JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BARABARA ENEO LA MANDERA HAIPITIKI, WASAFIRI WASHAURIWA KUBADILI NJIA

- Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha sehemu ya barabara katika eneo la Mandera Mkoani Tanga kujaa maji tangu jana

- Wanaosafiri kuelekea mikoa ya Kaskazini na wanaoelekea Dar kutoka mikoa hiyo wameshauriwa kupitia Handeni
MJADALA: MUHIMU KUWA NA UCHAGUZI SI UCHAFUZI WA DEMOKRASIA

- Mdau wa JamiiForums anadai katika Nchi ya Kidemorasia Uchaguzi unafanyika kwa sababu mbili kubwa, kwanza ni Wananchi kupima na kutoa hukumu kwa yale yaliyofanywa na pili ni Wananchi kufanya uamuzi juu ya utawala wao

- Amedai nchi zenye demokrasia iliyokomaa zimefanya mambo makubwa kadhaa ikiwemo kutengeneza na kusimika mfumo wa uchaguzi unaohakikisha aliyeko madarakani anaweza kushinda au kushindwa bila dhulma

Kujadili, tembelea https://jamii.app/UchaguziDemokrasiaWananchi
SERIKALI YAONGEZA SIKU 3 ZA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA

> Waziri Jafo ametangaza Serikali kuongeza siku 3 za Uandikishaji wa Wapiga Kura kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura

> Sasa zoezi hilo litakamilika Oktoba 17, 2019 badala ya Oktoba 14

Soma zaidi - https://jamii.app/UandikishajiV2
KISWAHILI CHAZIDI KUSAMBAA DUNIANI

- Klabu ya soka ya Italia ya AS Roma ipo kwenye mkakati wa kutumia Kiswahili katika moja ya kurasa zake za Mitandao ya Kijamii

- Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, imesema siku chache zijazo itafungua ukurasa wake rasmi wa Kiswahili
MWANARIADHA MWINGINE WA KENYA AVUNJA REKODI YA DUNIA

- Brigid Kosgei (25) avunja rekodi ya muda wa kukimbia marathon kwa Wanawake akiwa kwenye Marathon ya Chicago

- Ameweka rekodi ya kumaliza mbio kwa 2:14: 04 akivunja rekodi iliyokuwepo kwa dakika moja na Sekunde 21

Zaidi, soma https://jamii.app/KosgeiAwekaRekodi
SERIKALI KUZIPATIA RUZUKU KAYA ZOTE MASIKINI NCHINI

- Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imeahidi hayo baada ya kuridhishwa na Wananchi katika vijiji vilivyonufaika, walivyoboresha maisha yao na kujikwamua katika umasikini

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliRuzukuMasikini
MIAKA 20 YA KUMBUKIZI YA KIFO CHA BABA WA TAIFA

- Leo Oktoba 14, 2019 ni Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki katika Hospitali ya Mt. Thomas Jijini London, Uingereza

- Mwalimu Nyerere alizaliwa Butiama, Mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprill 1922, alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na ndiye mwasisi wa Itikadi ya ‘Ujamaa na Kujitegemea’
BAADA YA KUSTAAFU SOKA, PETR CECH AGEUKIA ICE HOCKEY

- Aliyewahi kuwa golikipa wa Chelsea na Arsenal, Petr Cech (37) ameanza kucheza mchezo wa Ice Hockey ambapo jana ameokoa penati 2 na kusaidia timu yake kushinda

- Wiki iliyopita aliingia mkataba na timu ya Guildford Phoenix inayocheza Ligi ya Kitaifa ya South 2, nchini England
BOEING YA PILI YA TANZANIA YAFANYIWA MAJARIBIO

- Boeing 787-8 Dreamliner imefanyiwa majaribio Jumamosi Oktoba 12, 2019 huko Marekani

- Hata hivyo, siku ya kupokea ndege hiyo iliyoandikwa ‘Rubondo Island - Hapa Kazi Tu’ haijawekwa wazi

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeRubondoMajaribioTZ
TISHIO LA UGAIDI KENYA: USALAMA WAIMARISHWA KAUNTI YA MANDERA

