JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SENEGAL: NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINES YALAZIMIKA KUTUA KWA DHARURA BAADA YA INJINI KUSHIKA MOTO

> Ndege aina ya Boeing 767 iliyokuwa ikianza safari kutoka Dakar kuelekea Addis Ababa, Ethiopia ilikuwa imebeba abiria 90 ambao wote wamesalimika

Soma > https://jamii.app/NdegeEthiopiaDakar
RWANDA: MHUBIRI AFUKUZWA BAADA YA KUWAITA WANAWAKE 'IBILISI NA MALAYA'

- Mhubiri na mmiliki wa kituo cha redio cha Amazing Grace, raia wa Marekani Gregg Schoof aliyekamatwa mapema wiki hii jijini Kigali, amefukuzwa nchini humo

Zaidi, soma https://jamii.app/MhubiriAfukuzwaRwanda
UGANDA: BOBI WINE AFANIKIWA KUTOROKA POLISI KWA KUTUMIA BODABODA

- Amefanikiwa kutoroka ulinzi mkali wa Polisi uliokuwa ukizingira nyumba yake huko Magere

- Inadaiwa anaelekea kwenye Tamasha lake la Muziki alilozuiwa kulifanya huko Busabala

Zaidi, soma https://jamii.app/BobiWineEscapeBodaboda
GEITA: WAFUNGA MADUKA KUSHINIKIZA MWENZAO KUTOA KRETI YA SODA

- Wafanyabiashara Kijiji cha Nyamigana, Kata ya Kagu, Wilayani Geita wamefunga maduka yao baada ya mfanyabiashara mgeni kijijini hapo kugoma kutoa kreti moja ya soda kama kiingilio

Zaidi, soma https://jamii.app/WafungaMadukaKreti-GIT
UTURUKI YAANZA MASHAMBULIZI KASKAZINI MASHARIKI MWA SYRIA

- Ndege za Kivita za Uturuki zimeshambulia baadhi ya sehemu za Kaskazini mwa Syria hatua inayotarajiwa kuleta mgogoro dhidi ya Wanamgambo wa Kikurdi wenye ushirikiano na Marekani

Zaidi, soma https://jamii.app/UturukiVsSyria
INDIA: OMBAOMBA AFARIKI, AACHA SARAFU ZILIZOHESABIWA KWA SAA 8

> Polisi wametumia muda huo kuhesabu sarafu hizo zilizoachwa na ombaomba aliyefariki akiwa na umri wa miaka 82

> Mzee huyo amefariki katika ajali ya treni iliyotokea huko Vashi

Zaidi, soma https://jamii.app/SarafuMumbai
MICHEZO: Klabu ya Yanga itakutana na klabu ya Pyramids ya Misri katika hatua ya kuwania nafasi ya kuingia kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

- Yanga itaanzia nyumbani Oktoba 27, 2019 na klabu hizo zitacheza mchezo wa marudiano Novemba 3, 2019 nchini Misri
LISSU: SIRUDI TANZANIA HADI NIHAKIKISHIWE USALAMA

> Amesema hawezi kurudi tena Tanzania kwa sasa kwani wasiojulikana bado hawajapatikana

> Azungumzia kutishwa mitandaoni bila hatua yoyote kuchukuliwa

Soma https://jamii.app/HatmaLissuKurudi
ATHARI ZA MVUA UKANDA WA PWANI: WATU 6 WAFARIKI DUNIA MKOANI TANGA, KAYA 300 ZAKOSA MAKAZI

- Waliofariki ni Mwanamke 1 na Watoto wake 2 pamoja na binti Asha Ambanyonge aliyekuwa amelala na wadogo zake 2 walioangukiwa na nyumba

Soma > https://jamii.app/MvuaTanga
KENYA: KURA ZAMUONDOA MADARAKANI GAVANA WA TAITA TAVETA

- Granton Samboja ameondolewa kwa kura zilizopigwa katika Baraza la Viongozi wa Kata baada ya Kiongozi wa Kata ya Rong’e, Harris Keke kuweka mezani hoja hiyo na kupata kura 30 kati ya 33

