JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UPUNGUFU WA MADINI CHUMA NA ULEVI NI SABABU ZA KUZAA WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO

> Upungufu wa madini ya chuma mwilini, viini lishe, ulevi uliopindukia, ugomvi uliokithiri wakati wa ujauzito, matumizi ya dawa bila maelekezo na kujifungua katika maeneo yasiyo salama zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia watoto kuzaliwa na mtindio wa ubongo

Soma - https://jamii.app/MaadhimishoUtindioUbongo
ENGLAND: LIVERPOOL YAPATA USHINDI WAKE WA 8 MSIMU HUU

- Liverpool imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Nchini England baada ya leo kupata ushidi katika dakika za lala salama dhidi ya Leicester City

- Norwich ikiwa nyumbani imeweza kupata kipigo kizito kutoka kwa Aston Villa baada ya kutandikwa goli 5-1
BUNGE LAIAMURU IKULU YA MAREKANI KUTOA NYARAKA ZOTE ZA MAWASILIANO YA TRUMP

> Kamati za Bunge la Marekani zinazoendesha uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump zimeiamuru Ikulu ya Marekani kuwasilisha nyaraka zote za mawasiliano kati ya Rais Donald Trump na Ukraine

> Amri hiyo imetolewa baada ya Ikulu ya Marekani kushindwa kutoa kwa hiari nyaraka hizo

Soma - https://jamii.app/CommitteesSubpoenaedWhiteHouse
WAZIRI MKUU AAGIZA DED ACHUNGUZWE KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA

> Ameiagiza TAKUKURU Mkoa wa Singida kumchunguze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama, Godfrey Sanga

> Baadhi ya tuhuma alizonazo ni kujilipa posho ya safari Mwezi Machi 2019 bila kusafiri, kuwasainisha watumishi wa chini yake vocha ya zaidi ya Tsh. milioni 1 na kisha kuwapa ‘Asante Kidogo’

Soma - https://jamii.app/DEDUchunguziUbadhilifu
JE, UNAMJUA ROBERT PERSHING MADLOW, MTU MREFU ZAIDI DUNIANI?

- Alizaliwa Februari 22, 1918 akiwa na uzito wa takriban Kilogram 3.94 lakini tofauti na watoto wengine alianza kukua kwa haraka na kuwa na urefu usio wa kawaida

- Alipofikisha mwaka mmoja alikuwa na uzito wa takriban Kilogram 20.4 na urefu wa Sentimita 100.33 na alipofikisha miaka 8 aliupita urefu wa baba yake wa Sentimita 180.34

Zaidi, soma https://jamii.app/MtuMrefuDunia
MAISHA: JE, ULIANZA MWAKA NA MIPANGO GANI, UNAENDELEA NAYO?

> Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kujiwekea malengo ya kuanza nayo mwanzo wa mwaka

> Imezoeleka watu kuanza mwaka kwa mikakati wa kufanya mazoezi, kula kwa afya na kuweka akiba ya fedha lakini mikakati hiyo huwa haidumu

Soma > https://jamii.app/MwanzoMwaka
HOJA: Miaka ya nyuma kulikuwa na tabia ya watu wanaozamia meli kwenda nchi za Ughaibuni, vijana wakiwa ni wahanga wakubwa

- Walikuwa wakikimbilia huko Ughaibuni kwa lengo la kutafuta maisha

Je, ni kweli Ughaibuni kuna maisha bora kuliko nyumbani?

Zaidi, fuatilia mjadala https://jamii.app/MaishaUghaibuni
MICHEZO: Kufuatia waliokuwa wachezaji wa Klabu ya Yanga kufikisha malalamiko yao katika Chama cha Haki za Wachezaji Tanzania (Sputanza), klabu hiyo imejikuta ikifikishwa katika Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kujibu mashitaka

Wachezaji hao ambao ni pamoja na Pato Ngonyani, Mwinyi Haji na Antony Matheo walipeleka malalamiko ya kudai fedha zao za mishahara ya miezi miwili pamoja na fedha ya usajili

Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoki amesema wamepokea malalamiko kutoka kwa wachezaji hao ambapo tayari wameshayawasilisha kwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kwa ajili ya kufanyia kazi
ENGLAND: MAN. CITY YACHEZEA KICHAPO IKIWA NYUMBANI

- Manchester City ikiwa ‘Etihad Stadium’ imepokea kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu

