JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFRIKA KUSINI: MTOTO WA JACOB ZUMA AKANA KUTAKA KUTOA RUSHWA YA ZAIDI YA TSH. BILIONI 92

> Duduzane Zuma(35) akiwa mbele ya Mahakama amezikana tuhuma kuwa alitaka kumpa rushwa hiyo aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mcebisi Jonas

Zaidi, soma > https://jamii.app/DuduzaneRushwa
MAREKANI YAZUIA MASHIRIKA YA CHINA KUNUNUA BIDHAA MAREKANI

- Imepiga marufuku mashirika 28 kununua bidhaa kutoka kwa Kampuni za Marekani bila idhini ya Ikulu kwa madai yanahusika katika unyanyasi wa kabila la Uighurs katika jimbo la Xinjianga

Zaidi, soma https://jamii.app/MashirikaChinaMarufukuUSA
KENYA: ASHTAKIWA KWA KUDAIWA KUSAMBAZA PICHA NA VIDEO ZA UTUPU ZA MPENZI WAKE WA ZAMANI

- Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu siku ya Jumatatu, mtuhumiwa ambaye ni Omar Seif amekana mashtaka hayo na kwa sasa yupo nje kwa dhamana

Soma > https://jamii.app/ChargedForSharingExNudes
RUKWA: MRATIBU WA TARURA ASIMAMISHWA KAZI KWA KUTOA ZABUNI KWA UPENDELEO

> Waziri Selemani Jafo ameagiza kusimamishwa kazi kwa wiki 2, Bonifas William ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma za kutoa zabuni ya matengenezo ya barabara kwa upendeleo

Zaidi, soma - https://jamii.app/MratibuAsimamishaZabuni
KIKWETE: KUJISHUSHA HAKUONDOI CHEO ULICHONACHO

- Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amewataka viongozi nchini kuacha kujikweza na kuishi kama binadamu wa kawaida

- Aidha, ameasa kuwa Mawazo hayapigwi rungu, bali yanashindwa na mawazo yaliyo bora zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/KikweteUongoziBora-KmbkmbNyerere
RUKWA: RAIS MAGUFULI AAGIZA MAMA ALIYEIBIWA NG’OMBE 25 KULIPWA TSH. MILIONI 15

- Ameagiza Polisi wakiongozwa na RPC na DC wa Nkasi, kumlipa Felista Mkombo fedha hizo kama fidia kutokana na Polisi kumwachia aliyedaiwa kuiba ambaye baadaye alitoroka

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKumlipaMfugaji-RKW
MFUMUKO WA BEI NCHINI WAPUNGUA HADI ASILIMIA 3.4

- Ofisi ya Takwimu imebainisha kuwa Mfumuko wa bei kwa mwezi Septemba, 2019 umepungua kutoka asilimia 3.6 kwa mwezi Agosti, 2019

- Ni kutokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula

Zaidi, soma https://jamii.app/MfumukoBei-Sep2019
KENYA: CHUO KIKUU KENYATTA CHAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA

- Ni baada ya Wanafunzi kuandamana na kuharibu baadhi ya mali za Chuo

- Walikuwa wakipinga masuala mbalimbali yakiwemo muda mdogo wa kulipa ada na wafanyakazi kufukuzwa bila taarifa

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamanoChuoKenyattaChafungwa
👍1
KATAVI: AVUNJA MADIRISHA YA KITUO CHA AFYA AKIDAI KUTOKULIPWA

- Mjenzi Boniface Exavery aliyejenga madirisha katika Kituo cha Afya cha Katumba, Halmashauri ya Nsimbo, ameyavunja madirisha hayo akidai kutokamilishiwa malipo yake na Halmashauri huku akiwa amemaliza kazi

Zaidi, soma https://jamii.app/AvunjaMadirishaKutolipwa
BANGLADESH: MWANAUME AMNYOA NYWELE MKEWE BAADA YA KUKUTA NYWELE KWENYE CHAKULA

> Bablu Mondal (35) amechukua uamuzi huo baada ya kukuta nywele kwenye Wali na Waziwa aliyoandaliwa na Mkewe

