JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ENGLAND: MAN. CITY YACHEZEA KICHAPO IKIWA NYUMBANI

- Manchester City ikiwa ‘Etihad Stadium’ imepokea kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu

- Chelsea imepata ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Southampton huku Arsenal ikipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Bournemouth
ENGLAND: MAN. UTD YAPOTEZA MECHI YA TATU KWENYE LIGI KUU

- Klabu ya Manchester United imepokea kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa klabu ya Newcastle United katika uwanja wa St. James’ Park kwenye mchezo wa Ligi Kuu Nchini England

- Kwa matokeo hayo Manchester United inabakia na alama 9 na kushuka hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi huku Newcastle ikapanda hadi nafasi ya 16 ikifikisha alama 8
RAIS MAGUFULI AAGIZA KAIMU RPC WA SUMBAWANGA ASIMAMISHWE KAZI NA KUSHUSHWA CHEO

> Polycarp Urio amesimamishwa kazi hadi Rais atakapotoa maelekezo mengine baada ya kushindwa kutekeleza maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola

Zaidi, soma => https://jamii.app/RaisVsPolisiSumbawanga
KOREA KASKAZINI YAGOMA KUENDELEA KUZUNGUMZA NA MAREKANI

- Haitaki kuzungumza kuhusu nyuklia hadi Marekani itakapochukua hatua za kumaliza mvutano baina yao

- Imesema hayo baada ya kuvunjika kwa mazungumzo yao yaliyosimamiwa na Sweden

Zaidi, soma https://jamii.app/NKoreaMazungumzoUSA
SAUDI ARABIA: WAPENZI RUKSA KULALA CHUMBA KIMOJA HOTELINI

- Raia wa kigeni ambao ni Wapenzi wasio wanandoa wanaweza kulala chumba kimoja hotelini

- Aidha, katika hatua hiyo ya kukuza Utalii, Wanawake wataruhusiwa kulala hotelini peke yao

Zaidi, soma https://jamii.app/WapenziChumba1-Saudia
TANZIA: MSANII NA ALIYEKUWA MKUU WA IDARA YA SANAA CHADEMA AFARIKI

> Fulgence Mapunda almaarufu Mwana Cotide amefariki dunia saa 10:20 usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu

> Alilazwa ktk Hospitali ya St Monica, Manzese Dar

Soma > https://jamii.app/MsaniiCHADEMAAfariki
SHINYANGA: WANAFUNZI 8 MBARONI WAKIDAIWA KUMSHAMBULIA MWENZAO

- Wanafunzi hao wa Sekondari ya Seeke wanatuhumiwa kumjeruhi Costantine Makoye

- Makoye aliyefariki akipatiwa matibabu, alivamia sherehe na wenzake na kunyang’anya Watu vitu

Zaidi, soma https://jamii.app/Wanafunzi8Mbaroni-KHM
AFISA MANUNUZI CHUO CHA KINAMPANDA ATAKIWA KUKAMATWA

- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Francis Muyombo akamatwe kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaManunuziKinampanda
MBEYA: WAWILI WAFARIKI BAADA YA DARAJA KUVUNJIKA KUTOKANA NA MVUA

- Wametumbukia mtoni wakati wakipita katika daraja hilo linalounganisha Kata ya Tembela na Mwakibete

- Watu 2 hawajulikani walipo akiwemo mtoto anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja

Zaidi, soma https://jamii.app/WawiliWafarikiDarajaMwakibete-MBY
MAHAKAMA YAMUACHIA MICHAEL WAMBURA

- Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura

- Imempa masharti ya kutokufanya makosa yoyote kwa miezi 12 na kulipa zaidi ya Tsh. Milioni 100 kwa awamu 5

Zaidi, soma https://jamii.app/MichaelWamburaHuru
MKURUGENZI MSTAAFU WA TISS, APSON MWANG'ONDA AFARIKI DUNIA

