JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: El CHAPO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

- Joaquin ‘El Chapo’ Guzman (62), amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia katika makosa 10 yakiwemo ya kusambaza #DawaZaKulevya na utakatishaji fedha

Zaidi, soma https://jamii.app/ElChapoLifeInPrison
DAR: AMPIGA NA KUMUUA MKE WAKE KABLA YA KUUCHOMA MWILI MOTO

- Polisi inamshikilia Khamis Luwongo(38) kwa tuhuma za kumuua na kumchoma moto mke wake, Naomi Marijani(36)

- Baada ya mauaji aliwataarifu ndugu wa Naomi kuwa mke haonekani nyumbani na hivyo kwenda Polisi kuripoti

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaMkeAmchoma-Dar
BEKI WA TOTTENHAM, KIERAN TRIPPIER AJIUNGA ATLETICO MADRID

- Amejiunga na kikosi cha Diego Simeone kwa kandarasi ya miaka mitatu kwa ada ya Paundi Milioni 20 (Tsh. 57,233,000,000)

- Anakuwa mchezaji wa kwanza raia wa England kuchezea Atletico ndani ya miaka 95 iliyopita
MWANZA: POLISI WALIOSINDIKIZA DHAHABU WAFUTIWA MASHTAKA

> Mkurugenzi wa Mashtaka nchini amewafutia kesi askari Polisi 8 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi

> Pia amefuta kesi nyingine 322 wakiwemo wafungwa 70 kutoka gereza la Butimba ambako Rais Magufuli alifanya ziara juzi

Soma - https://jamii.app/DPPAfutaMashtaka
BASHE: WALICHOFANYA KINANA NA MAKAMBA KINAKIUKA KATIBA YA CCM

- Mbunge Hussein Bashe(CCM) amesema barua ya Wazee hao kuhusu Musiba ina lengo la kumchafua Rais Magufuli na kuigawa CCM

- Amesema Musiba si mwanaCCM huwezi kumshtaki ndani ya CCM

Zaidi, soma https://jamii.app/BasheVsKinanaMakamba
TABORA: KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KAKAKUONA

- Thadeo Shahibu amefikishwa Mahakamani jana Julai 17, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi

- Amekutwa anamiliki mnyama, Kakakuona kinyume na sheria namba 5 ya Uhifadhi Wanyamapori ya mwaka 2009

Zaidi, soma https://jamii.app/KizimbaniAkutwaKakakuona
Pongezi toka kwa Balozi wa Denmark nchini kwa Mkurugenzi wetu Maxence Melo kupata Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Habari
Gazeti la The Monitor la nchini Uganda lilivyoandika kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Salaam za Pongezi toka Ubalozi wa Marekani nchini kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
UGONJWA WA EBOLA WATANGAZWA KUWA JANGA LA DHARURA DUNIANI

> Shirika la Afya Duniani limetangaza ugonjwa wa Ebola kuwa dharura ya kiafya duniani kutokana na ugonjwa huo kuua watu 1,668 katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwezi Agosti 2018

> Uamuzi huo umechukuliwa na jopo la wataalamu na shirika limezingatia vigezo kadhaa, ikiwemo hatari ya kusambaa kwa virusi vya Ebola duniani

Soma - https://jamii.app/EbolaGlobalEmergency
RASMI: MATTHIJS DE LIGT ASAJILIWA JUVENTUS

- Beki huyo raia wa Uholanzi mwenye miaka 19 amesajiliwa kwa ada ya Paundi Milioni 67.5 (Tsh.193,519,125,000) kutoka Ajax kwa mkataba wa miaka mitano

- Alikuwa akiwaniwa pia na vilabu vya Manchester United, Barcelona na PSG
Salaam za Pongezi toka kwa Balozi wa Sweden nchini kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
POLISI KUKATWA MSHAHARA ILI KUMLIPA WALIYEMVUNJA MGUU KWA KIPIGO

> Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Alli Hapi ameliagiza Jeshi la polisi kuwakata mshahara kiasi cha Tsh. milioni 1 askari wake 10 waliohusika kumvunja mguu Maiman Mwakajenge

> Inaelezwa kuwa walimshambulia kwa kipigo wakidai kuwa amewatukana

Soma - https://jamii.app/MakatoMshaharaPolisi
TCU YAKIFUTA CHUO KIKUU CHA ECKERNFORD

- TCU imesema Chuo hicho kilichopo Mkoani Tanga kimefutwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya udahili

- Ni takribani miezi 10 tangu kilipositishiwa kutoa mafunzo na kutakiwa kuhamisha Wanafunzi

Zaidi, soma https://jamii.app/ChuoEckernfordChafutwa
Kutoka Shirika la Human Rights Watch linalojishughisha na Masuala ya Uangalizi wa Haki za Binadamu Duniani kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kupata Tuzo ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
RIPOTI: VIFO VITOKANAVYO NA UKIMWI VYAPUNGUA

> Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa vifo vimepungua kwa 33% tangu mwaka 2010 ambavyo ni takribani vifo 770,000 tofauti na mwaka 2010 ambapo watu milioni 1.2 walifariki

> Aidha, maambukizi mapya yameongezeka hasa Mashariki ya Kati na Ulaya Mashariki ambapo kuna wagonjwa milioni 37.9

Soma - https://jamii.app/RipotiVifoUkimwi
INSTAGRAM KUFICHA IDADI YA ‘LIKES’ ILI KUONDOA KUTOKUJIAMINI

- Imefanya majaribio Canada mwezi Mei na mengine yanafanyika Australia, New Zealand, Ireland, Italy, Japan na Brazil

- Lengo ni watu waweke kile wanachokipenda wao

Zaidi, soma https://jamii.app/InstagramKuondoaLikes
KENYA: AMKATA KICHWA BABA YAKE AKIDHANI ANACHINJA MBUZI

> Dennis Mwangi (29) amemuua Peter Ndegwa (59) kwa kumkata kichwa akidai alidhani alikuwa anachinja mbuzi na kisha kukitia kwenye ndoo na kuanza kuzunguka nacho mjini

> Watu wanadhani huenda alikuwa akikabiliwa na matatizo ya kiakili

Soma - https://jamii.app/AkataKichwaBabake
IRAN YAKAMATA MELI YA MAFUTA YA KIGENI NA WAFANYAKAZI WAKE 12

- Imedai meli hiyo ilikuwa ikisafirisha mafuta kimagendo katika eneo la Ghuba siku ya Jumapili iliyopita

- Haijathibitishwa ikiwa meli hiyo ni ile ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) iliyopoteza mawasiliano siku hiyo ya Jumapili

Zaidi, soma https://jamii.app/IranYakamataMeliGhuba
UGANDA KUANZA KUTOA VYETI VYA USAJILI KWA WAFUGAJI NA NG'OMBE WAO

> Wafugaji wa ng'ombe watasajiliwa wenyewe na ng'ombe wao pia watasajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa kwasababu walaji wanahitaji nyama ya ng'ombe yenye umri kati ya miezi 15 hadi 24

Soma - https://jamii.app/UsajiliMifugoUG