- Chelsea imepata ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Southampton huku Arsenal ikipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Bournemouth
ENGLAND: MAN. UTD YAPOTEZA MECHI YA TATU KWENYE LIGI KUU

- Klabu ya Manchester United imepokea kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa klabu ya Newcastle United katika uwanja wa St. James’ Park kwenye mchezo wa Ligi Kuu Nchini England

- Kwa matokeo hayo Manchester United inabakia na alama 9 na kushuka hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi huku Newcastle ikapanda hadi nafasi ya 16 ikifikisha alama 8
RAIS MAGUFULI AAGIZA KAIMU RPC WA SUMBAWANGA ASIMAMISHWE KAZI NA KUSHUSHWA CHEO

> Polycarp Urio amesimamishwa kazi hadi Rais atakapotoa maelekezo mengine baada ya kushindwa kutekeleza maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola

Zaidi, soma => https://jamii.app/RaisVsPolisiSumbawanga
KOREA KASKAZINI YAGOMA KUENDELEA KUZUNGUMZA NA MAREKANI

- Haitaki kuzungumza kuhusu nyuklia hadi Marekani itakapochukua hatua za kumaliza mvutano baina yao

- Imesema hayo baada ya kuvunjika kwa mazungumzo yao yaliyosimamiwa na Sweden

Zaidi, soma https://jamii.app/NKoreaMazungumzoUSA
SAUDI ARABIA: WAPENZI RUKSA KULALA CHUMBA KIMOJA HOTELINI

- Raia wa kigeni ambao ni Wapenzi wasio wanandoa wanaweza kulala chumba kimoja hotelini

- Aidha, katika hatua hiyo ya kukuza Utalii, Wanawake wataruhusiwa kulala hotelini peke yao

Zaidi, soma https://jamii.app/WapenziChumba1-Saudia
TANZIA: MSANII NA ALIYEKUWA MKUU WA IDARA YA SANAA CHADEMA AFARIKI

> Fulgence Mapunda almaarufu Mwana Cotide amefariki dunia saa 10:20 usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu

> Alilazwa ktk Hospitali ya St Monica, Manzese Dar

Soma > https://jamii.app/MsaniiCHADEMAAfariki
SHINYANGA: WANAFUNZI 8 MBARONI WAKIDAIWA KUMSHAMBULIA MWENZAO

- Wanafunzi hao wa Sekondari ya Seeke wanatuhumiwa kumjeruhi Costantine Makoye

- Makoye aliyefariki akipatiwa matibabu, alivamia sherehe na wenzake na kunyang’anya Watu vitu

Zaidi, soma https://jamii.app/Wanafunzi8Mbaroni-KHM
AFISA MANUNUZI CHUO CHA KINAMPANDA ATAKIWA KUKAMATWA

- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Francis Muyombo akamatwe kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaManunuziKinampanda
MBEYA: WAWILI WAFARIKI BAADA YA DARAJA KUVUNJIKA KUTOKANA NA MVUA

- Wametumbukia mtoni wakati wakipita katika daraja hilo linalounganisha Kata ya Tembela na Mwakibete

- Watu 2 hawajulikani walipo akiwemo mtoto anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja

Zaidi, soma https://jamii.app/WawiliWafarikiDarajaMwakibete-MBY
MAHAKAMA YAMUACHIA MICHAEL WAMBURA

- Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura

- Imempa masharti ya kutokufanya makosa yoyote kwa miezi 12 na kulipa zaidi ya Tsh. Milioni 100 kwa awamu 5

Zaidi, soma https://jamii.app/MichaelWamburaHuru
MKURUGENZI MSTAAFU WA TISS, APSON MWANG'ONDA AFARIKI DUNIA

- Aliyekuwa Mkurugenzi wa TISS, Apson Mwang’onda (75) amefariki leo, Nchini Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa

- Alistaafu kazi hiyo Agosti 21, mwaka 2006 kwa mujibu wa sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/ApsonTISSAfariki
SINGIDA: WAZIRI MKUU AAGIZA WALIOAJIRIWA KINDUGU WAFUKUZWE

- Amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile awaondoe Watumishi watatu wanaokusanya mapato kwenye stendi ya mabasi, walioajiriwa kindugu na wanaodaiwa kuiba mapato

Zaidi, soma https://jamii.app/WalioajiriwaKinduguWaondoke-SND