JamiiForums
52.8K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FAHAMU: KIJIJI CHA WATU WALIOUZA FIGO ZAO

- Kijiji cha Hokse nchini Nepal kimebatizwa jina jipya la ‘Kidney Village’ baada ya Watu karibia wote wanaoishi kwenye kijiji hicho kuwa wameuza Figo zao

- Hali ngumu ya maisha imewasukuma kufanya hivyo

Soma > https://jamii.app/Hokse
UTEUZI: Rais Magufuli amemteua Dkt. Wilson Mahera kuwa Mkurugenzi mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akichukua nafasi ya Athuman Kihamia ambaye atapangiwa kazi nyingine

> Kabla ya uteuzi huo Mahera alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Arusha

Soma - https://jamii.app/UteuziMkrgnzNEC
#JFLeo
RAIS AFANYA TEUZI MBALIMBALI ZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI

> Amemteua Ndaki Stephano Muhuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Kilimanjaro

> Rehema Saidi Bwasi Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri Wilaya ya Morogoro na Sheillah Edward Lukuba Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

#JFLeo
UTEUZI: Rais Magufuli amemteua Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Balozi na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

> Ibuge anachukua nafasi ya Balozi Grace A. Martin ambaye atapangiwa majukumu mengine ya Kibalozi

#JFLeo
UGANDA: SERIKALI YATANGAZA KUBADILI KOFIA ZA JESHI; ZITAFANANA NA ANAZOVAA BOBI WINE

> Mabadiliko hayo yanamaanisha wananchi hawataruhusiwa kuvaa kofia zinazoendana na za jeshi

> Mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa Sheria ya Majeshi ya Uganda ya 2005

Soma > https://jamii.app/KofiaJeshiUganda
KATAVI: LUGOLA AAGIZA ASKARI WOTE WA KITUO CHA MAJIMOTO KUONDOLEWA

> Ni baada ya kero zilizowasilishwa na wananchi, kuonesha askari 15 wa kituo hicho wanajihusisha na rushwa, kupiga wananchi hovyo, kushindwa kudhibiti ulinzi na usalama na kutoshughulikia malalamiko ya wananchi

Soma - https://jamii.app/PolisiWatimuliwaKituoni
SIMU ZENYE iOS CHINI YA 9, ANDROID 2.3.7 NA WINDOW KUTOWEZA KUTUMIA WHATSAPP

> Hadi kufikia Februari 1, 2020, programu ya WhatsApp itakuwa inafanya kazi kwenye simu za iPhone zenye mfumo wa kuanzia iOS 9 na kuendelea

> Aidha hadi kufikia Desemba 2019 itasitisha kabisa upatikanaji wa programu yake kwenye simu za Window zote na Android 2.3 (Gingerbread)

Soma - https://jamii.app/WhatsAppDiscontinueAccess
#JFTeknolojia
MBEYA: ALIYESAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA AHUKUMIWA MIAKA 20 KWA UHUJUMU UCHUMI

> Mahakama Kuu imemhukumu Waziri Mizogi kifungo na kulipa faini ya zaidi ya Milioni 270

> Mizogi amekutwa na hatia ya kusafirisha #DawaZaKulevya aina ya Heroin na Cocaine

Soma > https://jamii.app/MizogiJela
ARUSHA: MKURUGENZI ALIYEMPIGA RISASI MENEJA AJISALIMISHA POLISI

> Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ulinzi ya Bonds Security, Frenk Kessy amejikabidhi kituo cha Polisi na kuwekwa mahabusu baada ya kumjeruhi kwa Risasi Meneja wa Kampuni ya Maxshield, Endrew Lubange wakigombea lindo la hoteli

Soma - https://jamii.app/KessyAjisalimishaPolisi
GHANA: WAZAZI WAPINGA MPANGO WA ELIMU YA NGONO KWA WANAFUNZI

> Wanadai kuwa programu hiyo iliyoandaliwa na UNESCO inachochea watoto kujiingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja au kuwa wanaharakati wa watu wenye jinsia mbili

> Jumuiya ya Walimu wanapinga somo hilo, kwa kuwa hawakushirikishwa kuandaa somo hilo