> Polisi katika Kaunti ya Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya wapo ktk tahadhari, baada ya kuripotiwa kuonekana kwa washukiwa 20 wa kundi la kigaidi la Al Shabaab

> Magaidi hao walionekana katika maeneo ya Bale-Ilman Mala na Kutulo siku ya Ijumaa

Soma - https://jamii.app/AlShabaabGangSpotted
FAO YATOA TAHADHARI YA MAGONJWA SUGU KUTOKANA NA MILO MIBOVU

> Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), limeitahadharisha Tanzania kuwepo kwa ongezeko la idadi ya watu walio katika hatari ya kupata Shinikizo la Damu, Kisukari, Magonjwa ya Moyo, Kiharusi na Saratani kutokana na milo mibovu, aina ya maisha ya kutofanyisha miili kazi na unene uliopitiliza

Soma - https://jamii.app/MagonjwaUlajiMbovu
KIMBUNGA HAGIBIS JAPAN: VIFO VYAFIKIA TAKRIBAN WATU 30

> Zaidi ya waokoaji 110,000 wamepewa kazi ya kuwatafuta na kuwaokoa watu walioathiriwa na kimbunga hicho kilichotokea Jumamosi

> Takriban watu 16 hawajulikani walipo na nyumba zaidi ya laki tano hazina umeme

Soma - https://jamii.app/DeathTollHagibisTyphoon
MDAU: BOYFRIEND WANGU MCHAFU SANA, KANISHINDA

- Mdau anasema “Mimi sio mtu msafi sana ila Mwanaume huyu amenishinda. Ni mtu mzuri na nimekuwa naye kwa miezi 8 sasa, mwanzo sikuwa nimemuelewa ila huyu Mwanaume ni mchafu sana.”

- Anaendelea “Chumba chake ni kichafu. Huna nasafisha, nisiposafisha hakutaniki. Akioga usiku kabla ya kulala asubuhi haogi, analala na Mwanamke asubuhi anaenda kazini hivyo hivyo. Nikisema anasema nampanda kichwani.”

Kushiriki mjadala, tembelea https://jamii.app/BoyfriendMchafuSana
UGANDA: ASKARI AKAMATWA KWA KUMUUA MTUHUMIWA KWA RISASI

> Askari Polisi ktk Wilaya a Sironko amekamatwa kwa kumpiga risasi Mathew Wodeya (23) akiwa nyumbani kwake baada ya kudaiwa alijaribu kukataa kukamatwa

> Wodeya alikuwa akituhumiwa kwa kosa la kunajisi ambapo alipigwa risasi tumboni, shingoni na kifuani

Soma - https://jamii.app/PoliceShotDeadSuspect
ZINGATIA MUONGOZO HUU KATIKA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

> Zingatia usafi wa vyombo na mazingira ya kuku kwani uchafu ni mama wa magonjwa. Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni

> Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe bandani na kufukiwa

> Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa na Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja

> Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na hakikisha unaziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia bandani

Kujua zaidi, soma - https://jamii.app/UfugajiKukuKienyeji
MAASKOFU WA KATOLIKI KURATIBU MPANGO WA KUMTANGAZA MWL. NYERERE MTAKATIFU

- Mpango huo ulioanzishwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Musoma Mkoani Mara umehamishiwa Jimbo Kuu la Dar chini ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC)

Zaidi, soma https://jamii.app/NyerereMtakatifu-TEC
RAIS MAGUFULI: TUMEMUENZI NYERERE KWA KUFUFUA MASHIRIKA YA UMMA NA KUSIMAMIA NIDHAMU

> Amesema Serikali imefanya mambo mengi katika kumuenzi Baba wa Taifa ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu Serikalini, kuyafufua Mashirika ya Umma, kurejesha nidhamu katika Utumishi wa Umma na kulinda Rasilimali za Taifa

> Amesema jitihada zote zimelenga katika kuziishi fikra za Baba wa Taifa ambaye alilijenga Taifa katika misingi ya Ujamaa na Kujitegemea

Soma - https://jamii.app/MagufuliKumuenziNyerere