> Polisi wamkamata kwa kukiuka #HakiZaBinadamu

Soma > https://jamii.app/BabluBangladesh
UTURUKI: MAANDALIZI YA MASHAMBULIZI KASKAZINI MWA SYRIA YAMEKAMILIKA

- Ni siku chache baada ya Marekani kuamuru Majeshi yake yaliyokuwa Syria mpakani mwa Uturuki yaondoke

- Imesema mashambulizi hayo ya Kijeshi yanaweza kufanyika wakati wowote

Zaidi, soma https://jamii.app/UturukiVsSyria
SENEGAL: NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINES YALAZIMIKA KUTUA KWA DHARURA BAADA YA INJINI KUSHIKA MOTO

> Ndege aina ya Boeing 767 iliyokuwa ikianza safari kutoka Dakar kuelekea Addis Ababa, Ethiopia ilikuwa imebeba abiria 90 ambao wote wamesalimika

Soma > https://jamii.app/NdegeEthiopiaDakar
RWANDA: MHUBIRI AFUKUZWA BAADA YA KUWAITA WANAWAKE 'IBILISI NA MALAYA'

- Mhubiri na mmiliki wa kituo cha redio cha Amazing Grace, raia wa Marekani Gregg Schoof aliyekamatwa mapema wiki hii jijini Kigali, amefukuzwa nchini humo

Zaidi, soma https://jamii.app/MhubiriAfukuzwaRwanda
UGANDA: BOBI WINE AFANIKIWA KUTOROKA POLISI KWA KUTUMIA BODABODA

- Amefanikiwa kutoroka ulinzi mkali wa Polisi uliokuwa ukizingira nyumba yake huko Magere

- Inadaiwa anaelekea kwenye Tamasha lake la Muziki alilozuiwa kulifanya huko Busabala

Zaidi, soma https://jamii.app/BobiWineEscapeBodaboda
GEITA: WAFUNGA MADUKA KUSHINIKIZA MWENZAO KUTOA KRETI YA SODA

- Wafanyabiashara Kijiji cha Nyamigana, Kata ya Kagu, Wilayani Geita wamefunga maduka yao baada ya mfanyabiashara mgeni kijijini hapo kugoma kutoa kreti moja ya soda kama kiingilio

Zaidi, soma https://jamii.app/WafungaMadukaKreti-GIT
UTURUKI YAANZA MASHAMBULIZI KASKAZINI MASHARIKI MWA SYRIA

- Ndege za Kivita za Uturuki zimeshambulia baadhi ya sehemu za Kaskazini mwa Syria hatua inayotarajiwa kuleta mgogoro dhidi ya Wanamgambo wa Kikurdi wenye ushirikiano na Marekani

Zaidi, soma https://jamii.app/UturukiVsSyria
INDIA: OMBAOMBA AFARIKI, AACHA SARAFU ZILIZOHESABIWA KWA SAA 8

> Polisi wametumia muda huo kuhesabu sarafu hizo zilizoachwa na ombaomba aliyefariki akiwa na umri wa miaka 82

> Mzee huyo amefariki katika ajali ya treni iliyotokea huko Vashi

Zaidi, soma https://jamii.app/SarafuMumbai
MICHEZO: Klabu ya Yanga itakutana na klabu ya Pyramids ya Misri katika hatua ya kuwania nafasi ya kuingia kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

- Yanga itaanzia nyumbani Oktoba 27, 2019 na klabu hizo zitacheza mchezo wa marudiano Novemba 3, 2019 nchini Misri
LISSU: SIRUDI TANZANIA HADI NIHAKIKISHIWE USALAMA

> Amesema hawezi kurudi tena Tanzania kwa sasa kwani wasiojulikana bado hawajapatikana

> Azungumzia kutishwa mitandaoni bila hatua yoyote kuchukuliwa

Soma https://jamii.app/HatmaLissuKurudi
ATHARI ZA MVUA UKANDA WA PWANI: WATU 6 WAFARIKI DUNIA MKOANI TANGA, KAYA 300 ZAKOSA MAKAZI

- Waliofariki ni Mwanamke 1 na Watoto wake 2 pamoja na binti Asha Ambanyonge aliyekuwa amelala na wadogo zake 2 walioangukiwa na nyumba

Soma > https://jamii.app/MvuaTanga