JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Gazeti la The Monitor la nchini Uganda lilivyoandika kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Salaam za Pongezi toka Ubalozi wa Marekani nchini kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
UGONJWA WA EBOLA WATANGAZWA KUWA JANGA LA DHARURA DUNIANI

> Shirika la Afya Duniani limetangaza ugonjwa wa Ebola kuwa dharura ya kiafya duniani kutokana na ugonjwa huo kuua watu 1,668 katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwezi Agosti 2018

> Uamuzi huo umechukuliwa na jopo la wataalamu na shirika limezingatia vigezo kadhaa, ikiwemo hatari ya kusambaa kwa virusi vya Ebola duniani

Soma - https://jamii.app/EbolaGlobalEmergency
RASMI: MATTHIJS DE LIGT ASAJILIWA JUVENTUS

- Beki huyo raia wa Uholanzi mwenye miaka 19 amesajiliwa kwa ada ya Paundi Milioni 67.5 (Tsh.193,519,125,000) kutoka Ajax kwa mkataba wa miaka mitano

- Alikuwa akiwaniwa pia na vilabu vya Manchester United, Barcelona na PSG
Salaam za Pongezi toka kwa Balozi wa Sweden nchini kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
POLISI KUKATWA MSHAHARA ILI KUMLIPA WALIYEMVUNJA MGUU KWA KIPIGO

> Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Alli Hapi ameliagiza Jeshi la polisi kuwakata mshahara kiasi cha Tsh. milioni 1 askari wake 10 waliohusika kumvunja mguu Maiman Mwakajenge

> Inaelezwa kuwa walimshambulia kwa kipigo wakidai kuwa amewatukana

Soma - https://jamii.app/MakatoMshaharaPolisi
TCU YAKIFUTA CHUO KIKUU CHA ECKERNFORD

- TCU imesema Chuo hicho kilichopo Mkoani Tanga kimefutwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya udahili

- Ni takribani miezi 10 tangu kilipositishiwa kutoa mafunzo na kutakiwa kuhamisha Wanafunzi

Zaidi, soma https://jamii.app/ChuoEckernfordChafutwa
Kutoka Shirika la Human Rights Watch linalojishughisha na Masuala ya Uangalizi wa Haki za Binadamu Duniani kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kupata Tuzo ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
RIPOTI: VIFO VITOKANAVYO NA UKIMWI VYAPUNGUA

> Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa vifo vimepungua kwa 33% tangu mwaka 2010 ambavyo ni takribani vifo 770,000 tofauti na mwaka 2010 ambapo watu milioni 1.2 walifariki

> Aidha, maambukizi mapya yameongezeka hasa Mashariki ya Kati na Ulaya Mashariki ambapo kuna wagonjwa milioni 37.9

Soma - https://jamii.app/RipotiVifoUkimwi
INSTAGRAM KUFICHA IDADI YA ‘LIKES’ ILI KUONDOA KUTOKUJIAMINI

- Imefanya majaribio Canada mwezi Mei na mengine yanafanyika Australia, New Zealand, Ireland, Italy, Japan na Brazil

- Lengo ni watu waweke kile wanachokipenda wao

Zaidi, soma https://jamii.app/InstagramKuondoaLikes
KENYA: AMKATA KICHWA BABA YAKE AKIDHANI ANACHINJA MBUZI

> Dennis Mwangi (29) amemuua Peter Ndegwa (59) kwa kumkata kichwa akidai alidhani alikuwa anachinja mbuzi na kisha kukitia kwenye ndoo na kuanza kuzunguka nacho mjini

> Watu wanadhani huenda alikuwa akikabiliwa na matatizo ya kiakili

Soma - https://jamii.app/AkataKichwaBabake
IRAN YAKAMATA MELI YA MAFUTA YA KIGENI NA WAFANYAKAZI WAKE 12

- Imedai meli hiyo ilikuwa ikisafirisha mafuta kimagendo katika eneo la Ghuba siku ya Jumapili iliyopita

- Haijathibitishwa ikiwa meli hiyo ni ile ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) iliyopoteza mawasiliano siku hiyo ya Jumapili

Zaidi, soma https://jamii.app/IranYakamataMeliGhuba
UGANDA KUANZA KUTOA VYETI VYA USAJILI KWA WAFUGAJI NA NG'OMBE WAO

> Wafugaji wa ng'ombe watasajiliwa wenyewe na ng'ombe wao pia watasajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa kwasababu walaji wanahitaji nyama ya ng'ombe yenye umri kati ya miezi 15 hadi 24

Soma - https://jamii.app/UsajiliMifugoUG
UCHAGUZI SINGIDA MASHARIKI: MGOMBEA WA CCM APITA BILA KUPINGWA

> Miraji Mtaturu amepita ktk uchaguzi mdogo baada ya wagombea 12 wa upinzani kutorejesha fomu

> Wenye pingamizi wametakiwa kuwasilisha mapingamizi yao kabla ya kesho saa 10 jioni

Soma https://jamii.app/MgombeaUchaguziSingida
#JFLeo
KUFUZU #AFCON2021: TANZANIA KUNDI MOJA NA TUNISIA NA LIBYA

- CAF yatangaza makundi ya kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2021 itakayofanyika Cameroon

- Tanzania ipo Kundi J, pamoja na Tunisia, Libya na Equatorial Guinea

Zaidi, soma https://jamii.app/KufuzuAfcon2021
SKYSPORTS: BARCELONA YAWEKA DAU KWA AJILI YA NEYMAR

- Barcelona inadaiwa kuweka dau la £90m na Wachezaji wawili ili imsajili Neymar kutoka PSG

- Inadaiwa imewapa PSG orodha ya Wachezaji 6 wakiwemo Philippe Coutinho, Ousmane Dembele, Ivan Rakitic, Nelson Semedo na Malcom
AFISA MIPANGO MIJI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUUZA ARDHI KINYUME NA TARATIBU

- Waziri Lukuvi amemsimamisha kazi Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Manase Nkuli

- Ameghushi nyaraka na kuuza hekari 6000 za ardhi kinyume na taratibu

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaMipangoSengerema
WAKULIMA WA PAMBA KUPEWA VITAMBULISHO

- Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ameiagiza bodi ya Pamba kuviandaa na kuvigawa bure ili kuwatambua wakulima

- Pia, ameahidi Serikali kufidia kiasi cha fedha ili kilo ya pamba inunuliwe kwa Tsh. 1,200

Zaidi, soma https://jamii.app/VitambulishoWakulimaPamba
UKUAJI WA UCHUMI TANZANIA 2018: BENKI YA DUNIA YATOFAUTIANA NA SERIKALI

- Benki ya Dunia inasema uchumi ulikuwa kwa 5.2% tofauti na Serikali iliyosema ulikuwa kwa 7%

- Moja ya sasabu iliyoathiri ukuaji ni kushuka kwa viwango vya uwekezaji

Zaidi, soma https://jamii.app/UchumiTanzania2018-WB
MOSHI: WAZIRI MKUU AAGIZA WALIOKUWA WALINZI WA KITUO CHA MABASI KUKAMATWA

> Ni walinzi waliokuwa lindo eneo la ujenzi wa stendi ya mabasi ya Ngangamfumuni siku ulipotokea wizi wa tani 5 za nondo

> Amesema endapo walinzi hao hawatapatikana, viongozi wa kampuni husika wakamatwe ili waseme walipo wafanyakazi wao

Soma - https://jamii.app/WiziNondoUjenzi