Soma https://jamii.app/GrantonSambojaImpeached
HARBINDER SETHI AANDIKA BARUA KWA DPP KUKIRI MAKOSA

- Sethi anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ameandikia barua ya kuomba msamaha

- Sethi na James Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka 12 wanayodaiwa kuyatenda sehemu mbalimbali

Zaidi, soma https://jamii.app/SethiAandikaBaruaKukiriMakosa
UINGEREZA: WAZAZI WAANDAMANA KUPINGA MASOMO YA ‘USHOGA’

- Wazazi hao wanapinga mafunzo ya Mapenzi ya Jinsia Moja katika Shule za Msingi

- Programu ya 'No Outsiders Equality' inahamasisha watoto kutambua utofauti kuhusu Dini, Familia na Mahusiano

Zaidi, soma https://jamii.app/WazaziMasomoUshoga-UK
UGANDA: MWANAUME AJIUA BAADA YA KUWATUPA WATOTO WAKE 2 ZIWANI NA KUMCHOMA MOTO 1

- Hannington Nuwamanya(32) amewatupa watoto wake 2 ndani ya Ziwa Magogo kisha kuchoma nyumba yake moto ikiwa na Mtoto mwingine

- Chanzo ni ugomvi na Mkewe

Soma > https://jamii.app/MwanaumeAtupaWatoto
TAKWIMU: DAR KINARA KWA WAGONJWA WA UGONJWA WA AKILI

- Mikoa inayofuata kuwa na Wagonjwa wengi ni Kilimanjaro, Tanga, Morogoro na Mwanza

- Hizi ni takwimu za hospitali za Mikoa na vituo vya Afya bila kujumuisha hospitali kubwa kama Muhimbili na Mirembe

Zaidi, soma https://jamii.app/TakwimuUgonjwaAkili-TZ
MSIMAMIZI WA MALI ZA MKE WA ALIYEKUWA GAVANA WA BOT, DAUDI BALALI ASHTAKIWA KWA KUTAKATISHA FEDHA

- Mfanyabiashara Elizabeth Balali(54), amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kujipatia kiasi cha shilingi milioni 25 kwa njia ya udanganyifu

Soma > https://jamii.app/MsimamiziMaliBalali
VIJUE VIASHIRIA MUHIMU VYA SARATANI YA MATITI

- Ugonjwa huu huwatokea zaidi Wanawake japokuwa unaweza kutokea kwa Wanaume

- Baadhi ya viashiria ni Uvimbe kwenye titi, Badiliko la Umbo au Muundo wa titi na Kutokwa na vipele vidogo

Zaidi, tembelea https://jamii.app/ViashiriaSarataniMatiti
GEITA: ATOZWA LAKI 3 KWA KUFYEKA MAHINDI KISA WIVU WA MAPENZI

- Mkazi wa Nyamigana, Ramadhani Bushemeli ametozwa faini ya Tsh. 300,000 na Serikali ya kijiji kwa kufyeka shamba la Dotto Magilima akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe

Zaidi, soma https://jamii.app/AfyekaMahindiWivuMapenzi
MEXICO: MEYA ABURUZWA NYUMA YA GARI KWA KUTOTIMIZA AHADI ZA UCHAGUZI

- Watu 11 wamekamatwa kwa kosa la kumkamata Meya wa Las Margaritas katika Jimbo la Chiapas, Jorge Luis Escandón Hernández kisha kumfunga katika gari na kumburuza mitaani

Zaidi, soma https://jamii.app/MeyaAburuzwaGari-Mexico
KIKWETE ASIKITISHWA KWA NAMNA HOTUBA YAKE ILIVYOTAFSIRIWA

- Ni hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere

- Imeelezwa hakufanya ulinganifu kati ya Mwalimu na Marais na hakutaja jina la mtu

Zaidi, soma https://jamii.app/KikweteAsikitishwaHotuba