JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UINGEREZA: WAZAZI WAANDAMANA KUPINGA MASOMO YA ‘USHOGA’

- Wazazi hao wanapinga mafunzo ya Mapenzi ya Jinsia Moja katika Shule za Msingi

- Programu ya 'No Outsiders Equality' inahamasisha watoto kutambua utofauti kuhusu Dini, Familia na Mahusiano

Zaidi, soma https://jamii.app/WazaziMasomoUshoga-UK
UGANDA: MWANAUME AJIUA BAADA YA KUWATUPA WATOTO WAKE 2 ZIWANI NA KUMCHOMA MOTO 1

- Hannington Nuwamanya(32) amewatupa watoto wake 2 ndani ya Ziwa Magogo kisha kuchoma nyumba yake moto ikiwa na Mtoto mwingine

- Chanzo ni ugomvi na Mkewe

Soma > https://jamii.app/MwanaumeAtupaWatoto
TAKWIMU: DAR KINARA KWA WAGONJWA WA UGONJWA WA AKILI

- Mikoa inayofuata kuwa na Wagonjwa wengi ni Kilimanjaro, Tanga, Morogoro na Mwanza

- Hizi ni takwimu za hospitali za Mikoa na vituo vya Afya bila kujumuisha hospitali kubwa kama Muhimbili na Mirembe

Zaidi, soma https://jamii.app/TakwimuUgonjwaAkili-TZ
MSIMAMIZI WA MALI ZA MKE WA ALIYEKUWA GAVANA WA BOT, DAUDI BALALI ASHTAKIWA KWA KUTAKATISHA FEDHA

- Mfanyabiashara Elizabeth Balali(54), amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kujipatia kiasi cha shilingi milioni 25 kwa njia ya udanganyifu

Soma > https://jamii.app/MsimamiziMaliBalali
VIJUE VIASHIRIA MUHIMU VYA SARATANI YA MATITI

- Ugonjwa huu huwatokea zaidi Wanawake japokuwa unaweza kutokea kwa Wanaume

- Baadhi ya viashiria ni Uvimbe kwenye titi, Badiliko la Umbo au Muundo wa titi na Kutokwa na vipele vidogo

Zaidi, tembelea https://jamii.app/ViashiriaSarataniMatiti
GEITA: ATOZWA LAKI 3 KWA KUFYEKA MAHINDI KISA WIVU WA MAPENZI

- Mkazi wa Nyamigana, Ramadhani Bushemeli ametozwa faini ya Tsh. 300,000 na Serikali ya kijiji kwa kufyeka shamba la Dotto Magilima akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe

Zaidi, soma https://jamii.app/AfyekaMahindiWivuMapenzi
MEXICO: MEYA ABURUZWA NYUMA YA GARI KWA KUTOTIMIZA AHADI ZA UCHAGUZI

- Watu 11 wamekamatwa kwa kosa la kumkamata Meya wa Las Margaritas katika Jimbo la Chiapas, Jorge Luis Escandón Hernández kisha kumfunga katika gari na kumburuza mitaani

Zaidi, soma https://jamii.app/MeyaAburuzwaGari-Mexico
KIKWETE ASIKITISHWA KWA NAMNA HOTUBA YAKE ILIVYOTAFSIRIWA

- Ni hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere

- Imeelezwa hakufanya ulinganifu kati ya Mwalimu na Marais na hakutaja jina la mtu

Zaidi, soma https://jamii.app/KikweteAsikitishwaHotuba
MAJESHI YA UTURUKI: MAGAIDI 277 WAUAWA KATIKA OPERESHENI YA SYRIA

- Maelfu ya Watu wamekimbia makazi yao huko Kaskazini Mashariki mwa Syria huku Vikosi vya Kijeshi vya Uturuki vikiendelea na Operesheni yake iliyoanza Jumatano Oktoba 09 inayodaiwa ni ya kuweka mazingira salama kwa Wakimbizi wa Syria kurejea

