JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA WAZIRI JANUARI MAKAMBA, SIMBACHAWENE ACHUKUA NAFASI YAKE

> Januari Makamba January Makamba ametenguliwa, nafasi yake inachukuliwa na George Simbachawene

> Ndg. Hussein Bashe anakuwa Naibu Waziri wa Kilimo

Soma > https://jamii.app/JanuariMakambaOut
JamiiForums
Photo
JANUARY MAKAMBA: NIMEYAPOKEA MABADILIKO KWA MOYO MWEUPE

> Asema ataongea zaidi siku zijazo

> Ni muda mchache baada ya kutangazwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
DERA ISMAIL KHAN, PAKISTAN: MASHAMBULIO DHIDI YA POLISI YAUA WATU 8

> Kati ya waliofariki, askari polisi ni wanne

> Imethibitika kuwa shambulio la pili lilikuwa la kujitoa mhanga lililofanywa na mwanamke katika lango la kuingilia hospitali

Soma https://jamii.app/PoliceAttackPakistan
HYDERABAD, INDIA: MTANZANIA MBARONI KWA KUENDESHA DANGURO

- Ramadhani Usanga Sabia Bayoni akishirikiana rafiki yake, huweka picha za wanaowauza kwenye tovuti za ngono ili kuwavutia wateja

- Wateja hao hulipa Rs 10,000(Sawa na Tsh. 334,162.72)

Soma https://jamii.app/TanzanianArrestedInIndia
KAGERA: KATIBU MWENEZI CHADEMA ADAIWA KUJINYONGA

- Ni Nurunet Bakaishumba(35) Katibu Mwenezi wa CHADEMA katika Kata ya Igurwa, Wilayani Karagwe

- Ameacha ujumbe kwamba familia yake haihusiki na kifo chake na wazo kujinyonga alikuwa nalo kwa muda wa mwezi mmoja sasa

Soma https://jamii.app/KatibuMweneziCHADEMAAjinyonga
#JFLeo
KENYA: MLINZI WA SPIKA AULIWA KWA KUPIGWA RISASI

> Mlinzi wa Spika wa Bunge la Kaunti ya Embu ameuliwa kwa kupigwa risasi mapema jana eneo la Kamiti Corner jijini Nairobi

> Aidha dereva wake amekamatwa baada ya uchunguzi wa mwanzo kubaini kuwa huenda alihusika

Soma - https://jamii.app/SpeakerGuardShortDead
TATHMINI YA CHAKULA: HALMASHAURI 46 ZAWEZA KUPATA UPUNGUFU WA CHAKULA

> Wizara ya Kilimo imebaini Halmashauri 46 katika Mikoa 13 zina dalili ya kukumbwa na upungufu wa chakula kutokana na changamoto zilizoathiri uzalishaji wa chakula kwa msimu wa 2018/19, ikiwa ni pamoja na upungufu wa mvua

> Tathmini hiyo huangalia baadhi ya mazao muhimu yanayohitajika zaidi ikiwamo Mahindi, Mtama, Ulezi, Mchele, Kunde, Ngano, Ndizi, Mihogo na Viazi

Soma - https://jamii.app/Halmshr46UpungufuChakula
IKULU, DAR: RAIS MAGUFULI AMEWAAPISHA SIMBACHAWENE NA BASHE

> Asubuhi ya leo, Rais Magufuli amemuapisha George Simbachawene kuwa Waziri wa Mazingira na Muungano na Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo

Fuatilia yaliyojiri hapa => https://jamii.app/SimbachaweneBasheKiapo
ALIYEWAHI KUWA MCHEZAJI WA MANCHESTER UNITED NA REAL MADRID AJA KUTALII TANZANIA

> Ruud van Nistelrooy ameweka picha za wanyama katika ukurasa wake wa Twitter

> Ameonesha kushangazwa na uzuri wa Wanyama hao, amewakaribisha watu Tanzania

Soma > https://jamii.app/VanNestelrooy-Tanzania
ZANZIBAR: MHANDISI MSAIDIZI WA MV MAPINDUZI AJINYONGA SAFARINI

> Tukio hilo limetokea wakati meli hiyo ikitoka Unguja kuelekea Pemba

> Tukio hilo limepelekea kukatizwa kwa safari na meli hiyo kurudi Unguja

Zaidi, soma => https://jamii.app/InjiniaWaMeliAjinyongaZNZ
WAZAZI WAKAMATWA KWA KUSABABISHA BINTI YAO AKIMBIE MASOMO