- Aliyekuwa Mkurugenzi wa TISS, Apson Mwang’onda (75) amefariki leo, Nchini Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa

- Alistaafu kazi hiyo Agosti 21, mwaka 2006 kwa mujibu wa sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/ApsonTISSAfariki
SINGIDA: WAZIRI MKUU AAGIZA WALIOAJIRIWA KINDUGU WAFUKUZWE

- Amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile awaondoe Watumishi watatu wanaokusanya mapato kwenye stendi ya mabasi, walioajiriwa kindugu na wanaodaiwa kuiba mapato

Zaidi, soma https://jamii.app/WalioajiriwaKinduguWaondoke-SND
MAREKANI YAONDOA WANAJESHI WAKE SYRIA KATIKA MPAKA NA UTURUKI

- Rais Trump amesema ni gharama kuendelea kuunga mkono vikosi vya Kijeshi katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Syria katika kukabiliana na kundi linalojiita Dola Ya Kiislamu

Zaidi, soma https://jamii.app/WanajeshiUSAWaondokaSyria
BENKI YA DUNIA YAIPATIA TANZANIA MKOPO WA TRILIONI 1.035

- Imeipatia mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani Milioni 450 (Tsh. Trilioni 1.035) ili kutekeleza kipindi cha pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini cha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), awamu ya 3

Zaidi, soma https://jamii.app/MkopoWB-TZ-TASAF
SIKU 9: UOPOAJI WA MIILI YA MAMA NA MWANAYE KATIKA FERI YA LIKONI UNAENDELEA

- Wazamiaji kutoka Serikalini, Sekta binafsi na Afrika Kusini wanashirikiana kutafuta miili ya Mariam Kighenda(35) na mwanaye(4) waliozama katika feri hiyo nchini Kenya

Zaidi, soma https://jamii.app/Siku9LikoniUpoajiBado
UGANDA: BABA AKAMATWA KWA KUMUUA MTOTO WAKE, AKIMTUHUMU KWA KULA CHAKULA CHAKE

- Isma Ssesanga anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Mtoto wake wa kike aliyekula chakula chake alichochukua kwenye sherehe moja aliyohudhuria

Zaidi, soma => https://jamii.app/FatherKillsDaughter
AFRIKA KUSINI: MTOTO WA JACOB ZUMA AKANA KUTAKA KUTOA RUSHWA YA ZAIDI YA TSH. BILIONI 92

> Duduzane Zuma(35) akiwa mbele ya Mahakama amezikana tuhuma kuwa alitaka kumpa rushwa hiyo aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mcebisi Jonas

Zaidi, soma > https://jamii.app/DuduzaneRushwa
MAREKANI YAZUIA MASHIRIKA YA CHINA KUNUNUA BIDHAA MAREKANI

- Imepiga marufuku mashirika 28 kununua bidhaa kutoka kwa Kampuni za Marekani bila idhini ya Ikulu kwa madai yanahusika katika unyanyasi wa kabila la Uighurs katika jimbo la Xinjianga

Zaidi, soma https://jamii.app/MashirikaChinaMarufukuUSA
KENYA: ASHTAKIWA KWA KUDAIWA KUSAMBAZA PICHA NA VIDEO ZA UTUPU ZA MPENZI WAKE WA ZAMANI

- Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu siku ya Jumatatu, mtuhumiwa ambaye ni Omar Seif amekana mashtaka hayo na kwa sasa yupo nje kwa dhamana

Soma > https://jamii.app/ChargedForSharingExNudes
RUKWA: MRATIBU WA TARURA ASIMAMISHWA KAZI KWA KUTOA ZABUNI KWA UPENDELEO

> Waziri Selemani Jafo ameagiza kusimamishwa kazi kwa wiki 2, Bonifas William ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma za kutoa zabuni ya matengenezo ya barabara kwa upendeleo

Zaidi, soma - https://jamii.app/MratibuAsimamishaZabuni