JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TCRA: ASILIMIA 12 YA LAINI ZOTE ZIMESAJILIWA KWA ALAMA ZA VIDOLE

- Laini za simu Milioni 5.2 sawa na 12%, kati ya zinazotumika nchini ndio zimesajili ikiwa bado miezi 3 usajili kuisha

- Watoa huduma za mawasiliano nchini wameanza kampeni ya kuhamasisha usajili huo

Soma https://jamii.app/AsilimiaUsajiliLainiVidole
URUSI KUISAIDIA UGANDA KUJENGA UWEZO WA MATUMIZI YA NYUKLIA

- Itasaidiwa kujenga miundombinu ya nyuklia kwa matumizi kwenye viwanda, sekta ya afya na kilimo

- Rwanda, Kenya, Afrika Kusini na Nigeria tayari zimekubali matumizi ya nishati hiyo

Soma https://jamii.app/UgandaMatumiziNyuklia
WAZIRI WA FEDHA, DKT. MPANGO: SIWASIKII WATU WAKISEMA VYUMA VIMEKAZA

> Asema hii ni kutokana na juhudi za taasisi za fedha katika kushusha riba za mikopo zinazoitoa kwa wateja wao

> Azipongeza benki zote za biashara kwa mikopo nafuu

Zaidi, soma => https://jamii.app/DktMpangoVyumaKukaza
KISUTU: AVEVA NA KABURU WAONDOLEWA SHTAKA LA UTAKATISHAJI FEDHA

- Aliyekuwa Rais wa Simba, Evance Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ wamebaki na makosa mengine

- Wameruhusiwa kupata dhamana baada ya kuondolewa shtaka hilo

Soma https://jamii.app/AvevaKaburuShtaka1
USHAURI: BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU, TUMIENI UBUNIFU ZAIDI KULIKO NGUVU NA VITISHO

> Mdau wa JamiiForums anasema siku chache zilizopita aliona picha ya ukurasa wa mbele wa gazeti ukionesha nukuu ya Mkurugenzi wa HESLB akisema 'Wadaiwa Bodi ya Mikopo Kusakwa Majumbani Usiku'

> Asema kuna changamoto ya upatikanaji wa taarifa za madeni/marejesho

> Mdau amegusia sheria ya ulipaji wa mikopo na kuishauri bodi hiyo kuongeza ubunifu na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano

Zaidi, soma => https://jamii.app/UshauriHESLB
SERIKALI YASAINI MKATABA WA KUNUNUA NDEGE MBILI AINA YA AIRBUS

- Wakala wa Ndege za Serikali na Kampuni ya Airbus wamesaini mkataba wa ununuaji wa ndege mbili aina ya Airbus A220-300 zitakazotumiwa na Shirika la ndege la Tanzania(ATCL)

Zaidi, soma https://jamii.app/TZAirbusMpya2
DAR: MKAZI WA MAKONGO AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUMCHOMA MIKONO MTOTO

> Nicholaus Makali(32), amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumshambulia Mtoto wa miaka 10

> Ashindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande

Soma > https://jamii.app/MakaliMahakamani
TANZANIA YAPANDA NAFASI MBILI KWENYE VIWANGO VYA FIFA

- Taifa Stars imepanda nafasi 2 katika orodha ya viwango vya ubora vya FIFA na kushika nafasi ya 135

- Kwa Afrika Mashariki, Uganda(80) inaongoza ikifuatiwa na Kenya(107), Rwanda(130), Tanzania(135) na Burundi (144)

#JFLeo
BONDO, KENYA: MWANAUME AMFUATA MKEWE NA KUMSHAMBULIA KWA KISU AKIMTUHUMU KWA USALITI

> Alifika katika shule ya St. Paul Gulf Academy na kumchoma Mkewe kisu shingoni na shavuni

> Evelyn Akinyi amesema Mumewe alitaka simu ili aikague

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuAshambuliwaKE
BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU YASHAURIWA KUTUMIA UBUNIFU ZAIDI KULIKO NGUVU NA VITISHO

> Mdau wa JamiiForums anasema siku chache zilizopita aliona picha ya ukurasa wa mbele wa gazeti ukionesha nukuu ya Mkurugenzi wa HESLB akisema 'Wadaiwa Bodi ya Mikopo Kusakwa Majumbani Usiku'

> Asema kuna changamoto ya upatikanaji wa taarifa za madeni/marejesho

> Mdau amegusia sheria ya ulipaji wa mikopo na kuishauri bodi hiyo kuongeza ubunifu na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano

Kuchangia mjadala, tembelea https://jamii.app/UshauriHESLB
SONGWE: AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KUUA KWA KUKUSUDIA

- Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imempa adhabu hiyo Amani Kalinga(21)

- Amekutwa na hatia ya kumuua kwa kukusudia Heroni Kalinga(12) na kuchukua nyeti zake mnamo mwaka 2017

Zaidi, soma https://jamii.app/AuaAhukumiwaKifo
DR CONGO: WATU 14 WAUAWA NA 4 KUJERUHIWA BAADA YA WAASI KUSHAMBULIA MAKAZI YAO

> Mauaji hayo yametokea Jimbo la Ituri ambako kumekuwa na muendelezo wa ghasia kwa miezi kadhaa sasa

> Mwezi Juni mwaka huu, watu 160 waliuawa katika jimbo hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiIturi
MICHEZO: Mechi za mapema kwa michezo ya kwanza ya hatua ya makundi katika michuano ya Ligi ya Europa kwa msimu wa mwaka 2019/20 imemalizika

- Katika baadhi ya matokeo, klabu ya Arsenal ya England imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani
MANYARA: KULI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIGOMBEA MALIPO YA TSH. 1,500

> Rajabu Said(22) ameuawa kwa kuchomwa kisu na Cleophace John(28)

> Mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa na yupo kwenye mikono ya Jeshi la Polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/KuliAuawaManyara
MAREKANI YAITAKA TANZANIA KUWEKA WAZI MATOKEO YA UCHUNGUZI WA ALIYEDHANIWA KUFARIKI KWA EBOLA

> Marekani kupitia Waziri wake wa Afya imeitaka Tanzania kuweka wazi matokeo ya Kimaabara

> Waziri Alex Azar, ametoa kauli hiyo akiwa Uganda

Soma > https://jamii.app/US-EbolaTz
SERIKALI YAUTAKA MGODI WA STAMIGOLD KUUZA DHAHABU KWENYE MASOKO YA NDANI

> Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko alipotembelea mgodi huo uliopo wilaya ya Biharamulo

> Mgodi huo umetakiwa kuanza utekelezaji Desemba 2019

Soma > https://jamii.app/StamigoldSokoNdani
KENYA AIRWAYS YASIMAMISHA SAFARI ZAKE ZA GABON NA BENIN

- Imetangaza kusimamisha safari za kwenda Libreville, Gabon na Cotonou, Benin kuanzia Oktoba 14, 2019

- Waliokata tiketi kusafiri baada ya Oktoba 14 watasafirishwa na mashirika mengine

Soma hapa > https://jamii.app/KQYasitishaBaadhiSafari
IRAN: SHAMBULIO LOLOTE DHIDI YETU LITALETA VITA KAMILI

- Waziri wa Mambo ya Nje amesema shambulio dhidi ya nchi yake, kufuatia hujuma dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia litaleta vita kamili na kuongeza mvutano katika Ghuba ya Uajemi

Zaidi, soma https://jamii.app/IranKulipaShambulio