wamepokea mabaki ya miili ya wapendwa wao waliofariki katika ajali ya Ndege ya Ethiopia iliyoanguka mwezi Machi na kuwaua watu wote 157 waliokuwemo

Zaidi, soma https://jamii.app/MiiliWakenyaEthiopianAirline
MCHEZO WA KIRAFIKI: TAIFA STARS YATOKA SARE NA RWANDA

- Taifa Stars ikicheza bila ya nahodha wake, Mbwana Samatta imefanikiwa kutoka sare ya bila kufungana (0-0) na Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo, Kigali

#JFLeo