> Jeshi la Polisi Wilaya ya Chamwino, Dodoma linawashikilia Athumani Salum (35) na Paulina Mazengo (45) kwa tuhuma za kusababisha binti yao (17) kutoroka shuleni kutokana na baba yake kumsumbua akimtaka kimapenzi mama mzazi kuficha siri hiyo

> Baba huyo anadaiwa kuwahi kumpa mimba binti mkubwa wa mke wake na kwamba alikwenda kumtoa mimba hiyo

Soma - https://jamii.app/WazaziMapenziMtoto
SHINYANGA: WATU 6 WAPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI

> Watu 6 wamefariki na wengine 22 wamejeruhiwa katika eneo la Nyambula, Kata ya Ngogwa, Wilayani Kahama baada ya gari aina ya Totoya Hiace namba T 710 AZZ na Land cruiser namba T 477 ATC kugongana

> Chanzo kinadaiwa kuwa ni mwendokasi wa dereva wa Hiace iliyokuwa na abiria

Soma - https://jamii.app/Vifo6AjaliKahama
KENYA: WAZIRI WA FEDHA AJISALIMISHA KWENYE OFISI YA DCI

> Waziri wa Fedha, Henry Rotich amejisalimisha kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma nchini humo leo na mpaka sasa yupo kwenye mahojiano kuhusu tuhuma zinazomkabili

> Hapo awali, Mkurugenzi wa mashtaka aliagiza kukamatwa na kushtakiwa kwa Waziri wa Fedha na Katibu wa Wizara hiyo kwa tuhuma za ufisadi kuhusiana na mradi wa ujenzi wa mabwawa wa thamani ya Ksh. billion 65

Soma - https://jamii.app/RotichInterrogationDCI
MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA ATOMIKI AFARIKI

> Sekretarieti ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limetoa taarifa kuhusu kifo cha Mkurugenzi wa shirika hilo, Yukiya Amano (73)

> Amano amekuwa akikamilisha muhula wake wa tatu, ambao ungemalizika Novemba 2021, lakini alikuwa anatarajiwa kutangaza kuachia ngazi Machi 2020 kwasababu za kiafya

#JFLeo
DRC YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA KISIASA

> Mamlaka za Jamhuri ya Demokrasia ya Congo zimepiga marufuku mikutano ya kisiasa kufuatia kuibuka kwa mvutano baina ya wafuasi wa Rais Felix Tshisekedi na wale wa Rais Joseph Kabila wakimpinga mgombea wa Waziri mstaafu wa Sheria kwa urais wa Seneti

Soma - https://jamii.app/DRCBansPolitics
WAZIRI LUGOLA AAGIZA MSAKO WA VIBAKA ENEO LA JANGWANI, DAR

> Waziri wa Mambo ya ndani ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala kufanya Operesheni Maalum ya kuwasaka na kuwakamata Vibaka na waporaji wanaoendesha vitendo vya wizi na uporaji hasa nyakati za jioni na usiku

> Amesema kama inawezekana kutokomeza mbu kwa kuvunja vifuu, anataka mazalia ya wahalifu yatokomezwe

Soma - https://jamii.app/LugolaMsakoVibaka
DRC: WAZIRI WA AFYA AJIUZULU KUTOKANA NA JANGA LA EBOLA

> Waziri Oly Ilunga, amejiuzulu kwenye nafasi yake huku akieleza sababu kuwa hakutendewa haki na uamuzi wa Rais Tshisekedi wa kusimamia jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ulioua watu zaidi ya 1,700 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, Mashariki mwa nchi hiyo

#JFLeo
JF EXCLUSIVE: MAURITIUS LEAKS NAME TANZANIA COMPANIES

> It has been revealed that at least four companies in Tanzania are in Mauritius Leaks – for now we are publishing one company, while continuing to track others

Continue reading > https://jamii.app/MauritiusLeaks1

#MauritiusLeaks
MWANZA: WATU 4 AKIWEMO AFISA MFAWIDHI WA RASILIMALI ZA UVUVI WAUAWA

> Wameuawa katika vurugu kati ya wakazi wa kisiwa cha Siza na Askari wa Jeshi la Polisi

> Afisa huyo wa Kanda ya Ukerewe amefariki dunia baada ya kupigwa na Wananchi

Soma => https://jamii.app/AfisaUvuviAuawa