Zaidi, soma https://jamii.app/UturukiYauaMagaidi277
KENYA: NDEGE YAANGUKA WAKATI IKIJARIBU KUPAA

- Ripoti inaonesha ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Lamu iliteleza kutoka kwenye njia ya kurukia katika Uwanja wa Wilson

- Abiria na Wafanyakazi kwenye ndege wametolewa, baadhi wakiwa na majeraha

Zaidi, soma https://jamii.app/AirplaneCrashesWilsonAirport
BAADA YA VIDEO NA PICHA ZA UTUPU ZA MENINA KUSAMBAA, BASATA YAMUITA

- Msanii Menina Abdulkareem ameitwa kwa mahojiano kuhusu video na picha zake za utupu zilizosambaa

- BASATA imemtaka msanii huyo kufika katika Ofisi zake leo mchana

Zaidi, soma https://jamii.app/MeninaAitwaBASATA
MAHAKAMA YATENGUA HUKUMU YA JOSEPH MBILINYI

- Mahakama Kuu leo imetengua Hukumu, Mwenendo na Kifungo alichohukumiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ kutokana na ubatili wa mwenendo katika kesi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/HukumuSuguYatenguliwa
TETESI: MATOKEO MABOVU YA MAN. UNITED YAMKIMBIZA MDHAMINI

- Inadaiwa Manchester United inatafuta Mdhamini mpya wa jezi zake baada ya kuonekana kuna uwezekano mkubwa Mdhamini wa sasa, Chevrolet kutosaini tena mkataba mpya kutokana na United kupata matokeo yasiyoridhisha
KABENDERA ATAKA KUJADILIANA NA DPP KUMALIZA KESI YAKE

- Erick Kabendera anataka kujadiliana na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) namna ya kumaliza kesi yake

- Anakabiliwa na kesi yenye mashtaka 3 likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Tsh. Milioni 173

Zaidi, soma https://jamii.app/KabenderaKuongeaDPP
WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ASHINDA TUZO YA AMANI YA NOBEL

> Abiy Ahmed, ametunukiwa tuzo hiyo kwa mwaka 2019 kutokana na juhudi zake za kuleta Amani na kusuluhisha Mgogoro wa mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea uliodumu kwa miaka 20

Zaidi, soma > https://jamii.app/AbiyNobel2019
UGANDA YAANDAA SHERIA YA KUNYONGA WAPENZI WA JINSIA MOJA

- Imetangaza mpango wa kuanzisha tena sheria inayopinga mahusiano ya jinsia moja, iliyofutwa mwaka 2014

- Wanaoshiriki watahukumiwa kunyongwa na wanaopigia debe wanaweza kushtakiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/SheriaKunyongaWapenziJinsia1-UG
TPA YAKANUSHA VIDEO INAYOSAMBAA IKIWATUHUMU WATUMISHI WAKE KWA WIZI

> Mamlaka ya Bandari(TPA) yasema taarifa inayosambazwa kuhusiana na wizi bandarini ni ya kupuuza

> TPA: video hiyo imelenga kuchafua taswira nzuri ya Bandari za Tanzania

Soma > https://jamii.app/WiziBandari
SIKU 13: HATIMAYE MIILI YA MARIAM NA MWANAYE YAOPOLEWA

- Gari lililo na miili ya Mariam Kighendi(35) na Mwanaye Amanda Mutheu(4) limeopolewa katika Feri ya Likoni, Mombasa

- Limeopolewa huku ndugu na Mume wa marehemu, John Wambua wakishuhudia

Zaidi, soma https://jamii.app/BodiesMariamDaughterRetrieved
DODOMA: MFANYAKAZI WA EXIM MBARONI KWA KUIIBIA BENKI HIYO TSH. MILIONI 120

- Mtunza Fedha, Martin Temu(33) mbaroni kwa madai ya kuiibia benki hiyo Tsh. Milioni 120 na USD 9,513

- Kati ya fedha alizoiba alikamatwa akiwa na Tsh. Milioni 37.5

Zaidi, soma https://jamii.app/MfanyakaziEximMbaroniWizi