Soma - https://jamii.app/SexualityEducationRejected
MOROCCO: MWANDISHI AHUKUMIWA KWA KUFANYA NGONO NA KUTOA MIMBA

> Hajar Raissouni na mpenziwe, Rifaat Al-Amin wamehukumiwa kifungo cha mwaka 1 akidaiwa kufanya ngono kabla ya ndoa na kutoa mimba

> Daktari anayedaiwa kumtoa mimba hiyo amehukumiwa miaka 2

Soma - https://jamii.app/JournalistJailAbortion
KENYA: GARI LA MAGEREZA LAPATA AJALI, MTUHUMIWA AFARIKI

> Mtu mmoja amefariki na wengine 7 kujeruhiwa baada ya gari la Magereza kupinduka leo katika eneo la Kathageri karibu na Daraja la Thuci, Wilaya ya Embu

> Watuhumiwa hao walikuwa wakisafirishwa kutoka Gereza la Embu kwenda Mahakama za Meru

Soma zaidi - https://jamii.app/AjaliKifoMfungwa
FAIDA ZA KUTUMIA ILIKI KIAFYA

> Huipa Figo uwezo wa kuondoa takamwili na kusaidia kuweka sawa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni

> Iliki inasaidia kuondoa hali ya kiungulia/gesi na tatizo la kukosa choo. Saga kisha tumia unga wake kijiko 1 cha chakula ktk maji moto kwa wiki 2

> Kwa kinywa kinachotoa harufu au vidonda tumia unga uliochanganywa na maji ya uvuguvugu kisha sukutua kila siku kwa wiki 3

Fahamu zaidi - https://jamii.app/FaidaIlikiAfya
#JFAfya
DAR: MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA NA KUPATIKANA NA SILAHA MBILI AINA YA BASTOLA NA RISASI 5
-
Jeshi la Polisi limefanikiwa kuzima tukio la ujambazi, Mbezi Msakuzi

- Raia wema waliwatonya Polisi kuwa majambazi wamepanga kuvamia SACCOSS ya Msakuzi

Soma > https://jamii.app/MajambaziMsakuzi
KISUTU, DAR: WANAWAKE WAWILI WALIOENDESHA MCHEZO WA UPATU WAHUKUMIWA MIAKA 20 JELA

> Halima Nsubuga na Magdalena Uhwello wametakiwa kulipa kiasi cha milioni 101 kama faini kwa kosa la utakatishaji fedha

> Walikuwa wakiendesha upatu

Zaidi, soma > https://jamii.app/WanawakeJela
DAR: WAFANYAKAZI 9 WA NSSF AKIWEMO KAIMU MKURUGENZI WA FEDHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

- Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Jamila Vullu pamoja na watumishi wengine 8 wamefikishwa Mahakamani wakikabiliwa na mashtaka 5 likiwemo la uhujumu uchumi

Soma > https://jamii.app/WatumishiNSSFKisutu
KENYA: WATANZANIA WALIOKUWA OMBAOMBA KENYA WARUDISHWA NCHINI

> Emmanuel Masabuko pamoja na msaidizi wake Deus Peter baada ya kukamatwa walifikishwa katika Mahakama ya Bomet kujibu tuhuma dhidi yao

Zaidi, soma => https://jamii.app/OmbaombaTzKenya
SERENGETI: TANESCO YAIKATIA UMEME MAMLAKA YA MAJI MUGUMU, WANANCHI WASOTA BILA MAJI SAFI

- Wakazi wa Mugumu wamekosa huduma hiyo baada ya TANESCO kuchukua hatua hiyo tarehe 25, Septemba

- MUGUWASA wanadaiwa na TANESCO Tsh. milioni 31

Zaidi, soma > https://jamii.app/TANESCOVsMUGUWASA
TRA YATANGAZA KUKUSANYA TRILIONI 1.767 KWA MWEZI SEPTEMBA, 2019

> Mamlaka ya Mapato Nchini imesema kiwango hiki hakijawahi kukusanywa tangu TRA ianzishwe

> Makusanyo haya ni sawa na ufanisi wa 97.20%. Lengo lilikuwa kukusanya Tsh. Trilioni 1.817

Zaidi, soma https://jamii.app/TRASeptmberRevenues