JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SINGIDA: WAZIRI MKUU AAGIZA WALIOAJIRIWA KINDUGU WAFUKUZWE

- Amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile awaondoe Watumishi watatu wanaokusanya mapato kwenye stendi ya mabasi, walioajiriwa kindugu na wanaodaiwa kuiba mapato

Zaidi, soma https://jamii.app/WalioajiriwaKinduguWaondoke-SND
MAREKANI YAONDOA WANAJESHI WAKE SYRIA KATIKA MPAKA NA UTURUKI

- Rais Trump amesema ni gharama kuendelea kuunga mkono vikosi vya Kijeshi katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Syria katika kukabiliana na kundi linalojiita Dola Ya Kiislamu

Zaidi, soma https://jamii.app/WanajeshiUSAWaondokaSyria
BENKI YA DUNIA YAIPATIA TANZANIA MKOPO WA TRILIONI 1.035

- Imeipatia mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani Milioni 450 (Tsh. Trilioni 1.035) ili kutekeleza kipindi cha pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini cha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), awamu ya 3

Zaidi, soma https://jamii.app/MkopoWB-TZ-TASAF
SIKU 9: UOPOAJI WA MIILI YA MAMA NA MWANAYE KATIKA FERI YA LIKONI UNAENDELEA

- Wazamiaji kutoka Serikalini, Sekta binafsi na Afrika Kusini wanashirikiana kutafuta miili ya Mariam Kighenda(35) na mwanaye(4) waliozama katika feri hiyo nchini Kenya

Zaidi, soma https://jamii.app/Siku9LikoniUpoajiBado
UGANDA: BABA AKAMATWA KWA KUMUUA MTOTO WAKE, AKIMTUHUMU KWA KULA CHAKULA CHAKE

- Isma Ssesanga anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Mtoto wake wa kike aliyekula chakula chake alichochukua kwenye sherehe moja aliyohudhuria

Zaidi, soma => https://jamii.app/FatherKillsDaughter
AFRIKA KUSINI: MTOTO WA JACOB ZUMA AKANA KUTAKA KUTOA RUSHWA YA ZAIDI YA TSH. BILIONI 92

> Duduzane Zuma(35) akiwa mbele ya Mahakama amezikana tuhuma kuwa alitaka kumpa rushwa hiyo aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mcebisi Jonas

Zaidi, soma > https://jamii.app/DuduzaneRushwa
MAREKANI YAZUIA MASHIRIKA YA CHINA KUNUNUA BIDHAA MAREKANI

- Imepiga marufuku mashirika 28 kununua bidhaa kutoka kwa Kampuni za Marekani bila idhini ya Ikulu kwa madai yanahusika katika unyanyasi wa kabila la Uighurs katika jimbo la Xinjianga

Zaidi, soma https://jamii.app/MashirikaChinaMarufukuUSA
KENYA: ASHTAKIWA KWA KUDAIWA KUSAMBAZA PICHA NA VIDEO ZA UTUPU ZA MPENZI WAKE WA ZAMANI

- Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu siku ya Jumatatu, mtuhumiwa ambaye ni Omar Seif amekana mashtaka hayo na kwa sasa yupo nje kwa dhamana

Soma > https://jamii.app/ChargedForSharingExNudes
RUKWA: MRATIBU WA TARURA ASIMAMISHWA KAZI KWA KUTOA ZABUNI KWA UPENDELEO

> Waziri Selemani Jafo ameagiza kusimamishwa kazi kwa wiki 2, Bonifas William ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma za kutoa zabuni ya matengenezo ya barabara kwa upendeleo

Zaidi, soma - https://jamii.app/MratibuAsimamishaZabuni
KIKWETE: KUJISHUSHA HAKUONDOI CHEO ULICHONACHO

- Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amewataka viongozi nchini kuacha kujikweza na kuishi kama binadamu wa kawaida

- Aidha, ameasa kuwa Mawazo hayapigwi rungu, bali yanashindwa na mawazo yaliyo bora zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/KikweteUongoziBora-KmbkmbNyerere
RUKWA: RAIS MAGUFULI AAGIZA MAMA ALIYEIBIWA NG’OMBE 25 KULIPWA TSH. MILIONI 15

- Ameagiza Polisi wakiongozwa na RPC na DC wa Nkasi, kumlipa Felista Mkombo fedha hizo kama fidia kutokana na Polisi kumwachia aliyedaiwa kuiba ambaye baadaye alitoroka

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKumlipaMfugaji-RKW
MFUMUKO WA BEI NCHINI WAPUNGUA HADI ASILIMIA 3.4

- Ofisi ya Takwimu imebainisha kuwa Mfumuko wa bei kwa mwezi Septemba, 2019 umepungua kutoka asilimia 3.6 kwa mwezi Agosti, 2019

- Ni kutokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula

Zaidi, soma https://jamii.app/MfumukoBei-Sep2019
KENYA: CHUO KIKUU KENYATTA CHAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA

- Ni baada ya Wanafunzi kuandamana na kuharibu baadhi ya mali za Chuo

- Walikuwa wakipinga masuala mbalimbali yakiwemo muda mdogo wa kulipa ada na wafanyakazi kufukuzwa bila taarifa

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamanoChuoKenyattaChafungwa
👍1
KATAVI: AVUNJA MADIRISHA YA KITUO CHA AFYA AKIDAI KUTOKULIPWA

- Mjenzi Boniface Exavery aliyejenga madirisha katika Kituo cha Afya cha Katumba, Halmashauri ya Nsimbo, ameyavunja madirisha hayo akidai kutokamilishiwa malipo yake na Halmashauri huku akiwa amemaliza kazi

Zaidi, soma https://jamii.app/AvunjaMadirishaKutolipwa
BANGLADESH: MWANAUME AMNYOA NYWELE MKEWE BAADA YA KUKUTA NYWELE KWENYE CHAKULA

> Bablu Mondal (35) amechukua uamuzi huo baada ya kukuta nywele kwenye Wali na Waziwa aliyoandaliwa na Mkewe

> Polisi wamkamata kwa kukiuka #HakiZaBinadamu

Soma > https://jamii.app/BabluBangladesh
UTURUKI: MAANDALIZI YA MASHAMBULIZI KASKAZINI MWA SYRIA YAMEKAMILIKA

- Ni siku chache baada ya Marekani kuamuru Majeshi yake yaliyokuwa Syria mpakani mwa Uturuki yaondoke

- Imesema mashambulizi hayo ya Kijeshi yanaweza kufanyika wakati wowote

Zaidi, soma https://jamii.app/UturukiVsSyria
SENEGAL: NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINES YALAZIMIKA KUTUA KWA DHARURA BAADA YA INJINI KUSHIKA MOTO

> Ndege aina ya Boeing 767 iliyokuwa ikianza safari kutoka Dakar kuelekea Addis Ababa, Ethiopia ilikuwa imebeba abiria 90 ambao wote wamesalimika

Soma > https://jamii.app/NdegeEthiopiaDakar
RWANDA: MHUBIRI AFUKUZWA BAADA YA KUWAITA WANAWAKE 'IBILISI NA MALAYA'

- Mhubiri na mmiliki wa kituo cha redio cha Amazing Grace, raia wa Marekani Gregg Schoof aliyekamatwa mapema wiki hii jijini Kigali, amefukuzwa nchini humo

Zaidi, soma https://jamii.app/MhubiriAfukuzwaRwanda
UGANDA: BOBI WINE AFANIKIWA KUTOROKA POLISI KWA KUTUMIA BODABODA

- Amefanikiwa kutoroka ulinzi mkali wa Polisi uliokuwa ukizingira nyumba yake huko Magere

- Inadaiwa anaelekea kwenye Tamasha lake la Muziki alilozuiwa kulifanya huko Busabala

Zaidi, soma https://jamii.app/BobiWineEscapeBodaboda
GEITA: WAFUNGA MADUKA KUSHINIKIZA MWENZAO KUTOA KRETI YA SODA

- Wafanyabiashara Kijiji cha Nyamigana, Kata ya Kagu, Wilayani Geita wamefunga maduka yao baada ya mfanyabiashara mgeni kijijini hapo kugoma kutoa kreti moja ya soda kama kiingilio

Zaidi, soma https://jamii.app/WafungaMadukaKreti-GIT